visit here again on mukebez.blogspot.com


CHANGE YOUR LIFE

CHANGE YOUR LIFE
Go to Amazon .com and get the copy of this book to make your life better.

Jumamosi, 27 Septemba 2014

WABUNGE WA TANZANIA SIO HALALI BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI

Mahakama ya Afrika Mashariki (EACJ), jana imesema uchaguzi wa wabunge wa Tanzania katika Bunge la Afrika Mashariki ni batili kutokana na kukiuka ibara ya 50 ya mkataba wa kuanzishwa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Jaji Kiongozi, Jean Bosco-Butasi akiwa na majaji wengine wa mahakama hiyo, Isaac Lenaola na Jaji Faustine Ntezilyayo, walitoa uamuzi huo katika hukumu ya kesi iliyofunguliwa na aliyekuwa mmoja wa wagombea ubunge wa Eala kutoka Tanzania, Anthony Komu (Chadema).
Jaji Faustine Ntezilyayo, walitoa uamuzi huo katika hukumu ya kesi iliyofunguliwa na aliyekuwa mmoja wa wagombea ubunge wa Eala kutoka Tanzania, Anthony Komu (Chadema).
Katika hukumu hiyo ya kurasa 38, mahakama hiyo, imempa ushindi Komu katika hoja zake zote tatu na kutupilia mbali pingamizi la Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika kesi hiyo na hivyo, kuitaka Serikali kulipa gharama za kesi hiyo.
Katika shauri hilo namba saba la mwaka 2012, katika madai yake ya msingi Komu alikuwa anapinga utaratibu uliotumika kupata wagombea wa Bunge la Eala kutoka Tanzania akidai ulikiuka Ibara ya 50 ya mkataba wa kuanzishwa kwa EAC inayoelekeza wabunge wapatikane kwa uwiano.
Ibara hiyo inaeleza kuwa, Bunge la Taifa kutoka kila nchi mwanachama litachagua wabunge tisa kutoka nje ya wabunge wa bunge husika kuwa wabunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa kuzingatia uwiano wa vyama vya siasa, jinsia na makundi mengine.
Komu pia alikuwa akitaka tafsiri ya kisheria kama taratibu zilikiukwa Spika kumpitisha, John Chipaka kutoka chama cha Tadea kugombea ubunge wa Bunge la Afrika Mashariki, hali ya kuwa chama chake hakina mbunge hata mmoja.
Pia Komu alitaka kujua kama ni halali chama ambacho ndiyo kikuu cha upinzani nchini, kinachounda baraza kivuli la mawaziri, kukosa uwakilishi katika Bunge la Afrika Mashariki.
Katika uamuzi wa majaji wa mahakama hiyo, wameamua kuwa uchaguzi huo ulikiuka ibara ya 50 ya kuanzisha Jumuiya ya Afrika Mashariki na upatikanaji wa wabunge wa Bunge hilo.
Uamuzi huo, ulieleza kuwa kanuni za Bunge la Jamhuri, ibara ya tano kifungu kidogo cha tano na cha 12 vilivyotumika katika uchaguzi huo, pia vinapingana na Ibara ya 50 na hivyo kusababisha kutopatikana kihalali wagombea wote wa uchaguzi huo.
Akisoma hukumu hiyo, Jaji alisema kwa mkataba wa Jumuiya hiyo, wabunge wa Bunge hilo, wanapaswa kuchaguliwa kutokana na uwiano wa wabunge katika Bunge la nchi husika na pia kushirikisha makundi mengine ambayo siyo ya vyama vya siasa.
Hata hivyo, mahakama hiyo ilieleza haina mamlaka ya kutangaza kutengua ubunge wa wabunge wa Tanzania kwa kuwa shauri hilo, sasa linatakiwa kutolewa uamuzi na Mahakama Kuu hapa nchini.
Wakizungumza na waandishi wa habari mara baada ya hukumu hiyo, Komu na Wakili wake John Mallya ambaye alikuwa akimwakilisha wakili, Damas Mbogoro, walisema kutokana na uamuzi huo, sasa watapeleka uamuzi huo Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma.
Wakili Mallya alisema shauri hilo, ambalo tayari lilikuwa Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma, linatarajiwa kutajwa Novemba 27 mwaka huu ili kupangiwa siku ya kuanza kusikilizwa.
“Tuna imani Mahakama Kuu itafuata tafsiri za kisheria zilizotolewa na majaji wa Mahakama ya Afrika Mashariki ili kutangaza rasmi kutengua uchaguzi wa wabunge wa Tanzania,”alisema Mallya.
Hata hivyo, alifafanua kuwa hukumu hiyo, pia imeeleza fursa za Watanzania wengine bila kupitia vyama vya siasa wanaweza kujitokeza kugombea kwa kupitia makundi ya kijamii.

WABUNGE WA TANZANIA SIO HALALI BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI

Mahakama ya Afrika Mashariki (EACJ), jana imesema uchaguzi wa wabunge wa Tanzania katika Bunge la Afrika Mashariki ni batili kutokana na kukiuka ibara ya 50 ya mkataba wa kuanzishwa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Jaji Kiongozi, Jean Bosco-Butasi akiwa na majaji wengine wa mahakama hiyo, Isaac Lenaola na Jaji Faustine Ntezilyayo, walitoa uamuzi huo katika hukumu ya kesi iliyofunguliwa na aliyekuwa mmoja wa wagombea ubunge wa Eala kutoka Tanzania, Anthony Komu (Chadema).
Jaji Faustine Ntezilyayo, walitoa uamuzi huo katika hukumu ya kesi iliyofunguliwa na aliyekuwa mmoja wa wagombea ubunge wa Eala kutoka Tanzania, Anthony Komu (Chadema).
Katika hukumu hiyo ya kurasa 38, mahakama hiyo, imempa ushindi Komu katika hoja zake zote tatu na kutupilia mbali pingamizi la Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika kesi hiyo na hivyo, kuitaka Serikali kulipa gharama za kesi hiyo.
Katika shauri hilo namba saba la mwaka 2012, katika madai yake ya msingi Komu alikuwa anapinga utaratibu uliotumika kupata wagombea wa Bunge la Eala kutoka Tanzania akidai ulikiuka Ibara ya 50 ya mkataba wa kuanzishwa kwa EAC inayoelekeza wabunge wapatikane kwa uwiano.
Ibara hiyo inaeleza kuwa, Bunge la Taifa kutoka kila nchi mwanachama litachagua wabunge tisa kutoka nje ya wabunge wa bunge husika kuwa wabunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa kuzingatia uwiano wa vyama vya siasa, jinsia na makundi mengine.
Komu pia alikuwa akitaka tafsiri ya kisheria kama taratibu zilikiukwa Spika kumpitisha, John Chipaka kutoka chama cha Tadea kugombea ubunge wa Bunge la Afrika Mashariki, hali ya kuwa chama chake hakina mbunge hata mmoja.
Pia Komu alitaka kujua kama ni halali chama ambacho ndiyo kikuu cha upinzani nchini, kinachounda baraza kivuli la mawaziri, kukosa uwakilishi katika Bunge la Afrika Mashariki.
Katika uamuzi wa majaji wa mahakama hiyo, wameamua kuwa uchaguzi huo ulikiuka ibara ya 50 ya kuanzisha Jumuiya ya Afrika Mashariki na upatikanaji wa wabunge wa Bunge hilo.
Uamuzi huo, ulieleza kuwa kanuni za Bunge la Jamhuri, ibara ya tano kifungu kidogo cha tano na cha 12 vilivyotumika katika uchaguzi huo, pia vinapingana na Ibara ya 50 na hivyo kusababisha kutopatikana kihalali wagombea wote wa uchaguzi huo.
Akisoma hukumu hiyo, Jaji alisema kwa mkataba wa Jumuiya hiyo, wabunge wa Bunge hilo, wanapaswa kuchaguliwa kutokana na uwiano wa wabunge katika Bunge la nchi husika na pia kushirikisha makundi mengine ambayo siyo ya vyama vya siasa.
Hata hivyo, mahakama hiyo ilieleza haina mamlaka ya kutangaza kutengua ubunge wa wabunge wa Tanzania kwa kuwa shauri hilo, sasa linatakiwa kutolewa uamuzi na Mahakama Kuu hapa nchini.
Wakizungumza na waandishi wa habari mara baada ya hukumu hiyo, Komu na Wakili wake John Mallya ambaye alikuwa akimwakilisha wakili, Damas Mbogoro, walisema kutokana na uamuzi huo, sasa watapeleka uamuzi huo Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma.
Wakili Mallya alisema shauri hilo, ambalo tayari lilikuwa Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma, linatarajiwa kutajwa Novemba 27 mwaka huu ili kupangiwa siku ya kuanza kusikilizwa.
“Tuna imani Mahakama Kuu itafuata tafsiri za kisheria zilizotolewa na majaji wa Mahakama ya Afrika Mashariki ili kutangaza rasmi kutengua uchaguzi wa wabunge wa Tanzania,”alisema Mallya.
Hata hivyo, alifafanua kuwa hukumu hiyo, pia imeeleza fursa za Watanzania wengine bila kupitia vyama vya siasa wanaweza kujitokeza kugombea kwa kupitia makundi ya kijamii.

MWANAMKE APIGWA MAWE HADI KUFA KWA KUZINI NJE YA NDOA

Mwanamke mmoja ameuawa kwa kupigwa mawe nchini Somalia na kundi la wanamgambo wa Al Shabaab.
Ripoti zinasema kuwa takriban watu 200 akiwemo gavana wa eneo hilo walishuhudia watu wakimpiga mawe mwanamke huyo kwenye mji wa Barowe.
Mwanamke huyo wa umri wa miaka 30 alikuwa ameshutumiwa kwa kufanya mapenzi nje ya ndoa.
Wadadisi wanasema kuwa mauaji hayo ini ishara ya ushawishi wa kundi la Al shabaab hata baada ya kushambuliwa na serikali ya Somalia pamoja na vikosi vya muungano wa Afrika.
Mji wa Barowe ambao uko umbali wa kiomita 200 kutoka mji mkuu Mogadishu umekuwa ngome ya Al Shabaab.

MWANAMKE APIGWA MAWE HADI KUFA KWA KUZINI NJE YA NDOA

Mwanamke mmoja ameuawa kwa kupigwa mawe nchini Somalia na kundi la wanamgambo wa Al Shabaab.
Ripoti zinasema kuwa takriban watu 200 akiwemo gavana wa eneo hilo walishuhudia watu wakimpiga mawe mwanamke huyo kwenye mji wa Barowe.
Mwanamke huyo wa umri wa miaka 30 alikuwa ameshutumiwa kwa kufanya mapenzi nje ya ndoa.
Wadadisi wanasema kuwa mauaji hayo ini ishara ya ushawishi wa kundi la Al shabaab hata baada ya kushambuliwa na serikali ya Somalia pamoja na vikosi vya muungano wa Afrika.
Mji wa Barowe ambao uko umbali wa kiomita 200 kutoka mji mkuu Mogadishu umekuwa ngome ya Al Shabaab.

JUMBE ZAIDI YA 50 ZATUMWA KUMTISHIA SITTA

Mwenyekiti wa Bunge la Katiba, Samuel Sitta amesema anapokea meseji za simu zaidi ya 50 kwa siku za kumtukana na kusisitiza ataendelea kupambana kuhakikisha Katiba inayopendekezwa inapatikana.
Sitta alitoa kauli hiyo bungeni mjini Dodoma jana wakati akielezea kutoridhishwa kwake na kile alichodai ni namna hukumu ya kesi iliyofunguliwa na Saed Kubenea inavyopotoshwa na wanaomchukia.
“Kuna baadhi ya vyombo vya habari wananichukia mimi binafsi. Wasichanganye chuki hizo na mchakato wa Bunge Maalumu,”alisema Sitta na kuongeza;
“Mimi napokea matusi kila siku. Meseji zisizopungua 50 viongozi wa Chadema wameweka namba zangu katika tovuti nitukanwe kila siku hilo mimi niko tayari na mnaniona niko safi tu wala sihangaiki nalo.”
“Lakini sasa Bunge Maalumu ni chombo cha kikatiba, kiko tofauti na mwenyekiti wake. Huwezi kuliadhibu Bunge Maalumu kwa sababu hupendi sura ya mwenyekiti wake,”alisema.
Sitta alienda mbali zaidi na kusema,“Kwa hiyo wale wanaoendeleza hayo mapambano tuendelee na tutaendelea kupambana, lakini kazi ya Bunge Maalumu itaendelea na ndugu zangu Watanzania mjue tunaandaa Katiba safi na rafiki kwa wananchi na itapatikana.”
Sitta alisema baada ya kutolewa kwa hukumu hiyo ya kesi ya Kubenea dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), kumekuwa na tafsiri alizosema ni potofu.
Baada ya maelezo hayo alimpa ruksa AG, Jaji Frederick Werema kutoa ufafanuzi.
Jaji Werema alisema Mahakama Kuu, katika kutafsiri kifungu cha 25(1) (2) inakiri kwamba kuna tofauti kati ya kifungu kilichoandikwa Kiswahili na kile kilichoandikwa Kiingereza.
Alisema Mahakama Kuu katika hukumu hiyo imesema mamlaka ya kuandika Katiba Mpya ina maana ni mamlaka ya kuandika na kupitisha katiba inayopendekezwa kwa ajili ya kupelekwa kwa wananchi kwa ajili ya kupigiwa kura ya maoni.
Takukuru yalitesa Bunge
Wakati hayo yakiendelea suala la kuingizwa ama kutoingizwa kwenye katiba, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), linaonekana kulitesa Bunge la Katiba baada ya kamati 10 kati ya 12 kulirejesha tena jana.
Rasimu iliyowasilishwa bungeni na Tume ya Mabadiliko ya Katiba, ililiacha suala hilo kwa maelezo kuwa siyo moja ya mambo ya Muungano na msimamo huo ukaungwa mkono na Kamati ya Uandishi ya Bunge hilo.
Credit: Mwananchi

JUMBE ZAIDI YA 50 ZATUMWA KUMTISHIA SITTA

Mwenyekiti wa Bunge la Katiba, Samuel Sitta amesema anapokea meseji za simu zaidi ya 50 kwa siku za kumtukana na kusisitiza ataendelea kupambana kuhakikisha Katiba inayopendekezwa inapatikana.
Sitta alitoa kauli hiyo bungeni mjini Dodoma jana wakati akielezea kutoridhishwa kwake na kile alichodai ni namna hukumu ya kesi iliyofunguliwa na Saed Kubenea inavyopotoshwa na wanaomchukia.
“Kuna baadhi ya vyombo vya habari wananichukia mimi binafsi. Wasichanganye chuki hizo na mchakato wa Bunge Maalumu,”alisema Sitta na kuongeza;
“Mimi napokea matusi kila siku. Meseji zisizopungua 50 viongozi wa Chadema wameweka namba zangu katika tovuti nitukanwe kila siku hilo mimi niko tayari na mnaniona niko safi tu wala sihangaiki nalo.”
“Lakini sasa Bunge Maalumu ni chombo cha kikatiba, kiko tofauti na mwenyekiti wake. Huwezi kuliadhibu Bunge Maalumu kwa sababu hupendi sura ya mwenyekiti wake,”alisema.
Sitta alienda mbali zaidi na kusema,“Kwa hiyo wale wanaoendeleza hayo mapambano tuendelee na tutaendelea kupambana, lakini kazi ya Bunge Maalumu itaendelea na ndugu zangu Watanzania mjue tunaandaa Katiba safi na rafiki kwa wananchi na itapatikana.”
Sitta alisema baada ya kutolewa kwa hukumu hiyo ya kesi ya Kubenea dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), kumekuwa na tafsiri alizosema ni potofu.
Baada ya maelezo hayo alimpa ruksa AG, Jaji Frederick Werema kutoa ufafanuzi.
Jaji Werema alisema Mahakama Kuu, katika kutafsiri kifungu cha 25(1) (2) inakiri kwamba kuna tofauti kati ya kifungu kilichoandikwa Kiswahili na kile kilichoandikwa Kiingereza.
Alisema Mahakama Kuu katika hukumu hiyo imesema mamlaka ya kuandika Katiba Mpya ina maana ni mamlaka ya kuandika na kupitisha katiba inayopendekezwa kwa ajili ya kupelekwa kwa wananchi kwa ajili ya kupigiwa kura ya maoni.
Takukuru yalitesa Bunge
Wakati hayo yakiendelea suala la kuingizwa ama kutoingizwa kwenye katiba, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), linaonekana kulitesa Bunge la Katiba baada ya kamati 10 kati ya 12 kulirejesha tena jana.
Rasimu iliyowasilishwa bungeni na Tume ya Mabadiliko ya Katiba, ililiacha suala hilo kwa maelezo kuwa siyo moja ya mambo ya Muungano na msimamo huo ukaungwa mkono na Kamati ya Uandishi ya Bunge hilo.
Credit: Mwananchi

Ijumaa, 26 Septemba 2014

MAXIMO AWATAKA WASHABIKI KUFURIKA UWANJANI JUMAPILI

Kikosi cha timu ya Young Africans kitashuka dimba la Uwanja wa Taifa siku ya jumapili kupambana na Wajela Jela timu ya Jeshi la Magereza nchini Prisons FC kutoka jijini Mbeya ikiwa ni mchezo wa pili wa mzunguko wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara msimu wa 2014/2015.
Akiongea na tovuti rasmi ya klabu leo mara baada ya mazoezi, kocha mkuu wa Young Africans mbrazil Marcio Maximo amesema vijana wake wako fit kuelekea mchezo huo wa siku ya jumapili huku wakiwa wamejipanga kuhakikisha wanaondoka na pointi tatu muhimu.
Maximo amesema baada ya kupoteza mchezo wa awali dhidi ya wakata miwa wa Mtibwa Sugar, kikosi chake kimekua kikiendelea na mazoezi kila siku katika uwanja wa shule ya sekondari Loyola huku wakiyafanyia marekebisho makosa yaliyojitokeza katika mchezo huo wa awali.
Kuhusu timu ya Tanzania Prisons mbrazil Maximo amesema anatambua walishinda mchezo wa awali dhidi ya Ruvu Shooting hivyo wana morali bado ya kuendeleza ushindi siku ya jumapili, lakini pia kikosi changu kipo fit kwa mchezo huo kwa kusaka pointi tatu muhimu.
Aidha Maximo amesema habari njema kwa wana Yanga ni kurejea dimbani kwa kiungo Andrey Coutinho pamoja na mshambuliaji Jerson Tegete ambao wanatarajiwa kuonekana kwenye mchezo huo na kuhakikisha wanaisaidia timu yao kupata ushindi.
Wachezaji watakaoukosa mchezo wa siku ya jumapili ni Oscar Joshua na Hussein Javu ambao wote ni majeruhi, wakisumbuliwa na maumivu ya nyama za paja, na jumatatu wanatarajiwa kuanza mazoezi mepesi baada ya kuwa kwenye matibabu chini ya usimamizi wa daktari wa timu Dr Suphian Juma.
Mwisho kocha Marcio Maximo amewaomba wapenzi, washabiki, wanachama na wadau wa soka kwa ujumla kujitokeza kwa wingi siku ya jumapili katika mechi dhidi ya Prisons kuja kuwapa sapoti vijana na kuwashangilia muda wote wa mchezo.

MUKEBEZI BLOG/(DOUBLE LL KIDS): KIPIMO CHA SKETI NI MBINO MOJAWAPO YA KUJUA UKO KA...

MUKEBEZI BLOG/(DOUBLE LL KIDS): KIPIMO CHA SKETI NI MBINU MOJAWAPO YA KUJUA UKO KA...: Baadhi ya watafiti wana sahuku ikiwa vipimo vya sketi vitamtahadharisha mwanamke kuhusu tisho la Saratani Utafiti unaonyesha kuwa wanawake ...

KIPIMO CHA SKETI NI MBINO MOJAWAPO YA KUJUA UKO KATIKA HATARI YA CANCER

Baadhi ya watafiti wana sahuku ikiwa vipimo vya sketi vitamtahadharisha mwanamke kuhusu tisho la Saratani
Utafiti unaonyesha kuwa wanawake wanaonenepa maishani bila ya kuwa waangalifu wanajiweka katika hatari ya kupata Saratani.
Watafiti kutoka chuo Kikuu cha London wanasema kwamba wanawake walio kati ya umri wa miaka 24-28 ambao huendelea kunenepa kila baada ya miaka 10, wako katika hatari zaidi ya kupata Saratani ya Matiti baada ya kupitisha umri wa kuzaa.
Sasa je ni nini ishara ya mwanamke kunenepa? Watafiti wanasema vipimo vya sketi yake vinaweza kukusaidia kujua ikiwa uko katika hatari ya kpatwa Saratni ya Matiti au la.
Kila unapogundua kuwa sketi yako inaendelea kuwa ndogo kiunoni, basi inakubidi ujue kuwa mwili wako unaongekeza kwa unene. Na pia ni rahisi kwa wanawake kukumbuka kipimo cha sketi kuliko kitu kingine chochote.
Kwa hilo watafaiti wanasema mwanampe anapaswa kutahadhari kila sketi yake inapoendelea kuwa ndogo kwake maana kwamba amenenepa zaidi. Ikiwa ukubwa wake unazidi kwa kipimo cha sketi mbili katika kipindi kimoja basi mwanamke anakuwa katika hatari ya kupatwa na Saratani hata zaidi.
'Mfumo wa maisha'
Tisho hili linawakabili zaidi wanawake waliopitisha umri wa kupata watoto
Akizungumzia utafiti huo, Simon Vincet kutoka shirika la kupambana na saratani ya Matiti la Breakthrough Breast Cancer, alisema kuwa saratani ya Matiti miongoni mwa wanwake inaweza kupunguka ikiwa watu watabadilisha mfumo wa maisha kwa kujiuzia kunenepa kupita kiasi na kufanya mazoezi sana.
Utafiti huu unaangazia njia rahisi sana kwa wanawake kuwa waangalifu kuhusu unene wa miili yao.
Kuangalia kipimo cha sketi kati ya wanawake walio kati ya miaka 24 na 28 wenye miaki katikati ya 20 na zaidi wanaweza kuwa na njia rahisi ya kufuatilia uzito wa miili ya Unene wa kupita kiasi unajulikana kwa sababu ni hatari kubwa inayochangia katika ugonjwa wa saratani , hususan mafuta ya yaliyoko tumboni.
Prof Usha Menon wa shirika lakupambana na satratani ya matiti, ndiye aliyeongoza utafiti huo na kuambia BBC kuwa "Kama kipimo cha sketi kinaweza kuthibitishwa na wengine kama kigezo cha wanawake watu wazima kuapa Saratani, basi hii itakuw anjia nzuri na rahisi ya mtu kuwa mwangalifu ili asinenepe kupita kiasi.
'Changamoto'
Unene kupita kiasi ni moja ya mambo yanayohatarisha afya ya wanawake waliopitisha umri wa kuzaa
Watafiti hao walisema utafiti wao ulikuwa na changamoto kadhaa kwamba uliangazia zaidi wanawake kukumbuka vipimo vya sketi zao tangu tangu wawe na umri wa miaka 20
Lakini ikiwa matokeo ya utafiti huo yatathibitishwa, itakuwa njia rahisi kwa wanawake kuelewa hatari zinazowakabili hasa wanapoendelea kunenepa.
Tom Stansfeld kutoka shirika la utafiti wa Saratani nchini Uingereza,anasema utafiti huo unaweza kuaminika lakini unazingatia zaidi wanawake kukumbuka vipimo vya sketi walizovalia miaka ya zamani.
Utafiti unasema kuwa baadhi ya mambo muhimu ambayo mwanamke anaweza kufanya kupunguza tisho la kuugua Saratani ya Matiti , hasa baada ya kupitisha miaka yake ya kuzaa ni pamoja na kufanya mazoezi , kula vizuri na kupunguza ulevi.
Kupunguza unene ni njia moja wapo ya kupunguza tisho la kupata Saratani baada ya kupitisha miaka ya kuzaa na kuangalia vipimo vya sketi za wanawake kuwahamasisha wanawake.

MCHUNGAJI ALIEWALISHA WAUMINI MAJANI SASA AWANYWESHA PETROL

Mchungaji wa Afrika Kusini aliyewahi kuwalisha waumini wake majani, sasa anawanywesha petrol.
Pastor Lesego Daniel wa Rabboni Centre Ministries aliwahi kuandikwa sana na vyombo vya habari duniani kwa kuwaagiza wafuasi wake kula majani kama wanyama kwa madai kuwa binadamu wanaweza kula chochote kilichotoka kwa Mungu.
Kitendo hicho kiliwaacha waumini wengi wakitapika na kuharisha. Na sasa anawataka waumini wake kunywa petroli kwa madai kuwa itageuka kuwa juice ya nanasi.

Jumanne, 23 Septemba 2014

OBAMA AAHIDI KUWAANGAMIZA ISLAMIC STATE

Rais Obama ameahidi kuangamiza Wanamgambo wa Islamic State
Rais wa Marekani Barack Obama amesema Marekani itashambulia kundi linalojiitaa Islamic state kote nchini Syria na Iraq ili kuwanyima kabisa makao ya kujificha .
Bw Obama amesema kushiriki kwa mataifa kadhaa ya kiarabu katika mapambano hayo kunaonyesha wazi hivyo si vita vya Marekani pekee bali wao ni sehemu ya muungano wa mataifa yanayopigana na kundi hilo liitwalo pia ISIL.
Pia amekiri kuwa mashambulio hayo yamelenga pia wale aliowataja kuwa wanamgambo sugu wa al Qaeda wa kundi liitwalo Khorasan ambao anasema wanalenga kuishambulia Marekani.
Nazo taarifa za jeshi la Marekani zasema malengo ya mashambulio yaliyofanywa yametimia.
Wapiganaji wa Islamic State wamekuwa wakifanya mauaji na utekaji nyara
Wanamgambo kadhaa wa IS wameripotiwa kuuliwa japo vifo vya raia pia vimeripotiwa.
Mapema msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Urusi Alexander Lukashevichy amesema mashambulio yoyote dhidi ya ISIL ni sharti yazingatie sheria za kimataifa.
Kadhalika Obama, amesema kuwa kuhusika kwa nchi za kiarabu katika vita dhidi ya wanamgambo wa Islamic State nchini Syria ni dalili toshja kuwa vita hivi sio vya Marekani pekee.
Obama amesema ataendelea kukusanya jeshi la kimataifa dhidi ya wapiganaji hao.
Saudi Arabia, Milki za kiarabu,Jordan na Bahrain zote zilituma ndege za kijeshiu katika opereshei hiyo.

BREAKING NEWSSSSSSSSSSSSSSS

BREAKING NEWSSSS: TI KUDONDOKA DAR ES SALAAM

Katika kilele cha serengeti Fiesta mwaka huu ambayo inatarajiwa kufanyika pale viwanja vya Leaders club siku ya tarehe 18 october msanii anaetarajiwa kuja ni mwanamuziki wa Hiphop kutoka Marekani anaefahamika kwa jina la T.I.

BREAKING NEWSSSSSSSSSSSSSSS

BREAKING NEWSSSS: TI KUDONDOKA DAR ES SALAAM

Katika kilele cha serengeti Fiesta mwaka huu ambayo inatarajiwa kufanyika pale viwanja vya Leaders club siku ya tarehe 18 october msanii anaetarajiwa kuja ni mwanamuziki wa Hiphop kutoka Marekani anaefahamika kwa jina la T.I.

MASHAMBULIZI YA MAREKANI YAANZA NCHINI SYRIA

Majeshi ya Marekani yameanza rasmi mashambulizi ya anga nchini Syria yakilenga kundi la kigaidi la ISIS (Islamic State of Iraq and Syria).
Makao Makuu ya Ulinzi ya Marekani yameeleza kuwa wanafanya mashambulizi ya mchanganyiko kwa kutumia mabomu, wapiganaji wa ardhini pamoja na majeshi ya Anga kutoka nchi za Mashariki ya Kati zinazowaunga mkono.
Lakini habari za mashambulizi yaliyoanza zilitolewa na raia wa Syria aliyetweet kuhusu kile anachokisikia katika mji aliopo wa Raqqa ambako kuna makao makuu ya kundi hilo.
Mtu huyo anaetumia jina la Abdulkader Hariri aliandika kuwa milipuko mikubwa imelenga makao makuu ya ISIS na kwamba anga lote limejaa ndege za kivita na drones.
Baadae Agency ya wanaharakati nchini Syria ilipost video fupi inayoonesha kwa mbali mashambulizi ya Marekani.

KIJANA AMKODISHA MCHUMBA WAKE APATE PESA YA KUNUNULIA SIMU

Mwanafunzi wa Chuo kikuu kimoja cha China ambaye jina lake halikutambulika kwa haraka ameamua kufanya ‘uchizi’ ili mradi tu aipate pesa ya kununua aina mpya ya iPhone iliyoingia sokoni, iPhone6.
Kijana huyo wa alionekana akiwa nje ya chuo kikuu cha Songijiang akiwa na bango kubwa lililoandikwa kwa kichina na kutafsiriwa ‘Girlfriend Sharing’.
Katika tangazo hilo kijana huyo anaeleza kuwa yuko tayari kumkodisha mpenzi wake kwa mtu yeyote atakayeweza kutoa pesa ili jamaa apate kiasi cha kutosha kuinunua iPhone 6 yenye screen kubwa.
Picha ya kijana huyo imesambaa kwa kasi katika mtandao wa kijamii unaotumiwa na wachina uitwao ‘Weibo’ ambao ni kama Twitter.
Tangazo hilo limeambatana na picha za mpenzi wake na amewatoa hofu wateja wanaosita kuingia nae mkataba kuwa hata mpenzi wake ameridhia na yuko tayari kudate na mtu yeyote atakaejitokeza.
Muda wa kuwa na msichana huyo baada ya kumkodi umebainishwa kutokana na malipo yatakayofanywa na mteja. Viwango ni vya saa 1 (10 yuan), siku 1 (50 yuan) au mwezi mmoja (500 yuan).
Hata hivyo, wapenzi hawa sio wa kwanza kujiweka sokoni ili wapate bidhaa ya kampuni ya Apple. Mwaka jana katika uzinduzi wa iPhone 5, wanandoa wa Shaghai waliwaweka sokoni watoto wao watatu ili wapate pesa ya kununua computer na simu za iphones lakini walikamatwa na kufunguliwa mashitaka.
Lakini pia kijana mdogo wa Hunan alijitolea kuuza figo lake ili apate pesa ya kununua iPad na iPhone.
Siyo hayo tu, hivi karibuni mwanaume mmoja wa Saudi Arabia ametaka kupewa iPhone 6 kama mahari ya dada yake hata kabla aina hiyo ya simu haijazinduliwa Bahrain.

MKUU WA MKOA ARUSHA AWA MGENI RASMI MKUTANO MKUBWA WA UTALII

Mkutano mkubwa unaohusu mambo yate ya utalii unafanyika jijini Arusha na kuhudhuriwa na washiriki kutoka nchi mbalimbali duniani ukiwa na lengo la kukuza na kuendeleza utalii.

Mkutano huo ambao umeandaliwa na kampuni ya MPINGO TOURISM SUMMIT na mgeni rasmi akiwa ni mkuu wa mkoa wa Arusha mheshimiwa Magesa Mulungu unahusu mambo yote ya utalii,changamoto na faida kutokana na fulsa za utalii zilizopo Tanzania hususani jijini Arusha.

Wawakilishi wanaohudhuria katika mkutano huo wanatoka katika nchi mbalimbali duniani ikiwa ni pamoja na Austraria,South Africa,Marekani,Zimbabwe,United Kingdom,Netherland pamoja na kutoka makampuni mbalimbali ya utalii ambayo yalishiriki kupata fulsa hizo.

Akizungumza wakati wa mkutano huo,mkurugenzi bwana Bakiri Angalia ambae ni CEO Grobal Skills aliwashukuru washiriki wote kwa kuchangia mada kama ambavyo ilikuwa ikiwasilishwa kutoka kwa wasemaji.

Mkutano huo uliofunguliwa september 22 unatarajiwa kumalizika september 23 jijini arusha na washiriki wanamatumaini makubwa kuwa tasnia ya utalii itapiga hatua kubwa sana kutokana na maazimio ya mkutano huo.

Chanzo:mshiriki mwanahabari mshiriki kutoka Arusha.

Jumatatu, 22 Septemba 2014

BARUA HII YA MBASHA KWA GWAJIMA IWE FUNZO KWA WANAUME WENYE WAKE WANAOSHIRIKI KATIKA MAKUNDI MBALIMBALI YA JAMII,ZIKIWEMO KWAYA MAKANISANI

Hii barua ya Mume wa Mwimbaji wa Nyimbo za injili nchini - Flora Mbasha kwenda kwa mchungaji maarufu nchini, Mchungaji Gwajima inakuhusu....
"Mchungaji ...yapata kama wiki mbili zilizopita nilihoji kupitia vyombo vya habari juu ya ‘utajiri' wa ghafla wa mkewangu Mara baada ya mgogoro kutokea kati yangu na yeye, bila kupoteza muda mkewangu akanijibu kupitia gazeti moja la udaku kuwa amechangiwa fedha kiasi cha milioni 9 na waumini kanisani kwakoMchungaji,naomba uelewe kuwa nafahamu juu ya mipango yote mnayoipanga kuliko unavyodhani!!
Kwanza ni kweli kuwa mlipitisha harambee ya kumchangia mkewangu, lakini kiwango kilichopatikanakilikuwa ni milioni 2 na laki tatu na si milioni tisa kama mlivyotangaza!!Lakini mlitangaza uongo huo makusudi iwe rahisi kutimiza malengo yenu ya kidhalimu mliyoyapanga juu yangu!!Mnamo tarehe 3 mwezi juni mwaka huu, mlifungua akaunti mpya kwa jina la mkewangu katika benki ya crdb morogoro, na siku nne baadae mkewangu aliingiziwa fedha kiasi cha milioni 18 kutoka akaunti ya MWANAMAPINDUZI FOUNDATION ambayo hyo accnt ipo nmb mwanza! Ambapo asasi hii inamilikiwa na mchungaji wako msaidizi Maximilian Machumu pamoja na mbunge wa viti maalumu kutoka mikoa ya kaskazini!
Nashukuru kama ulimpa fedha hizi kwa nia ya kumsaidia, lakini hofu yangu ni kuwa kwanini kitendo hiki kifanyike kwa kificho?? Kwanini mtumie njia za siri ambazo si rahisi watu kujua kama mmempa fedha??
Pia napatwa na mashaka zaidi kwani siku moja baada ya fedha hizi kuingizwa taarifa ya benki inaonyesha kuwa kiasi cha milioni sita cash zilitolewa na siku hiyo hiyo wapo waandishi watatu wa magazeti ya udaku ambao wanaonekana waliingiziwa fedha kiasi cha milioni moja kila mtu na aliyedeposit hizo fedha ni moja ya viongozi wako hapo kanisani!! Kuna nini hapo??
Mchungaji, naomba tusizunguke mbuyu! Ni dhahiri shahiri kuwa umekuwa na uhusiano wenye utata na mkewangu kwa muda mrefu sasa!
Binafsi nilianza kupata wasiwasi mwaka jana mwezi desemba tulipoenda katika mkutano wako wa injili pale morogoro! Mimi na mkewangu tulifikia hoteli ya kingsway msamvu na wewe ulifikia Nashera Hotel maeneo ya forest hill!!
Baada ya siku tatu za mahubiri mkutano wako ulipigwa marufuku na serikali kwasababu ya maneno yakichochezi uliyokuwa unahubiri, hvyo ikatulazimu waimbaji wote turejee dar es salaam!!
Lakini uliniomba mkewangu abaki na wewe kwani ulipanga uwe unawafanyia watu maombi pale kanisani kwako kihonda kwa muda wa siku nne!! Nilikubali na nikamuacha mkewangu nyumbani kwa dada yako pale mazimbu!! Lakini kesho yake dada yako alisafiri kwenda mwanza na ikabidi mkewangu arudi hotelini kingsway!!
Kwaa taarifa nilizonazo na nimezithibitisha kupitia wahudumu wa pale hotelini ni kuwa mkewangu hakuwahi kulala pale hata siku moja ingawa chumba kililipiwa kwa siku zote zile!! Unaweza kunijibu alikuwa analala wapi?? Je unaweza kunieleza kwanini mkewangu alikuwa analetwa nashera hoteli na taxi kila siku usiku!! Sibahatishi katika hili kwani hata namba ya dereva taxi ninayo!!
Yote haya nilivumilia, na hapa kati kati kuna mengi sana yametokea lakini nikajifanya mjinga nikajishusha nikavumilia kwa lengo la kulinda ndoa yangu isiharibike lakini naona wenzangu hambadiliki wala hamjishitukii sana sana mapenzi ndio yanzidi kuwa motomoto kati yenu!! Ulikuwa unategemea nivumilie mpaka lini, nijishushe kiasi gani, niwe mjinga kiasi gani Nilikuvumilia sana mchungaji lakini sasa imefika point hapana, imetosha lazima nikuondelee uvivu watanzania na dunia ikufahamu jinsi ulivyo na kitendo ulichonifanyaiana unataka kuniziba mdomo kwa kunitishia jela miaka 30!!!
Wewe ni mpuuzi na shetani anaishi ndani yako... na nataka nikuahidi kitu kimoja kuwa NITAKUSHINDA! Najua utanisumbua sana kutokana na hela zako but at the end, I will be the last man standing!! Narudia tena, nitakushinda.!!
Bila kusahau naomba niongee na wewe pia mkewangu, hivi ni nini kilichokukuta ndani ya moyo wako How did we get here?? Je ni fedha zilizokufanya ukengeuke kiasi hicho au kuna kingine?? Kama unanichukia mimi kiasi hiki je, uwahurumii hata watoto wetu?? Mbona tunawatengenezea mikosi wakiwa wadogo hivi?? Hivi unadhani watoto wanajisikiaje watakaposikia kuwa baba ameenda jela kwa kosa la kubaka lakini aliyechongesha muvi yote hiyo ni mama?? Hivi kisaikolojia hawa watoto watakuwaje Si watakuwa huku wanatuchukia sisi wote wawili kwa aibu na mikosi hii tunayowatengenezea Kwanini tunataka kuwataabisha watoto kwa dhambi ambayo hawajaitenda
Yes nafahamu nimekukosea mengi and am very sory for that, lakini basi embu kumbuka mkewangu nimekuvumilia mambo mangapi mkewangu, kumbuka makosa mazito uliyonifanyia lakini nikakusamehe ni sijamsimulia hata ndugu yako ama ndugu yangu ili kulinda heshima yako!! Kumbuka jinsi tulivyopogana na changamoto mbalimbali mpaka leo hii umefikia kuwa moja ya icons wa muziki wa injili hapa nchini?? Kumbuka shida, manyanyaso, dhuluma, kuchekwa na kudharauliwa ambako tumepitia mpaka leo hii tuko hapa!!!
Mkewangu, kwa miaka yote hii nimekubali nionekane bushoke tu huku watu hawajui kuwa mimi ndiye ninayechora ramani ya kila ishu yako!! Mimi ndiye nimekuwa nafatilia na kufanikisha kila kitu chako from scratch!!!
Lakini nimekubali jamii inione bushoke kwani nilikuwa najua nini mimi na wewe tunatengeneza kwa maisha yetu ya sasa na baadae!!! Nini kilichokubadilisha mkewangu Fedha Au huyo mchungaji mwanamazingaombwe
Hivi kweli kabisa umefikia hatua ya kulipa waandishi wa habari ili wanikandamize nionekane sifai katika jamii Ni nini kilichokuoata mkewangu??
Naomba uelewe kuwa binafsi siogopi kwenda jela kwasababu ya hiyo muvi mliyonizushia, kwani ni bora nikakae jela kuliko kuishi huru huku mkininyanyasa kiasi cha kuondoa utu wangu kama bidamu, lakini kinachoniuma ni familia yetu!! Kwanini watoto wateseke kwa sababu ya tamaa zetu binafsi!! Nikifikiria hilo naumia sana!
Najua kwa sasa inaonekana kama vile ni impossible kwa mimi na wewe kurudiana tena, lakini binafsi naamini tunaweza!! Najua haitakuwa rahisi kwani tumeharibu mno, lakini ni heri ya kujaribu kuliko kuendelea kufanya huu upuuzi tunoufanya sasa!!
Kumbuka hiki tunachokifanya sasa hatujajipaka matope sisi tu pekee, bali mziki wote wa injili Tanzania, na tusipotubu tukajirudi Mungu atatuhukumu kwa dhambi hii!!
Kumbuka kuwa hakuna kati yenu atakayeshinda katika hii vita, vyombo vya habari pekee ndivyo vitakavyo nufaika lakini mimi, wewe na mchungaji wote tuta loose!!
Mwisho nimalizie na wewe mchungaji, tulipokutana mara ya kwanza nilikuchukulia kama kaka na kama mlezi wetu wa kiroho!! Lakini umegeuka shetani mwenye pembe saba, umeparaganyishafamilia yangu, umeleta maumivu makali kwenye ukoo!!
Nakuonya tena kwa mara nyingine, muache mkewangu!! Huyo ni mkewangu, nilimtolea mahali mimi mwenyewe na wazazi wake waliniamini na kunikabidhi!!! Nasema niachie mkewangu!!
Wewe ni nyoka, imefika time watanzania wakujue ukweli wako wewe mbwa mwitu mkali uliyevaa ngozi ya kondoo!!!
Umedanganya watu vya kutosha na umefarakanisha ndoa nyingi sana kwa sababu ya kiburi cha pesa zako chafu za sembe!! Umeudhalilisha ulokole kiasi cha kutosha imefika time tuwaeleze watanzania ukweli na wakufahamu kuwa wewe ni nyoka!!
Sitakubali kuona ukiendelea kuitesa familia yangu, nitapambana na nitakushinda!!!Siogopi fedha zako wala connection ulizonazo, ni bora nife nikiwa nimesimama kuliko kuishi nimepiga magoti!
Nitapambana na wewe mpaka mwisho ili historia isomeke vizuri ili hata wanangu wakiwa wakubwa wajue kuwa baba yao sikuwa lofa kiasi cha kupiga magoti na kuelekeza shingo kibla kuruhusu mdhalimu kama wewe uichinje familia yangu, bali licha ya umasikini wangu nilisimama kiume na kupigana kutetea familia yangu!!!
Narudia tena mchungaji, nitapambana na nitakushinda.."
Kwako - Mchungaji Gwajima

IDADI YA WALIOFARIKI KATIKA KANISA LA TB JOSHUA LILILOPOROMOKA

Idadi ya watu waliopoteza maisha kufuatia kuanguka kwa jengo lililopo kwenye kanisa la TB Joshua jijini Lagos, Nigeria, imefikia watu 115, kwa mujibu wa serikali ya Afrika Kusini.
Waziri Jeff Radebe wa Afrika Kusini Jumatatu hii ameitaka serikali ya Nigeria inayokosolewa vikali kufanya uchunguzi juu ya tukio hilo. Tukio hilo lililotokea Sept 12 kwenye eneo la kanisa la mhubiri maarufu, T.B. Joshua, limesababisha vifo vya raia 84 wa Afrika Kusini kutoka kwenye vikundi vya makanisa yaliyomtembelea.
Ajali hiyo imesababisha uhasama wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili kubwa kiuchumi barani Afrika.
Waafrika Kusini wamechukizwa na kile wanachokiona kama serikali ya Nigeria inajivuta kufanya uchunguzi juu ya kuanguka kwa jengo hilo na kushindwa kuchukua hatua za haraka kuwaokoa waliokuwa wamenaswa kwenye vifusi.
Joshua na wafuasi wake wanadai kuwa ajali hiyo ni shambulio linalohusishwa na ndege ya ajabu iliyokuwa ikipaa juu ya jengo hilo kabla haijaanguka.

AUAWA BAADA YA KUMUUA MKEWE

.
Watu wawili wameuawa Wilayani Mpwapwa Mkoani Dodoma katika matukio mawili tofauti.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna msaidizi mwandamizi wa Polisi DAVID MISIME – SACP amesema tukio la kwanza limetokea mnamo tarehe 20/09/2014 majira ya saa 23:30hrs katika Kijiji cha Mzogole Wilayani Mpwapwa Mkoani Dodoma ambapo mtu mmoja aliyetambulika kwa jina la MWAJUMA D/O CHOMOLA mwenye umri wa miaka 48, Mgogo mkazi wa Mzogole aliuawa kwa kupigwa na Rungu tumboni upande wa kushoto na mumewake aliyefahamika kwa jina la RICHARD S/O KODI mwenye umri wa miaka 55, Mhehe mkulima na mkazi wa kijiji cha Mzogole Wilayani Mpwapwa Mkoani Dodoma ambaye nae aliuawa tarehe 21/09/2014 majira ya saa 09:00hrs baada ya kushambuliwa na wananchi waliojichukulia sheria mkononi na alifariki dunia akiwa anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Wilaya ya Mpwapwa baada ya wananchi hao kupata taarifa kuwa mwanamke huyo kafariki kutokana na kipigo cha mume wake.
Kamanda MISIME amesema uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa chanzo cha mauaji hayo ni wivu wa mapenzi kwani RICHARD aliuawa na wananchi baada ya kumuua MWAJUMA ambaye alikuwa mkewake aliyekuwa akiishi nae, baada ya kuchelewa kurudi kutoka kwenye sherehe iliyokuwa hapo kijijini akidhani kuwa ameenda kwenye masuala mengine.
Aidha Kamanda MISIME amesema wananchi waliojichukulia sheria mkononi bado wanatafutwa ili wafikishwe mahakamani.

Jumapili, 21 Septemba 2014

WASIRA NAE ATANGAZA KUGOMBEA URAIS 2015

WAZIRI wa Ofisi ya Rais, Mahusiano na Uratibu, Stephen Wasira, amesema bado ana nia ya kuwania urais katika uchaguzi mkuu utakaofanyika mwakani.
Kauli hiyo, aliitoa wakati akifanya mahojiano kwenye kipindi cha Medani za Siasa na Uchumi kinachorushwa na Star Tv.
Itakumbukwa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kiliwaadhibu makada wake sita akiwemo Wassira, mwaka mmoja kutojihusisha na masuala ya kampeni za urais.
Katika kipindi cha jana, Wasira alisema licha ya kupewa adhabu na chama chake kwa kuanza kampeni mapema, bado hajafuta dhamira ya kuwania nafasi hiyo.
Alisema adhabu hiyo ya chama haimzuii kuwania nafasi hiyo, bali imelenga kuzuia makada wa chama hicho kufanya mambo kinyume na taratibu za chama.
“Nia ya kuwania urais bado ninayo, nitaendelea nayo kulingana na taratibu za chama, mimi ni mtu safi na nimeanza siasa tangu nikiwa na umri wa miaka 15,” alisema.
Wasira, aliulizwa swali na mtangazaji wa kipindi hicho atawezaje kugombea urais wakati Katiba inazuia mtu aliyeshatakiwa kwa jinai na yeye alishawahi kushtakiwa.
Waziri huyo alikiri kushtakiwa na Jaji Joseph Warioba katika kesi ya uchaguzi, lakini kesi hiyo ni ya madai na si jinai.
“Kesi zote uchaguzi ni za madai, mtu aliyeshtakiwa kwa madai hazimkoseshi mtu kuwania urais, kesi ya jinaI ndiyo yenye kutoa zuio hilo…..mimi nipo ‘clean’ kwa kuwa nilishtakiwa kwa madai,” alisema.
Alisema rushwa katika sekta mbalimbali ni hatari kwa maenedeleo ya taifa na mtu mmoja mmoja hivyo kila mtu anapaswa akichukie na kuipiga vita.

MR,BLUE ATAJA ANAEPENDA KUFANYA NAE MZIKI KATI YA DIAMOND NA ALLY KIBA

Kihistoria, Diamond na Alikiba ni wadogo zake Mr Blue. Wakati Mr Blue anatamba na ngoma zake ikiwemo Mapozi, hakuna aliyekuwa akiwafahau wawili hao.
Na kuna wakati Blue aliwahi kusimulia namna alivyokerwa na tabia ya Diamond ya kutembea na ex wake akiwe Wema na Najma. Hata Hivyo rapper huyo wa Pesa, amesema anawakubali wote Alikiba na Diamond na wote ni washkaji.
“Unajua mie wale wote washkaji zangu nawala sina tatizo nao kwahiyo nipo tayari kufanya kazi na yeyote yule ambaye atakuwa tayari si unajua hii kazi na kazi mkishirikiana pamoja ndo inakuwa nzuri zaidi,” Blue ameiambia Bongo5.
Akizungumzia kuhusu video, rapper huyo amesema anatarajia kutoa video mbili kwa pamoja.”Nimeshaulizwa sana kuhusu natoa video lini. Jibu sasa lipo tayari kwa mashabiki wangu. Nitaachia video mbili hivi karibuni na hizo video nimefanya zote na Adam Juma. Video ya Pesa ipo tayari na namalizia kushoot video ya Mapenzi pia kwahiyo muda wowote nitaziachia.”
Kwa upande mwingine Kabasyer amesema kama akitaka kurudi shule basi atasomea tu muziki na utayarishaji.

UFAHAMU UGONJWA WA KUOTA MATITI KWA WANAUME

Kwa kawaida mwanaume ameumbwa kuwa na matiti madogo, ugonjwa wa wanaume kuwa na matiti makubwa kama wanawake huleta usumbufu hasa wa kisaikologia kwa mwanume husika.
Kuna hatua au makundi matatu katika ukuaji wa kawaida kwa mwanaume ambapo huweza kuwa na matiti makubwa na baadaye huisha na kurudi kuwa ya kawaida.
Kundi la kwanza ni mtoto mchanga wa kiume, ambapo karibu asilimia 60 hadi 70 huwa na matiti makubwa hii ni kwa sababu ya homoni ya ‘estrogen’ ya mama kwa mtoto, ambapo baada ya wiki mbili au tatu homoni hii huisha katika damu ya mtoto, hivyo matiti kunywea.
Kundi la pili ni katika kipindi cha kubalehe kwa mtoto wa kiume, asilimia 30 hadi 60 huota au hukua matiti kuliko kawaida, lakini hurudi katika hali ya kawaida kati ya umri wa miaka 16 hadi 18.
Kundi la tatu ni asilimia 50 ya wanaume wenye umri wa miaka 50 na kuendela huanza kuota matiti na kuwa makubwa.
Matitizo yanayosabisha kukua kwa matiti kwa mwanaume ni pamoja na shida katika vinasaba (genetic) vinavyohusiana na matiti, saratani mfano ya korodani, saratani ya mapafu au ya Ini au ya tezi dume.
Magonjwa mengine yanayosababisha kukua kwa matiti kwa mwanaume ni pamoja na kufeli kwa figo, magonjwa ya Ini, matatizo ya tezi ya madini joto (thyroid) na kutokuwa na nguvu za kiume.
Dawa nazo huchangia kukua kwa matiti kwa mwanaume, mfano; dawa za kulevya, dawa zenye homoni za kike iwe za kunywa au za kupaka, pia dawa ya saratani na kadhalika.
Dawa nyingi zimechangia wanaume kuwa na matiti makubwa bila kutambua kwamba amekuwa akishika au kutumia kemikali hizo. Ukimwi pia una husiano na kukua kwa maititi kwa mwanaume.
Hivyo, kukua kwa matiti kwa mwanaume ni kiashiria kwamba kuna shida au ugonjwa katika moja ya viungo vya mwili wake, au matiti yake moja kwa moja.
Ni vyema kwenda hospitali kufanyiwa uchunguzi wa kina, kujua ni ugonjwa gani unanyemelea.
Vipimo vya damu hufanyika kuangalia shida ya viungo mbalimbali, pia ‘ultrasaundi’ ya matiti au mamografu hufanyika, pia kipimo cha kufyonza sehemu ya titi na kupima maabara huweza kuhitajika, hasa iwapo ni titi moja limevimba au ukuaji wa matiti ni wa kasi.
Matibabu ya kukua kwa matiti ni pamoja na kutibu ugonjwa au shida ya awali, mfano kuacha dawa husika, kutibu saratani na kadhalika.
Iwapo uchunguzi wa kina umefanyika na kuonyesha matiti yamekuwa yenyewe bila kuwepo kwa ugonjwa wowote, basi matibabu mazuri na halisi kundoa ukubwa wa matiti ni kufanyiwa upasuaji wa matiti.

DIAMOND ASABABISHA VURUGU UINGEREZA

Mwanamuziki Diamond Platnumz kwa mara nyingine tena usiku wa kuamkia jana alisababisha vurugu kubwa nchini Uingereza baada ya kushindwa kutumbuiza katika ukumbi wa LaFace Club uliopo jijini London.
Hii ni mara ya pili kwa Diamond kusababisha vurugu nchi za ughaibuni baada ya Septemba 1, kusababisha vurugu katika mji wa Stuttgart nchini Ujerumani aliposhindwa kufika kwa wakati ukumbini.
Akizungumza na mwandishi, shuhuda wa tukio ambaye ni Mtanzania anayefanya shughuli zake nchini Uingereza, Flora Lyimo alionyesha wazi kukerwa na tukio hilo ambalo alieleza kuwa huenda likaharibu sifa ya nyota huyo ughaibuni.
Lyimo ambaye alihudhuria shoo hiyo alisema Diamond alisubiriwa na zaidi ya watu 200 tangu saa sita usiku bila nyota huyo kutokea na ilipofika saa 10:00 alfajiri, ndipo walipoanzisha vurugu kudai kurudishiwa pesa zao.
Shoo hiyo ambayo ilitozwa kiingilio cha pauni 20 sawa na fedha za Tanzania Sh54,280 iliishia kwa dosari ya aina yake baada ya polisi kulazimika kuingilia kati kusimamia urudishwaji wa fedha hizo.
Alisema waliamuru watu warudishiwe fedha zao, hivyo walipanga mstari na kurudishiwa fedha zao, kila mmoja akiamuriwa kuondoka eneo hilo huku wenye klabu hiyo wakinyang’anywa leseni.
“Ni jambo la ajabu na aibu kwa msanii ambaye Watanzania tunamtegemea atuwakilishe nje ya nchi anakubali vipi kutangazwa kwenye shoo kama hajalipwa pesa zake, watu wanamchukulia kama tapeli kwani yeye mwenyewe amewatangazia mashabiki wake halafu hajatokea.
“Wengi tunapata shaka kama hajashirikiana na huyo promota kwani hata huo ukumbi ambao shoo ilitakiwa kufanyika hauna jukwaa maalumu ambalo msanii anaweza kutumbuiza binafsi nilishangaa haikuwa eneo sahihi, lakini nikasema ngoja niende kumuunga mkono Mtanzania mwenzangu,”alisema Lyimo.
Hata hivyo, pesa zilizopatikana hazikutosha kuwarudishia watu wote ikizingatiwa kuwa wengi walikata tiketi kabla ya siku ya shoo, hapo ndipo vurugu zilipotokea na polisi kulazimika kumshikilia promota wa shoo hiyo ambaye alifahamika kwa jina la Victor.
“Polisi wengi sana waliofika hapa ukumbini kwa ajili ya kulinda usalama, walichokifanya ni kumchukua promota aliyeandaa shoo hii na kumweka chini ya ulinzi kwa kosa la utapeli, kwa sharti kwamba mpaka watakapompata Diamond, lakini mpaka sasa bado haijajulikana alipo,”alisema Lyimo.
Lyimo alionyesha wasiwasi wake na kueleza kuwa kutokana na mfululizo wa matukio hayo huenda Diamond akazuiliwa kufanya shoo katika nchi za Ulaya, kutokana na kuanza kupoteza imani kwa mashabiki wake.
Mwandishi alimtafuta balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Peter Kallaghe ambaye alieleza kwamba hafahamu chochote kuhusu tukio hilo na kuahidi kulifuatilia kujua undani wake.
“Kama unasema tukio hilo limetokea usiku mimi sijapata taarifa zozote mpaka sasa, lakini ngoja nijaribu kuwasiliana na mtu ambaye anaweza kufahamu chochote,”alisema Balozi Kallaghe.
Kwa msaada wa Balozi Kallaghe Mwandishi alifanikiwa kuzungumza na Ofisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza, Rahma Pompy ambaye pia alikuwa kwenye tukio hilo na kufafanua kuwa kasoro hiyo imetokana na uzembe wa promota.
Alisema mwandaaji wa shoo hiyo alitakiwa kumalizana na Diamond kabla ya kuwajaza watu ukumbini, lakini hakufanya hivyo hali iliyosababisha nyota huyo kushindwa kufanya kilichompeleka na kufafanua kuwa hii siyo mara ya kwanza kwa promota huyo mwenye asili ya Tanzania kufanya uzembe wa aina hiyo.
“Kwa mimi niliyekuwepo eneo la tukio nafahamu fika kuwa Diamond hakuwa na kosa lolote, hakulipwa na wala promota hakumfuata hotelini. Unafikiri angeweza vipi kufanya kazi ya namna hiyo,”alisema.
Ingawa mashabiki wengi hawakumwona, lakini Pompy alibainisha kuwa Diamond alifika eneo hilo saa tisa usiku, hata hivyo alishindwa kuingia ndani ya ukumbi huo kutokana na kutomalizana na promota.
“Watu wengi hawakumwona ila mimi nilimwona Diamond, alifika na alionyesha wazi namna alivyokuwa akihangaika kutafuta ufumbuzi wa tatizo hilo ili kuwaridhisha mashabiki wake, lakini alishindwa kwa sababu hakuwa amelipwa na muda ulikuwa umekwisha,”alisema.
Ilikuwaje Diamond akawasili saa tisa usiku?
Kwa mujibu wa Pompy, baada ya Diamond kusubiri kwa muda mrefu hotelini bila kufuatwa na promota, akaamua kwenda mwenyewe kwenye ukumbi alikotakiwa kufanya shoo. Hata hivyo, alikumbana na usumbufu mkubwa njiani kutokana na barabara nyingi kufungwa nyakati za usiku kutokana na matengenezo.
“Kuna matengenezo ya barabara nyingi zinafungwa, hivyo akajikuta anazunguka kwa muda mrefu kutafuta njia mbadala. Mpaka alivyofika ukumbini, ilikuwa tayari imeshafika saa tisa, hata hivyo asingeweza kufanya chochote kwa kuwa hakumalizana na promota na ukumbi aliotakiwa kufanya shoo unafungwa saa 9:30, nadhani hata yeye alikuwa hafahamu,”alifafanua.
Kuhusu taarifa za Diamond kutafutwa na polisi kutokana na tukio hilo, Pompy alisema hana uhakika na uvumi huo kwa kuwa makosa yalionekana wazi kuwa ni ya promota.
Meneja wa Diamond afunguka
Kutokana na tukio hilo, Meneja wa mwanamuziki huyo, Hamis Taletale maarufu Babu Tale ambaye hakuambatana naye, amesema kuwa Diamond alipokea mwaliko kutoka kwa promota huyo, lakini hakulipwa fedha hata kidogo, jambo ambalo lilimfanya ashindwe kufanya uamuzi wowote.
“Diamond alipofika Uingereza yule promota alimdaka juu kwa juu kwa kuwa kule alikwenda kwa ajili ya shoo ya Ujerumani itakayofanyika usiku wa leo (jana) akimtaka afanye shoo jijini London, Uingereza, alikubali na baada ya hapo alisema kuwa angemlipa siku ya shoo, lakini kwa wakati wote hakufanikiwa kuonana naye tena, alikuwa akiwasiliana naye kwa simu tu,”anaeleza Taletale.
Alisema Diamond alimsubiri promota huyo kwa muda mrefu, licha ya kufanya matangazo aliamini kuwa kabla muda wa shoo haujafika angemlipa fedha ili aende ukumbini.
“Diamond alishangaa kuona ilipofika saa nne usiku wa kuamkia jana promota yule hapatikani, kwa kuwa hakulipwa hata dola moja (Sh1,600) aliamua kutulia hotelini kwani promota ndiye anatakiwa amfuate msanii, na yeye hakufanya hivyo wala hakumlipa hata kidogo. Msanii wangu hana makosa ndiyo sheria ya kazi ilivyo,”alisema Taletale.
Hata hivyo, Taletale alisema wamiliki wa ukumbi ndio walioamua kuita polisi baada ya kuona viashiria vya vurugu, na hapo ndipo ilipogundulika kuwa promota huyo hakulipia ukumbi pia.
“Licha ya kwamba hakumlipa msanii wangu, pia ukumbi hakuulipia. Alichokifanya mmiliki ni kurudisha fedha kwa watu waliohudhuria mbele ya polisi na promota yule akakamatwa.”
Akizungumzia usalama wa Diamond, Taletale alisema,“Msanii wangu yupo katika mikono salama na hivi tunavyoongea ameshapanda ndege kuelekea Ujerumani kwa ajili ya shoo jioni ya leo. Hana kosa lolote, hakuna mkataba baina yake na promota unaoonyesha kwamba alilipwa,hivyo hakuwa na kizuizi na polisi hawajashughulika naye,”alisema Taletale.
Hata hivyo, alipoulizwa kwa nini anamwacha msanii wake asafiri peke yake na kufanya makubaliano na mapromota kazi ambayo alitakiwa aifanye yeye (Taletale) alisema:
“Ilikuwa nisafiri naye, lakini kwa bahati mbaya kulikuwa na matatizo ya kifamilia ambayo ilinilazimu nibaki nchini. Yeye alikwenda kwa ajili ya shoo mbili zilizofanyika Jumamosi Afronation na hii ya leo itakayofanyika Sturtgart. Huyu promota alimdaka tu,”alisema Babu Tale.
Baada ya kutokea kwa vurugu hizo, mwanamuziki Diamond alisema promota huyo amemtapeli kwa kuwa hayakuwa makubaliano yao awali.
“Tafadhali ndugu zangu wa Uingereza haikuwa dhamira yangu, kuweni makini sana na promota huyu Victor Dj Rule, mnaposikia kaandaa shoo, pati au hafla yoyote ni vyema kuziepuka na kutohudhuria kabisa kwa sababu ni tapeli, si unajua aisifiaye mvua imemnyeshea, basi miye nimeloa kabisa,”aliandika kwenye ukurasa wake wa Instagram.
Akizungumzia sakata hilo, Rais wa Shirikisho la Muziki Tanzania, Ado Novemba alisema tatizo alilopata Diamond limepokewa kwa masikitiko makubwa na wanamuziki wote nchini.
“Tunasikitika kwani hii ni mara ya pili inatokea tena kwa kipindi cha mwezi mmoja, lakini baada ya kufanya mawasiliano, tumegundua tatizo lilikuwa la promota, mwanamuziki wetu hana hatia na ameshaondoka Uingereza leo (jana) asubuhi na sasa yupo Ujerumani kwa ajili ya shoo nyingine ya usiku wa leo,”alisema Ado.

Jumamosi, 20 Septemba 2014

SIERALEONE WATII AGIZO LA SERIKALI LA KUTOKUTOKA MAJUMBANI MWAO

Mitaa ya Siera Leone
Raia wa Sierra Leone wamesalia majumbani mwao kwa siku ya pili mfululizo wakati ambapo taifa hilo linatekeleza agizo la kutotoka nje la masaa 72 ili kujaribu kusitisha ueneaji wa ugonjwa wa Ebola.
Mwandishi wa BBC katika mji mkuu wa Freetown anasema kuwa barabara nyingi za miji ambazo zimekuwa zikijaa watu hazina watu kwa sasa.
Mwandishi wetu anasema kuwa kituo cha oparesheni za dharura kilipokea zaidi ya simu 900 katika siku ya kwanza ya agizo hilo,kupitia kuwaripoti wagonjwa ama kutaka miili ya wafu kuchukuliwa.
Amesema kuwa kuna vituo viwili pekee katika taifa hilo na kwamba kituo kimoja katika eneo la Kenema kimejaa wagonjwa.

Ijumaa, 19 Septemba 2014

SIKU moja baada ya Jeshi la Polisi kudhibiti maandamano yaliyoandaliwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), wafuasi watatu wa chama hicho wamefikishwa mahakamani jijini Dar es Salaam na wengine watano wanashikiliwa na polisi mkoani Morogoro.
Wafuasi hao watano wa mkoani Morogoro wanashikiliwa na polisi wakidaiwa kupinga agizo lilitolewa na viongozi wa jeshi hilo la kuwataka kutoandamana.
Wanachama waliokamatwa ni pamoja na Witnes Makoyola (29), Katibu wa Chadema tawi la Kiwanja cha ndege, Shukuru Makamba(46), Maria Lissu (28) mkazi wa Kilakala na Katibu wa Baraza la Wanawake wilaya ya Morogoro Mjini, Hussein Hassani (28) mkazi wa Mafiga na Odwin Peter (65) mkazi wa Kiwanja cha ndege.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda wa Polisi mkoani Morogoro, Leonard Paul alisema tukio hilo lilitokea jana majira ya saa 5:30 asubuhi katika maeneo ya mtaa wa Konga.
Kamanda Paul alisema Septemba 17 viongozi wa chama hicho waliandika barua ya kuomba kuandamana, huku wakidai kuwa lengo la maandamano hayo ni kupinga hatua ya wabunge wa Bunge la Katiba kuendelea na vikao huku wakijua kuwa katiba haitapatikana.
Aidha Kamanda Paul alisema kuwa barua hizo zilienda kwa wakuu wa polisi na kwamba jeshi hilo lilizuia maandamano kutokana na taarifa za kiintelijensia kuwa wapo baadhi ya wananchi walipanga kufanya uhalifu wakati wa maandamano, ikiwa ni pamoja na kuwa kesi ya suala hilo bado iko mahakamani.
Hata hivyo, kamanda huyo alisema kuwa jeshi hilo liliwaita viongozi wa chama hicho, lengo likiwa ni kuwazuia kuandamana ambapo alisema kuwa jana majira ya saa 5:30 asubuhi katika maeneo ya mtaa wa Konga kulianza kufanyika mkusanyiko wa watu wakijiandaa kuandamana baada ya kuweka ulinzi katika maeneo yote waliyopanga kuanzia maandamano ya wafuasi wa chama hicho.
Hata hivyo, kamanda huyo alisema walifanikiwa kutawanya mkusanyiko huo kwa kurusha mabomu ya machozi sambamba na kuwakamata watuhumiwa hao ambapo alisema kuwa watafikishwa mahakamani muda wowote kuanzia sasa.
Kwa upande wake katibu wa chama hicho mkoani hapa, Boniface Ngonyani alisema kuwa maandamano hayo yaliyotarajiwa kufanyika jana majira ya saa 5.00 asubuhi yalizuiwa na jeshi la polisi ambapo jeshi hilo lilidaiwa kuingia ndani ya ofisi za chama hicho na kuanza kupekua nyaraka na kuzitwaa nyingine na kuondoka nazo.
Aidha alisema baada ya hekaheka hiyo baadae wakabaini kwamba kompyuta mpakato ya Mwenyekiti wa Chadema Wilaya, James Mkude pamoja na simu yake ya mkononi havionekani.
Hata hivyo, alisema kutokana na kukamatwa kwa wanachama hao ofisi ya Chadema mkoa wa Morogoro tayari imewatuma wanasheria wake wawili ili kuweza kufika polisi na kuangalia tatizo lililofanya kukamatwa kwa wanachama hao.
Habari kutoka mkoani Dar es Salaam:
Wafuasi watatu wa Chadema wamefikishwa mahakamani kwa tuhuma za kuingia katika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi kinyume na utaratibu.
Wafuasi hao ambao walifikishwa mahakamani hapo jana ni Ngaiza Kamugisha (28) dereva, mkazi wa Vingunguti, Benito Mwapinga (30) Fundi nguo mkazi wa Mtoni kwa Azzi Ally na Eliasante Bugeji (51) Mhasibu wa Hospitali ya CCBRT mkazi wa Komakoma Kinondoni, Dar es Salaam.
Akisoma hati ya mashitaka Wakili wa Serikali Mkuu, Bernard Kongola akisaidiana na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Tumaini Kweka na George Barasa, ambapo alidai kuwa wafuasi hao wanakabiliwa na mashtaka matatu.
Mbele ya Hakimu Mkazi Frank Moshi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Kongola alidai mashtaka hayo ni kuingia kwa nguvu Makao Makuu ya Jeshi la Polisi, kukaidi amri halali na kutoa lugha ya matusi.
Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa Septemba 18 mwaka huu, washtakiwa waliingia kinyume cha sheria ndani ya Makao Makuu ya Jeshi la Polisi kwa hali ya fujo.
Aidha, ilidaiwa katika tarehe hiyo na maeneo hayo washtakiwa walikataa kutii amri ya halali ya kutawanyika kutoka eneo la makao hayo ya polisi iliyotolewa na Mkaguzi wa Jeshi la Polisi, Inspekta Zuhura, ambaye alitoa amri hiyo baada ya kuruhusiwa na viongozi wake.
Akiendelea kusoma mashitaka hayo, alidai katika kosa la tatu linalomkabili Bugeji peke yake, inadaiwa akiwa katika mazingira ya Makao Makuu ya Jeshi la Polisi alitoa lugha ya matusi kwa maofisa wa Polisi. Ilidaiwa maneno hayo yaliyotolewa na mshitakiwa huyo yalikuwa yakiashiria uvunjivu wa amani.
Upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na upande wa mashitaka umeomba tarehe nyingine ya kuwasomea washtakiwa maelezo ya awali.
Wakili wa wafuasi hao Peter Kibatala alidai mashtaka yanayowakabili washtakiwa yanadhaminika, hivyo akaomba mahakama iwapatie masharti nafuu kwa mujibu wa sheria.
Hata hivyo, Kongola aliendelea kudai kuwa mahakama inatakiwa itoe masharti yanayoendana na mazingira ambayo washtakiwa wametenda kosa hilo.
Kibatala alidai kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania dhamana ya washtakiwa ni haki yao na pia washtakiwa bado haijawatia hatiani, kwa hiyo dhamana ni haki yao.
Hakimu Moshi alisema ili washtakiwa wawe nje kwa dhamana wanatakiwa wawe na wadhamini wawili wa kuaminika wakiwemo watumishi wa Serikali au watumishi kutoka katika Taasisi inayotambulika wakiwa na barua za waajili wao na vitambulisho vya kazi na wadhamini watasaini bondi ya Sh 500,000 kwa kila mmoja.
Kesi hiyo iliahirishwa hadi Septemba 24 mwaka huu kwa washtakiwa kusomewa maelezo ya awali na akaamuru washtakiwa warudishwe rumande kwa sababu hawakuwa na wadhamini.
Mpaka mwandishi anaondoka katika eneo la Mahakama washtakiwa walikuwa hawajapata dhamana, ambapo kulikuwa na jitihada za kupiga simu Makao Makuu ya Chadema ili wapate wadhamini.
Nje ya mahakama Mratibu wa Chadema Kanda ya Pwani, Nickson Tugala alikuwa aking'ang'ania kuingia mahabusu kuwaona washtakiwa, jambo ambalo lilisababisha fujo katika eneo hilo.
Tugala alionekana kubishana na Insepkta wa Jeshi la Polisi, Mussa Mkini mpaka kufikia hatua ya kusogelea kwa karibu hali iliyowatia hofu watu waliyokuwa katika eneo hilo kuwa watu hao wanataka kupigana.
Kutokana na hali hiyo, ilimlazimu Mkini aombe nguvu kutoka Polisi na ilipofika saa 6:10 mchana ziliingia gari mbili za polisi namba PT 1846 na PT 1145 zikiwa na askari wenye silaha za moto.
Mkini alitoa amri ya Tugala kuchukuliwa na kupelekwa Kituo Kikuu cha Polisi cha Mkoa wa Dar es Salaam kutokana na fujo ambazo alikuwa anafanya, lakini bado Tugala alikuwa akiwagomea askari hao.
Baadaye alikubali kuondoka nao, ambapo askari wawili walipanda kwenye gari ambalo alikuwa akiendesha la M4C namba T 351 CAY. Askari mmoja alipanda ndani ya gari na mwingine alipanda nyuma ya gari hilo wakiongoza kwenda Central.

WACHARAZWA VIBOKO KWA KUCHEZA MUZIKI IRANI

Watu sita nchini Iran waliokamatwa baada ya kuonekana kwenye kanda ya video iliyokuwa inaiga wimbo wa 'Happy' wake mwanamuziki mashuhuri Pharrell William, wamehukumiwa kifongo cha hadi mwaka mmoja jela kila mmoja pamoja na adhabu ya kuchapwa mijeledi 91.
Wakili wa sita hao amesema kuwa hukumu hiyo itaahirishwa kwa miezi sita ikmaanisha kuwa watafungwa tu jela ikiwa watarejelea kosa hilo.
Kanda hiyo inaonyesha wanaume watatu na wanawake watatu ambao hawajafunika vichwa vyao wakicheza densi kwenye barabara na katika paa za nyumba mjiniTehran.
Kanda hiyo iliyowekwa kwenye mtandao wa kijamii wa You Tube, imetazamwa na zaidi ya watu milioni moja.
Wengi wa waliohusika kuitengeza kanda hiyo, walifungwa kwa miezi sita , huku mmoja wao akifungwa kwa mwaka mmoja, alinukuliwa akisema wakili wao Farshid Rofugaran.
Mmoja wa watu waliokamatwa kwa kucheza densi
Kanda hiyo kwa jina, "Happy we are from Tehran" ilifikishwa kwa maafisa wakuu nchini Iran mwezi Mei baada ya kutazamwa na watu 150,000 kwenye You Tube.
Waliohusika pia walikamatwa na kushitakiwa kwa kosa la kukiuka sheria za kiisilamu ambazo zinawazuia wanaume kucheza densi na wanawake na pia wanawake kutoka nje bila hijab.
Baadaye washukiwa walionekana kwenye televisheni wakijitetea kwamba wao ni waigizaji walihadaiwa kushiriki katika kanda hiyo
Kukamatwa kwa vijana hao kulizia ghadhabu kutoka anga za kimataifa huku watetezi wa haki za binadamu wakianzisha kampeinii kwenye mitandao ya kijamii kutaka waachiliwe.
Mwanamuziki Paharrel Williams mwenyewe, ambaye wimbo wake huo, uliteuliwa kwa tuzo la Oscar, pia alieleza kukerwa na kukamatwa kwa watu hao.
"inachukiza kwamba vijana waliokuwa tu wakijaribu kujifurahisha wanakamatwa,'' aliandika kwenye ukurasa wake wa Facebook.

POLISI KWA HILI LA KUWAPIGA WAANDISHI MMEBORONGA

HILI LA POLISI KUWANYANYASA WAANDISHI HATUWEZI KUNYAMAZA HATA KIDOGO

Alhamisi ya tarehe 18 palitokea kutokuelewana kati ya polisi na wananchi wachache waliokuwa wamefika makao makuu ya polisi kwa lengo la kumsindikiza mwenyekiti wa chama cha Demoklasia na Maendeleo(CHADEMA),mheshimiwa Freeman Mbowe ambae aliitwa na polisi kwaajili ya mahojiano kwa kile kilichodaiwa kuwa ni kuchochea vurugu kwa kuitisha maandamano.

Sina haja ya kuzungumzia mgogoro huo kati ya polisi na Mwenyekiti wa CHADEMA na wafuasi wake kwa kuwa mambo hayo ni ya kisheria na sijui ni nani yuko sahihi na nani hayuko sahihi.

Kilichonisikitisha katika tukio lile ni kitendo cha Askali wa Jeshi la polisi kuamua kuwashambulia waandishi wa habari kana kwamba hawakuwa na haki ya kufanya kazi yao!

Ni juzi tu serikali kupitia makamo wake wa Rais imetoka kuongea na wahariri na kusisitiza uhusiano mzuri kati ya taasisi za serikali likiwemo jeshi la polisi na vyombo vya habari.

Nina imani kubwa kuwa serikali ilifanya hivyo ikijua kuwa waandishi ni kundi kubwa sana katika nchi ambalo linaweza kuiamulia nchi kwenda kushoto au kulia.

Ni wazi wanajua kuwa waandishi ni kundi ambalo likiamua nchi isitawalike haitawaliki na wakiamua nchi itawalike inatawalika.

Waandishi wanaweza kuligeuza jambo dogo kabisa kwenye utawala likawa kubwa na kubadilisha kabisa hali ya hewa..

Hii ina maana kuwa kundi hili la waandishi lina nguvu kuliko pengine hata hao polisi lakini wanajua taaluma yao na kuheshimu taaluma nyingine na ndio mana nchi inaendelea kuwa na amani mpaka leo.

Tuna mifano ya waandishi ambao wametumia taaluma yao kuzibadilisha nchi na kuleta maafa makubwa kama KENYA na RWANDA,kwahiyo kama vile ambavyo waandishi wanaheshimu taaluma nyingine nao pia wanapaswa kupewa heshima stahiki na kulindwa ipasavyo kama taaluma ambayo ni hatari sana umakini usipokuwepo na taaluma ambayo ikitumiwa vizuri inaweza kusukuma maendeleo haraka sana nchini na kudumisha amani.

Nimeamua kuandika haya yote nikiwa na fikra kuwa pengine taasisi hii ya jeshi la polisi imesahau wajibu na haki ya muandishi!,au pengine wanaidharau taaluma ya uandishi kutokana na kutokuwa na ufahamu juu ya kile ambacho waandishi wanaweza kukifanya, au pengine wameigeuza heshima ya waandishi kwao kuwa utumwa.

Naomba niwakumbushe polisi kurudi kwenye mstari na kujua wajibu na haki za makundi mbalimbali katika jamii.Waandishi wanalindwa mpaka vitani vipi kuwanyanyasa kwenye vimatukio vya kawaida ka hiki cha Mbowe!!!Acheni bana hilo jipu mnalililemba siku moja litatumbuka!!

Alhamisi, 18 Septemba 2014

JINSI YA KUJENGA UHUSIANO NA WATU

Unaweza kuwa hujui kwamba kujenga uhusiano mzuri na wenzako au wafanyakazi wenzako kunaweza kukusaidia kufanikiwa kitaaluma na maisha yako kwa ujulma. Kwa makala hii utagundua kuwa muda mwingi unoutumia kwenye maisha yako ni kuwa pamoja na wafanyakazi wenzako hata kuliko na familia yako au kwingineko. Kuboresha mahusiano yako na watu ni vizuri kibiashara kwani inaongeza ufanisi katika eneo lako la kazi.
Kwa nyongeza ni makampuni machache ambayo watu wake wanafanya kazi bila kutegemea wengine ila makampuni mengi yanategemea watu kufanya kazi pamoja na watu hao hawawezi kufanya kazi pamoja kama hawana mahusiano mazuri.
Hivyo kuna njia tano za kuboresha mahusiano ninazozijua ingawa unaweza kuongeza za kwako kulingana na mazingira na uzoefu ulionao;
1. Unatakiwa kuwa muwazi, mkweli na mwenye kuwasiliana
“Linapokuja suala la mahusiano kazini au nyumbani na watu wanaokuzunguka unahitaji kuwa muwazi na mkweli kwa gharama yoyote hapo ndipo utakapofanikiwa, ” Nukuu kutoka kwa mwandishi mmoja aitwaye Harry.
Harry anasema hupenda kuwashauri watu kuwa wawazi na wakweli ili waweze kufanya kazi pamoja na kuwa ufanisi mkubwa. Ingawa wengine wanachukulia mazingira ya kazi ni sehemu ya kujionyesha, kufanya wanachotakiwa kufanya na kwenda nyumbani na wengine wanachukulia ni sehemu ambayo wanatumia nusu ya maisha yao na kujenga fulsa na kuboresha mahusiano kwa kiasi kikubwa.
2. Uwe ni mtu unayependeka
Wakati mwingine kuwa muwazi na mkweli peke yake hakutakupa mahusiano unayohitaji hivyo usikate tamaa. Unahitaji kuwa rafiki wa watu na mtu ambaye unajihusihsa kwenye matukio ya pamoja ya kijamii kazini. Kwa ufupi usiwe mtu wa kujitenga na watu wengine hata kama si watu wa rika yao au imani yako uwe na hekima ya kutosha kuweza kujihusisha nao kwa umakini na uelewa mkubwa bila kuathiri msimamo wako.
3. Unatakiwa kuwa mchunguzi au mwangalifu katika kujenga mahusiano
Kuna wengine wanajua jinsi ya kujenga mahusiano mazuri au bora kazini, kitu ambacho ninakushauri jaribu kuangalia na kuchunguza utamaduni wa hapo ofisini kabla ya kuchuakua hatua ya kwanza. Kama unaona italeta shida au huna uhakika wa kuwakaribisha wafanyakazi wenzako kwaajili ya chakula cha jioni unaweza kuanza na kuwakaribisha chakula cha mchana. Hautakuwa na mambo la kupoteza kwani inaanza kidogo kidogo halafu kitakuwa kitu cha kawaida.
4. Tafuta watu wenye mwelekEo sawa na wa kwako
Kwa watu wengine ni shida kuwa marafiki na wageni kabisa lakini kitu ambacho unatakiwa kujua marafiki ulionao sasa walikuwa wageni kwako kipindi fulani cha maisha yako. Ila kitu cha msingi kama kuna mambo ambayo mnafanana au mna mweleko mmoja ni rahisi kuanza mahusiano hapo kazini. Mfano watu ambao wanakunywa pombe hukutana bar au maeneo ya starehe, watu wa kanisani hukutana kanisani na wa msikitini hukutana huko na wenye kupenda michezo hukutana kwenye michezo. Hivyo unatakiwa kujua nanai anaendana na mfumo wa maisha yako.
5. Usiogope kufikiri makubwa au madogo
Siku zote ni rahisi kuanzisha mahusiano na watu ambao uko kwenye mazingira sawa kiuchumi au cheo. Haimaanishi kwamba huwezi kujenga mahusiano na watu walio chini yako au juu yako. Kinachobakia ni wewe mwenyewe kuchukua maamuzi binafsi katika kujenga mahusiano yako na watu wengine.

KINGUNGE ATAKA WAFANYAKAZI WASIFANYE BIASHARA

Mwanasiasa mkongwe nchini, Kingunge Ngombale-Mwiru, ameitaka Serikali kutunga sheria itakayowabana wafanyabiashara wanaojiingiza kwenye siasa na kugombea uongozi kujitenga na biashara zao kwa kipindi chote wanachofanya kazi za utumishi wa umma ili kuimarisha uadilifu wa viongozi.
Kingunge aliyasema hayo wakati wa mahojiano maalumna NIPASHE mjini Dodoma na kuzungumzia changamoto mbalimbali zinazolikabili taifa pamoja na namna ya kukabiliana nazo.
Alisema kuwa biashara ni muhimu sana katika maisha ya binadamu, lakini na uongozi pia ni muhimu, hivyo mtu akichanganya mambo hayo na kuyafanya kwa wakati mmoja, lazima kutatokea madhara kwa jamii anayoitumikia.
Alisema kwa kawaida lengo kubwa la kufanya biashara ni kupata faida wakati kwa upande wa uongozi kazi kubwa ni kufanya maamuzi yenye maslahi kwa jamii, hivyo mtu akijihusisha na mambo hayo mawili kwa wakati mmoja kinachotokea kwa upande wa uongozi ni kutumia madaraka kwa maslahi binafsi.
“Ukichanganya uongozi na biashara utapata mambo makubwa mawili, kwanza hutakuwa na muda wa kutosha wa kufanya kazi za wananchi huku ukijihusisha na biashara zako, badala yake utafanya nusu nusu na kutokana na mvuto wa fedha, akili yako yote itaishia kwenye biashara,” alisema Kingunge ambaye ni mfuasi mzuri wa itikadi ya Ujamaa na Kujitegemea.
Alisema kutokana na watu wengi hivi sasa kukosa uzalendo kwa nchi yao, umefika wakati ambao sasa taifa linapasa kuchukua hatua kwa kutenganisha kabisa shughuli za uongozi na biashara.
Alisema kinachopaswa kufanyika ni kutunga sheria ambayo itamlazimu mtu yeyote anayetaka kuwania nafasi za juu za uongozi wa taifa kwanza kutangaza mali zake na kisha kujitenga nazo kwa kipindi chote anachotumikia umma.
“Uwekwe utaratibu ambao mtu akishachaguliwa kuwa kiongozi wa umma, akabidhi kisheria mali au biashara zake kwa mtu au kampuni iziendeshe na yeye asijihusishe nazo kabisa mpaka atakapokuwa amemaliza muda wake wa uongozi,” alisema Kingunge.
Alisema kuwa chimbuko la mahitaji ya sheria ya aina hiyo ni kuporomoka kwa uzalendo miongoni mwa Watanzania hususan viongozi kubainika kuwa wanaweka mbele maslahi yao zaidi kuliko maslahi ya umma na taifa kwa ujumla.
Mwaka 2008 kwenye mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilichofanyika Butiama, mkoani Mara, Mwenyekiti wa Chama hicho, Rais Jakaya Kikwete, pia alizungumzia suala la kutenganisha uongozi na biashara.
Suala hilo lilizua mjadala mkali miongoni mwa wajumbe na baada ya kikao, muingoni mwa maazimio yaliyosomwa na aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Pius Msekwa, ni kutenganisha uongozi na biashara.
Ingawa tamko hilo maarufu kama Azimio la Butiama kueleza kuwa iingetungwa sheria ya kaainisha suala hilo ili liwabane wanasiasa wa vyama vyote vya siasa, hadi leo sheria hiyo haijatungwa na wanasiasa wengi ni wafanyabiashara.
AZUNGUMZIA UBINAFSI
Kingunge pia alielezea jinsi ambavyo Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, alivyojitahidi kukabiliana na tabia ya ubinafsi hata kabla ya nchi kupata Uhuru.
Kingunge alisema kuwa tabia ya ubinafsi miongoni mwa Watanzania lilianza miaka ya 1960 baada ya kuonekana kuwa kuna dalili ya Uhuru kupatikana na kwamba ilibidi Watanzania waanze kujipanga namna watakavyoendesha taifa lao baada ya kujipatia Uhuru.
Alisema kabla ya wakati huo hapakuwapo ubinafsi ndani ya Tanu kwa kuwa watu wote walikuwa na nia moja tu ya kuhakikisha wanamng’oa mkoloni.
Alisema Uhuru ulipokaribia iliwabidi waanza kujipanga na kugawana vyeo ndani ya chama na serikalini, hali ambayo ilisababisha kuanza kwa ubinafsi nchini kutokana na watu kuhitaji madaraka na vyeo vikubwa.
Alisema hali ilianza kuwa mbaya zaidi baada ya Uhuru kupatikana, kwa kuwa watu walihitaji kujilimbikilizia vyeo na mali, kitu ambacho kilimsukuma Mwalimu Nyerere kuanzisha Azimio la Arusha kwa ajili ya kukabiliana na tatizo hilo.
“Kwa kuona hali inazidi kuwa mbaya, Mwalimu Nyerere akaanzisha Azimio la Arusha na ndiyo sababu unaona ndani ya Azimio la Arusha kuna miiko ya kuzuia viongozi kujineemesha wenyewe,lakini pamoja na kuwapo kwa Azimo la Arusha, bado ubinafsi ulikuwapo, kwa kweli tulishindwa kabisa kumaliza tatizo hili,” alisema Kingunge ambaye ameshika nafasi za kichama na serikali katika awamu zote nne za uongozi.
Kingunge, alisema baada ya kuvunjika kwa Azimio la Arusha, viongozi wa umma walianza kuonyesha ubinafsi wao wazi wazi huku wakishambulia mashirika na mali nyingine za Umma, hali iliyopelekea Serikali kutunga sera ya ubinafsishaji wa mali za umma ili kunusuru mali za umma na kurejesha uzalendo.
Hata hivyo, alisema ubinafsishaji haukusaidia kurejesha uzalendo kwa Watanzania na badala yake uliudhoofisha zaidi kwa kuongeza ubinafsi na tamaa ya viongozi kujilimbikizia mali.
Alisema mbaya zaidi katikati ya ubinafsishaji huo likaingia suala la rushwa ambalo pia liliongeza ukubwa wa tatizo na kusababisha wanyonge kushindwa kufaidi matunda ya taifa lao.
“Rushwa na ubinafsi ulianzia kwenye sekta ya uchumi, ukaingia kwenye huduma za kijamii na sasa unaelekea kwenye siasa, lakini tutambue kuwa siasa ni muhimu sana katika kuendesha huduma za kijamii, ubinafsi ukiingia huko siasa itakuwa kama biashara na hapo hali itazidi kuwa mbaya zaidi,” alionya Kingunge na kuongeza:
“Kutokana na kutoweka kwa uzalendo na uadilifu miongoni mwa viongozi, kwa sasa watu hawaendeshi mambo kwa unyoofu wala usawa, badala yake wanaongozwa zaidi na msingi wa mimi nitapata nini katika hili, suala la kujitolea sasa hivi halina nguvu.”
Alisema kutokana na hali hiyo, ndiyo sababu kuna umuhimu wa Serikali kutunga sera na sheria zinazombana kiongozi ajitenge na mali pamoja na biashara zake kwa kupindi chote anachotumikia wananchi kwa lengo la kudhihirisha suala la uadilifu.
Katika toleo la kesho, Kingunge ataendelea kuzungumzia mambo mbalimbali ikiwamo suala la elimu na changamoto zake.

Jumatano, 17 Septemba 2014

KOCHA WA SMBA AMUHOFIA JAJA

KOCHA wa Simba, Patrick Phiri, ameangalia uchezaji wa straika Mbrazili wa Yanga, Genilson Santos ‘Jaja’ kwenye mechi dhidi ya Azam kisha akasema:“Huyu jamaa ni mfungaji, tuache unazi.”
Lakini Jaja mwenyewe akasisitiza kwamba mabao mawili aliyoichapa Azam yamempa mzuka wa hatari na kuanzia sasa atachapa kila timu na anaitamani sana mechi nyingine ngumu dhidi ya Simba itakayochezwa Oktoba 12 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam akisema ana uhakika wa kucheka na nyavu.
Jaja ambaye awali alikuwa akibezwa na mashabiki wakiwamo wa Yanga, alifunga mabao mawili juzi Jumapili wakati Yanga ilipoishinda Azam 3-0 katika mechi ya Ngao ya Hisani kwenye Uwanja wa Taifa. Bao jingine la Yanga lilifungwa na Simon Msuva.
Mchezaji huyo amefunguka na kuwaambia mashabiki watulie bado mambo matamu zaidi yanakuja na lengo lake ni moja tu kucheka na nyavu kila mechi kutetea heshima ya Yanga, lakini akawasisitiza kwamba wasitegemee mbwembwe nyingi kutoka kwake.
Alisema kwamba kazi yake ni kujiweka kwenye nafasi na kuhakikisha timu inashinda mambo mengine baadaye.
“Niliwaza siku nzima nikipanga nini nifanye uwanjani, nilijua kuwa naweza kupata nafasi lakini nilitaka kila nafasi mbili nitakazopata nizitumie, nafurahi kuona hilo limefanikiwa,” alisema.
“Sasa kwangu hali ya kujiamini imeimarika zaidi ilikuwa ngumu kuweza kuzoea mazingira haya ya hapa nchini kwa haraka, nikiendelea kuwa sawa kiafya nitafunga zaidi ya nilivyoifunga Azam, kila mechi ni magoli tu.
“Nataka mashabiki wafahamu kuwa soka ni mchezo wa kutumia akili, hivyo timu ama mchezaji inaweza kufanya makosa kila mara, cha msingi ni kuvumiliana na kupeana nafasi kwa kusapoti ili mambo yaende vizuri.
“Mimi binafsi nafanya makosa wakati mwingine, naweza hata kupoteza mpira na kuchukiwa, lakini lengo langu ni kupambana ili nifunge.”
Kocha Marcio Maximo alisisitiza: “Jaja amenipa furaha, amewafurahisha Wanayanga na pia ninawashukuru wachezaji wangu wote na benchi la ufundi kwa kazi waliyofanya. Nawaomba mashabiki waelewe kuwa Jaja si mchezaji wa mambo mengi, kazi yake ni kufunga na anacheza kwa nafasi, anakuwepo eneo la kufunga ambako ndiko anakotakiwa kucheza.”
Phiri afunguka Taifa
Phiri ambaye alilazimika kusafiri kwa ndege kuwahi mchezo huo akitokea Mtwara, alisema amemuangalia Jaja akicheza kwa dakika 80 na amegundua kwamba mshambulaiji huyo ni mchezaji hatari na jasiri ambaye hatakiwi kufanyiwa masihara.

Jumatatu, 15 Septemba 2014

TANGAZO LA KAZI CHUO CHA UFUNDI

CHUO CHA UFUNDI STADI CHA MASIGITUNDA KILICHOPO PERAMIHOKATIKA KIJIJI CHA MSHIKAMANO KINATANGAZA NAFASI ZIFUATAZO ZA
A. MKUU WA CHUO NAFASI MOJA (1):
AWE NA SIFA ZIFUATAZO;
1. AMEMALIZA KIDATO CHA NNE
2. AWE NA DEGREE YA UALIMU NA UONGOZI
3. AWE NA UFAHAMU WA UTUMIAJI COMPUTER
4. AWE NA UZOEFU WA UTAWALA
5. AWE NA UZOEFU WA KAZI MIAKA MIWILI (2)
B. MWALIMU WA UASHI NAFASI MOJA (1):
AWE NA SIFA ZIFUATAZO;
1. AMEMALIZA KIDATO CHA NNE
2. AWE NA CHETI CHA UFUNDI UASHI GRADE I AU CBET LEVEL III
3. AWE NA CHETI CHA UALIMU (MVTTC)
4. AWE NA UJUZI WA COMPUTER
5. AWE NA UZOEFU WA KAZI MIAKA MIWILI (2)
C. MWALIMU WA USHONAJI NAFASI MOJA (1):
AWE NA SIFA ZIFUATAZO;
1. AWE AMEMALIZA KIDATO CHA NNE
2. AWE NA CHETI CHA UFUNDI USHONAJI GRADE I AU CBET LEVEL III
3. AWE NA CHETI CHA UALIMU (MVTTC)
4. AWE NA UJUZI WA COMPUTER
5. AWE NA UZOEFU WA KAZI MIAKA MIWILI (2)
D. MWALIMU UFUNDI WA MAGARI NAFASI MOJA (1):
AWE NA SIFA ZIFUATAZO;
AWE AMEMALIZA KIDATO CHA NNE
2. AWE NA CHETI CHA UFUNDI MAGARI (MV MECHANICS) GRADE I AU CBET LEVEL III
3. AWE NA CHETI CHA UALIMU (MVTTC)
4. AWE NA UJUZI WA COMPUTER
5. AWE NA UZOEFU WA KAZI MIAKA MIWILI (2)
E. MWALIMU WA KAWAIDA (ALIYE NA DIPLOMA):
AWE NA SIFA ZIFUATAZO;
1. AWE AMEMALIZA KIDATO CHA NNE
2. AWE NA CHETI CHA DIPLOMA YA UALIMU
3. AWE NA UFAHAMU WA COMPUTER
4. AWE NA UZOEFU WA KAZI MIAKA MIWILI (2) KATIKA KUFUNDISHA TECHNICAL DRAWING NA ENGINEERING SCIENCE
F. MWALIMU WA UDEREVA NAFASI MOJA (1):
AWE NA SIFA ZIFUATAZO;
1. AMEMALIZA KIDATO CHA NNE
2. AWE NA LESENI DARAJA C
3. AWE AMEPITIA NIT (CHUO CHA USAFIRISHAJI)
4. AWE NA UZOEFU WA KAZI MIAKA MIWILI (2)
G. MLINZI
AWE NA SIFA ZIFUATAZO
1. AMEMALIZA DARASA LA SABA NA KUENDELEA
2. AWE AMEPITIA MGAMBO
3. AWE NA UZOEFU WA KAZI MIAKA MIWILI (2)
KAMA UNA SIFA TAJWA HAPO JUU TUMA BARUA YA MAOMBI YA KAZI IKIWA IMEAMBATANISHW
NA VIVULI VYA VYETI NA CV KABLA YA TAREHE 26/10/2014 SAA 11 JIONI KWA:
MENEJA RASILIMALI WATU
MASIGITUNDA VTC
P.O.BOX 164
PERAMIHO

Ijumaa, 12 Septemba 2014

MZEE WARIOBA AMSHUKIA SITTA TENA

Dar es Salaam. Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba, amesema anashangazwa na Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba, Samuel Sitta kung’ang’ania kuendelea na Bunge hilo licha ya Rais Jakaya Kikwete kuridhia lifikie kikomo Oktoba 4 mwaka huu.
Hivi karibuni, Rais Kikwete alikutana na viongozi wa vyama vya siasa vilivyo chini ya Kituo cha Demokrasia (TCD) na kukubaliana kusitisha mchakato wa Katiba hadi baada ya Uchaguzi Mkuu wa 2015.
Akizungumza katika mahojiano maalumu wiki hii jijini Dar es Salaam, Jaji Warioba alisema ameshangazwa na uongozi wa Bunge Maalumu la Katiba kuendelea na vikao wakati uwezekano wa kukamilisha mchakato haupo.
“Hivi kuna haraka gani ya kuwa na rasimu katika Bunge hili? Mimi nilivyoelewa makubaliano ya Rais na TCD ni kama walikuwa wanasema kwa ustaarabu hebu twende polepole. Nimeambiwa kuwa Rais alitoa muda mpaka Oktoba 4, lakini uongozi wa Bunge ukapanga mpaka mwisho wa Oktoba,” alisema Jaji Warioba na kuongeza:
“Mimi nafikiri makubaliano kati ya Rais na viongozi wa vyama ni kukataa kuongeza muda. Hiyo kwangu ni lugha ya kistaarabu kwa Bunge kwamba hamwezi kumaliza kazi hii kwa kipindi hiki,” alisema Jaji Warioba.
Alimtaka Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba, Sitta kukubali kukosolewa kama yeye anavyokubali kukosolewa kuhusu Rasimu ya Katiba iliyoandaliwa na Tume yake, badala ya kujihami.
“Nilipoanza wakati ule mengi yalisemwa, lakini nilijua, ukipewa kazi maalumu lazima upate maoni ya watu ya kila aina. Kuna wale ambao watakusifu na wengine watakusema vibaya. Nilisemwa mengi sana. Lakini kwa kuwa nimefanya kazi ya Taifa siwezi kuhangaika na mtu mmoja mmoja,” alisema na kuongeza:
“Sitta asikilize wale wanaosema kuwa ana kasoro, asije akafikiri kuwa hana kasoro.”
Aliongeza: “Nashangaa sana mambo yanavyoendelea kwenye Bunge, hata siku hizi siangalii tena. Ni wakati fulani mtu anaweza kunipigia simu, hebu angalia wanavyosema....”
Alisema hatua ya uongozi wa Bunge kung’ang’ania kuendelea na mchakato ni kupingana na Rais Kikwete.
“Lakini mimi inanishangaza ilikuwaje Rais anatoa nyongeza ya hadi Oktoba 4, uongozi wa Bunge unaongeza hadi mwisho wa mwezi? Rais anasema hivi na Bunge linasema hivi. Mimi naomba uongozi wa Bunge utafakari tena,” alisema na kuongeza:
“Kinachofanywa na uongozi wa Bunge la Katiba hakina shinikizo la CCM , bali ni uamuzi ambao unatokana na matakwa yao.
1 | 2 | 3 | 4 | 5 | 6 | 7 | 8

Alhamisi, 11 Septemba 2014

CHEYO AELEZA WALIYOKUBALIANA NA RAIS KATIKA KIKAO NA TCD NA UKAWA

Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, ambaye ni Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Tanzania(TCD)Mhe. John Cheyo amesema kwamba mchakato mzima wa Katiba utamalizwa kwa kura ya maoni ya wananchi, hivyo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt. Jakaya Kikwete haiwezi kutamka leo kulihairisha Bunge Maalum la Katiba kwa kuwa liko Kisheria.
Aidha Mhe. Cheyo alisema kilichoahirishwa ni mchakato wa kura ya maoni ya wananchi na si Bunge hilo kwa kuwa walikubaliana katika kikao cha mashauriano, baina Rais Kikwete na Viongozi Wakuu wa Vyama vya Siasa vyenye wabunge vinavyounda TCD kuwa bunge hilo liendelee.
Kauli hiyo imetolewa leo Bunge Mjini Dodoma na Mhe. Cheyo wakati wa mjadala wa kujadili sura zilizobakia za Rasimu ya Katiba Mpya, ambapo alisema hayo ndiyo makubaliano yaliyofikiwa.
Aidha Mhe. Cheyo alisisitiza Katiba Mpya inayopendekezwa itakayopatikana itadumu kwa njia ya maridhiano.
“ Bunge hili linaendeshwa kwa mujibu wa sheria , Tangazo la Serikali (Government Notice) Na 254 hili ndilo uhai wa Bunge hili hadi Oktoba 4, mwaka 2014, na wote tukakubaliana haiwezekani Mhe. Rais akasema leo Bunge likasitishwa.
“ Vitu viwili vikukutana kwa nia ya maridhiano, vitu vingine vinaweza kuwekwa pembeni sawa na sasa na baadae vinaweza vinashughulikiwa kwa wakati huo,” alisema Mhe. Cheyo.
Mhe. Cheyo alisema anamwomba Rais Kikwete atoe ruhusa ya kuwepo kwa kipindi maalum cha kitakachorushwa na televisheni (video) ili kila mtu aonekana alichokisema, huku akionesha kusikitishwa na upotoshwaji wa makubaliano hayo, uliofanywa na baadhi ya wanasiasa.
“ Mojawapo ambayo tuliyokubaliana Bunge hili lipate Katiba ambayo inapendekezwa na wananchi pia kwa hali tulinayo haiwezekani mchakato mzima ukamalizika, mchakato utamalizika kwa kura ya maoni ya wananchi. Kama tukifika huko itabidi tuhairishe uchaguzi wa mwaka 2015. Niliyoyasema ndiyo makubaliano tuliyokubaliana,” alisisitiza.
Mhe. Cheyo alisema Rais Kikwete alikubali kukaa chini pamoja na TCD na hao wanaojiita Ukawa.
Alisema Rais Kikwete alifanya mazungumzo na viongozi wa Vyama vya Siasa vyenye wabunge vinavyounda TCD mara kwa mara ya kwanza, Agosti 31, mwaka 2014 kwa saa nne na mara ya pili, Septemba 8, mwaka 2014 kwa saa mbili.
Kikao hicho cha mashauriano kilihusisha kamati ya makatibu wakuu, kamati ya wenyeviti wa vyama vya CCM, CHADEMA,CUF na NCCR- Mageuzi.

USIMAMIZI WA MAADILI CBE WAONGEZA UFAULU

Hatua iliyochukuliwa na uongozi wa Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es salaam (CBE) kuendelea kuweka msisitizo katika usimamizi wa maadili kwa wanafunzi imeanza kuzaa matunda kufuatia kuogezeka kwa ufaulu wa masomo kwa wanafunzi wanaosoma chuoni hapo.
Hayo yamebainishwa leo jijini Dar es salaam na mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es salaam (CBE) Prof. Emanuel Mjema wakati akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu maadhimisho yanayoendelea ya chuo hicho kutimiza miaka 50 tangu kuanzishwa kwake Januari, 1965.
Amesema suala la usimamizi wa maadili kwa wanafunzi na jamii nzima inayoingia chuoni hapo limepewa kipaumbele kikubwa na uongozi wake tofauti na miaka iliyopita hali ilinayokifanya chuo hicho kuwa mfano wa kuigwa vyuo pamoja na taasisi nyingine za elimu ya juu hapa nchini.
“Chuo chetu sasa ni mfano wa kuigwa na vyuo vingine hapa nchini kwa sababu tumeweza kusimamia suala la maadili hasa uzingatiaji wa mavazi yenye staha kwa wanafunzi hali iliyoongeza heshima kwa chuo chetu”.
Mbali na suala la usimamizi wa mavazi kwa wanafunzi Prof amesema chuo hicho kimeendelea kuhakikisha ulinzi na usalama kwa wanafunzi na jamii nzima inayoingia na kutoka katika mazingira ya chuo hicho, kuimarisha ukaguzi katika maeneo yote muhimu ya kuingilia wanafunzi na kuwatambua wanafunzi wote kwa kutumia vitambulisho vyao.
Amefafanua kuwa chuo hicho sasa kinafurahia matunda ya mafanikio ya kutimiza miaka 50 tangu kuanzishwa kwake yakiwemo mabadiliko na maboresho makubwa katika sekta ya elimu hasa ongezeko la udahili wa wanafunzi, ongezeko la fani za masomo na kampasi za chuo hicho katika mikoa mingine nchini ikiwemo Dodoma, Mwanza, Mbeya na Zanzibar.
Prof. Mjema amefafanua kuwa chuo cha CBE sasa kinatimiza miaka 50 kikiwa chuo pekee Afrika ya Mashariki na katika nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) kinachotoa wanafunzi wa shahada ya vipimo.
“Chuo hiki pekee ndicho kinachotoa mafunzo kwa ngazi ya shahada ya vipimo, ni chuo kinachotegemewa sana katika ukanda huu wa nchi za Afrika Mashariki na SADC” Amesisitiza.
Ameeleza kuwa tangu kuanzishwa kwake Januari, 1965 na aliyekuwa Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mwalimu Julius Kambarage Nyerere , chuo hicho kimepata mafanikio makubwa kwa kuongeza idadi ya wanafunzi wanaodahiliwa kila mwaka kutoka wanafunzi 25 mwaka 1965 hadi 14,000 mwaka 2014.
Mafanikio mengine ni kuongezeka kwa kozi za masomo na ngazi za mafunzo hadi kufikia shahada, kuongezeka kwa wakufunzi wenye shahada za uzamivu (PhD) chuoni hapo pamoja na chuo kuanzisha ushirikiano wa elimu na vyuo vikuu vingine nje ya nchi kikiwemo Chuo Kikuu cha Eastern Finland katika utoaji wa mafunzo ya shahada za uzamivu kwa kutumia TEKNOHAMA kwa nchi za SADC.
Ameongeza kuwa katika kipindi cha miaka 50 ya chuo hicho idadi ya kampasi imeongezeka kutoka 1 ya jijini Dar es salaam na kufikia 4 katika mikoa ya Mbeya, Mwanza, Dodoma na upande wa Zanzibar huku idadi ya wahitimu wa chuo hicho ikiongezeka kwa kipindi chote ikiwa zaidi ya wanafunzi Laki moja.
Aidha, katika kuhakikisha chuo hicho kinaendelea kuimarisha ubora wa elimu inayotolewa kwa wanafunzi katika maadhimisho hayo,chuo kinaandaa matukio mbalimbali ya ukusanyaji wa fedha kupitia chakula cha hisani, matembezi, midahalo ya wasomi na mikutano wanafunzi wahitimu wa chuo hicho Zanzibar, Dodoma, Mwanza, Mbeya na Dar es salaam kwa ajili ya ujenzi wa maabara, vyumba vya mihadhara ya wanafunzi na madarasa.
Pia chuo hicho kinaandaa mafunzo ya ujasiriamali yatakayotolewa kwa jamii ikiwa ni sehemu ya kurudisha huduma kwa jamii kwa kuwajengea uwezo wajasiriamali, na kuwajengea uelewa wanafunzi ili waweze kuwa na uchaguzi sahihi wa hatima yao ya baadaye pindi wanapohitimu mafunzo.

Jumatano, 10 Septemba 2014

KATIBA MPYA MWISHO!!

Dodoma.Makubaliano baina ya Rais Jakaya Kikwete na viongozi wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD), kutaka Bunge Maalumu lifikie ukomo Oktoba 4, mwaka huu yamezua sintofahamu mjinihapa huku uamuzi huo ukionekana kuwachanganya viongozi wa Bunge hilo.
Kutwa nzima ya jana, viongozi wa Bunge Maalumu walishinda kwenye vikao vya mashauriano huku wabunge wa CCM wakitarajiwa kukutana jana usiku kwenye makao makuu ya chama hicho kupewa taarifa rasmi za uamuzi huo.
Katika makubaliano baina ya TCD na Rais Kikwete, imeamuliwa kuwa uamuzi wa Rais kupitia Tangazo la Serikali (GN) 254 la kuongeza siku 60 hadi Oktoba 4 uheshimiwe na baada ya tarehe hiyo Bunge liahirishwe.
Uamuzi huo ni kinyume cha azimio la Bunge Maalumu la Agosti 5, 2014 ambalo lilirekebisha Kanuni ya 14 (4) na kuifuta Jumamosi katika siku zilizotajwa kuwa za kazi, pia sikukuu na siku za Jumapili.
Mwenyekiti wa Bunge, Samuel Sitta alikaririwa akiwaambia wajumbe wa Bunge hilo kwamba Rais alikuwa ameridhia kwamba siku 60 alizotoa hazingejumuisha Jumamosi, Jumapili na siku za sikukuu.
Ni kwa msingi huo, Bunge hilo likapanga kwamba lingeendelea na shughuli zake hadi Oktoba 31, wakati Mwenyekiti wa Bunge atakapokabidhi Katiba inayopendekezwa kwa Rais Kikwete.
Hata hivyo, makubaliano yaliyofikiwa baina ya viongozi wa TCD na Rais yanaonekana kuvuruga kabisa ratiba ya Bunge hilo ambalo jana na juzi, Kamati ya Uongozi ilikutana mara kadhaa kuona jinsi ya kunusuru mchakato huo.
Ingawa haikufahamika mara moja kama vikao hivyo vya kamati ya uongozi inayoongozwa na Sitta mwenyewe vinajadili nini, lakini taarifa zimedai huenda kukawa na mabadiliko makubwa ya ratiba.
Habari nyingine zinadai kwamba mabadiliko hayo huenda yakapunguza muda wa baadhi ya shughuli za kazi za Bunge hilo ili liweze kukamilisha kazi yake ikiwamo wajumbe kupiga kura ya uamuzi.
Katika kikao cha jana asubuhi, kamati hiyo ilishindwa kurekebisha ratiba yake ili iendane na siku zilizosalia, hivyo kuahirishwa kwa kuwapa kazi wataalamu wake kuleta mapendekezo ambayo yangejadiliwa jana mchana.
Katibu wa Bunge Maalumu, Yahya Khamis Hamad alithibitisha jana kwamba ratiba ya Bunge imebadilika kutokana na hoja nyingi kukubalika ndani ya kamati.
“Kamati ya uongozi itakutana baadaye (jana) kuangalia vipengele ambavyo hawakukubaliana kwenye kamati ndivyo wavipangie muda na ratiba itajulikana baada ya kikao hicho,” alisema Hamad.
Hofu ya akidi
Hata hivyo, habari zaidi zinadai kwamba uongozi wa Bunge Maalumu ulichanganywa na kuwapo kwa hoja za baadhi ya wajumbe wake kutaka kwenda Makka kwa ajili ya kushiriki Ibada ya Hijja, hali inayotishia akidi kwa ajili ya kuendesha vikao.
Kanuni za Bunge Maalumu zinataka kuwapo kwa nusu ya wajumbe kutoka pande zote za Muungano wakati wa kuendesha vikao vyake na theluthi mbili ya wajumbe hao kila upande wakati wa kufanya uamuzi au kupiga kura.
“Tumetoka kwenye kikao mchana huu na pengine tutaitana tena maana hatujafikia mwafaka, kuna mambo mengi yamejitokeza lakini kubwa ni hili la wenzetu ambao wanataka kwenda Hijja, kuondoka kwao kunaweza kuathiri akidi kwa kiasi kikubwa,” kilisema chanzo chetu kutoka ndani ya kamati hiyo.
Kutokana na matakwa hayo, hivi sasa Ofisi ya Katibu wa Bunge inafanya tathmini ili kufahamu idadi ya wajumbe ambao watakwenda Hijja Septemba 22, mwaka huu, ambao wengi wanatoka Zanzibar.
Hamad alikiri kwamba kuna mambo mengi ambayo ofisi yake inayafanyia kazi na kwamba hilo la Hijja ni mojawapo… “Kwa sasa siko katika nafasi ya kuzungumza kwa kirefu, kikao cha Kamati ya Uongozi kimeisha na bado kuna kazi nyingi za kuona jinsi tunavyoendelea.”
Tayari Bunge hilo limetikiswa na kutokuwapo kwa wajumbe waliosusia vikao tangu Aprili 16, mwaka huu ambao ni wajumbe wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) ambao unaundwa na vyama vya CUF, Chadema na NCCR Mageuzi na baadhi kutoka Kundi la 201.

Jumapili, 7 Septemba 2014

KIGWANGALLA ATANGAZA NIA YA KUGOMBEA URAIS

September 7 2014 Dr. Hamisi ambae ni mbunge wa Nzega kwa ruhusa ya CCM alikutana na Waandishi Dar es salaam akiwa ameongozana na mke wake pamoja na watoto wao na kisha kuweka wazi kwamba yuko tayari kugombea kiti cha Urais kwa tiketi yaCCM 2015.
Yafuatayo ndio ameyasema:
1.‘Leo nitasema neno zito kidogo, litabadilisha sura ya historia yangu milele… kinachotokea hapa kina maana kubwa sana kwa watu wenye historia inayofanana na mimi, wale ambao wameyajua maisha ya shida na kukosa uhakika toka wakiwa tumboni mwa wazazi kutokana na hali za uchumi wa familia zao’
2.
‘Nimeyajua maisha ya mtu mnyonge na masikini kwa kuyaishi na sio kwa kusoma ama kusikia, ninajua mtu akiongelea njaa anamaanisha nini’
3.’Watanzania wanataka kupata huduma bora za afya, elimu, maji, miundombinu…… ukienda kwa Wafanyabiashara wakubwa pale Pugu viwandani ama kwa Matabibu wenzangu hospitali ya taifa Muhimbili au kwa Wafanyabiashara pale sokoni Kariakoo wote watakwambia hawapendi kuona kodi zao zikitafunwa na wachache wasio waadilifu’
HK 16
4.’Watu hawatarajii serikali itabeba mizigo yao yote lakini wanaamini kabisa kwamba tukibadili vipaumbele vyetu, tukibadili namna tunavyoendesha serikali na uchumi wetu, tunaweza kwa kiasi kikubwa kubadili mwelekeo mzima wa maisha ya baadae na kuiondoa Tanzania miongoni mwa nchi masikini kabisa duniani’
1.‘Na mimi kama Watanzania wenzangu wengi nina imani kubwa kabisa kwamba tunaweza kubadili mustakabali wa taifa letu, kufungua milango ya maisha bora zaidi kwa Watanzania, tutatoa fursa sawa kwa kila Mtanzania kuishi kwa matumaini kwamba atabadili maisha yake wakati wowote ule kuanzia leo, tutaweza kuamsha ari ya kila Mtanzania kuongeza bidii kwenye kazi’
‘Ninaamini kabisa kutokea ndani ya mifupa yangu kuwa tukifanya uchaguzi sahihi wa vipaumbele vyetu, tukibadili namna tunavyoendesha uchumi wetu na serikali yetu……. haya ninayoyasema sio ndoto za mchana’
h13Baada ya kuyazungumza yake ya moyoni baadhi ya Waandishi walipata nafasi ya kumuuliza maswali ambapo hili lilikua mojawapo >>> ‘Umetangaza nia kwamba unagombea Urais lakini sijasikia unapitia chama gani au utasimama binafsi?……… na kama ni chama, mpaka sasa hakuna chama chochote ambacho kimefungua milango kwa Wanachama wake kutangaza nia, kwa kufanya hivyo huwezi kuona unakiuka taratibu za chama?
JIBU:‘Nitapitia chama cha mapinduzi, sijawahi kuwa Mwanachama wa chama chochote kile cha siasa zaidi ya CCM na sijawa na fikra za kubadili chama, natangaza nia ya kugombea Urais kupitia chama changu cha CCM, hii ya kwamba sasa hivi ni mapema mno kutangaza nia kwa sababu vyama havijafungua milango ya watu kutangaza nia, sio kweli…. watu wameweka nia za kuutaka Urais toka mwaka 1995 lakini pia kuweka nia sio kufanya kampeni, kinachokatazwa ni kuanza kufanya kampeni kabla ya muda wa kampeni kutangazwa’ –Dr. Hamisi Kigwangalla
‘Nimeamua kuweka wazi nia yangu, sitaki ule unafiki wa kujificha chini ya kivuli cha Ooooh!!….. nimeshauriwa, nimeombwa, nasubiri kuota, mimi ni mkweli na nimetia nia ya dhati kwamba nataka Urais’ –Dr. Kigwangalla
h15‘Vipaumbele vyangu kama napata fursa ya kuwa Rais ni kuboresha huduma za jamii kama maji, afya, elimu… kipaumbele cha pili ni kujenga na kuimarisha miundombinu kama barabara, ndege, reli na bandari…….. kipaumbele cha tatu ni utawala bora, nchi haiwezi kuongozwa bila kuwa na utawala wa sheria yani kila mtu apate haki yake bila kudhulumiwa ‘ –Dr. Kigwangalla

OKWI HURU KUITUMIKIA SIMBA

BREAKING NEWZZZZZZ: MKATABA WA YANGA, OKWI HAUPO NA SASA YUPO HURU KUCHEZEA TIMU YOYOTE AITAKAYO
Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imekutana leo (Septemba 7 mwaka huu) na kupitia masuala mbalimbali ikiwemo mgogoro wa kimkataba kati ya klabu ya Yanga na mchezaji Emmanuel Okwi (pichani kushoto akipokea jezi baada ya kusajiliwa na Simba).
Mkataba huo ulipitiwa na Kamati ikiwemo kumsikiliza mchezaji mwenyewe pamoja na upande wa Yanga, na kuridhika kuwa mkataba kati ya pande hizo umevunjika.Ukiwa ni mkataba wa pande mbili, Yanga ilikiuka kipengele namba 8 kuhusu malipo ya ada ya usajili.
Yanga ikiwa mwajiri, haikutekeleza kipengele hicho cha kimkataba hadi kufikia Juni 27 mwaka huu ilipoandika barua TFF kuomba mkataba huo uvunjwe. Kwa maana hiyo Okwi ni mchezaji huru, hivyo yuko huru kujiunga na timu yoyote.
Mkataba ni uhusiano kati ya mwajiri (Yanga) na mwajiriwa (Okwi), ambapo Kamati imebaini kuwa uhusiano huo haupo, hivyo hakuna mazingira ya pande hizo mbili kuendelea kufanya kazi pamoja.
Pamoja na Yanga kuwasilisha pingamizi la kuwepo mmoja wa wajumbe katika kikao kwa sababu za kimaslahi (conflict of interests), walifahamishwa kuwa kilichopo mbele ya kamati ni mgogoro wa kimkataba kati ya Yanga na Okwi, na si usajili.
Pia lilijitokeza suala la Okwi kutakiwa na klabu ya Wadi Degla ya Misri. Kamati imeiagiza Sekretarieti ya TFF kulifanyia uchunguzi suala hilo na kulitolea taarifa katika kikao kijacho.
Hata hivyo mjumbe huyo hakushiriki katika kuchangia hoja na kutoa maamuzi. Uamuzi wa kamati ulifanyika baada ya majadiliano, hivyo hakukuwa na suala la kupiga kura.
Kuhusu pingamizi la Coastal Union kwa Abdi Banda, Kamati imebaini kuwa klabu hiyo imevunja mkataba kati ya pande hizo mbili kwa kushindwa kumlipa mchezaji huyo mshahara wa miezi mitatu mfululizo kama takwa la mkataba.
Klabu ya Coastal Union iliwakilishwa na mmoja wa viongozi wake, wakati Banda aliwakilishwa na mwanasheria wake.
Vilevile Kamati imekubaliana na pingamizi la Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Morogoro (MRFA) kuhusu wachezaji waliofanyiwa uhamisho kutoka katika mkoa wake bila kulipiwa ada za usajili, hivyo klabu husika zinatakiwa kulipa ada hizo.
Pia Kamati imeagiza klabu zote zilizosajili wachezaji bila kuwafanyia uhamisho, kulipa ada za uhamisho kwa pande husika kabla ya kuanza ligi, vinginevyo leseni zao zitazuiwa hadi watakapolipa.
Mashauri mengine ya pingamizi yatasikilizwa baadaye kwa vile klabu husika hazikupata fursa ya kufika mbele ya kamati.Kamati inasisitiza kwa wanachama wa TFF kuheshimu mikataba.
BONIFACE WAMBURA
KAIMU KATIBU MKUU
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA VYUO VYA UALIMU 2014

MAJINA YA WALIOCHAGULIWA VYUO VYA UALIMU 2014/2015
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
WAOMBAJI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA UALIMU NGAZI YA STASHAHADA YA JUU (MIAKA 3) MWAKA WA MASOMO 2014/2015
MAELEKEZO:
Waombaji waliochaguliwa kujiunga na Mafunzo ya Ualimu mwaka wa
masomo 2014/2015 wanatakiwa kuripoti katika Vyuo walivyopangiwa
tarehe 06/10/2014. Fomu za maelekezo (Joining Instructions) zitatolewa
na chuo husika na zitatumwa kwa waliochaguliwa tu. Waliochaguliwa
wanatakiwa kufika vyuoni wakiwa na mahitaji yaliyoainishwa kwenye fomu
ya kujiunga na Chuo. Aidha, fomu hizi zinapatikana pia kwenye Tovuti ya Wizara: www.moe.go.tz; NACTE: www.nacte.go.tz; na TAMISEMI:
www.pmoralg.go.tzMuhimu:
1. Waombaji waliochaguliwa ni wale wenye ufaulu wa Daraja la I hadi III
2. Waliochaguliwa wanatakiwa kuwasilisha Vyeti halisi vya Baraza la Mitihani
la Tanzania Kidato cha NNE na SITA (CSEE na ACSEE) na vyeti vya kuhitimu
Elimu ya Sekondari na Mafunzo ya Ualimu.
3. Ada ya mafunzo Stashahada ya Juu ni 600,000/= kwa mwaka (Muhula wa
kwanza 300,000/= na muhula wa pili 300,000/=)
4. Wanafunzi watakaosajiliwa Chuoni ni wale waliopo kwenye orodha hii tu na
SIYO vinginevyo, waweza pata orodha hyo kwa kufungua kiunganishi kimoja
wapo hapo chini au kwa kutembelea mfumo wenye majina - bonyeza hapa

Jumatano, 3 Septemba 2014

HATIMA YA BUNGE LA KATIBA MIKONONI MWA RAIS

Dodoma. Hatima ya Bunge Maalumu la Katiba imebaki mikononi mwa Rais Jakaya Kikwete, ambalo limemwandikia barua kiongozi huyo wa nchi kutaka ufafanuzi wa kisheria kuhusu tarehe ya mwisho ya kumaliza vikao vyake.
Hiyo ni kutokana na muda uliopangwa kwenye ratiba ya bunge hilo kuzua utata wa kisheria na kuwapo uwezekano wa mwingiliano na Bunge la Jamhuri ya Muungano na Baraza la Wawakilishi (BLW), Zanzibar.
Ratiba ya Bunge Maalumu la Katiba inaonyesha kuwa limepanga kuhitimisha vikao vyake mwishoni mwa Oktoba, tofauti na tarehe iliyotolewa na Rais Jakaya Kikwete Julai 28, mwaka huu ambayo ilitangazwa katika Gazeti la Serikali (GN) namba 254 la Agosti Mosi.
Tangazo la Rais linaonyesha kuwa awamu ya pili ya Bunge Maalumu ingeanza Agosti 5, 2014 na kumalizika Oktoba 4, lakini ratiba ya Bunge hilo inaonyesha kuwa litamalizika Oktoba 31, siku ambayo mwenyekiti wa Bunge hilo atakabidhi kwa Rais Katiba inayopendekezwa.
Hata hivyo, uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa hadi sasa Serikali bado haijatoa tangazo (GN) lingine kuongeza muda hadi mwishoni mwa Oktoba kama alivyosema Mwenyekiti wa Bunge Maalumu, Samuel Sitta wakati akitoa ufafanuzi wa siku 60 zilizotengwa kwa ajili ya Bunge hilo, Agosti 5 mwaka huu.
Sitta alisema kwa kadiri ya tafsiri, siku za kazi ni Jumatatu hadi Ijumaa ambazo wajumbe wanapaswa kufanya kazi na kwamba Jumamosi na Jumapili siyo sehemu ya siku 60 zilizoongezwa na Rais.
Hata hivyo, Katibu wa Bunge Maalumu, Yahya Khamis Hamad alisema hadi sasa hawajapata maelekezo ya ziada kutoka serikalini ambako waliandika barua ya kuomba ufafanuzi wa kisheria kuhusu suala hilo.
“Tulimwandikia barua, Katibu Mkuu Kiongozi (Ombeni Sefue) kuomba ufafanuzi wa siku hizo kama ambavyo sisi tungependa iwe, lakini hadi sasa bado hatujajibiwa lakini bado siku zipo nadhani tutajibiwa tu wakati mwafaka,” alisema Hamad ambaye pia ni Katibu wa Baraza la Wawakilishi.
Sefue alikiri ofisi yake kupokea barua kutoka Bunge Maalumu ikiomba ufafanuzi ambao ungeliwezesha kuongeza siku kwa lengo la kukamilisha kazi ya kujadili na kuandika Katiba inayopendekezwa na kwamba maombi yao bado yanafanyiwa kazi.
“Bado tuna muda wa kutosha tu, ni kweli tulishayapokea maombi ya Bunge Maalumu kuhusu suala hilo na Mheshimiwa Rais akikamilisha kazi yake watajulishwa tu,”alisema Sefue.
Utata wa kisheria
Licha ya ahadi iliyotolewa na Sitta ni dhahiri kwamba suala hilo lina utata wa kisheria kutokana na kauli iliyowahi kutolewa na Mwanasheria wa Serikali (AG), Jaji Frederick Werema wakati akitoa ufafanuzi wa maana ya siku 70 ambazo Bunge lilikaa mara ya kwanza.
1 | 2 | 3

Jumanne, 2 Septemba 2014

SHUKRANI KWA NDUGU, JAMAA, MARAFIKI NA TAASISI

Siku ya jumatano usiku ilikuwa ni siku ambayo niliuona kabisa mwisho wa mimi kuendelea kufurahia uumbaju wa Mungu katika dunia hii hasa pale nilipokuwa na saini kwaajili ya kufanyiwa upasuaji lakini kwa kwa nguvu zake ameniponya.NAMSHUKURU SANA MWENYEZI MUNGU KWA UPONYAJI WAKE HUU MKUU.

Katika mchakato huo Mwenyezi aliwatumia watu mbalimbali ambao sina budi kuwashukuru hapa kwasababu najua Mungu alikuwa na makusudio yake kuwatumia wao badala ya wengine: