LICHA ya mabadiliko yasiyo ya kawaida yaliyojitokeza katika utabiri wa hali ya hewa kuhusu mvua za El Nino hafifu, Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imesema kuna uwezekano wa kuwapo kwa vipindi vifupi vya mvua kubwa.
Mabadililko hayo yanahusu utabiri uliotolewa na TMA kuanzia Oktoba hadi Desemba, mwaka huu kuwa kungekuwa na El Nino hafifu maeneo mengi nchini.
Akizungumza ofisini kwake jana, Mkurugenzi wa Huduma za Utabiri wa TMA, Dk Hamza Kabelwa alisema katika utabiri waliofanya siku mbili zilizopita, umeonyesha uwezekano wa kuwapo kwa vipindi vifupi vya mvua kubwa hivyo wananchi wanatakiwa kuchukua tahadhari.
Mamlaka hiyo tangu Septemba mwaka huu, ilisema joto la Bahari ya Pacific limeongezeka ikiwa ni kiashiria kingine cha mwendelezo wa mvua za El Nino hafifu.
Iliwataka wananchi kuwa makini na mabadiliko hayo ambayo yanaweza kusababisha mafuriko.
“Kuna uwezekano wa mvua kubwa kunyesha kwa kipindi hiki kifupi kama zinavyoendelea, wananchi wanatakiwa kuchukua tahadhari hasa wale wanaoishi mabondeni,” alisema Kabelwa. Kabelwa alisema mabadiliko hayo ya hali ya hewa hayajawahi kutokea katika miaka iliyopita na yamekuwa ni yakushangaza. Alisema kutokana na hali hiyo, taasisi zinazohusika na hali ya hewa Afrika (ICPAC) watakutana.
na Kanda ya Kusini mwa Afrika (SADC-CSC) kwa mara ya kwanza zitakutana kufanya uchambuzi wa mifumo ya hali ya hewa Desemba 5, mwaka huu.
“Novemba 5 hadi 13, mwaka huu mkutano utafanyika nchini Kenya na kumalizikia Zambia, baada ya mikutano ya kikanda kumalizika mamlaka yetu itatoa marejeo ya utabiri wa mvua kwa nchi nzima,” alisema Kabelwa.
Haba
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni