Wapiganaji wa kiisilamu nchini Syria
Maafisa sita wa kikosi cha Umoja wa Mataifa waliokuwa wanachunguza madai ya kutumiwa kwa gesi ya Chlorine nchini Syria pamoja na madereva watano wameshambuliwa.
Taarifa kutoka wizara ya mambo ya nje ilisema maafisa hao walishambuliwa walipokuwa wanajaribu kufika kijiji cha Kafr Zaita katika mkoa wa Hama.
Punde tu baada ya kutoka katika gari lao kwenda kuanza kazi, papohapo mlipuko wa bomu ukatokea.
Hata hivyo duru zinasema kuwa maafisa hao wote wako salama.
Serikali ya Syria hapo awali ilisema kuwa maafisa hao walikuwa wametekwa nyara na magaidi walipokuwa wanasafiri kupitia mkoa wa Hama.
Mkurugenzi wa shirika la kudhibiti silaha za kemikali, Ahmet Uzumcu, alielezea wasiwasi kuhusu usalama wa maafisa hao.
"Wachunguzi wetu walikuwa nchini Syria kuchunguza madai ya matumizi ya gesi ya Chlorine kushambulia watu,'' alisema afisa huyo.
Wachunguzi hao walikuwa wanajaribu kufika kijiji cha Kafr Zaita kilicho chini ya udhibiti wa waasi, ambako inadaiwa mashambulizi sita ya kutumia gesi ya Chlorine yamefanyika katika miezi miwili.
Wiki jana wanaharakati, walitoa kanda inayodaiwa kuonyesha wanaume na watoto wakitibiwa katika hospitali moja baada ya bomu lililokuwa na Chlorine kurushwa na ndege ya jeshi na kumuua msichana mmoja.
Chlorine ni kemikali ya viwandani ambayo imepigwa marufuku ya shirika la kudbibiti zana za kemikali.
Credit:BBC.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni