visit here again on mukebez.blogspot.com


CHANGE YOUR LIFE

CHANGE YOUR LIFE
Go to Amazon .com and get the copy of this book to make your life better.

Jumapili, 17 Aprili 2016

JINSI YA KUTENGENEZA BATIKI #HOW TO MAKE BATIK#


PICHA(ubatik.wordpress.com)

Hujambo mpenzi msomaji na karibu sana katika ukurasa huu ambao pamoja na habari tutakuwa tunajifunza mambo mbalimbali ambayo yanaweza kutusaidia kujikwamua na umaskini.Kama mna kumbukumbu nzuri,siku za karibuni nimekuwa nikiwaambia kuwa nitawaletea masomo ya jinsi ya kutengeneza bidhaa mbalimbali za viwandani.Leo katika somo letu tutaanza kujifunza jinsi ya kutengeneza BATIKI na naomba mnifuatilie kuanzia mwanzo mpaka mwisho wa masomo haya na myafanye kwa vitendo na MUNGU atawabariki.



MAHITAJI:

1.Vibanio vyenye urembo mbalimbali.
2.Sponji zenye urembo mbalimbali.
3.Brash kubwa/ndogo.
4.Meza kubwa yenye urefu wa mita moja mpaka mbili.
5.Sufuria.
6.Vitambaa vya mpira.
7.Misumari midogo.
8.Jiko.

MADAWA:

1.Sodium hydrosulphate.
2.Caustic soda
3.Mshumaa.

KAZI ZAKE:

1.Sodium hydrosulphate ni kuimarisha rangi isichuje,kama itachanganywa na caustic soda.Madawa haya huwa kazi yake ni moja lakini ikikosekana moja nyingine haifanyi kazi.

2.Kazi ya mshumaa ni kuweka urembo kwenye nguo au kwenye vitambaa kwa kutumia vibao au sponji zenye urembo wa tembo,twiga,matunda au aina yoyote ya urembo unayotaka mtengenezaji.
PICHA(printablecolouringpages.co.uk);mfano wa urembo unaoweza kutumika kutengeneza BATIKI.

JINSI YA KUTENGENEZA.
(a)JINSI YA KUGONGA MISHUMAA:

Chemsha mshumaa uchemke sawasawa kisha ipua upoekidogo.Andaa kitambaa cha cotton na kukitandika mezani,chovya kibao chenye picha kwenye mshumaa kisha gonga kwenye kitambaa na kuacha nafasi kidogo.Endelea kugonga picha hizo mpaka kitambaa kiishe.

(b)JINSI YA KUWEKA RANGI:

Chemsha maji ya moto yachemke sawa sawa kisha pima lita tano mpaka sita.Baada ya hapo pima caustic soda vijiko3 na sodium hydrosulphate vijiko vinne mpaka vitano.Changanya na maji ya moto,weka rangi kijiko kimoja.Baada ya hapo pima maji lita kumi na tano na changanya na mchanganyiko wa madawa ili maji yawe vuguvugu.Tumbukiza vitambaa vya vinne vya mita tatu kwa wakati mmoja na kuvigeuzageuza viingie rangi kwa dakika kumi mpaka kumi na tano.Suuza kwa maji baridi na uanike kwenye kivuri ili mshumaa usiyeyuke.

(c)KUWEKA RANGI YA PILI:

Katika kuweka rangi hii kinachofanyika ni kuongeza vipimo vya ranagi tu.Ongeza vipimo vya rangi viwili na zaidi ya mala ya kwanza,maji,mudani uleule,

Weka mshumaa sehemu ambayo haina mshumaa kwa kutumia urembo uleule.Pima rangi kwa kufuata hatua zilezile.Tumbukiza vitambaa vitatu,geuza kwa mda uleule kisha anika.

(d)JINSI YA UFUA MSHUMAA:

Chemsha maji yachemke vizuri,changanya na sabuni ya unga jikoni,tumbukiza kitambaa kimoja kimoja jikoni ili kutoa mshumaa,geuza kwa mti,suuza kwenye maji ya baridi yaliyochanganywa na maji.
PIGA PASI TAYARI KWA KUUZA.


Mendwa msomaji ni matumaini yangu kuwa umenielewa katika somo hili.Kwa maoni ,ushauri na mengineyo nicheki Instagram @mukebezi_blog nifollow au nicheki kwenye mdeonidas@yahoo.com

Tukutane katika somo jingine wakati mwingine.TCHAO

Maoni 2 :

  1. Nimeipenda
    Tupe ningine ya kutengeneza sabuni

    JibuFuta
  2. Nimeipenda
    Tupe ningine ya kutengeneza sabuni

    JibuFuta