visit here again on mukebez.blogspot.com


CHANGE YOUR LIFE

CHANGE YOUR LIFE
Go to Amazon .com and get the copy of this book to make your life better.

Jumatano, 30 Aprili 2014

TAARIFA KWA UMMA

Wednesday, April 30, 2014
TAARIFA YA MABADILIKO YA ANUANI YA OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma inapenda kuwafahamisha wadau wake kuwa anuani yake imebadilika hivyo kuanzia sasa mawasiliano yafanyike kwa kutumia anuani ifuatayo;
OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA
UTUMISHI HOUSE
8 BARABARA YA KIVUKONI
11404 DAR ES SALAAM
au
PRESIDENT’S OFFICE, PUBLIC SERVICE MANAGEMENT
UTUMISHI HOUSE
8 KIVUKONI ROAD
11404 DAR ES SALAAM
Anuani hii inachukua nafasi ya Sanduku la Posta 2483, Dar es salaam. Hivyo, mawasiliano yote yazingatie anuani mpya.
Limetolewa na
Katibu Mkuu
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma
Barua pepe; permsec@utumishi.go.tz
CHANZO MICHUZI WEBSITE.

TAARIFA KWA UMMA

Wednesday, April 30, 2014
TAARIFA YA MABADILIKO YA ANUANI YA OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma inapenda kuwafahamisha wadau wake kuwa anuani yake imebadilika hivyo kuanzia sasa mawasiliano yafanyike kwa kutumia anuani ifuatayo;
OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA
UTUMISHI HOUSE
8 BARABARA YA KIVUKONI
11404 DAR ES SALAAM
au
PRESIDENT’S OFFICE, PUBLIC SERVICE MANAGEMENT
UTUMISHI HOUSE
8 KIVUKONI ROAD
11404 DAR ES SALAAM
Anuani hii inachukua nafasi ya Sanduku la Posta 2483, Dar es salaam. Hivyo, mawasiliano yote yazingatie anuani mpya.
Limetolewa na
Katibu Mkuu
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma
Barua pepe; permsec@utumishi.go.tz

Jumanne, 29 Aprili 2014

KUMBE WENYE VIBARI NDIO WANAUA TEMBO WETU!

Dar es Salaam.Ongezeko la kasi ya ujangili nchini limedaiwa kusababishwa na vitendo vya rushwa, matumizi mabaya ya madaraka na mfumo dhaifu wa usimamizi wa sheria katika Wizara ya Maliasili na Utalii.
Kwa mujibu wa ripoti iliyopewa jina la Urasimishaji wa Ujangili wa Kitaalamu Afrika, tangu mwaka 2000 wizara hiyo imejikuta katika kashfa za rushwa na kusababisha mawaziri na watendaji wakuu kuvuliwa nyadhifa zao.
Katika ripoti hiyo, Taasisi ya Kimarekani ya Utunzaji Wanyamapori ya Born Free USA kwa ushirikiano na Shirika la Ripoti za Kichambuzi na Takwimu la C4ADS, imeeleza pia jinsi vikundi vya waasi barani Afrika wanavyoendesha shughuli za ujangili.
Ripoti hiyo iliyozinduliwa mwezi huu nchini Kenya, inaitaja Tanzania kama kitovu cha kusafirisha pembe za ndovu katika ukanda wa Afrika Mashariki na Bandari ya Dar es Salaam imekuwa ikishindana na ile ya Mombasa katika kutumia bandari kibiashara.
Kutoka mwaka 2008 mpaka 2013, inaelezwa zaidi ya tani 20 za pembe za ndovu ama zilikamatwa zikisafirishwa kuingia au kutolewa katika Jiji la Dar es Salaam, hii ni kwa mujibu wa taarifa ya Taasisi ya C4ADS.
Ripoti hiyo inafafanua kuwa uchunguzi wa vinasaba (DNA), katika tani 11 za pembe za ndovu zilizokamatwa Taiwan, Japan na Hong Kong mwaka 2006, ilibainika kuwa pembe 1,500 zilitoka Tanzania (Selous).
Uchunguzi huo ulibaini kuwa vinasaba vya pembe hizo vilifanana, hivyo kujenga dhana kwamba baadhi ya watu wamekuwa wakiwinda katika hifadhi hiyo mara kwa mara katika utaratibu maalumu unaotambuliwa na Serikali.
“Kuna udhaifu mkubwa katika usimamizi wa uwindaji halali na wawindaji wenye vibali hawasimamiwi ipasavyo kufanya uwindaji kwa taratibu zilizowekwa kisheria. Hivyo hutumia nafasi hiyo kufanya vitendo vya ujangili,” inasema sehemu ya ripoti hiyo.
Serikali yakanusha
Hata hivyo, Mkurugenzi wa Wanyamapori, Paul Sarakikya alikanusha madai hayo akisema siyo kweli kwamba wawindaji halali huachwa bila usimamizi, bali wana mifumo ya kusimamia shughuli hiyo.
“Sikubaliani na ripoti hiyo, tumeshaongea sana juu ya suala hili, Rais alishalizungumzia na waziri pia. Ufafanuzi ndio huo, hamna ukweli wowote katika ripoti hiyo,” alisisitiza Sarakikya.
Salakikya alisema idadi ya tembo nchini inazidi kuongezeka katika hifadhi tofauti na upungufu unaoelezwa katika ripoti hiyo

GUADIOLA AUHARIBU MPIRA WA BAYANI,WAUONA MOTO KWA MADRID.

Tuesday, April 29, 2014
UEFA CHAMPIONS LEAGUE..LIVE MATCH: BAYERN MUNICH 0 vs REAL MADRID 4, (Agg 0-5) SERGIO RAMOS NA RONALDO WAWAZIMA BAYERN ALLIANZ ARENA!!
Real Madrid Usiku huu wameitawanya timu ya Bayern Munich bao 4-0 (Agg.5-0) na kwa matokeo hayo Real wanasonga mbele wakisubiri mshindi wa kesho jumatano kati ya Chelsea na Atletico Madrid. Bao za Real zimefungwa kipindi cha kwanza na cha pili. Dakika ya 16 kipindi cha kwanza Sergio Ramos anaifungia bao tamu la kichwa Real Madrid baada ya kupokea mpira uliopigwa na Luka Modric. Dakika ya 20 tena Sergio Ramos anafunga bao la pili na kufanya 2-0 dhidi ya Bayern na kwa kichwa tena baada ya kukwea kichwa hicho mpira uliopigwa na Pepe. (Agg: ni 0-3).
Dakika ya 34 C. Ronaldo anaifungia bao la tatu baada ya kupokea pasi kutoka kwa Bale!! Bao hilo la Ronaldo linaongeza Agg. kuwa 4-0. Dakika za lala salama Ronaldo anafunga bao la mwisho la nne na kufanya 4-0 huku Agg. Ikiwa ni 5-0 dhidi ya Bayern Munich
VIKOSI:
Bayern Munich:Neuer; Lahm, Dante, Boateng, Alaba; Schweinsteiger, Kroos; Ribery, Muller, Robben; Mandzukic
Subs:Raeder, van Buyten, Martínez, Rafinha, Pizarro, Gotze, Hojbjerg
Real Madrid:Casillas, Carvajal, Pepe, Ramos, Coentrao; Alonso, Modric; Di Maria, Ronaldo, Bale; Benzema
Subs:Diego Lopez, Varane, Marcelo, Casemiro, Morata, Isco, Illarra

ASKARI WA KUONGOZA MAGARI AVAA KIMINI.

Ripota wa TZA kutoka Kenya Julius Kipkoech ameamplify taarifa kutoka Kiambu Kenya ambapo hisia tofauti zimetolewa kuhusiana na picha ya askari wa kike wa usalama barabarani iliyofanya mabosi wake kumkemea.
Sababu kubwa ni picha ya Trafiki huyo aliyekua amevalia sketi fupi iliyombana huku akiongoza doria wakati wa mashindano ya magari katika kaunti ya kiambu ilisababisha picha iliyopigwa na mwanahabari wa gazeti moja nchini Kenya kuzua mjadala kwenye mitandao ya kijamii Redioni na Televisheni nchini Kenya.
Linda Okello ni afisa wa trafiki mwenye cheo cha koplo aliitwa ofisini na mkuu wa Trafiki kaunti ya kiambu James Mugeria na kumkemea vikali akitaja kwamba vazi hilo linakiuka maantiki ya kikazi katika kikosi cha polisi.
Baadhi ya watu waliotoa maoni yao kwenye mitandao ya kijamii wamesema Trafiki huyu alilengwa na wakuu wake bila kosa ikizingatiwa kwamba sare ama magwanda ya maafisa wa polisi hutolewa kwao na serikali na pia kumekua na madai kwamba Linda alikua amepewa uhamisho kaunti ya Mandera japo maafisa wakuu wa polisi wemekanusha madai hayo.
Haya yanajiri miezi kadhaa baada ya Naibu wa Inspekta mkuu wa polisi Grace kaindi kuwaonya vikali maafisa wa kike wa polisi dhidi ya kutumia lipstick, kuvalia mavazi ya kimtindo, bangili na vipuri virefu wakiwa kazini.
Kifupi taarifa kwa mafisa wa polisi iliyotolewa ilisema afisa yeyote atakayepatikana na mavazi yaliyopigwa marufuku atakua amevunja sheria Nambari 37 na sheria kwa maafisa wa polisi wa mwaka 2011 kipenge numbari 87-88 na atakabiliwa kisheria.

Jumatatu, 28 Aprili 2014

HEBU SOMA MKASA HUU WA MZEE ALIEKATWA NYETI KAMA ANAVYOSIMULIA MWENYEWE.

Mbeya. Aprili 19, Mzee London Haonga (61) alipatwa na tukio la kutisha kwa kukatwa sehemu zake za siri. Ni tukio la kusikitisha ambalo linadaiwa kufanywa na vijana wadogo.
Haonga alipatwa na masahibu hayo akiwa nyumbani kwake Kijiji cha Mapogolo wilayani Ileje. Majirani walisikia yowe kutoka kwa mzee huyo na kufika eneo la tukio, lakini walikuwa wamechelewa kwa kuwa wahalifu hao walikuwa tayari wameshatokomea na viungo vya siri kwa mzee huyo.
Hata hivyo, majirani hao walimbeba mzee huyo hadi Hospitali ya Wilaya ya Ileje ambako alihamishia Hospitali ya Rufaa Mbeya alikolazwa mpaka sasa.
Akizungumza na gazeti hili akiwa Wodi 1, Haonga anasema tukio hilo kwake lilikuwa la kinyama na ukatili kwani wahusika walimchinja bila huruma na kumsababishia maumivu makali ambayo yalisababisha apoteze fahamu.
“Ilikuwa Jumamosi saa 8.00 mchana alipokuja mjukuu wa kaka yangu nyumbani kwangu na kunieleza kuwa alitumwa kuja kuchukua dawa ya kizunguzungu. Nilimjibu kuwa sina dawa hiyo hapa ndani hadi niende kutafuta porini. Hivyo tukakubaliana kuwa atakuja jioni kuchukua dawa,” anasema mzee huyo ambaye ni mtaalamu wa dawa za asili.
Anasimulia kuwa ilipofika saa 2:30 usiku alifika kijana huyo na akampa dawa hiyo. Alipotaka kuondoka alimwomba amsindikize na akampa fimbo kwa ajili ya kujilinda njiani kwa kuwa nje kulikuwa na giza nene.
“Tulipotoka nyumbani, tukiwa mbali kidogo na nyumbani kwangu, ghafla akanifunika usoni na kofia aliyokuwa amevaa na kunikaba shingo huku akiniambia kuwa ‘Wewe mzee leo utaona,’ baadaye akaniangusha chini,” anasema.
Akisimulia huku akionyesha kujisikia maumivu makali, Haonga anasema baada ya kuanguka chini, aligundua kuwa mjukuu wake hakuwa peke yake.
“Walikuwa zaidi ya watu wawili kwa kuwa nikiwa nimezibwa uso na kofia na kukabwa shingo, mwingine alinimvua suruali,” anakumbuka.
Anasema kuwa baada ya muda mfupi alipoteza fahamu na alizinduka akiwa wodini Hospitali ya Rufaa na kuelezwa na wauguzi na madaktari kuwa sehemu zake za siri zimeondolewa na kubakia kidonda ambacho anaendelea kupatiwa matibabu.
Mzee Haonga anasema kuwa bado hali yake siyo nzuri kwani maumivu anayoyapata ni makali na kwamba maumivu mengine anayapata katika sehemu ya shingo na kifua.
Anasema kuwa nyumbani kwake anaishi peke yake katika kipindi cha miaka minne kutokana na kufiwa na wake zake wawili na kubakiwa na watoto ambao wote wanajitegemea, hivyo anaamini watu hao walitumia nafasi hiyo ya kumlaghai na kumfanyia unyama huo .
CHANZO:MWANANCHI.

GIROUD HAS NO STRESS OVER ARSENAL RESULTS!

Giroud: Fourth and the FA Cup would be a good season for Arsenal
Though the Gunners have seen their Premier League title challenge fall away, the striker would settle for Champions League qualification and an end to their trophy drought
By Dejan Kalinic
Apr 28, 2014 12:44:00 PM Arsenalstriker Olivier Giroudbelieves that an FA Cupwin and fourth-placed Premier Leaguefinish would be a "good season" for his team.
Arsene Wenger's men dropped out of the title race after a four-match winless run starting in late March and are fighting with Everton for the final Champions League spot but the Gunners enter an FA Cup final against Hull on May 17 as hot favourites, looking to end a nine-year trophy drought.
"If we finish fourth, we have not lost anything and it will be a good season. I think that, if we finish fourth, that will be a successful season and the FA Cup, if we win, would be a bonus," Giroud told the press. Source:goal.com

UTEKELEZAJI WA MABADILIKO YA MATUMIZI YA BARABARA DAR KUANZA LEO.

Dar es Salaam.Utekelezaji wa mabadiliko ya matumizi ya barabara katikati ya Jiji la Dar es Salaam unaanza leo na alama za kuonyesha njia hizo zimeshawekwa katika barabara zote zitakazohusika.
Mabadiliko makubwa yanafanywa katika Barabara za Samora na Sokoine. Barabara ya Samora sasa itakuwa inatoka badala ya kuingia katikati ya jiji kama ilivyokuwa na ile ya Sokoine itakuwa inaingia tu badala ya kuingia na kutoka katikati ya jiji.
Akizungumzia mabadiliko hayo Meneja wa Barabara za Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka (BRT), Mohamed Kuganda alisema kutakuwa na askari wa usalama barabarani katika maeneo hayo ili kuwaongoza watumiaji.
Kuganda alisema lengo la mabadiliko hayo ni kupunguza msongamano wa magari na kuwaandaa wananchi katika mabadiliko mengine madogo yatakayofuata baadaye mradi wa BRT utakapoanza kazi rasmi.
Mhandisi huyo alisema baada ya kukamilika kwa mradi wa mabasi yaendayo haraka, daladala zote zinazotumia Barabara ya Morogoro hazitaruhusiwa kufika katikati ya jiji, badala yake mabasi yaendayo haraka yatafanya kazi hiyo.
Mabasi yatumiayo barabara za Kilwa na Ali Hassan Mwinyi yataendelea kufika katikati ya jiji hata baada ya mradi wa BRT kukakamilika kwa sababu barabara hizo hazina mabasi yaendayo haraka.
“Pia, daladala zote zinazotoka Mnazi Mmoja kwenda Posta, hazitaruhusiwa tena kufika Posta Mpya, badala yake zitatumia Barabara ya Uhuru na kuishia kituo cha Stesheni na kurudi kupitia Barabara ya Samora,” alisema.
Meneja wa Malalamiko ya Waathirika wa Mabadiliko wa Wakala wa Usafiri wa Haraka (Dart), Deus Mutasingwa alisema Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (Dart), unashirikiana kwa karibu na wadau wengine kama Sumatra, Manispaa ya Ilala, trafiki na Wizara ya Ujenzi katika kuhakikisha shughuli hiyo inafanyika kwa ufanisi.
Mutasingwa alisema wanatarajia kupokea malalamiko mbalimbali kutoka kwa wananchi kwa sababu jambo hilo ni geni na litaonekana kuleta usumbufu.
Aliwataka watumiaji wote wa barabara kuwa makini katika kufuata alama za barabarani au mwongozo utakaotolewa.
Mabadiliko yaliyofanyika, pia yanahusisha mabasi yote yanayopita Barabara ya Kilwa ambayo yataishia Stesheni na kurudi kupitia njia hiyohiyo.
Mabasi yanayopita Barabara ya Nyerere na Uhuru yataishia Kituo cha Mnazi Mmoja na kurudi kupitia njia zao. Pia kutakuwa na mabasi yatakayoanzia Mnazi Mmoja kupitia Bibi Titi, Maktaba hadi Posta ya Zamani - Benki ya NBC na kurudi kupitia njia hiyohiyo. Mabasi yote yanayopita Barabara ya Ali Hassan Mwinyi kwenda katikati ya jiji yataishia katika Kituo cha YMCA Barabara ya Upanga na kurudi kupitia njia hiyo.
KUTOKA MWANANCHI.

Jumapili, 27 Aprili 2014

DIAMOND NA WEMA HAOO KUHAMIA MTWARA.

Monday, April 28, 2014
Diamond na Wema kuhamia Mtwara, kufanya shoo ya nguvu Mei 2, 2014 MAKONDE CLUB
Wakazi wa kusini mwa Tanzania yaani mkoa wa Mtwara wametakiwa kukaa mkao wa kula burudani ya nguvu ya muziki itapigwa moja kwa moja jukwaani siku ya tarehe 2 ya mwezi wa Mei katika ukumbi wa Makonde Club.
Shoo hiyo ya kipekee na ya aina yake italetwa na si mwingine bali ni mkali wa muziki wa bongo flava nchini anayepasua anga ya Afrika ya Mashariki kwa sasa kupitia vibao vyake vitamu kama vile cha My Number One remix alichomshirikisha msanii Davido kutoka nchini Nigeria, Raisi wa wasafi ama Diamond Platinumz”Asali ya warembo”kama mashabiki wake wanavyomwita.
Mwanamuziki Diamond atafanya shoo laivu mkoani Mtwara chini ya udhamini mkubwa wa kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania akisindikizwa na kipenzi chake, Malkia wa Bongo Movie nchini, Wema Sepetu – ‘Beautiful Onyinye’ au Madame kama mashabiki wake wanavyopenda kumwita.
Msanii Diamond ambaye kwa sasa ndiyo mwenye mafanikio makubwa ya kimuziki nchini amekuwa ni kivutio kikubwa kwa mashabiki wa ndani na nje ya nchi kila mahali anapoalikwa kufanya shoo na hivyo kujizolea sifa lukuki na hata kuchaguliwa kuwania tuzo mbali mbali za muziki barani Afrika.
Akizungumzia juu ya shoo hiyo ya kukata na shoka kwa wakazi wa mkoa wa Mtwara, Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Kelvin Twissa amebainisha kuwa tukio hili limeandaliwa ikiwa ni sehemu ya burudani kwa wateja wetu, kufurahi kwa pamoja na kuwashukuru wateja wetu kwa kuendelea kutumia huduma zetu.
“Hakuna kitu ambacho tunajali na kukithamini kama wateja wetu, haijalishi wawe kona gani ya Tanzania, walipo popote tutawafikia. Vodacom imekuwepo nchini kwa zaidi ya miaka kumi sasa na kwa kipindi chote hicho watanzania wameonyesha kutuunga mkono na kutufanya tuwe mtandao unaaongoza kwa mawasiliano nchini.” Alisema Twissa.
Kwa kuongezea Twissa amewataka wakazi na mashabiki wote wa Diamond na muziki wa Bongo Flava kujitokeza kwa wingi kwani mbali na burudani kutakuwepo na huduma na bidhaa mbali mbali za Vodacom.
Katika kunogesha shoo hiyo kwa wakazi wa kusini Malkia wa Bongo Movie nchini, Wema Sepetu naye akasema haitokuwa poa kama asipomsindikiza asali wake wa moyo kwenda kujivinjari pande hizo na mashabiki wao. Kwa tafsiri nyingine mashabiki wa Mtwara wanabahati kubwa ya kutembelewa na mastaa wawili wakubwa kutoka tasnia mbili tofauti nchini.
“Hii shoo si ya kukosa kabisa kwani hakuna kiingilio bali ni uwepo wako tu na kujiandaa kwako kwa burudani ndio kinachohitajika. Tunawapenda sana wateja wetu wa Mtwara, hatuna uwezo wa kulipa kutokana na kuwa wateja wetu waaminifu siku zote lakini ninaamini kwa pamoja tunaweza kujumuika na kufurahia wakati tulionao. Naombeni mjitokeze kwa wingi, rafiki amlete rafiki yake ili tuwe pamoja siku hiyo.” Alimalizia Twissa.

BAADA YA KUFUNGWA SERIKALI TATU JANA KOCHA WA TAIFA STARS AONGEZA WACHEZAJI HAWA KATIKA KIKOSI.

Kocha mpya wa Taifa Stars Mart Nooij ameongeza wachezaji tisa katika kikosi hicho kinachojiandaa kwa mechi ya kirafiki na timu ya Malawi(The Flames) ambayo itakachezwa Mei 4 mwaka huu katika Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
Wachezaji walioongezwa ni Edward Charles Manyama (JKT Ruvu),Elias Maguli (Ruvu Shooting), Hassan Dilunga (Yanga), Hussein Javu (Yanga), John Bocco (Azam), Kelvin Friday (Azam), Oscar Joshua (Yanga), Nadir Haroub (Yanga) na Shomari Kapombe (AC Cannes, Ufaransa).
Walioondolewa ni pamoja na beki Kelvin Yondani wa Yanga ambaye aliitwa awali na sababu za kuondolewa ni kushindwa kuripoti kambini,Taifa Stars inategemewa kuingia kambini kesho Aprili 28 jijini Mbeya kujiandaa kwa mechi dhidi ya Malawi.
Wakati huo huo, Tanzania (Taifa Stars) imepangiwa kucheza na Zimbabwe katika raundi ya pili ya mechi za mchujo kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Afrika (AFCON) zitakazofanyika mwakani nchini Morocco.
Kwa timu ya Taifa Stars itaanzia nyumbani ambapo mechi ya kwanza itachezwa kati ya Mei 16 na 18 wakati ile ya marudiano itachezwa Harare kati ya Mei 30 na Juni 1 mwaka huu.

WAZIRI AJIUZURU AKISEMA KUKAA OFISINI NI MZIGO.

Waziri mkuu nchini Korea Kusini amejiuzulu kutokana na vile serikali yake ilivyolichukulia swala lote la ferry iliozama siku kumi na moja zilizopita.
Chung Hong Won amesema kuwa kusalia afisini ni mzigo mkubwa kwake.
Bwana Chung alizomwa alipozitembelea familia za waathiriwa waliotoweka katika ferry hiyo ya Sewol,baada ya kuzama katika hali ya kutatanisha.
Takriban watu 200 wanadaiwa kufa maji katika tukio hilo huku zaidi ya mamia wengine wakiwa hawajulikani waliko,wengi wao wakiwa wanafunzi na walimu waliokuwa wakielekea katika ziara ya shule.
Wapiga mbizi bado wanaendelea kuwasaka waathiriwa chini ya ferry hiyo iliozama.
Ripoti za awali zimedai kuwa watu wote wametolewa katika boti hiyo.
CHANZO BBC.

BAADA YA RAIS KIKWETE KUWATAKA UKAWA KURUDI BUNGENI WAMEMJIBU HIVI..

SIKU moja baada ya Rais Jakaya Kikwete kuwataka wajumbe wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) warudi bungeni akidai hawana sababu ya kwenda kushitaki kwa wananchi kwa sababu watawacheka na kuwasikitikia, umoja huo umemjibu wakisema wapo tayari kuchekwa.
Akihutubia vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) juzi, siku moja kabla ya sherehe za miaka 50 ya muungano, Rais Kikwete alisema kuwa huko nje wanakotaka kwenda UKAWA siko na siku yake sio sasa, hivyo akawaomba wasipoteze fursa hiyo muhimu ya kutoa mawazo yao bungeni ili yafanyiwe kazi.
Alisema wananchi hawahusiki wala hawana namna ya kuwasaidia kwani mengi ya hayo yanayowakasirisha ni matatizo waliyoyazusha wao.
Mwenyekiti wa UKAWA, Freeman Mbowe, aliliambia Tanzania Daima Jumapili kuwa
kama Kikwete anafikiri kwamba watarudi bungeni kwenye mijadala ya dharau, ubaguzi na matusi inayofanywa na wajumbe wa CCM, basi hajui chimbuko la tatizo.
“Kadiri anavyoendelea kuliacha Bunge liendelee na mijadala ya kibaguzi na matusi, taifa linazidi kupasuka na washauri wake hawamwelezi tatizo hilo,” alisema.
Mbowe ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), alisema kuwa Rais Kikwete asipokuwa makini atalitumbukiza taifa kwenye machafuko ingawa yeye anafanya utani kwa kuipasua nchi na kushangilia kauli za kibaguzi, kejeli na matusi zinazotolewa na baadhi ya wajumbe wa CCM.
“Rais na wasaidizi wake inaelekea hawajasikiliza hata kauli zinazotolewa na viongozi wa dini kuhusu rasimu ya Warioba, atuache twende kwa wananchi, wao ndio wataamua. Tumevumilia kwa kiwango fulani, lakini itafika mahali uvumilivu utaisha, kwani hatuwezi kuendelea kuzuiliwa kufanya mikutano na jeshi la polisi wakati mikutano ya CCM inafanyika kote nchini kutuchafua,” alisema Mbowe.

ANGALIA JINSI BABA ALIVYOMUUA MTOTO WAKE KWA KUMTWANGA NGUMI,KATIKA TAARIFA HII YA POLISI MBEYA.

Sunday, April 27, 2014
TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LEO TAREHE 27.04.2014.
KATIKA TUKIO LA KWANZA:
MTOTO ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LAVANESA PATRICK NJOJO(03)MKAZI WA ISISI, WILAYANI MBARALI ALIUAWA KWA KUPIGWA NGUMI NA BABA YAKE MZAZI AITWAYEPATRICK NJOJO(23)MKAZI WA ISISI.
TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE26.04.2014MAJIRA YA SAA23:45USIKUHUKO KATIKA KIJIJI CHAISISI,KATA NA TARAFA YARUJEWA,WILAYA YA MBARALI, MKOA WA MBEYA. INADAIWA KUWA CHANZO CHA TUKIO HILI ULEVI WA POMBE ZA KIENYEJI WA BABA HUYO. MTUHUMIWA AMEKAMATWA, MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA WILAYA MBARALI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISIAHMED Z. MSANGIANATOA WITO KWA JAMII KUEPUKA ULEVI KWANI NI HATARI KWA AFYA ZAO NA UNA MADHARA KATIKA JAMII. AIDHA ANATOA WITO KWA WAZAZI/WALEZI KUWAFUNDISHA WATOTO WAO KWA UTARATIBU MZURI ILI KUEPUKA MATATIZO.
KATIKA TUKIO LA PILI:
MTOTO MWENYE UMRI WA MIAKA4 – 5ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LAFESTO MBIGA, MKAZI WA NSALAGA AMEFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA KUGONGWA NA GARI LENYE NAMBA ZA USAJILISM 9124AINA YAFAWLILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVARAMADHANI MWALYOYO (30)MKAZI WA ILOMBA JIJINI MBEYA.
TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE26.04.2014MAJIRA YA SAA14:45 MCHANAHUKO KATIKA KIJIJI CHA NSALAGA, KATA YA UYOLE, TARAFA YA IYUNGA, BARABARA KUU YA MBEYA/IRINGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA. CHANZO CHA AJALI KINACHUNGUZWA, MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA. MTUHUMIWA AMEKAMATWA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISIAHMED Z. MSANGIANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA NA KUFUATA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOEPUKIKA.
Signed by:
[A HMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

KANISA KATHOLIC KATIKA MCHAKATO WA KUWATANGAZA MAPAPA KUWA WATAKATIFU LEO.

Kanisa katoliki leo linategemea kuwatangaza watakatifu ambao huandikwa katika kitabu cha maisha ya watakatifu,Papa John Paul II na John XXIII wanatarajiwa kutangazwa watakatifu katika tukio litakaloongozwa na kiongozi mkuu wa kanisa Katoliki duniani Papa Francis huko St Peter’s Square jijini Vatican.
Watu milioni moja wanatarajiwa kuhudhuria tukio hili la kihistoria.

KANISA KATHILIC KATIKA MCHAKATO WA KUWATANGAZA MAPAPA KUWA WATAKATIFU LEO.

Kanisa katoliki leo linategemea kuwatangaza watakatifu ambao huandikwa katika kitabu cha maisha ya watakatifu,Papa John Paul II na John XXIII wanatarajiwa kutangazwa watakatifu katika tukio litakaloongozwa na kiongozi mkuu wa kanisa Katoliki duniani Papa Francis huko St Peter’s Square jijini Vatican.
Watu milioni moja wanatarajiwa kuhudhuria tukio hili la kihistoria.

Jumamosi, 26 Aprili 2014

MANCHESTER UNITED ULIKUWA MGOMO AU!MBONA MAMBO SAFI SASA BAADA YA MOYES KWENDA.

Ikiwa ni mechi ya kwanza toka Ryan Giggs achaguliwe kuchukua kwa muda nafasi ya David Moyes alietimuliwa, Manchester United imemiliki headlines kwa sauti kubwa baada ya ushindi mkubwa ilioupata leo April 26 2014.
Magoli ya Man U dhidi ya Norwich yalifungwa na Rooney kwenye dakika ya 41 kwa panati na dakika ya 48 huku mawili yaliyobaki yakifungwa na Mata kwenye dakika ya 63 na 73

WENGINE NI USHABIKI TU MUUNGANO!MUUNGANO WAKATI HAWAUJUI,HEBU ICHEKI HISTORIA YAKE VIZURI HAPA.

MUUNGANO
Mkataba wa Muungano ulitiwa saini na Mwalimu Julius Nyerere na Abeid Amani Karume, Aprili 22, 1964, Zanzibar.Ulithibitishwa na Bunge la Tanganyika na Baraza la Mapinduzi Aprili 26, 1964, na Aprili 27, 1964 viongozi hao walikutana katika ukumbi wa Karimjee, jijini Dar es Dalaam kubadilishana hati za Muungano.
Sheria za Muungano ilitamka kwamba, Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar zililazimika, kuwa dola ya Jamhuri kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, jina ambalo lilibadilishwa Oktoba 28, 1964 na kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kupitia sheria ya Jamhuri ya Muungano, sheria namba 61, ya mwaka 1964.
Msingi wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 na katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 ni Hati za Muungano za Mwaka 1964.
Hati za Muungano zilitiwa saini na Nyerere na Karume, Aprili 22, 1964 na hapo Tanganyika na Zanzibar kuwa dola moja kwa misngi inayotambulika kimataifa. Baada ya kuungana, Mwalimu Nyerere alikuwa rais wa kwanza na Karume alikuwa makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Aprili 26, 1964, bunge la Tanganyika lilipitisha sheria za Muungano, ambazo baadayezilithibitishwa na Baraza la Mapinduzi Zanzibar.
Mnamo Aprili 27, 1964 waasisi wa Muungano walibadilishana Hati za Muungano na wajumbe saba wa Baraza la Mapinduzi waliapishwa kuwa wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Watanganyika na Zanzibar ambao ni Amani Karume, Kassim Abdallah Hanga, Abdulrahman Babu, Hassan Nassor Moyo, Aboud Jumbe, Hasnu Makame na Idris Abdul Wakil. Kati yao, Aboud Jumbe na Hassan Nassor Moyo wangali hai.
Katiba ya muda ya mwaka 1965 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilianisha mambo 11 ambayo yalikubalika kuwa ni ya Muungano ambayo ni; Katiba na Serikali ya Muungano, Mambo ya nchi za nje, Ulinzi, Polisi, Mamlaka juu ya mambo yanayohusika na hali ya hatari, Uraia, Uhamiaji, Mikopo na Biashara za nje, Utumishi katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano, Kodi ya Mapato inayolipwa na watu binafsi na mashirika, ushuru wa forodha na ushuru wa bidhaa zinazotengenezwa Tanzania unaosimamiwa na idara ya forodha, Bandari, mambo yanayohusika na usafiri wa anga, posta na simu.
Katiba ya muda ya mwaka 1965 ilianisha utawala wa serikali ya mfumo wa chama kimoja, TANU kwa Bara na ASP kwa Zanzibar. Katiba hii, ilizingatia misingi ya makubaliano ya Muungano ya mwaka 1964 na sheria za Muungano wa Tangayika za Zanzibar.
Katiba hiyo ilianisha serikali mbili, uwakilishi wa Zanzibar katika bunge la Muungano ikiwa na mamlaka juu ya mambo yote ya Muungano na mambo yasiyo ya Muungano kwa upande wa Tanganyika. Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ikiwa na mamlaka juu ya mambo yote yasiyo ya Muungano yahusuyo Zanzibar.
Hata hivyo mambo ya Muungano yaliongezwa kutoka 11 hadi 22 kutokana na mahitaji ya ndani ya nchi pamoja na mabadiliko yaliyokuwa yanaendelea kutokea ulimwengini baada ya Muungano.
Mwaka 1985, jambo la 12 linalohusu sarafu na fedha kwa ajili ya malipo na kurahisisha usimamizi wa fedha za kigeni na benki katika Jamhuri ya Muunagno wa Tanzania, liliingizwa.
Kufuatia kuundwa kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki mwaka 1967, mambo matatu ya Muungano yaliyongezwa, ambayo ni leseni za viwanda na takwimu; elimu ya juu; na usafirishaji wa anga.
Mwaka 1968, mambo ya maliasili ya mafuta, pamoja na mafuta yasiyochujwa ya magari na ama ya petroli na aina nyingine za mafuta au bidhaa na gesi asilia yaliyongezwa kwenye orodha hiyo.
Aidha mambo ya Muungano yaliendelea kuongezeka hadi kufikia 21 kufuatia kuvunjika kwa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Mwaka 1992 kufuatia mabadiliko ya mfumo wa siasa nchini suala la 22 la uandikishaji wa vyama vya siasa na mambo mengine yanayohusiana navyo liliongezwa kwenye orodha hiyo.
MJADALA KUHUSU MUUNGANO
Katika miaka hivi karibuni kumekuwa na mijadala mbalimbali kuhusiana na muundo wa Muungano, baadhi wakitaka uwe wa zaidi ya serikali mbili, wengine serikali moja, wapo wanaotaka Tanganyika iwe kivyake na Zanzibar kivyake.
Hata hivyo hekima inaonyesha kwamba Muungano wa Tanganyika na Zanzibar unabaki kuwa ni fahari ya Watanzania, kwani mwelekeo wa dunia katika nyanja mbalimbali, mataifa kuungana kwa ushirikiano wa aina mbalimbali ni muhimu kuliko taifa moja kupambana kivyake.
Urejeaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki baada ya kuvunjika mwaka 1977, uwepo wa SADC, ECOWAS, COMESA, na jumuiya nyingine nyingi duniani kote, ni vielelezo kwamba ushirikiano baina ya mataifa ni suala lisilohitaji mjadala.
Ieleweke kwamba hakuna ushirikiano usio kuwa na matatizo kama ilivyo kwa Muungano wa Tanzania, vivyo hivyo muungano mwingine kama vile ya United Kingdom (UK), Uingereza na United States of America (USA) kwa maana ya Marekani na United Arabs Emirate (UAE), nayo ina matatizo, lakini hata mara moja mjadala juu ya matatizo hayo siyo kuvunja ushirikiano bali kutatua na wale wanaotaka kuvunja hushughulikiwa ipasavyo.
"Matatizo ya Muungano kama wa UK ni mabaya zaidi, na hata UAE hawana ahueni, ila wanajua kwamba Muungano wao ni lazima. Wamarekani wanapambana na watu wenye mawazo haya ya kuvunja miungano kwenye majimbo ya Alaska, Hawaii na Texas na mwishowe wameamua kuweka kambi kubwa ya jeshi la nchi kavu Texas; utitiri wa kambi za anga Alaska; na vituo vikubwa kupindukia vya majini kule Hawaii. Hivi, hawa mabingwa wa demokrasia wanapoamua kulinda nchi yao namna hii, unafikiri ni wajinga? Walimwaga damu na waliyanunua majimbo haya na wamepitia shida kubwa, ndiyo maana leo wanajidai," anaandika mchangiaji katika mjadala kuhusu Muungano.
Ni vyema Watanzania wakati huu wa kusheherekea miaka 49 ya Muungano, kila mmoja akajisikia ufahari wa kuwa na kitu kizuri kilichoasisiwa na Waafrika wenyewe na kudumu kwa umri huo. Mawazo ya kubaguana kwa sababu zisizo na msingi, pengine kukidhi matakwa na wakati kama vile ya kibinafsi na kisiasa, yasipewe nafasi kuisambaratisha nchi. Chambilecho wahenga, umoja ni nguvu utengano ni udhaifu.MUUNGANO! KWA HAKIKA NI MADE IN TANZANIA!

INAKUWAJE UNASABABISHA KIFO CHA MMEO.

Mbaroni kwa kumuua mumewe
MKAZI wa Kata ya Kisemvule, Tarafa ya Vikindu, wilayani Mkuranga, Husna Kisoma (16), anashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani kwa tuhuma za kusababisha mauaji ya mumewe.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Kamishina Msaidizi Mwandamizi (SACP) Ulrich Matei, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na amemtaja marehemu kuwa ni Jumanne Mwarami (21).
Tukio hilo limetokea juzi usiku na linadaiwa kusababishwa na wivu wa mapenzi baada ya marehemu kuibua ugomvi kati yake na mkewe akimtuhumu kuwa si muaminifu katika ndoa yao.
Katika ugomvi huo Husna alimvuta mumewe sehemu zake za siri, hali iliyosababisha kupoteza maisha alipokuwa akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Wilaya ya Mkuranga.

KWELI PALIPO NA WAKUBWA HAPAHARIBIKI JAMBO.KINGUNGE ADHIHIRISHA UTU UZIMA WAKE.

MWANASIASA mkongwe na Mjumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, Kingunge Ngombale – Mwiru, amesema makada wenzake wanaomshambulia aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba, wanakitukana Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Alisema kumtukana au kumshambulia Jaji Warioba, au wajumbe wengine wa tume hiyo ni sawa na kukitukana Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinachoongoza serikali.
Kingunge alitoa kauli hiyo jana bungeni alipokuwa akichangia sura ya kwanza na ya sita ya rasimu ya Katiba, ambapo alisema wanaomshambulia Jaji Warioba wanaonyesha utovu wa adabu, kwa kuwa chama kina maadili na adabu katika kushughulikia masuala mbalimbali.
“Mimi sitakubali hata kidogo wajumbe watumie msimamo wa chama kumshambulia Warioba au wajumbe wengine wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, si halali kumshambulia Warioba au mjumbe yeyote yule binafsi.
“Mimi ni Mwana CCM niliyeondoka madarakani siku nyingi lakini naamini kuwa kumtukana mwenzetu ni sawa na kukitukana chama na sisi tuliopo hapa, wanaomshambulia Warioba wanakosea sana, hapa tuna rasimu ya Katiba ambayo ina mawazo tu, hakuna watu ndani ya rasimu hiyo, hatupaswi kukiuka maadili kwa kuwatukana au kuwakashifu watu,” alisema.
Alisema kilichomo ndani ya rasimu ya Katiba si uamuzi wa mwisho, hivyo wajumbe hawana sababu ya kumsema, kumtukana au kumkejeli mtu yeyote aliyekuwa kwenye Tume ya Mabadiliko ya Katiba.
Kingunge pia alitumia fursa hiyo kukemea lugha za matusi, vijembe na kejeli zilizokuwa zikitolewa na baadhi ya wajumbe kwenye mijadala mbalimbali.
“Hatuwezi kukaa hapa ndani kwa kudhalilishana, wale waliokuwa wakitumia lugha hizo walikuwa wanatudhalilisha wote. Wengine walitumia lugha hizo kwa waasisi wetu…Unyenyekevu ni sura moja ya msomi ambaye ametumia fedha za Watanzania kupata elimu yake,” alisema.
Alisema wajumbe wamekwenda bungeni kuwatafutia wananchi wenzeo Katiba mpya, iliyo bora na lazima izingatie miaka 50 ya muungano ambao umekuwa na mafanikio makubwa.
“Katiba bora lazima iimarishe yale mafanikio tuliyoyapata katika kipindi hicho ikiwemo muungano, umoja wa kitaifa, mshikamano, udugu na kuunda mazingira ya amani na utulivu, kama haiimarishi, haifai hata kidogo. Haya mafanikio yote yametokana na muundo wa serikali mbili ulioasisiwa na wazee wetu,” alisema.
Hakuna Katiba bila UKAWA
Kingunge alisema kuwa ili Tanzania ipate Katiba mpya iliyo bora, lazima kuwepo maelewano ya kuwashirikisha wajumbe wa Bunge hilo wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA).
Alisema kitendo cha wajumbe wa UKAWA kususia vikao vya Bunge, kinaonyesha upungufu mkubwa walionao lakini Katiba mpya haitaweza kupatikana bila ya wao.
Kingunge aliwaomba wajumbe wa UKAWA warejee bungeni kushiriki kikamilifu katika mchakato wa kuandaa Katiba ya wananchi.
Alisema hata UKAWA wakirejea bungeni ni vema wajumbe wakatambua kuwa kupatikana kwa Katiba mpya kunahitaji maridhiano ya pande hizo mbili.
“Hatuwezi kupata theluthi mbili ya kura hasa kwa wajumbe wa kutoka Zanzibar watakaohalalisha maamuzi yetu bila kushirikiana na wenzetu, lazima tuzungumze, theluthi mbili ni takwa la kisheria, hatuwezi kulikwepa,” alisema.
Kingunge alisema kwa muda mrefu Zanzibar kulikuwa na mfarakano mkubwa kati ya CCM na CUF lakini yalifanyika mazungumzo yaliyodumu kwa takriban miaka 13.
“Tumezungumza kwa muda mrefu tangu 1998 lakini hatimaye tulibuni suala la kugawana madaraka…katika hali ya Zanzibar tulisema haiwezekani lazima tukubaliane, sasa Zanzibar imetulia. Ni kutokana na mazungumzo hayo.
“Suala la Katiba mpya si utani ni lazima tukubali tuzungumze mpaka tuelewane….humu ndani sisi wajumbe tuzungumze lakini na wakubwa huko nje nao ni lazima wazungumze,” alisema.
UKAWA waliteka Bunge
Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Makamu wa Pili wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi Seif Alli Idd, wamewataka wajumbe wa UKAWA wabatilishe uamuzi wa kususia vikao vya Bunge Maalumu.
Kauli hizo walizitoa jana walipokuwa wakichangia sura ya kwanza na ya sita za rasimu ya Katiba, ambapo walisema Katiba inayotungwa ni ya Watanzania wote, hivyo ni vema UKAWA wakarejea bungeni.
Balozi Iddi alisema taifa limetumia fedha nyingi kugharimia ujenzi wa Bunge Maalumu pamoja na kuwagharimia posho wajumbe wake ambapo mpaka jana lilitumia zaidi ya sh bilioni 20, hivyo si busara kwa UKAWA kususia vikao.
Alisema UKAWA ni sehemu muhimu katika utungaji wa Katiba na wajumbe wake wametumwa na wananchi ambao wanataka matatizo yao yawekewe utaratibu wa kushughulikiwa kwenye Katiba.
Alisema kutokana na umuhimu wa kutunga Katiba, Rais Jakaya Kikwete, amekubali kuliongezea muda wa siku 60 zaidi Bunge hilo ambalo jana limeahirishwa hadi Agosti 5, mwaka huu.
Alisema kuongezewa siku huko kumetokana na kutokamilisha kazi yake kwa siku 70 zilizopangwa awali ambazo zimemalizika jana hivyo UKAWA wanapaswa kutambua unyeti wa vikao vya bunge na umuhimu wao.
“Pamoja na serikali kutumia fedha nyingi kutengeneza ukumbi na kulipana posho UKAWA wameamua kususia vikao vya Bunge. Nawasihi warudi tuendelee na kazi hii tuliyopewa na wananchi. Katiba haitungwi barabarani au kwenye mikutano ya hadhara bali bungeni.
“Nawasihi warejee bungeni tuifanye kazi hii tuliyotumwa na wananchi, tumetumia fedha nyingi na tutaendelea kutumia, kila mmoja wetu analipwa sh 300,000 kwa siku na serikali inatumia sh milioni 188 kwa siku kulipa posho.”
Naye Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, alisema anaamini katika umoja, hivyo kukosekana kwa wajumbe wa UKAWA ndani ya Bunge kumemsikitisha lakini ataendeleza jitihada za mazungumzo nao.
Pinda ametoa rai hiyo wakati ni takriban wiki moja imepita tangu alipokaririwa akitamba kuwa wanawafuata UKAWA huko huko kwa wananchi kwenda kusema ukweli.
Pinda aliwasihi wajumbe wa UKAWA warejee bungeni huku akiwasihi wajumbe wengine wajiepushe na lugha za kejeli na vijembe ambazo alidai zimechangia mijadala kuwa katika mazingira magumu.
‘Mimi kila siku huwa nasema kuwa yaliyopita si ndwele…tugange yajayo, naomba wenzetu UKAWA warejee bungeni, Katiba mpya inahitaji ushirikiano wetu sote,” alisema.
Pinda pia alisema Tume ya Jaji Warioba imefanya kazi nzuri kwa kuwa yapo mambo mengi ambayo hayamo kwenye Katiba ya sasa lakini yameorodhoshwa kwenye Rasimu ya Katiba.
Alibainisha kuwa anapingana na rasimu hiyo katika eneo moja la muundo wa serikali tatu kwa kuwa anaamini ni mzigo mkubwa kwa taifa na litachangia kuvunja muungano.
Alisema kuwa wanaosema kuwa kutofuata mapendekezo ya tume ya Warioba kwa kuwa imetumia fedha nyingi, wanakosea kwani wajumbe wa Bunge Maalumu wamepewa fursa ya kuondoa, kuboresha na kuingiza mawazo wanayoona yanafaa kuwemo kwenye Katiba mpya.
Naye Mwenyekiti wa Bunge Maalumu, Samuel Sitta, alisema kiti chake kiliamua kuwaacha wajumbe wajadili kwa uhuru zaidi na wananchi waamue kipi kinafaa.
‘Huko mitaani tunalaumiwa kwa kuwaachia wajumbe, sisi tulifanya hivyo pasipo kutumia nguvu, kanuni au askari ili wananchi wajue tabia za wajumbe wao na kuamua, tungebanana sana najua lazima tungepigana na kutoana ngeu,” alisema.

Ijumaa, 25 Aprili 2014

KINGUNGE AWATAKA WAJUMBE WA BUNGE LA KATIBA KUUFYATA JUU YA WARIOBA.

Dodoma.Wajumbe wa Bunge Maalum wametakiwa waache kumsakama aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Mstaafu Joseph Warioba na timu yake, kwani maoni alowasilisha si yake, bali ni ya wananchi.
Rai hiyo imetolewa Bungeni hapa leo na Mwanasiasa Mkongwe, Mzee Kingunge Ngombale-Mwiru wakati akitathmini mwenendo wa Bunge hilo katika mjadala wa Rasimu ya Pili ya Katiba.
Mzee Ngombale-Mwiru amewatahadharisha wajumbe wasivuke mipaka, akiwaeleza hawakwenda Dodoma kuipiga vijembe timu ya Warioba, bali wana wajibu wa kuhakiki na kuboresha Rasimu ya Katiba Mpya.
“Kero ya wananchi kubwa kabisa ni kero ya umasikini,” amekumbusha Kingunge, akiliambia Bunge kuwa wana wajibu wa kuhakikisha Katiba wanayoandika inaakisi matatizo haya na inazungumzia “hatma ya wananchi.”
Huku hayo yakiendelea, Waziri Mkuu Mizengo Pinda amewataka wajumbe wa Ukawa walosusia vikao warejee Bungeni hapa, na wamalize tofauti zao ili Katiba ya Wananchi ipatikane.
Bunge hilo limeahirishwa hadi Agosti 05 mwaka huu, litakapokutana tena mjini hapa kwa miezi miwili ili kuhitimisha kazi waliyoianza ya kuandaa Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania.

KWELI WAKENYA WALIBUGI!ANGALIA SHERIA YA KUWAABUDU VIONGOZI INAYOTUNGWA SASA HIVI

Sheria mpya inatengenezwa Kenya sheria hiyo itawataka wanaowazungumzia wakuu wa serikali kufanya mazoezi ya kutosha kwani sheria hii ikipitishwa basi inamaana kwamba Rais,Naibu wake na wake zao pekee ndiyo watakao pewa jina Mtukufu au His/Her Excellency.
Unaambiwa yeyote atakaye kosa kuzingatia hilo adhabu yake atafungwa mwaka mmoja Gerezani au kutozwa faini ya shilingi milioni moja pesa za Kenya sawa na dola elfu 12 za Marekani.
Yeyote atakaye vunja sheria ya kukosa kumuita Mbunge kwenye bunge la kitaifa Mheshimiwa au Honorable atafungwa mwaka mmoja au faini ya shilingi milioni mbili pesa za Kenya.
Kwenye mpangilio Rasmi wa Itifaki ama pecking order Rais atafatiwa na Naibu wake kisha Spiker wa bunge la taifa,Jaji mkuu,Seneta,Mbunge wa Jimbo na wa mwisho ni Gavana.
Sheria hiyo pia inapendekeza kwamba spika wa bunge la taifa kuitwa Right honourable ama Mheshimiwa mkuu na Jaji mkuu kuitwa his/herloadship,itakua kosa vile vile kumuita mwakilishi wa Jimbo Mheshimiwa hilo ni jina la Mbunge wa Bunge la Taifa peke yake.
Muswada huo uliotungwa na kuwasilishwa Bungeni na Mbunge Mheshimiwa Aden keynan anaye sema kwamba sheria hiyo itasaidia kutoa mpangilio wa vyeo kwa Taifa pia anapendekeza kwamba watumishi wa umma watakao jilimbikizia vyeo watatozwa faini ya Dola milioni mbili.
Mswada huo unajadiliwa Bungeni wakati magavana serikali ya kitaifa, wabunge na mahakama wako kwenye vita vya kubaini ni nani anauwezo wa kutekeleza majukumu na mamlaka ya kutoa muelekeo kwenye maswala mbali mbali yanayo husu usimamizi.

Alhamisi, 24 Aprili 2014

SOMA MAGAAZETI YA LEO HAPA.


DU!ANGALIA IDADI YA WATOTO WALIORAWITIWA TANZANIA MWAKA 2013

Ripoti ya kituo cha sheria na haki za binadamu nchini Tanzania imesema watoto wapatao 800 walilawitiwa mwaka 2013.Ripoti ya shirika hilo inasema kwamba kumekuwa na ongezeko kubwa la vitendo vya ukatili kwa wanawake na watoto nchini Tanzania ambapo kumi kati yao wakiwa wamefanyiwa ukatili huo na wazazi wao wenyewe.
Akiongea na BBC mkurugenzi mtendaji wa taasisi hiyo Dr Helen Kijo-Bisimba amesema watoto wamekuwa katika maisha ya hatari zaidi nchini humo kutokana na watu wa karibu wakiwemo wazazi wa kiume na hata kaka na wajomba zao kubainika wanawafanyia vitendo vya ubakaji.
Pia utafiti huo umeonyesha kuwa watu zaidi ya 1600 wakiwemo askari polisi wanane, waliuawa na wananchi wenye hasira kali katika matukio tofauti huku askari polisi nao waliwaua raia 28 katika kipindi cha mwaka 2013.
Bbc swahili.

SIMU GHARI ZAIDI KULIKO ZOTE DUNIANI 2014


HII NDIO NAMBA MOJA INAITWA IPHONE5 BLACK DIAMOND INAUZWA DOLA 15.3 MILLION.

WATU WENYE SURA MBAYA KULIKO WOTE DUNIANI. #THE AGLIEST PEOPLE IN THE WORLD#


Mimi siamini swala la ubaya au uzuri lakini angalia picha za watu wanaosadikika kuwa ndio wanasura mbaya zaidi kuliko wote duniani,sitawataja majina kwasababu za maadili.