visit here again on mukebez.blogspot.com


CHANGE YOUR LIFE

CHANGE YOUR LIFE
Go to Amazon .com and get the copy of this book to make your life better.

Ijumaa, 6 Juni 2014

AAMUA KUKATA MIGUU YA MAITTI BAADA YA KUSHINDWA KUTOSHA KWENYE JENEZA

Miguu ya maiti inasemekana ailikuwa ndefu sana na kukwaza waandalizi wa mazishi
Mwandalizi mmoja wa mazishi nchini Afrika Kusini,anayedaiwa kuwaagiza wafanyakazi wake kuikata miguu ya maiti moja aliyodai kuwa ndefu sana alifikishwa mahakamani Ijumaa.
Ronel Mostert anayemiliki chumba cha kuhifadhi maiti ambacho pia huendesha shughuli za mazishi, alitoa amri hiyo kwa lengo la kuhakikisha kuwa maiti hiyo ingetosha katika jeneza.
Anakabiliwa na kosa la kumkata miguu maiti.
Mfanyakazi mmoja aalimbia mahakama kuwa Ronel alimuagiza kuchukua kifaa kimoja cha kukata ili kuikata miguu hiyo ya marehemu na kwamba jambo hilo limekuwa likimsumbua sana kimawazo.
Mwili marehemu ulifukuliwa ili kusaidia katika uchunguzi wa polisi.
BBC

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni