visit here again on mukebez.blogspot.com


CHANGE YOUR LIFE

CHANGE YOUR LIFE
Go to Amazon .com and get the copy of this book to make your life better.

Jumatano, 9 Aprili 2014

ELIMU MUHIMU YA UJASILIAMALI

Elimu ya Ujasiriamali: Kuelekeakwenye MaendeleoEndelevu Tanzania

Hakielimu.
1.0. Utangulizi
Ulimwengu unabadilika kwa kasi kubwa. Kwa hakika jamii yoyote ambayo haijajiandaa kikamilifu kuendana na kasi ya mabadiliko hayo, kuna uwezekano wakuwajamii yenye kutegemea misaada. Jamii hiyohaitakuwa na mbadala zaidi ya kutembeza bakuli kwa ajili ya kuomba chochote. Na cha kusikitisha zaidi,hali hii haitaathiri kizazi kilichopo tu, bali hata kizazi kijacho ambacho hakitakuwa na uwezo wa kulipamadeni yaliyokopwa na baba zao. Kwa halihiyo, laana ya utamaduni wa kuwa ombaomba itaendelea kuwepo kwa vizazi hadi vizazi kwa kuwa mtoto wa ombaomba ni ombaomba pia.Uchumi wa duniaunaonesha kuwa nchi nyingi zilizoendelea zimeimarika katika nyanja za kijamii, kisiasana kiuchumi. Zinaweza kuamua nini cha kufanya, jinsi ya kufanya na nini cha kufanya lini kwa ajili yamaendeleo yao. Hali hii ni tofauti kwa nchi zinazoendelea kama Tanzania ambazo bajeti zake kwa zaidi
ya asilimia 60 hutegemea kile kinachojulikana kama misaada ya washirika wa maendeleo (wafadhili). Nchikama hizo hukosa uhuru wa kufanya uamuzi.
Nchi nyingi zinazoendelea ikiwemo Tanzania kwa mfano, zimejaliwa raslimali ambazo zinaweza kubadilishwa kuwa mali. Lakini suala ni jinsi ya kuzigeuza raslimali hizo ili kuwa vitu halisi. Elimu isiyofaaimeelezwa kuwa ndiyo kikwazo kikubwa kinachokwamisha kuzibadilisha raslimali hizo kuwa vitu halisi.
Elimu ya Tanzania inasemekana kuwa ni elimu inayowaandaa watu kuwa waajiriwa wa maofsini, japokuwanafasi za kazi ni chache ukilinganisha na idadi ya watu wanaotafuta kazi za kuajiriwa. Kwa ufupi, elimuyetu haijengi ubunifu na udadisi ambao ungewawezesha watu ama kujiajiri (ujasiriamali) au kuzipanua
fursa za ajira ambazo zingewawezesha watu wengi kupata ajira. Fursa za ajira hazijatumiwa kwa kiwangokikubwa kiasi cha kuweza kuwachukua watu wote wenye sifa za kuajiriwa. Chapisho hili kwa hiyo linaibuajinsi elimu ya ujasiriamali inavyoweza kuibadilisha nchi kutoka kwenye utegemezi na kuwa nchi yenyekujitegemea.
2.0. Maana ya Ujasiriamali
Dhana ya ujasiriamali imeelezwa kwa namna tofautitofauti. Baadhi ya watu hufikiri kuwa ujasiriamalini kufanya biasharatu.Baadhiwanauangaliaujasiriamali katika muktadha mpana unaohusisha ujuzi namaarifa ya mtu katika kutumia fursa zilizopo. Tranchet na Rienstra, (2009), kwa mfano, wanaelezea dhana
ya ujasiriamali kama uwezo binafsi wa mtu wa kubadilisha mawazo na kuwa vitendo. Ujasiriamali unajumuisha ubunifu, kutengeneza kitu kipya na kuwa tayari kukabiliana na ugumu; vilevile kuwa na uwezo wakupanga na kuendeleza miradi ili kufikia malengo. Dhana hii humsaidia mtu katika maisha yake ya kilasiku akiwa nyumbani na katika jamii. Huwafanya waajiriwa kuwa na uelewa kuhusu muktadha wa kazi zaona kuwa katika nafasi nzuri katika kutumia fursa. Pia ujasiriamali hutoa msingi kwa wajasiriamali kujengashughuli za kijamii au kibiashara. Olomi, (2009) anakubalina na dhana kuwa ujasiriamali kwa ujumla unaweza kuelezewa kama namna ya kufikiri, kutafakari na kutenda inayosababisha utengenezaji, uimarishaji,utambuzi na ufanyaji mpya wa vitu kwa maslahi ya mtu mmoja mmoja, kikundi cha watu na jamii.
1Baadhi huelezea ujasiriamali kwa kutumia sifa za mjasiriamali. Sifa kubwa za mjasiriamali ni pamoja na :

Kuwa tayari kupambana na hatari yoyote

Huchukua uamuzi mapema na hasubiri tatizo likue

Mvumbuzi

Mbunifu

Mwenye kuleta tija

Mwenye kujitegemea

Mwenye kutumia fursa zilizopo

Mwenye kufikia malengo yake
Kwamba, ujasiriamali ni mtazamo katika akili ya mtu katika kutafuta fursa, kuwa tayari kukabiliana namatatizo na kuwa na uwezo wa kutengeneza faida, kwa kuanzisha ama biashara mpya au kuongeza tijakatika taasisi. Ujasiriamali hujumuisha shughuli nyingi ikiwa ni pamoja na kuwa na wazo, kutengeneza
na kuendesha biashara. Kwamba mjasiriamali ni mtu anayefikiri kwa ubunifu na uvumbuzi akiwa tayarikukabiliana na hatari inayoweza kusababishwa na fursa zilizopo kwa lengo la kuzalisha faida, ajira naustawi wa kijamii na kiuchumi. Ujasiriamali siyo lazima uhusishe kuanzisha biashara lakini pia kuleta tijaau kubadili utamaduni wa shirika au taasisi. Wajasiriamali huanzisha kampuni ambazo huwa injini katikaukuaji wa uchumi na utengenezaji wa utajiri. Kompyuta, simu za mkononi, mashine za kufulia, ATM, kadiza benki na huduma za usafirishaji ni mifano wa mawazo ya ujasiriamali yaliyobadilishwa kuwa bidhaa auhuduma.


3.0. Historia ya Elimu ya Ujasiriamali
Asili ya elimu ya ujasiriamali katika vyuo na vyuo vikuu ilianzia Marekani ambapo kozi ya kwanza ya MBAilianzishwa mwaka1947 katika Shule Kuu ya Biashara ya Harvard chini ya kichwa cha habari “Uendeshajiwa Biashara Mpya” (Katz 2003). Kuanzia miaka ya 1980 na kuendelea, elimu ya ujasiriamali ilianza kuenea kwanza Ulaya Kaskazini, na kisha kuenea katika sehemu za Ulaya ya Kati na Ulaya ya Kusini katikamiaka ya 1990. Elimu ya ujasiriamali baadaye ilienea katika sehemu zingine za dunia. Kimataifa, Amerikaya Kaskazini ndio mfano wa kuigwa katika ustawi wa miradi na pia Amerika ya Kaskazini ni kiongozikatika elimu ya ujasiriamali. Hakuna asiyejua mchango mkubwa wa kiuchumi wa Kampuni ya Microsoft, Amazon, Intel, Cisco au Google na makampuni mengine yenye ustawi mkubwa huko Marekani.Ukilinganisha na nchi zingine, Marekani ndiyo nchi yenye historia kubwa katika elimu ya ujasiriamali, napia ndiyo nchi yenye mpangilio, utamaduni na mazingira rafiki ya ujasiriamali kuliko nchi yoyote duniani(Kourilloff, 2000).
Nchini Tanzania, elimu ya ujasiriamali haikuwepo enzi za ujamaa wakati wa Azimio la Arusha.Wakati huo Watanzania walisadikishwa kuchukia kila kitu kinachohusiana na ubepari, ujasiriamali ukiwemo.Mjasiriamali alichukuliwa ni kama shetani na alilinganishwa na mnyama katili wa mwituni. Msemo
“Ubepari ni Unyama” ulisikika kwenye radio kila baada ya taarifa ya habari. Ujasiriamali uliwavutia tu waleambao walichukuliwa kuwa ni watu waliopotoka kimaadili. Watumishi wa umma walizuiwa kujishughulisha na biashara (Rutihinda, 2002). Kwa kuwa karibu watumishi wote wa umma walikuwa ni Waafrika, hii
ina maanisha kuwa shughuli za kibiashara zilibaki kuwa za Watanzania wenye asili ya Asia pamoja na walewazawa ambao walikuwa hawana ajira katika ofisi za umma. Watu wa aina hii walikuwa ni wale ambaohawakuwa na kiwango kikubwa cha elimu (Olomi, 2009). Hata hivyo, maendeleo ya hivi karibuni katika
2
ulimwengu, pamoja na sababu za ndani zimeilazimisha nchi kuridhia mabadiliko. Baada ya kuanguka kwaujamaa na Azimio la Arusha, nchi ilianza kubadilika kimfumo. Mamlaka zinazohusiana na masuala yaelimu zilianza kuiona elimu ya ujasiriamali kuwa ni muhimu kwa maendeleo ya nchi katika miaka ya 2000
katikati. Walianza kuiweka elimu ya ujasiriamali kwenye mihtasari yao.

4.1. Je, Wajasiriamali huzaliwa au hufundishwa?
Watu wamekuwa wakibishana iwapo wajasiriamali hufundishwa au huzaliwa. Baadhi ya watu wanasemakuwa wajasiriamali huzaliwa. Wanasema kwamba hakuna haja ya kuwafundisha au kuwapatia mafunzo yaujasiriamali watu kwa sababu mtu huzaliwa akiwa na tabia za kijasiriamali ambazo humfanya awe mjasi
-riamali moja kwa moja. Wanabainisha kuwa watu wenye tabia au sifa za ujasiriamali hufanya vizuri katikashughuli za kijasiriamali kwa kuwa wana tabia walizozaliwa nazo ambazo hulelewa kupitia elimu rasmi.Wanasema kwamba cha msingi ni kupatikana kwa utamaduni wa kijasiriamali katika jamii husika.
Hata hivyo wengine wanabainisha kuwa ujasiriamali unasomewa. Ujasiriamali si “muujiza’, “si siri’ nahauhusiani na nasaba ya mtu. Ni taaluma. Na kama zilivyo taaluma zingine mtu anaweza kujifunza ujasiriamali”. Hata hivyo swali kuwa mtu anaweza kujifunza ujasiriamali ama la siyo suala la msingi. Kinachohitajika ni utamaduni utakaoufanya uchumi wa taifa ukue (Drucker, 1985). Wajasiriamali waliofanikiwa niwale wenye elimu ya ujasiriamali. Egeln (2000) anabainisha kuwa utafiti umeonesha kuwa wajasiriamaliwaliofanikiwa katika Bara la Ulaya ni wale wenye elimu ya kutosha ukilinganisha na wale wasiokuwa naelimu kubwa katika ujasiriamali. Barani Ulaya waanzilishi wengi wa miradi inayohusiana na teknolojiampya ni wale wenye elimu ya chuo kikuu. Utafiti uliofanyika nchini Ujerumani umeonesha kuwa biasharazilizoanzishwa na watu wenye elimu ya kiwango cha shahada ya kwanza, biashara zao hukua kwa harakakuliko miradi inayoanzishwa na watu wenye kiwango cha chini ya elimu.Olomi, (2009) anabainisha kuwa elimu ni muhimu kwa wajasiriamali. Aliona kwamba wale wenye elimuya ujasiriamali hufanya vizuri katika biashara zao ukiliganisha na wale wasiokuwa na elimu ya ujasiriamali. Anabainisha kuwa wajasiriamali wenye elimu ya ujasiriamali wana uwezo wa kufanya mabadilikomakubwa katika biashara zao ukilinganisha na wale wasiokuwa na elimu ya ujasiriamali. Anahitimisha kwakusema kwamba katika biashara kitu cha msingi si kiwango cha elimu aliyonayo mtu bali ni uwezo wake
wa kutimiza malengo pamoja na ufanisi katika mchakato wa elimu. Tranchet na Rienstra (2009) wanasemakwamba katika nchi nyingi, utamaduni na ukosefu wa uelewa katika ujasiriamali vinaweza kuwa vikwazokatika ubunifu na ukuaji wa uchumi. Kwa kuongeza maarifa na kujenga ujuzi muhimu katika ngazi zote
za elimu, kizazi kipya chenye mawazo ya ujasiriamali kinaweza kuubadilisha na kuukuza uchumi wa dunia.Wanafunzi wanaojikita katika fani ya ujasiriamali huwa si watu wa kukubali kila kitu, huwa si watu wenyekujiangalia wao tu, ni watu wenye utayari wa kupambana na hatari yoyote, ni watu wanaokaribisha mabadiliko, wana nguvu katika kiwango cha juu, wana sifa kama zile za wajasiriamali waliofanikiwa (Sextonna Browman, 1985). Pia, tafiti zinaonesha kuwa wale wanaochukua kozi za ujasiriamali wana uwezekanomkubwa wa kuanzisha biashara ukilinganisha na wale ambao hawasomi kozi za biashara (Vijverberg,
1984; Bird, 1989 katika Olomi, 2009).Ulimwengu umekuwa kama kijiji. Ili kuweza kudumu katika utandawazi, mtu anapaswa kuwa na maarifaya kutosha ili aweze kuishi katika ulimwengu huu. Ulimwengu umeshuhudia mafanikio makubwa katikabiashara. Mafanikio hayo yanahusishwa na utamaduni wa watu wake ambao unawahamasisha wajasiriamali kukuza uchumi wa taifa. Kwa maneno mengine, elimu ya ujasiriamali hujenga utamaduni wa kijasiriamali katika akili za watu, na hivyo ni muhimu kwa maendeleo ya wajasiriamali.
Wallen buffet moja kati ya wajasiriamali wakubwa dunian akishika namba nne kwa utajiri.

5.0. Malengo ya elimu ya ujasiriamali
Kama ilivyo katika fani zingine, Elimu ya ujasiriamali ina malengo yake. Kwa mfano malengo makuu yaelimu ya ujasiriamali katika vyuo na vyuo vikuu vya Marekani kwa kawaida ni kuendeleza uwezo wa kijasiriamali katika akili za walengwa na kukuza utambuzi wa kijamii katika mikakati inayohusu ujasiriamali
(Tume ya Ulaya, 2008).Tanzania imejaliwa raslimali nyingi. Ni kama ndiyo kitovu cha raslimali duniani. Lakini changamoto nijinsi ya kuzigeuza raslimali hizi ili ziweze kuleta tija na kutumika kama inavyostahili ili ziweze kumnufaishamtu mmoja mmoja na nchi kwa ujumla. Kushindwa kuzibadili raslimali hizi kunatokana na kuwa na maar
-
ifa na ujuzi kidogo katika kutambua nafasi ya elimu ya ujasiriamali. Watu wengi hufikiri kuwa ujasiriamalihauhusiani na elimu: Kwamba kila mtu anaweza kufanya shughuli za kijasiriamali bila kuwa na seminaau mafunzo juu ya ujasiriamali. Hii si sahihi. Malengo ya elimu ya ujasiriamali yanajumuisha mabadilikokatika mtazamo wa watu ili wawe wajasiriamali katika maeneo yao ya kazi: kutatua tatizo la ajira kwa kuzalisha watengeneza kazi miongoni mwa wasomi: kugundua na kutumia fursa zilizopo kwa maendeleoya mtu mmoja mmoja na nchi kwa ujumla; kuiona dunia kama fursa na wala si sehemu mbaya yakuishi.

6.0. Hali ya Elimu ya Ujasiriamali nchini Tanzania
Kama zilivyo nchi zingine ambazo zimepitia hatua mbalimbali katika maendeleo, Tanzania piaimepitia hatua mbalimbali katika mabadiliko ya mfumo. Baada ya miaka saba tu ya uhuru, iliridhia kuwana mfumo wa ujamaa katika maendeleo yake. Vilevile, mfumo wa elimu ulikuwa wa kijamaa. Nchi ilijenga
elimu ya kujitegemea ambapo mtu aliandaliwa kujitegemea katika maisha yake ya baadaye. Kusema kweli,falsafa hii ilikuwa nzuri kwa ustawi wa watu. Kwa kuangalia maudhui ya falsafa, Elimu ya Kujitegemeaililenga katika kuzalisha watengenezaji wa ajira badala ya watafuta ajira ambayo pia ndiyo malengo ya elimuya ujasiriamali. Hata hivyo, kwa kuwa wafanyabiashara walichukuliwa kama watu waliopotoka kimaadilina hawakuwa na elimu kubwa elimu ya ujasiriamali haikupewa msisitizo. Rutihinda (2002) kwa mfano,amebainisha kwamba nchini Tanzania, enzi za ujamaa, Watanzania walisadikishwa kuchukia karibu kilakitu kinachohusu ubepari. Mjasiriamali alichukuliwa kama shetani na alifananishwa na mnyama mkaliwa mwituni. Msemo kama “Ubepari ni Unyama” ulisikika kwenye radio kila baada ya taarifa ya habari.Ujasiriamali ulionekana kufaa kwa wale tu waliopotoka kimaadili ambao wana uelewa mdogo. Watumishiwa umma walipigwa marufuku kujishughulisha na biashara.Baada ya kuanguka kwa mfumo wa ujamaa na elimu ya kujitegemea, Tanzania haikuridhia ujamaa walaubepari. Hata hivyo, katiba ya taifa inatamka wazi kuwa Tanzania ni nchi ya kijamaa inayofuata sera yaujamaa na kujitegemea ingawa kiuhalisia ni nchi ya kibepari. Huduma za jamii kama elimu na afya kwasasa ni za kulipia na siyo bure tena kama zilivyokuwa hapo mwanzoni. Kwamba, hata muundo na maudhui ya elimu yamebadilika kutoka kwenye mfumo wa elimu ya kujitegemea na kuwa kitu kingine katikakipindi hiki cha soko huria na ubinafsishaji. Hakika, sera na mtaala mpya umeandaliwa na kuwekwa kwenye utekelezaji. Kuanzishwa kwa Sera ya Elimu ya Juu, sera ya TEHAMA katika shule za msingi, Sera yaMaendeleo ya Viwanda Vidogo na vya Kati, kwa uchache tu ni mifano bayana ya sera zinazoendana na
ubinafsishaji na soko huria.Sera ya Elimu ya mwaka 1995 ambayo ndiyo mama wa sera zingine zote katika ngazi zote za elimuhaisemi chochote kuhusu elimu ya ujasiriamali. Inatilia mkazo maarifa na ujuzi utakaomfanya mlengwaajitegemee baada ya kumaliza mafunzo yake.Sera ya elimu ya juu inatilia mkazo kuhusu elimu itakayotolewa kwa wanafunzi na ambayo itawapatiamaarifa na ujuzi utakaowawezesha kujiajiri. Mihtasari ya vyuo vikuu inatofautiana sana. Hakuna mfanano
4
wa mambo yanayotakiwa kufundishwa katika vyuo vikuu vilivyosajiriwa nchini Tanzania. Kila chuo kikuuhuandaa kozi na maudhui kwa kufuata taratibu na falsafa yao. Matokeo yake, kila chuo kikuu hutumiauzoefu wake katika kupanga na kufundisha somo husika. Kwamba kukosekana kwa mfanano juu ya kile
ambacho kinatakiwa kufundishwa na jinsi ya kufundishwa, na kile ambacho kimepewa baraka na Tume yaVyuo Vikuu huzidi kuongeza ukubwa wa tatizo.
Vyuo vikuu vingi hufundisha ujasiriamali. Cha kushangaza, hufundisha ujasiriamali kama mada au madandogo ambayo hujumuishwa katika Taaluma ya Maendeleo. Katika vyuo au vyuo vikuu vingine nchiniTanzania ujasiriamali hufundishwa kama somo la hiari! Hata vile vyuo vikuu ambavyo hutoa mafunzo
ya uzamili, vyuo vingi hujumuisha ujasiriamali katika shahada ya Uzamili katika Uongozi wa Biashara,lengo likiwa ni kuwapatia wanafunzi utamaduni wa ujasiriamali utakaowawezesha kuongoza taasisi zaokwa kufuata utaratibu wa kijasiriamali. Pia ujasiriamali hufundishwa kama mada kuu au mada dogo. Hata
vile vyuo au vyuo vikuu vichache ambavyo vimeanzisha mafunzo ya shahada za uzamili au stashadaza kawaida na za juu katika ujasiriamali vimekuwa vikipanga kozi kwa kufuata utaratibu wao; wakatimwingine vikikosa mwelekeo katika somo. Ndiyo maana baadhi ya vyuo na vyuo vikuu hufundisha
ujasiriamali kama mojawapo ya vigezo vya uzalishaji au somo linalohusu uendeshaji wa biashara (biasharaza mitaani) tu! Mbaya zaidi, somo hufundishwa na watu ambao hawana maarifa ya kutosha kuhusu somo.Vyuo vikuu vingi huajiri watu wenye shahada za uzamili za MBA ambao hufanya kazi kama wahadhiri
wasaidizi. Hawana uelewa kuwa watu wenye shahada za MBA wana elimu ndogo ya ujasiriamali na hivyowanawanyima wanafunzi haki ya kupata elimu bora ambayo wanastahili kuipata.Katika shule za sekondari hali ni mbaya vilevile. Muhtasari wa elimu ya sekondari hausemi chochotekuhusu elimu ya ujasiriamali. Katika ngazi za juu za elimu ya sekondari, ujasiriamali unachukuliwa kamakigezo cha uzalishaji kwa wanafunzi wa kidato cha tano na sita wanaosoma somo la uchumi. Pia katikaMasomo ya Jumla, ujasiriamali hauchukuliwi ama kama mada kuu au mada ndogo. Wanafunzi wengi wasekondari wanaomaliza elimu yao hawaelewi chochote kuhusu ujasiriamali kama taaluma bali husikia tukuwa ujasiriamali unahusishwa na biashara ndogondogo za mitaani!Muhtasari wa elimu ya msingi hausemi chochote kuhusu elimu ya ujasiriamali. Huzungumzia kuhusumaarifa ya jamii ambayo yamelenga kuwapatia wanafunzi maarifa na ujuzi wa kuwa wabunifu na wavumbuzi. Hata hivyo walimu wanaofundisha maarifa ya jamii hawana maarifa ya kutosha kuwawezesha wana
-
funzi wawe wa uwezo wa ziada wa kufikiria. Kwa kawaida wanatilia mkazo katika utengenezaji wa vyunguna upambaji na kazi zingine zinazofanana na hizo na ambazo zimekuwa ndiyo utaratibu wa maisha ya kilasiku. Wanakosa mbinu na ujuzi wa kuwafanya wanafunzi wafikirie na kubuni mambo yasiyo ya kawaida.
Ukosefu wa elimu ya ujasiriamali kwa shule za msingi ni miongoni mwa sababu za kuandaa watafuta kazibadala ya watengeneza kazi.

7.0. Athari za Kukosekana Msisitizo kuhusu Elimu ya Ujasiriamali
Nguvu ya ujasiriamali imethibitisha kuwa yenye matokeo makubwa katika nchi nyingi ambazo huchukulia elimu ya ujasiriamali kama ndiyo inayotengeneza kazi, injini katika ukuaji wa uchumi na silaha yakupambana na umasikini kwa uchache tu. Kourilloff (2000) anabainisha kwamba hakuna anayeweza
kuhoji mchango mkubwa wa kiuchumi wa kampuni ya Microsoft, Amazon, Intel, Cisco au Google namakampuni mengine makubwa nchini Marekani ambayo ni matokeo ya wajasiriamali. Kwamba kwakulinganisha na nchi zingine, Marekani ndiyo nchi yenye historia ndefu katika elimu ya ujasiriamali,na pia miongoni mwa nchi zenye utamaduni rafiki juu ya ujasiriamali duniani. Marekani imejipambanuakuwa ni nchi inayoongoza katika ubunifu na uvumbuzi kuliko nchi zote.
5
Ukweli ni kwamba iwapo nchi haitatilia mkazo elimu ya ujasiriamali itasababisha kuwa na tatizo la ajira,ukuaji mdogo wa uchumi, umasikini na upeo mdogo wa kufikiri kwa watu wake. Elimu ya ujasiriamalihuchangia katika ukuaji wa uchumi. Imegundulika kuwa wajasiriamali wa ndani huchangia kwa kiwango
kikubwa katika Pato la Taifa (GDP). Kwa mfano, mtu anapaswa kujiuliza kuhusu mchango wa Makampuni ya IPP au Bakhresa katika uchumi wa taifa hasa kwa kuzingatia mapato ambayo nchi hupata kupitia(kodi) na utengenezaji wa ajira, achilia mbali mchango wa makampuni hayo katika upatikanaji wa huduma
za jamii. Iwapo elimu ya ujasiriamali haitatiliwa mkazo, nchi itakuwa tegemezi kwa bidhaa za nje na hivyo
kushindwa kupiga vita ujinga, maradhi na umasikini.

8.0. Mahitaji ya Elimu ya Ujasiriamali yenye Ufanisi nchini Tanzania
Elimu ni mchakato usioisha wa upataji maarifa. Mtu anaweza kupata maarifa kwa njia rasmi au isiyo rasmi.Elimu rasmi ni ile tunayoipata kutoka kwenye taasisi za elimu kama vile mashule. Elimu isiyo rasmi ni ainaya elimu ambayo haimlazimu mtu kwenda shule. Inaweza kupatikana muda wowote na popote. Lengokubwa la elimu ni kutengeneza maisha bora kwa watu.Tunapozungumzia elimu ya ujasiriamali tunamaanisha elimu inayotilia mkazo katika kufikiri kwa ubunifukatika kutumia fursa zilizopo kwa lengo la kutengeneza ajira ambazo husaidia katika ustawi wa kijamii naukuaji wa uchumi. Hii ndiyo aina ya elimu ambayo inaweza kuyafanya maendeleo ya taifa kuwa endelevu.Maendeleo endelevu ni aina ya maendeleo yanayokidhi mahitaji ya kizazi cha sasa na kizazi kijacho. Niaina ya maendeleo ambayo hayatikisiki upesi bali yanaweza kudumu na kuhimili vikwazo vya, kijamii kisiasa na kiuchumi.
Nchini Tanzania elimu ya ujasiriamali inahitajika sana ili kuzitumia kwa ufanisi fursa na raslimali zilizopo.
Tanzania imejaliwa maziwa, mito, bahari, mabwawa n.k. ambayo siyo kwamba yamejaa samaki tu baliyamejaa pia viumbe wengine kama vile viboko, mamba n.k. Nchi imejaliwa ardhi kubwa ambayo haijatumika, misitu na wanyama mwitu na wale wa kufugwa. Pia nchi imejaliwa kuwa na gesi na madini kama
vile almasi, dhahabu, Tanzanite, makaa ya mawe kwa uchache tu. Hata hivyo, vitu vyote hivi havijatumiwakikamilifu ili kuleta maendeleo ya watu. Kwa maneno mengine, tunakosa maarifa na ujuzi wa kiujasiriamali katika kuzibadilisha fursa hizo kuwa maendeleo. Iwapo tunataka maendeleo endelevu lazima tutengeneze/tuandae watu ambao wanaweza:

Kuendeleza bidhaa mpya

Kugundua huduma na njia mpya zinazotilia mkazo matumizi halisi katika kiwanda au shirika

Kugundua na kutumia masoko mapya ambayo kiwanda au shirika halijayatumia

Kugundua na kutumia nyenzo mpya za utoaji raslimali ambazo hazijawahi kutumika

Kuwa tayari kupambana na hatari yoyote kwa faida ya nchi
Nchini Tanzania tunahitaji watu ambao wanaweza kuleta tija katika uzalishaji kwenye taasisi au mashirika.Utafiti uliofanyika hivi karibuni umeonesha kwamba huduma za afya nchini Tanzania ni duni sana. Kwamfano, asilimia 53 ya wagonjwa wanaofika hospitalini huhudumiwa baada ya kusubiri kwa muda wa
masaa mawili au matatu na asilimia 19 ya wagonjwa ambao hufikishwa hospitalini huombwa rushwa.Haya yote hutokea kutokana na kukosekana kwa elimu ya ujasiriamali. Hawaijali raslimali watu nawanadhani kuwa uzalishaji unaweza kupatikana kwa njia ya hongo. Ili kuleta ufanisi na tija katika
upatikanji wa huduma na bidhaa, taasisi au shirika lolote linapaswa kuwajumuisha wajasiriamali ambaowanaweza kuleta tija kwenye huduma na bidhaa kwa lengo la kuongeza uzalishaji.
6
Pia tumeshuhudia ku
shuka kwa ubora wa elimu kunakoendana na matokeo yasiyoridhisha kwawanafunzi wa shule za msingi na sekondari nchini Tanzania. Mengi yamesemwa kuhusu suala hilo.Mambo hayo yanajumuisha miundombinu isiyoridhisha na vifaa visivyoridhisha vya kufundishia nakujifunzia. Hata hivyo kuna sababu nyingine ambayo huwa tunaisahau. Sababu yenyewe ni kwambatunakosa ubunifu na uvumbuzi miongoni mwa walimu na wanafunzi katika michakato ya ujifunzaji na
ufundishaji. Wanatumia njia za zamani za ufundishaji na ujifunzaji. Juhudi za kugundua njia mpya zaufundishaji na ujifunzaji ni ndogo. Kinachosababisha hali hii ni ukosefu wa utamaduni wa kijasiriamaliambao unaweza kubadili mtazamo wa mtu katika kukabiliana na ulimwengu. Wakati walimu na wanafunzi
katika nchi zingine wakijaribu kuvumbua na kubuni njia mpya za ujifunzaji na ufundishaji, sisi bado tunashikilia njia za zamani za ujifunzaji, ufundishaji na upimaji wa wanafunzi wetu. Matokeo yake, baadhi yawanafunzi (wakati mwingine, kwa kushirikiana na walimu wao) wanafanya udanganyifu katika mitihani.Pia ukweli uliodhahiri ni kwamba kutokujua kusoma na kuandika kunaongezeka. Kwa mfano, kulikuwana wanafunzi 308 wa Kidato cha Kwanza wasiojua kusoma na kuandika katika kata ya Nansimo katikawilaya ya Bunda. Pia, mkoa wa Arusha unaongoza katika udanganyifu kwenye mitihani. Unaongoza
kwa asilimia 48. Pia ilibainika kwamba ni asilimia 14 tu ya wahitimu wa shule za msingi walifaulu mtihaniwa hisabati mwaka jana. Hali hii kwa mujibu wa utafiti ilitokana na ukosefu wa uvumbuzi na ubunifumiongoni mwa walimu wa hisabati katika kulifanya somo hilo lieleweke vizuri. Pia ukosefu wa mbinu
zinazowapatia wanafunzi motisha ya kulipenda somo la hisabati huchangia katika ufaulu duni wa wana
-
funzi. Iwapo walimu wangefundishwa kuhusu ujasiriamali (ujasiriamali wa mashirika), hali hii ingekuwaimepungua kama siyo kuondolewa kabisa.

9.0. Nini kifanyike?
Ili kuwa na elimu ya ujasiriamali yenye ufanisi kwa ajili ya maendeleo endelevu ya mtu mmoja mmoja nanchi kwa ujumla, mambo yafuatayo inabidi yafanyike:

Mihtasari/programu na moduli za elimu ya ujasiriamali ni lazima ziwe na malengo ya kuendelezaari ya ujasiriamali kwa wanafunzi (kujenga motisha na ufahamu). Hii inajumuisha kuendelezauwezo wa kijasiriamali ili kuweza kubainisha na kutumia fursa zilizopo, kuwapatia wanafunzi ujuziunaohitajika katika kuanzisha biashara na kuziendesha ili zikue. Katika hali hizi zote, ni muhimukuwahamasisha wanafunzi ili waweze kufikiri na kutenda kama wajasiriamali na pia ili wawe wenye kuwajibika kimaadili na kijamii.

Ujasiriamali ni sharti ufundishwe na wataalamu ambao wanafahamu jinsi ya kulifundisha somohili. Inapaswa kufahamika kwamba ujarisiarimali ni vitendo na kwamba ili kuwapatia motisha wanafunzi, njia/mbinu mbalimbali za kufundishia inabidi zitumike. Kwa mfano, ni muhimu somola ujasiriamali lifundishwe na wajasiriamali wenye moyo wa kufanya hivyo. Mbinu ya kuiga nimuhimu zaidi katika ufundishaji wa ujasiriamali kwa sababu watu hupenda kumsikiliza yule wa
nayemwamini na yule aliyefanya kitu kwenye jamii.

Shule ni sharti zifungamanishwe na kazi. Uhusiano huu wa shule na kazi husaidia kupunguzamatarajio ya kazi kwa vijana na pia husaidia kupunguza tatizo la ajira kwa wasomi walioajiriwa nawale wasio na ajira.

10.0. Hitimisho
Elimu ya ujasiriamali si ya zamani kama zilivyo fani nyingine kama vile sayansi ya siasa, falsafa na sosholojia, lakini ujasiriamali umeleta mabadiliko makubwa tangu kuanza kwake. Kompyuta, mashine za ATM,simu za mikononi, kwa uchache tu ni bidhaa zinazotokana na ujasiriamali. Ijapokuwa mtu anaweza kuwa
na sifa za ujasiriamali, ni sharti afundishwe somo hilo ili kumpatia maarifa na ujuzi wa kushindana katikaulimwengu kwa ujumla wake. Ufundishaji makini wa ujasiriamali utawezesha kupatikana kwa maendeleo endelevu na hivyokuwawezesha watu kuwa na maisha mazuri katika nchi zao.


Marejeo
Coleman, J.
et al
(1982),
High School Achievement, New York, Basic Books.Drucker, P (1985),Innovation and Entrepreneurship, New York, HarperCollins.
European Commission (2008),Final Report of the Expert Group Entrepreneurship in Higher Education, especially within non-business studies
. Brussels, European Commission.
Fridolin,S & Zimbandu, L (2012) “Walimu wa Hisabati Watakiwa Kujipanga” in Nipashe News Paper
,
The Guardian Limited; Wednesday, September 19.
Katz, J. A. (2003), “The Chronology and Intellectual Trajectory of American Entrepreneurship Education 1876– 1999,”Journal of Business Venturing,pp283-300.
Kourilloff, M.(2000), “Exploring perceptions of a priori barriers to entrepreneurship: a multidisciplinary approach,”Entrepreneurship: Theory & Practice
, pp59-80.
Lazaro, H (2012) “Walimu wa Hisabati Watakiwa Kujipanga” inMwananchi News Paper, Mwnanchi Communications Ltd; Wednesday, September 19.Makongo, A. (2012) “Kata ina Wanafunzi 300 Mbumbumbu” in
Nipashe News Paper
, The GuardianLimited; Wednesday, September 19.
MIT (2003),Small and Medium Enterprises Development Policy,Dar es Salaam, Business Printers Limited.MSTHE (1999),National Higher Education Policy,
Dar es Salaam.
Nyang’oro, G. (2012) “Twaweza: Huduma za Afya Nchini Haziridhishi” inMwananchi News PaperMwananchi Communications Ltd; Wednesday, September 19.
Olomi, D.R. (2009), “Influences on Entrepreneurial Behaviour and Business Success”.
African Entrepreneurshipand Small Business Development: Context and Process, Dar es Salaam, Otme Company Limited.
Rutihinda, C. (2002), “Entrepreneurial Process in African Economies in Transition”,Business Management Review,
8,. pg 11-2,
Sexton, D.L. and N. Brownman. (1985), ”The Entrepreneur: A capable Executive and More,”Journal ofManagement Studies,
95-100.
Tranchet , N & D. Rienstra. Eds.(2009),Educating the Next Wave of Entrepreneurs: Unlocking entrepreneurialcapabilities to meet the global challenges of the 21st Century A Report of the G

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni