visit here again on mukebez.blogspot.com


CHANGE YOUR LIFE

CHANGE YOUR LIFE
Go to Amazon .com and get the copy of this book to make your life better.

Jumatatu, 30 Juni 2014

JINSI YA KUTENGENEZA SABUNI YA KUNAWIA MIKONO

Moja kati ya mahitaji makubwa ya watu ikiwemo wafanyabiashara za mama lishe,mabucha na nyingine,ni sabuni ya kunawia.Kutokana na mahitaji makubwa waliyonayo watu na kukosekana kwa bidhaa hiyo wahitaji hujikuta wakitumia sabuni ambazo hazikutengenezwa kwa kazi hiyo kama sabuni za unga,shampoo na sabuni za vipande ambazo huwasababishia madhara bila kujijua.
Leo katika somo letu tutajifunza jinsi ya kutengeneza sabuni za kunawia mikono.fuatana nami mwanza mpaka mwisho.



MAHITAJI;
.Sulphonic acid
.soda ash
.maji yaliyochujwa vizuri
.pafyum
.Rangi yoyote inayovutia
.sless
.Chumvi

JINSI YA KUTENGENEZA.
Andaa vizuri chombo chako kwaajili ya kutengenezea sabuni yako kama ndoo au pipa pamoja na kuandaa malighafi zako huku ukizingatia usafi.

Tanguliza kumimina ssulphonic acid vijiko vitano vya chakula kwenye chombo chako.
Endelea kuweka soda ash iliyochanganywa na maji vijiko vitatu vya chai.

Weka maji lita tano ukifuatiwa na sless robo lita,chukua pafyum yoyote na uweke kijiko kimoja na nusu cha chai.

Ongeza rangi kijiko kimoja cha chai na uanze kunyunyizia chumvi ambayo huleta uzito na kufanya sabuni yako isiharibike na kukaa muda mrefu.

Koroga vyote kwa pamoja kwa muda wa dakika ishirini na sabuni yako itakuwa tayari.

Asanteni sana kwa wale mnaoendelea kunitafuta katika namba yangu ya watsap.Kama ulivyo utaratibu wetu kwa wale ambao watahitaji maelezo zaidi na jinsi ambavyo wanaweza kupata malighafi na vifungashio pamoja na lebo wanaruhusiwa kunitumia ujumbe katika namba yangu ya watsap 0654627227,utatuma 2000 katika namba hiyo na nitaanza kukupa maelekezo.Huna haja ya kwenda kwenye semina,jifunze ukiwa nyumbani.

ASANTENI NA KAZI NJEMA.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni