aji wa kata na vijiji wapewa onyo kali kwa kutokuhifadhi mihutasari ya vikao na kutokuweka mipango thabiti ya matumizi ya ardhi kwa wanavijiji wao hali ambayo inachangia kuwapo kwa migogoro ya muda mrefu.
Onyo hilo limetolewa na Mbunge wa Viti Maalum wilayani, Mbulu mkoani Manyara, Martha Umbula kwa watendaji wa vijiji viwili vya Endahagichan na Endanawish wanaogombania eneo la malisho.
Aidha, aliwataka kuweka mipango mizuri ya kumilikisha ardhi kwa wananchi wao na kuweka sheria na taratibu ili kama ikitokea watu wakivunja sheria hatua kali zichukuliwe.
“Kuacha mambo bila kuyashughulikia kwa wakati maana yake ni kukaribisha migogoro isiyo na ulazima, hivyo nawaombeni muandae taratibu na sheria za ardhi mapema ili kunusuru migogoro,” alisema.
Naye Apasiana Paulo, mkazi wa Kijiji cha Endanawesh Kata ya Daudi, wilayani Mbulu alisema kuwa alishangaa siku moja kundi la vijana wakiwa na silaha za jadi kuvamia nyumbani kwake na kudai wametumwa na mkuu wa wilaya kumwondoa kijijini hapo
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni