Msigwa alisema hayo wakati akiwasilisha taarifa ya kambi ya upinzani katika uwasilishaji wa hotuba ya makadilio ya mapato na matumizi ya wizara ya maliasili na utalii bungeni Dodoma jioni ya leo.
Pamoja na hayo, pia Msigwa alizituhumu kampuni mbalimbali zinazojihusisha na maswala ya utalii na uwindaji kuwa ndio yamekuwa yakufanya ujangiri wa hali ya juu kwa wanyama katika mbuga mbalimbali nchini na hivyo kuongoza katika uvunjifu wa sheria za nchi.
Katika kukazia hilo Mh.Msigwa aliweka CD mezani yenye ushahidi wa jinsi moja kati ya kampuni za uwindaji, zinavyokiuka sheria za uwindaji kwa wanyama.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni