visit here again on mukebez.blogspot.com


CHANGE YOUR LIFE

CHANGE YOUR LIFE
Go to Amazon .com and get the copy of this book to make your life better.

Jumatatu, 19 Mei 2014

TAARIFA KUTOKA TANZANIA MOVIE TALENTS KUHUSIANA NA MSIBA WA MSANII KUAMBIANA.

Uongozi wa Kampuni ya Proin Promotions Limited na Timu nzima ya Kampuni ya Proin Promotions Limited ambao ni Waandaaji na waendeshaji wa Shindano la Tanzania Movie Talents tunapenda kutoa pole zetu za dhati kwa Wazazi wa Marehemu Adam P.Kuambia, Ndugu wa Marehemu , Jamaa, Marafiki kwa ujumla na Rais wa Klabu ya Bongo Movie, Ndugu Steve Nyerere kwa kuondokewa na Mmoja kati ya Wasanii Mahiri kabisa katika tasnia hii ya filamu nchini vilevile tunatoa Pole zetu kwa Wasanii wa sanaa ya Maigizo Tanzania na Klabu ya Bongo Movie kwa kuondokewa na Msanii mwenzao Adam P Kuambiana.
Kutokana na Msiba huo wa Marehemu Adam Philip Kuambiana, Uongozi wa Kampuni ya Proin Promotions Limited ambao ni waandaaji na waendeshaji wa Mashindano ya Tanzania Movie Talents unapenda kutangaza kusitisha Zoezi la Usaili wa Shindano hilo lililokuwa linaendelea Mkoani Arusha kwa siku moja kwaajili ya Kuungana na Watanzania katika Msiba huu Mkubwa ulioikumba Tasnia ya Filamu Nchini Katika kuomboleza na Kushiriki katika Mazishi ya Marehemu Adam Philip Kuambiana yanayotarajiwa kufanyika kesho Jumanne tarehe 20 Mei 2014 katika Makaburi ya Kinondoni.
Kutoka Kwenye timu ya Tanzania Movie Talents iliyopo Mkoani Arusha, Timu hiyo itawakilishwa na Mmoja wa Majaji katika Shindano la Tanzania Movie Talents, Ndg Single Mtambalike ambae anatarajia kusafiri kesho kwa Ndege kutoka Mkoani Arusha kwaajili ya Kuungana na Watanzania wote na wasanii wengine katika msiba na mazishi ya Marehemu Adam Philip Kuambiana. Vilevile Ndg Single Mtambalike ataungana na Wafanyakazi wa Proin Promotions Limited waliopo jijini Dar Es Salaam katika Msiba huo.
Timu nzima ya Tanzania Movie Talents iliyopo Mkoani Arusha tunapenda kutoa Pole zetu za Dhati kwa wafiwa wote na watanzania wote tulioguswa na msiba huu wa Msanii wa Filamu Nchini Adam Kuambiana.
Shindano la Tanzania Movie Talents litaendelea kama kawaida siku ya Jumatano asubuhi kama ratiba ilivyopangwa.
Tunamuomba Mwenyezi Mungu ailaze Roho ya Marehemu Mahala Pema Peponi - Amina
Bwana ametoa na Bwana Ametwaa Jina la Bwana lihimidiwe
Imetolewa na
Josephat Lukaza
Afisa Mahusiano - Tanzania Movie Talents
Proin Promotions Limited

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni