visit here again on mukebez.blogspot.com


CHANGE YOUR LIFE

CHANGE YOUR LIFE
Go to Amazon .com and get the copy of this book to make your life better.

Jumanne, 27 Mei 2014

MKURUGENZI WA TANESCO NA MKEWE WAFIKISHWA KIZIMBANI KWA WIZI WA MILION 31

ni
ALIYEKUWA Mkurugenzi wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), William Mhando, mke wake Eva Mhando, na wenzao watatu, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, wakikabiliwa na mashitaka sita ikiwemo matumizi mabaya ya madaraka, kughushi na kujipatia Sh. Milioni 31.7 kwa njia ya udanganyifu.
Kadhalika, Mhando anakabiliwa na matumizi mabaya ya madaraka kwa kuipa zabuni Kampuni ya Santa Clara Supplies Ltd, huku akijua ana maslahi nayo na kwamba anaimiliki yeye, mke na watoto wake.
Washtakiwa hao walisomewa mashitaka yake mbele ya Hakimu Mkazi Frank Moshi.Mbali na Mhando na Eva, washtakiwa wengine ni, France Mchalange, Sophia Misidai na Naftali Kisinga.
Mwendesha Mashitaka wa Taasisi wa Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Leonard Swai alidai kuwa kati ya Aprili Mosi na Desemba 31, mwaka 2011 katika ofisi za Makao Makuu ya Tanesco jijini Dar es Salaam, Mhando akiwa mwajiriwa kama Mkurugenzi wa shirika hilo, alitumia vibaya mdaraka yake.
Alidai kuwa, Mhando alitumia vibaya madaraka yake kwa kuamgalia maslahi yake binafsi baada ya kuipa zabuni ya kusambaza vifaa vya ofisi kampuni hiyo inayongozwa na mke wake, Eva na watoto wake, vyenye thamani ya Sh. Milioni 884.5 na kuisababishia kampuni hiyo kupata faida ya Sh. 31,747,000 kinyume cha sheria .
Katika shitaka la pili, ilidaiwa kuwa kati ya Januari 6 na Julai 30, mwaka 2011, mahali pasipofahamika, jijini Dar es Salaam, Eva alighushi taarifa ya ukaguzi wa fedha ya Kampuni ya Santa Clara Ltd, akionyesha kwamba imekaguliwa na Finx Capital House Desemba mwaka 2010.
Swai alidai katika shitaka la tatu, Agosti 9, mwaka 2011 jijini Dar es Salaam, mshtakiwa Eva alighushi nyaraka za umiliki wa hisa kutoka Santa Clara Supplies Ltd kwenda Eveta John Shing’oma huku akijua siyo kweli.
Upande huo wa Jamhuri ulidai katika shitaka la nne, Agosti 5, mwaka 2011 katika ofisi za Makao Makuu ya Tanesco, jijini, mshtakiwa Eva aliwasilisha nyaraka za manunuzi za kughushi akionyesha kwamba taarifa hiyo imeandaliwa na Finx Capital House huku akijua siyo kweli.
Katika shitaka la tano, ilidaiwa kuwa kati ya Aprili Mosi na Oktoba 31, mwaka 2011 jijini Dar es Salaam, Eva akiwa kama Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Santa Clara Limited kwa nia ovu, alijipatia faida ya Sh. Milioni 31.7 kutoka Tanesco baada ya kuwasilisha nyaraka za ukaguzi za kughushi.
Ilidaiwa katika shitaka la sita, Oktoba 17, mwaka 2011 katika ofisi za Tanesco, mshtakiwa wa tatu hadi wa tano, Mchalange, Misidai na Kisinga wakiwa watumishi wa shirika hilo, walipokea nyaraka za kughushi na kusababisha Kampuni ya Santa Clara Supplies Limited kupewa mkataba wa kusambaza vifaa vya ofisini.
Ilidaiwa kuwa mkataba huo ulisababisha kampuni hiyo kupata mkataba wa zabuni ya kusambaza vifaa vya Sh. Milioni 884.5 na kupata faida ya Sh. Milioni 31.5.
Washtakiwa walikana mashitaka hayo na mahakama iliwataka washtakiwa kuwa nawadhamini wawili watakaosaini hati ya dhamana ya Sh. Milioni 8, kuwasilisha hati za kusafiria mahakamani na wasitoke nje ya Mkoa wa Dar es Salaam, bila kibali cha mahakama.
Washtakiwa walitimiza masharti hayo na wako kwa dhamana hadi Juni 13, mwaka huu kesi hiyo itakapotajwa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni