visit here again on mukebez.blogspot.com


CHANGE YOUR LIFE

CHANGE YOUR LIFE
Go to Amazon .com and get the copy of this book to make your life better.

Jumanne, 21 Oktoba 2014

KUNDI LA DIAMOND LAONGELEA TUKIO LA MSANII HUYO KUZOMEWA

Meneja wa Diamond Platnumz, Babu Tale amesema haoni kama wameathirika na kundi la watu waliomzomea msanii huyo wakati akitumbuiza Jumamosi hii kwenye show ya Serengeti Fiesta, Leaders Club jijini Dar es Salaam.
Tale amekiambia kipindi cha XXL cha Clouds FM kuwa walikuwa na taarifa kuhusu mpango huo hata kabla ya show na hivyo walijiandaa. “Tulikuwa tumemjenga kisaikolojia, kwahiyo hiyo ni sehemu ya kazi na mashabiki ingekuwa wanapiga kelele kama tumekosea show kweli, lakini sio hivyo. Show ilikuwa sawa,” amesema Tale.
“Tunachojua sisi msanii wetu anafanya vizuri na sasa hivi nguvu zetu tumeelekeza katika tuzo. Wananchi wakaze kumpigia kula katika tuzo Channel O na MTV, sie sasa hivi tunasonga mbele, tunachojua chema chajiuza, kibaya chajitembeza.”

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni