visit here again on mukebez.blogspot.com


CHANGE YOUR LIFE

CHANGE YOUR LIFE
Go to Amazon .com and get the copy of this book to make your life better.

Jumanne, 20 Mei 2014

MAPENZI YAMFANYA HUYU JAMAA KUJINYONGA.

Geita.Mkazi wa Kijiji cha Shilabela, mkoani Geita, ambaye amefahamika kwa jina moja la Daud (35) amekufa kwa kujinyonga chooni kutokana na kinachodaiwa ni wivu wa mapenzi.
Tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia juzi maeneo ya General Tyre, nyumbani kwa mkwe wa marehemu huyo, Lusia Juma.
Taarifa zilizopatikana zinadai Daud alikutwa amejinyonga chooni na kwamba, kabla ya kuchukua uamuzi huo alikwenda nyumbani kwa mama mkwe wake kupeleka matumizi kwa mkewe, Irene Jackson (18) ambaye anaishi kwao baada ya kutokea ugomvi wa kindoa.
“Alikuja jana (juzi) hapa akaniambia nina maongezi na wewe, nikamwambia anisubiri kwani muda ule nilikuwa naelekea sokoni kwa mama,” alisema Jackson.
Jackson alisema baada ya kutoka sokoni alimkuta mume wake akila chakula cha mchana na majirani na kwamba, alimweleza amepeleka matumizi ya mtoto na kumtaka wazungumze lakini mwanamke huyo alikuwa bado ana kazi.
“Nilikuwa na kazi zangu nikamwomba awe na subira, baadaye jioni niliporejea nikamkuta yupo akaniambia tuongee nikamwambia sasa hivi ni usiku arudi kesho tuongee,” alisema Jackson.
“Aliniomba kitenge changu, nikamwambia mwanangu mimi sina kitenge, akasema basi hata cha mke wangu, nikamwambia mke wako hana kitenge,” alisema Mama mkwe wa Daud.
Anasema baada ya kumweleza hivyo akaondoka na geti likafungwa saa 2:45 usiku na kwamba, alirejea tena saa 4:00 usiku na kuwagongea lakini hawakuamka.
“Baada ya muda mfupi kama nusu saa hivi, tukapewa taarifa kuwa mume wangu amejinyonga chooni,” alisema Jackson.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Joseph Konyo alikiri kuwapo kwa tukio hilo na kwamba wanaendelea na uchunguzi.
BBC

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni