visit here again on mukebez.blogspot.com


CHANGE YOUR LIFE

CHANGE YOUR LIFE
Go to Amazon .com and get the copy of this book to make your life better.

Jumamosi, 19 Aprili 2014

HAYA SASA WALE WALEVI,KAZI HII HAPA!

ananchi mkoani Mbeya wametakiwa kuacha kuzitumia sikukuu za kidini kwa ulevi, badala yake wajikite kuimarisha upendo na amani.
Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Ahmed Msangi alisema hayo alipozungumzia kuimarishwa kwa ulinzi katika kipindi chote cha maadhimisho ya Pasaka yanayofanyika katika makanisa mbalimbali.
Msangi alisema kwa kawaida Mkoa wa Mbeya una waumini wengi wa dini, lakini wapo watu wanaoharibu imani za wenzao kwa kuandaa pombe na kufanya vurugu wakati wa sikukuu.
“Polisi inawatakiwa kila heri na baraka wakati wote wa Sikukuu ya Pasaka, lakini lazima tuoe angalizo kuwa wale watakaoshindwa kujiheshimu kwa sababu ya ulevi watashughulikiwa,” alisema.
Kamanda huyo pia aliwataka wazazi na walezi wa watoto kuwa makini na watoto wao watakapokwenda sehemu mbalimbali kufurahia sikukuu. “Tutapita katika kumbi za starehe kufanya ukaguzi, lengo letu ni kuhakikisha usalama unakuwepo na watu wanapata nafasi ya kufurahia sikukuu.”
KUTOKA MWANANCHI.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni