visit here again on mukebez.blogspot.com


CHANGE YOUR LIFE

CHANGE YOUR LIFE
Go to Amazon .com and get the copy of this book to make your life better.

Jumatano, 23 Aprili 2014

DU!KWELI MOYES ALICHUKIWA,HEBU ANGALIA SOKO LA HISA LILIVYOPANDA BAADA YA KUFUKUZWA.

Kilichotokea kwenye hisa za Man United baada ya Moyes kufukuzwa
Wakati kocha Sir Alex Ferguson alipostaafu kama meneja wa Manchester United mwezi wa tano mwaka jana, hisa za klabu hiyo kwenye soko la hisa la New York thamani yake ilishuka kutoka kuuzwa $18.44 mpaka $15.16 ndani ya kipindi cha mwezi mmoja tu!
Chini ya utawala wa David Moyes thamani yake iliendelea kushika kwa kasi, mpaka kufikia wiki ya 52 ya utawala wa Moyes thamani ya hisa hizo ilifikia $14.26 kwa hisa moja.
Lakini tangu mwishoni mwa mwezi tano, wakati tetesi za kutimuliwa kwa David Moyes zilipoanza kusambaa thamani ya hisa hizo ikaanza kupanda, na jana tu baada ya kuthibitishwa kwa taarifa kwamba Moyes kibarua kimeota nyasi, thamani ya hisa za Man United ikapanda kwa kasi.
Mpaka kufikia jana jioni thamani ya hisa za MUFC ilikuwa ni $18.78 kwa hisa moja.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni