visit here again on mukebez.blogspot.com


CHANGE YOUR LIFE

CHANGE YOUR LIFE
Go to Amazon .com and get the copy of this book to make your life better.

Alhamisi, 8 Mei 2014

JINSI YA KUTENGENEZA SABUNI YA NGA.


Karibu tena msomaji kwenye somo letu kama tulivyozoea kupata masomo haya ya kujikwamua na umaskini.leo nakuletea somo ambalo litakua la mwisho kwa masomo amboyo utayapata bure na atakaetaka masomo zaidi basi atanipigia simu kwenye namba inayoonekana pembeni na tutapatana kwa malipo kidogo tu.
Somo la leo linahusu jinsi ya kutengeneza sabuni za unga.



MAHITAJI.
.Optical bytina.
.sodium carbonate.
.sulphonic acid.
.Sodium sulphate.
.Hoda ash.
.Hydrogen peroxide.
.Rangi.
.Perfume.

JINSI YA KUTENGENEZA.
Andaa chombo chochote kinachoendana na wingi wa sabuni unayotaka kutengeneza na anza kutengeneza kwa kufuata hatua zifuatazo.

.weka sodium carbonate kwenye chombo ulichoandaa kg2 na nusu.
.Baada ya hapo weka optical bytina vijiko kumi(10)vya chakula.
.halafu weka sodium sulphate vijiko vitano vya chakula.
.weka soda ash kg7 na ukoroge kwa muda wa dakika kumi.

HATUA YA PILI.
.Sulphonic acid kilo 2 na nusu.
.nausa vijiko 15 vya chakula.
.Hydrogen peroxide kama ni ya unga weka kilo mbili kama ya maji weka lita mbili.
.rangi vijiko vitano vya chakula.
. changanya na perfume vijiko sita vya chakula.
.baada ya mchanganyiko huo anika kwenye kuvuli kwa kuwa juani inaweza kuyeyuka.sabuni yako itakauka kwa kujiachia.Kusanya weka kwenye mifuko tayari kwa kuuza.

ONYO:Baadhi ya malighafi ni acid kwahiyo umakini unatakiwa wakati wa kutengeneza,hakikisha mikono yako imelindwa kwa gloves na usishike acids au kula wakati unafanya kazi.Tafadhari watu wazima ndio wafanye kazi hii.KAZI NJEMA KUPAMBANA NA UMASKINI.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni