PICHA (Getty Images);WEWE NA WAFANYAKAZI WAKO MNAHITAJI MOTISHA.
Katika kila tunachokifanya binadamu
motisha ni kitu ambacho kinahitajika sana.Motisha ni msukumo au shinikizo unalolipata kufanya jambo fulani kwa mategemeo fulani.Motisha zinaweza kuwa hasi au chanya.
Mwili wa binadamu umeumbwa katika mfumo wa kutamani na kukinai mambo.Unaweza kutamani sana kufanya jambo fulani lakini baada ya kulifanya kwa muda fulani ukakinai na kutaka kufanya jambo lingine kutokana na sababu mbalimbali.
Kuna mbinu mbalimbali unazoweza kuzitumia kujipa motisha wewe na wafanyakazi wako ili kuendelea kufanya kazi kwa ari ileile;
>>LIKIZO<<
Mwili wa binadamu pia huchoka na inafikia kipindi unahitaji kupumzika.Wafanyabiashara wamekuwa na tabia ya kufanya kazi siku zote 365 za mwaka bila kupumzika kitu ambacho kinaweza kupunguza morali ya kufanya kazi.
Unapaswa kuwa na utaratibu maalum ambao utakufanya wewe na wafanyakazi wako kuwa na mapumziko walau mala moja kwa mwaka kwenda kutembelea ndugu na marafiki.
Kumbuka swala la likizo halijalishi unafanya biashara ndogo kiasi gani,unahitaji mapumziko!!.
>>MAFUNZO<<
Unapaswa pia wewe kama mfanyabiashara kujipa motisha kwa kuhudhuria mafunzo mbalimbali yanayotolewa kwaajili ya biashara.Mafunzo haya yatainua tena ari ambayo itakuwa inaonekana kupotea kwani watoa mafunzo wengi huwa na tabia ya kuhamasisha.Lakini pia kama kuna mambo mapya utayapata katika mafunzo hayo utakuwa na ari ya kutaka kuyaongeza katika biashara yako na hivyo kuifanya biashara yako kuwa bora zaidi.
>>KUFANYA TOUR<<
Ni vizuri sana wewe kama kiongozi kupanga safari za kutembelea maeneo mbalimbali ya kihistoria na mbuga za wanyama kama sehemu ya motisha.
Pamoja na kuwapa ari wafanyakazi wako,pia hii husaidia kubadili mazingira waliyozoea na hatimae kupata changamoto mpya ambazo huweza kuwasaidia katika utendaji wao.
Asante sana mpendwa msomaji kwa leo na tukutane tena wakati mwingine kuendelea na mada zetu hizi za biashara na maendeleo.