visit here again on mukebez.blogspot.com


CHANGE YOUR LIFE

CHANGE YOUR LIFE
Go to Amazon .com and get the copy of this book to make your life better.

Jumatatu, 21 Aprili 2014

KWA HILI SLAA UNAJITETEA!SEMA UONE ALICHOSEMA.

Monday, April 21, 2014 Majibu ya Mh.Jerry Silaa kuhusiana na taarifa zinazosambazwa mitandaoni Nimepokea kwa Masikitiko makubwa taarifa zinazosambazwa mitandaoni ikidaiwa ni mawasiliano baina yangu na Ridhiwani Kikwete, Mjumbe wa NEC na Mbunge mteule wa Jimbo la Chalinze. Ingawa si tabia yangu kukanusha mambo yaliyotengenezwa kwa sababu anazojua muandaaji lakini kwa idadi ya simu nilizopokea kwa faida ya wengi ni bora niseme yafuatayo. 1.Kwa wanaofahamu matumizi ya whatsapp, screen shot hii ilipaswa kutoka kwenye simu yangu, kwa maana nyingine ni mimi mwenyewe ndiye chanzo cha jambo hili. 2. Wanaonifahamu whatsapp sio moja ya njia yangu ya mawasiliano, situmii simu aina ya samsung ambayo ndiyo inayoonekana ilikuwa inatumika katika mawasiliano hayo,na pia siifahamu na wala sijawahi kuwa na namba ya Airtel ya Ridhiwani. 3. Ukiiangalia Lugha na aina ya uchaguzi wa maneno uliotumika si aina yangu ya uandishi na maneno hata ambayo huwa nayatumia katika mazungumzo ya kawaida,mtu yoyote anayejua siasa atatambua mazungumzo hayo hayana mantiki yanaongelea mambo mengi na watu wengi kwa wakati mmoja. 4.Tarehe 5 April nilikuwa kwenye hall of fame Chuo kikuu Mzumbe na si Chalinze nilikokuwa tarehe 2,3 na 7. Muda wa ujumbe unatofautiana sana 5 am, 6.30am na 2.32pm. Screenshots zinaonyesha kwamba majadiliano hayo yalifanyika tarehe 5 April ambayo mimi nilikuwa tayari Chuo Kikuu Mzumbe. Mimi niliondoka Dar kwenda Chalinze rasmi siku ya tarehe 2 nikitokea katika shughuli za ugawaji wa madawati katika shule ya Sekondari Pugu ambapo nilikuwepo huko tangu asubuhi bila kupitia sehemu yoyote na niliongozana na MNEC Anthony Mavunde kwa kupitia njia ya kisarawe ili kukwepa foleni. Na tarehe 7 nilienda tena Chalinze kusherehekea ushindi. 5. Jambo hili ni rahisi sana kulitengeneza kwa simu mbili na kusave majina unayotaka na unawezo hata wa kutoa ya upande wa pili inayoonyesha jina langu.Matumizi haya ya teknolojia ni vyema yatumike katika mambo ya msingi badala ya kujaribu kuleta fitna zisizo na maana na kujaribu kuwapa watu tabia ambazo hawajawahi kuwa nazo. 6. Ushauri wangu ni kwa kila mmoja wetu hasa wanasiasa kuwa makini na kuepuka kufitinishwa kwa fitina nafuu kama hii. Kwa jambo lilozungumzwa kwanza wakati bado na pili wanasiasa wa ngazi yangu na Ridhwan si wakulijadili jambo kubwa namna hiyo kwa hoja dhaifu hivyo na tena kwenye whatsapp. -JERRY SILAA. Source ya majibu ni facebook page ya Jerry Silaa. Monday, April 21, 2014~Copyright: mukebezi blog

 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni