Baadhi ya wanasiasa waliofika kupigania kata hiyo ni pamoja na wale wa CIVIC UNITED FRONT(CUF) Wakiongozwa na kiongozi wao ambae ni katibu wa chama hicho taifa maalim Seif Sharif Hamad,Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi wakiongozwa na katibu wao mwenezi bwana Nape Nnauye pamoja na wale wa Chama Cha Demoklasia na maendelea(CHADEMA).
Kata hiyo ya Magomeni inafanya uchaguzi wake mala baada ya aliekuwa diwani wa kata hiyo kuiaga dunia ghafla mwishoni mwa mwaka jana na hivyo nafasi yake ya udiwani kubaki wazi.
Nao wananchi waliohudhuria kampeni hiyo walisema kuwa wanahudhuria kwa wingi katika kampeni hizo ili kusikiliza sera za wagombea na hatimae kuchagua diwani wao kulingana na sera zake na sio chama chake.
Walisema wanasiasa wa sasa wamekuwa na tabia ya kuwadanganya wananchi wakati wa kampeni lakini mwisho wa siku hawatekelezi ahadi zao.
NAPE NNAUYE AKIONGEA NENOWANANCHI WAKISIKILIZA KWA MAKINI
WANANCHI WAKIWA MAKINI KUSIKILIZAMSIFANYE MAKOSA
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni