Wasichana wanaozuiliwa na Boko Haram
Taarifa kutoka mjini Buni Yadi katika jimbo la Yobe Kaskazini mwa Nigeria, zinasema kuwa watu 24 wakiwemo wanajeshi 11 wameuawa katika shambulizi dhidi ya kambi za wanajeshi.
Inaarifiwa kuwa kundi la Boko Haram ndilo linashukiwa kufanya mashambulizi hayo.
Wakaazi wanasema washambuliaji waliwasili katika eneo hilo kwa magari kumi ya kawaida na gari moja la kijeshi.
Waliwaambia wanakijiji kutokuwa na hofu kwani nia yao haikuwa kuwadhuru raia bali maafisa wa usalama.
Wanajeshi 11, polisi 13 akiwemo mwanamke mmoja waliuawa.
Pia waliteketeza majengo na magari ikiwemo makazi ya kiongozi mmoja wa kijadi na kituo kimoja cha polisi.
Taarifa zaidi bado zinajitokeza pole pole hasa kwa kuwa mawasiliano yamekuwa magumu kutokana na miundo mbinu mibovu.
Jimbo la Yobe ni moja ya majimbo matatu ambayo serikali imeweka sheria ya kutotoka nje usiku. Licha ya sheria hiyo mashambulizi ya mara kwa mara yamekuwa yakishuhudiwa mengi yakifanywa na Boko Haram.
BBC
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni