visit here again on mukebez.blogspot.com


CHANGE YOUR LIFE

CHANGE YOUR LIFE
Go to Amazon .com and get the copy of this book to make your life better.

Alhamisi, 11 Septemba 2014

CHEYO AELEZA WALIYOKUBALIANA NA RAIS KATIKA KIKAO NA TCD NA UKAWA

Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, ambaye ni Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Tanzania(TCD)Mhe. John Cheyo amesema kwamba mchakato mzima wa Katiba utamalizwa kwa kura ya maoni ya wananchi, hivyo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt. Jakaya Kikwete haiwezi kutamka leo kulihairisha Bunge Maalum la Katiba kwa kuwa liko Kisheria.
Aidha Mhe. Cheyo alisema kilichoahirishwa ni mchakato wa kura ya maoni ya wananchi na si Bunge hilo kwa kuwa walikubaliana katika kikao cha mashauriano, baina Rais Kikwete na Viongozi Wakuu wa Vyama vya Siasa vyenye wabunge vinavyounda TCD kuwa bunge hilo liendelee.
Kauli hiyo imetolewa leo Bunge Mjini Dodoma na Mhe. Cheyo wakati wa mjadala wa kujadili sura zilizobakia za Rasimu ya Katiba Mpya, ambapo alisema hayo ndiyo makubaliano yaliyofikiwa.
Aidha Mhe. Cheyo alisisitiza Katiba Mpya inayopendekezwa itakayopatikana itadumu kwa njia ya maridhiano.
“ Bunge hili linaendeshwa kwa mujibu wa sheria , Tangazo la Serikali (Government Notice) Na 254 hili ndilo uhai wa Bunge hili hadi Oktoba 4, mwaka 2014, na wote tukakubaliana haiwezekani Mhe. Rais akasema leo Bunge likasitishwa.
“ Vitu viwili vikukutana kwa nia ya maridhiano, vitu vingine vinaweza kuwekwa pembeni sawa na sasa na baadae vinaweza vinashughulikiwa kwa wakati huo,” alisema Mhe. Cheyo.
Mhe. Cheyo alisema anamwomba Rais Kikwete atoe ruhusa ya kuwepo kwa kipindi maalum cha kitakachorushwa na televisheni (video) ili kila mtu aonekana alichokisema, huku akionesha kusikitishwa na upotoshwaji wa makubaliano hayo, uliofanywa na baadhi ya wanasiasa.
“ Mojawapo ambayo tuliyokubaliana Bunge hili lipate Katiba ambayo inapendekezwa na wananchi pia kwa hali tulinayo haiwezekani mchakato mzima ukamalizika, mchakato utamalizika kwa kura ya maoni ya wananchi. Kama tukifika huko itabidi tuhairishe uchaguzi wa mwaka 2015. Niliyoyasema ndiyo makubaliano tuliyokubaliana,” alisisitiza.
Mhe. Cheyo alisema Rais Kikwete alikubali kukaa chini pamoja na TCD na hao wanaojiita Ukawa.
Alisema Rais Kikwete alifanya mazungumzo na viongozi wa Vyama vya Siasa vyenye wabunge vinavyounda TCD mara kwa mara ya kwanza, Agosti 31, mwaka 2014 kwa saa nne na mara ya pili, Septemba 8, mwaka 2014 kwa saa mbili.
Kikao hicho cha mashauriano kilihusisha kamati ya makatibu wakuu, kamati ya wenyeviti wa vyama vya CCM, CHADEMA,CUF na NCCR- Mageuzi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni