visit here again on mukebez.blogspot.com


CHANGE YOUR LIFE

CHANGE YOUR LIFE
Go to Amazon .com and get the copy of this book to make your life better.

Ijumaa, 29 Aprili 2016

KWA WALE WANAOLALA NJE HAYA NDIO MADHARA YAKE.

PICHA;BWANA LAWAL AKIWA AMEUNGUA VIBAYA.


Maeneo kama Dar es salaam,Tanga pamoja na Mafia ni mfano wa maeneo ambayo yanakuwa na vipindi vya jato kupita kiasi.Hali hii ya hewa imekuwa ikiwakera sana wakazi wa maeneo hayo hasa nyakati za usiku kiasi cha wakati mwingine kuamua kulala nje.Ukiachilia sababu hiyo ya joto,majiji makubwa pia kama Dar es salaam,Kigari,Lagos na mengine yamekuwa yakipokea watu wengi sana kutoka vijijini kila siku ambao wakati mwingine wanakuwa hawana maeneo ya kufikia na kuwalazimu kulala nje.

Jamaa mmoja aliefahamika kwa jina la Muhammed Lawal amejikuta akiingia kwenye kadhia ya kumwagiwa mafuta ya Gasoline,kuchomwa moto na kupelekea kuungua vibaya mwilini mwake akiwa amelala nje nyakati za usiku huko Nigeria.

Akisimulia tukio hilo bwana Lawal alisema kuwa alikuwa amelala nje nyakati za usiku kutokana na joto kali na ndipo alipostukia anamwagiwa mafuta aina ya Gasoline na kuchomwa moto na hakufanikiwa kumuona aliefanya tukio hilo.

Tuandikie maoni yako hapa kama kuna jambo limekugusa.Pia usisahau kutazama video mbalimbali mpya kwenye MUKEBEZI TV chini kabisa ya blog hii.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni