visit here again on mukebez.blogspot.com


CHANGE YOUR LIFE

CHANGE YOUR LIFE
Go to Amazon .com and get the copy of this book to make your life better.

Jumapili, 24 Aprili 2016

AMUUA MKEWE BAADA YA KUGOMA KUMZALIA WATOTO.


PICHA;MAREHEMU HELEN PRECIOUS.

Polisi katika jimbo la Nassarawa nchini Nigeria wamemkamata jamaa mmoja aliefahamika kwa jina la Okala Joseph kwa kumuua kwa kumpiga risasi mke wake Helen Precious kutokana na kuwa na ugomvi wa muda mrefu juu ya mpango wa uzazi katika familia hiyo.



Akizungumzia tukio hilo,Kamishna wa polisi jimboni hapo Lawal Shehu alisema kuwa Okala alimtuhumu mkewe kwa kutoa mimba kadhaa baada ya mkewe huyo kukataa kumzalia watoto zaidi.

Nae mtuhumiwa akiongelea tukio hilo baada ya kufanyiwa uchunguzi alikuwa na haya ya kusema;
''Mke wangu alinikatalia mimi kuendelea na shule.Baba yangu alinionya kutokumuoa na badala yake niendelee na shule.Lakini kwasababu mke wangu alinisisitiza niache shule na kumuoa yeye nilimpuuza baba nikaacha shule na kumuoa yeye mwaka 2013.Nilijaliwa kupata mtoto wa kiume.Kuanzia hapo mke wangu amekuwa akipata mimba mala kadhaa lakini akawa anazitoa.Mwezi wa kumi na mbili tarehe 25 kaka mkubwa wa mke wangu alikuja nyumbani kwangu akamwambia mke wangu afungashe mizigo yake na akaondoka nae kutokana na kugombana mala  kwa mala kuhusiana na swala hilo.Tarehe 4 mwezi wa 4 mwaka 2016 mida ya saa 2:00 mchana nilienda kijijini Nindama, Kijijini kwa mama yake na mke wangu na nika wakuta shambani.Nilikuwa na hasira sana na nikachukua bunduki yangu na kumfyatulia risasi mke wangu na kumuua mbele ya mama yake.Nilitaka kutoroka lakini polisi walifanikiwa kinikamata.Sijutii kumuua mke wangu,Amesababisha nimeshindwa kusoma.Nimekuwa mkulima katika kijiji cha Angwani Sark nikijaribu kupambana kuwa na maisha bora'' Alisema mtuhumiwa huyo.

Nao ndugu wa marehemu aliefanyiwa kitendo hicho cha kinyama walisema kuwa jamaa alikuwa anamnyanyasa sana ndugu yao kitu kilichofanya familia ikaamua kumtuma kaka yake mkubwa kwenda kumchukua ndugu yao Lakini cha kushangaza ni kuwa jamaa huyo alitokea shambani kwao na kumuua ndugu yao huyo bila sababu.

Walisema kuwa polisi waliwapa mwili wa marehemu baada ya kuufanyia uchunguzi na wamemzika Tarehe 8 mwezi 4 na wangependa kuona sheria inafata mkondo wake.
 Andika maoni yako hapa kuhusiana na story hii au uliza swali kama lipo nasi tutakujibu kwenye comment yako hapa.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni