Kurasa

Ijumaa, 30 Mei 2014

MASKINI:PIGO JINGINE BONGO MUVIE,MSANII MWINGINE AFARIKI DUNIA BAADA YA RACHEL NA KUAMBIANA

Kwenye watu ambao wana mkono mkubwa kwenye filamu Tanzania basi na huyu ni miongoni mwao, amehusika kwenye movie nyingi sana zikiwemo za mke wake ambae ni mwigizaji Monalisa kama ile ya ‘Girlfriend’ aliyocheza na kina GK, T.I.D Ay na wengine miaka hiyo.
Screen Shot 2014-05-31 at 1.02.00 AMKuanzia saa tatu usiku wa May 30 2014 zilianza kusambaa taarifa kwamba Director George Tyson amefariki dunia ila sasa ndio zimethibitika kuwa ni rasmi ambapo Mwigizaji Wema Sepetu na mtangazaji Zamaradi Mketema ni miongoni mwa waliopata uthibitisho.
Wakati inaendelea kufatilia chanzo na mengine kwa ujumla kuhusu hizi taarifa Wema Sepetu ameandika ‘Kwa mara ya tatu bila kupumzika week tunamzika mwenzetu mwingine George Tyson dah.. sina cha kuongea, RIP Brother, Daah sijui Da Mboni wangu ana hali gani aisee…. pole dada akee Mungu akupe nguvu wewe pamoja na team yote ya The Mboni show, pigo kubwa tena kwa wasanii, tunaisha tu jamani.

MALAWI YAPATA RAIS MPYA

Peter Muthirika anayeongoza chama cha DPP ndiye rais mteule nchini Malawi
Hatimaye Malawi imepata Rais mpya baada ya mivutano ya kisheria kwa wiki nzima.
Mwandishi wetu amesema kutoka mjini Blantyre kuwa Profesa Peter Mutharika ameshinda uchaguzi huo kwa kupata asilimia 36.4 ya kura zote akifuatiwa na Dr Lazarus Chakwera mwenye asilimia 27.8 huku Rais anayemaliza muda wake Dr Joyce Banda akishika nafasi ya tatu kwa asilimia 20.2 na Atupele Muluzi amekuwa wa nne na asilimia 13.7
Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Jaji Mackson Mbendera amesema uchaguzi huo ulikumbwa na changamoto nyingi lakini mwishowe nchi ni lazima ipate kiongozi wake na kuwaomba wananchi kuwa na utulivu .
Kesi Mahakamani
Awali Jaji Kenyata Nyirenda wa mahakama kuu mjini humo jana usiku alitoa uamuzi kuwa hawezi kuvunja sheria kwa kuruhusu tume iongeze muda wa kuhesabu upya kura kwenye maeneo yenye utata.
Na kwamba sheria inaitaka tume kutangaza matokeo ndani ya siku nane na si vinginevyo.
Uchaguzi wa Malawi ulifanyika Mei 20 nchini kote lakini siku moja tu baada ya kupiga kura, malalamiko yakiambatana na mapingamizi ya kisheria yakatawala kwenye mahakama kuu za Lilongwe na Blantyre.

MTUHUMIWA WA UBAKAJI AMBAKA MWANAMKE MWINGINE MAHAKAMANI

Hii ni stori nyingine tena ya 2014 ambayo inaingia kwenye list ya zile stori ambazo ukishaisoma au kuipata unaanza kufikiria mara mbilimbili na kujaribu pia kutengeneza picha yako mwenyewe kama upo eneo la tukio.
Watu wa karibu wa Mtuhumiwa huyu walijitokeza Mahakamani ili kuangalia kama ndugu yao aitwae Simon Ngozi (21) ataweza kupata dhamana kwenye kesi inayomkabili ya kubaka mtoto wa miaka tisa.
Imetokea Kenya ambapo jamaa alikua amepelekwa Mahakamani Makadara Nairobi lakini ghafla akamshangaza kila mtu baada ya kutaka kumaka Mwanamke aliekua karibu yake baada ya kuanza kumshikashika.
Screen Shot 2014-05-31 at 2.41.44 AM
Nje ya Mahakama ya Italia
Mshukiwa huyu alikuwa kortini kujibu tuhuma za kumbaka mtoto wa miaka tisa April 2014 ambapo wakati anataka kumbaka Mwanamke huyu Mahakamani tena kwenye eneo la wazi, alimpiga mtama kwanza Mwanamke huyo lakini kwenye purukushani zake hakufanikiwa manake Polisi walimuwahi.
Shughuli za Mahakama zilisimama kwa muda baada ya tukio hilo kutokea ambapo baada ya hapo Mwanamke alietaka kubakwa alisema ‘nilikua nimeketi karibu naye na mara ya kwanza alilishika begi langu nikalisogeza mbali nikidhani ni mwizi lakini bila aibu akanishikashika tumboni kabla ya kunisukuma nikaanguka sakafuni
Baada ya hapo dada wa mtuhumiwa alimuomba mwanamke huyo kumsamehe ndugu yake akisema yuko katika hali hiyo baada ya mchumba wake kumtoroka kwa sababu ya kesi ya ubakaji.
Screen Shot 2014-05-31 at 2.41.21 AM
Tukio la Mwanza
Hili linakua tukio jingine mimi kulisikia mwaka 2014 la kituko Mahakamani baada ya mawili ya Mwanza ambapo moja ni Mahabusu kujipaka kinyesi na kujaribu kutoroka akidhani hiyo mbinu itasaidia mtu asimshike, mwingine ni alievua nguo zote kushinikiza atendewe haki kwa kisa cha mauji alichobambikiwa.
Kituko kingine ambacho kilivunja rekodi kabisa ni cha Wafanyakazi wawili wa Mahakama nchini Italia kufanya Hakimu kuahirisha kesi baada ya wawili hao kuonekana wakifanya mapenzi kwenye chumba cha pili pembeni ya chumba kilichokua kinaendeshewa kesi.
Tza

Alhamisi, 29 Mei 2014

ZITO ATUHUMIWA Inaendelea kutoka uk 1

Mbilinyi alizihusisha Sh12.2 milioni za Hifadhi ya Taifa ya Saadan na maandalizi ya filamu fupi ya kuhamamisha shughuli za utalii wa hifadhi kwa kuwatumia wasanii kutoka mkoani Kigoma na kusisitiza kuwa wana nakala ya mkataba huo.
Alisema ofisi ya kampuni ya Gombe Advisors zipo jengo moja na zilipo ofisi za Kampuni ya Leka Dutigite na kusisitiza kuwa nyaraka walizo nazo zinaonyesha kuwa Zitto na Raphael Ongangi ndiyo wakurugenzi, huku Zitto akitajwa kuwa mchumi katika kampuni hiyo.
“Zitto siyo mchumi kama ambavyo zinaeleza nyakara za usajili wa kampuni hiyo. Ni mbunge na kiongozi na kwa mujibu wa sheria viongozi wanatakiwa kuwa waadilifu, wenye huruma, utulivu na umakini,” alisema Mbilinyi.
Aliongeza: “Kwa kadri ya ufahamu wa Kambi Rasmi ya Upinzani ya Bunge lako tukufu, Zitto hajawahi kutangaza masilahi aliyonayo kwenye mikataba ya Gombe Advisors na Leka Dutigite.”
Alisema Zitto kwa kampuni hizo mbili amefanya biashara na mashirika yanayosimamiwa na kamati yake na kulipwa fedha za umma.
“Kambi Rasmi ya Upinzani inaitaka Serikali kutoa maelezo kwa kuwa suala hili linahusu mbunge na mwenyekiti wa Kamati ya Bunge inayohusika na usimamizi wa fedha za umma,” alisema.
Alifafanua kuwa Kamati ya Kinga, Haki na Madaraka ya Bunge nayo ifanye uchunguzi wake juu ya madai ya masharti ya Katiba ya Nchi, Sheria ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge na Kanuni za Bunge juu ya maadili ya kiongozi wa umma, yakiwamo yanayohusu utangazaji wa masilahi.
Zitto ajibu mapigo
Hata hivyo, Zitto mwenyewe alipohojiwa jana, alijibu kwa ujumbe mfupi wa maandishi (sms) akisema amesikitishwa na kitendo cha kuingizwa katika siasa za majitaka katika kipindi hiki akimuuguza mama yake.
“Kampuni ya Leka Dutigile inamilikiwa na wasanii na Gombe Advisors ni kampuni isiyofanya faida na haina masilahi yoyote ya kiabiashara,” alisema.
“Wasanii wa Kigoma wamefanya kazi na Tanapa na NSSF kazi ambazo zipo na zinajulikana,” alisema Zitto aliyekuwa naibu kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani bungeni kabla ya kuondolewa.
“Kwa namna yoyote, hii ni ishara ya kukosa ubinadamu maana waliyoyasema wanajua sina faida yeyote ya kifedha, leo wala kesho na Leka Dugitile na Gombe Advisors,” alisisitiza Zitto.

ZITO ATUHUMIWA NA NDUGU ZAKE KWA WIZI WA FEDHA ZA UMMA

Dodoma.Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni jana ilimlipua mbunge kutoka kambi yao, Zitto Kabwe ikimhusisha na ufisadi wa Sh119 milioni kutoka Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) na Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa).
Hii ni mara ya kwanza kwa kambi ya upinzani kumhusiaha mbunge ‘mwenzao’ na tuhuma za ufisadi tofauti na kawaida yao ya ‘kuwashughulikia’ ubadhirifu katika Serikali.
Zitto, mbunge wa Kigoma Kaskazini kwa tiketi ya Chadema na ambaye pia ni mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), anadaiwa kuchota fedha hizo kupitia kampuni ya Leka Dutigite ambayo ina hisa nyingi katika kampuni nyingine ya Gombe Advisors Limited ambayo Zitto ni mkurugenzi wake.
Akiwasilisha maoni ya upinzani bungeni jana kuhusu makadirio na matumizi ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo mwaka 2014/15, waziri kivuli wa wizara hiyo, Joseph Mbilinyi alisema Zitto hakutakiwa kuchota fedha hizo kwa kuwa anabanwa na sheria ya maadili ya viongozi wa umma.
Alisema Zitto, ambaye katika miezi ya karibuni aliingia kwenye mgogoro na uongozi wa chama chake, ni mwenyekiti wa PAC, kamati ambayo jukumu lake ni kushughulikia maeneo yenye matatizo sugu ya matumizi mabaya ya fedha za umma katika wizara na mashirika ya umma, yakiwamo Tanapa na NSSF, hivyo kulikuwa na mgongano wa kimasilahi katika suala hilo.
Tuhuma za Zitto
Katika hotuba yake, Mbilinyi alisema taarifa za kibenki ambazo kambi hiyo imezipata zinaonyesha kuwa Desemba 10, 2012, Hifadhi ya Taifa ya Saadani ilihamisha Sh12 milioni kwenda katika akaunti ya kampuni ya Leka Dutigite.
“Siku moja baadaye fedha hizo zilitolewa kwa pesa taslimu kutoka kwenye akaunti hiyo. Januari 14 na Februari 7, 2013 akaunti ya Leka Dutigite iliingiziwa Sh28.6 milioni,” alisema Mbilinyi.
Sugu alisema fedha hizo ziliingizwa na mtu aitwaye Mchange na kwamba ilipofika Februari 7 zote zilikuwa zimetolewa.
Alisema Februari 28 mwaka jana, akaunti ya Leka Dutigite iliingiziwa Sh32.3 milioni kutoka NSSF na kwamba siku hiyo hiyo fedha hizo zilitolewa kwenye akaunti hiyo. Siku nne baadaye shirika hilo lilifanya malipo mengine kwenye akaunti ya Leka Dutigite.
“Ziliingizwa Sh46.6 milioni ambazo zilitolewa kutoka kwenye akaunti hiyo kwa mikupuo miwili. Katika kipindi cha miezi mitatu, kati ya Desemba 10, 2012 na Machi 4, 2013 kampuni hiyo (ya Zitto) ililipwa Sh119.9 milioni kwa utaratibu huohuo wa ingiza-toa fasta,” alisema Mbilinyi.
Alisema kati ya fedha hizo Sh12.2 milioni zililipwa na Tanapa na Sh79 milioni zililipwa na NSSF.
1 | 2 |inaendelea hapa chini...

WAALIPUAJI MABOMU ARUSHA WAKAMATWA

WATU 17 wamepandishwa kizimbani katika mahakama ya hakimu Mkazi jijini Arusha, kujibu mashitaka 16 yakiwemo ya kuua kwa kutumia bomu,kutesa binadamu na kusajili vijana na kuwapeleka nje ya nchi kufanya ugaidi.
Watu hao walifikishwa mahakamani hapo leo na kusomemewa shitaka hilo mbele ya Hakimu Mkazi Mustafa Siama ambapo hawakutakiwa kujibu chochote kutokana na kile kilichoelezwa kuwa mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza kesi hiyo.
Watuhumiwa hao wanadaiwa kutenda tukio hilo Aprili 13,katika nyumba ya kulala wageni na baa ya Arusha Night Park iliyopo Mianzini jijini hapa,ambapo kesi hiyo imeahirishwa hadi juni 11 mwaka huu kwa mtuhumiwa namba moja na namba nne na watuhumiwa wengine waliobaki kesi yao itatajwa tena juni 12
Katika tukio hilo la mlipuko huo wa bomu watu 14 walijeruhiwa vibaya katika maeneo mbalimbali ya miili yao hali iliyopelekea mmoja wa majeruhi hao aliyefahamika kwa jina la Sudi Ramadhani mkazi wa Kaloleni jijini hapa kufariki dunia akiwa anapatiwa matibabu katika hospitali ya Mkoa wa Arusha ya Mount Meru.
Akizungumza na waandishi wa habari Makao Makuu ya Polisi Arusha,kabla ya watuhumiwa hao kufikishwa mahakamani,Mkurugenzi wa Mashitaka ya Jinai nchini (DCI) Isaya Mngulu amesema kuwa mara tu baada ya kutokea kwa tukio hilo, polisi kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama walianza upelelezi na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa hao.
Ameongeza kuwa pia siku hiyo hiyo ya tukio hilo la mlipuko wa bomu katika baa ya Arusha Night Park muda mfupi baadae bomu lingine la aina ileile liligundulika kutegwa katika baa ya Washington ya jijini hapa ambapo bomu hilo liliondolewa katika eneo hilo bila kuleta madhara .
"Aidha baadhi ya watuhumiwa hawa pia walibainika kuwa na mikakati ya mashambulizaya namna hiikatika maeneo mengine na sehemu mbalimbali hapa nchini ambazo ni taasisi za Serikali na sehemu zenye mikusanyiko ya watu,ambapo pia wanajihusisha na uandaaji wa vijana kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini na kuwapeleka nchi za nje ili kujiunga na makundi ya kiuhalifu"alisema Mkurugenzi huyo wa Mashitaka nchini.
Mkurugenzi huyo amesema kwamba upelelezi wa matukio haya bado unaendelea ili kuwakamata watiliwa shaka wenginewaliobaki katika matukio ya milipuko ya mabomu katika Kanisa Katoliki Olasitna uwanja wa Soweto yaliyotokea mwaka jana jijini hapa na sehemu nyingine nchini.
Ametoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi kwa lengo la kuwafichua wahalifu wa ndani na nje wa matukio haya ya kihalifuna matukio mengine kwa lengo la kuvuruga amani na utulivu wan chi.

BAADA YA MAMBO KUWA SAFI UDSM MIGOMO YAHAMIA SAUTI KUDAI MIKOPO KUTOKA BODI

Wanachuo wa chuo cha saut tawi la mtwara leo wameandamana mpaka kwa mkuu wa mkoa wa Mtwara kutaka ufumbuzi juu ya mikopo yao kama wanachuo kutoka kwenye bodi ya mikopo.
Madai yao kwa sasa ni miezi 4 hawajalipwa ndipo wakaamua kuandamana maandamano ambayo hayakuwa rasmi hivyo jeshi la polisi mkoa wa mtwara likaingilia kati na kuzima maandamano hayo yaliyoanza mchana majira ya saa 8 mpaka saa 1o.

Jumatano, 28 Mei 2014

FAMILIA YAMUUA NDUGU YAO KWA MAWE KWA KUJICHAGULIA MUME

Mwanamke mmoja nchini Pakistan amepigwa mawe na familia yake wakiwemo babake na ndugu zake wa kiume hadi kufariki. Aliuawa nje ya jengo la mahakama mjini Lahore.
Mwanamke huyo aliuawa kwa kuolewa na mtu ambaye alikuwa chaguo lake mwenyewe.
Farzana Bibi, mwenye umri wa miaka 31, aliolewa na Muhammad Iqbal miezi michache iliyopita bila ya idhini ya familia yake.
Polisi wanasema kuwa mwanamke huyo alishambuliwa na familia yake.
Kaka zake na binamu yake mmoja walimshika alipokuwa akiingia mahakamani na kuanza kumpigwa kwa mawe . Alifariki popo hapo.
Waliomuua walikimbia kabla ya polisi kufika katika eneo hilo.
Babake msichana huyo amekamatwa ingawa washukiwa wengine wangali hawajulikani waliko.
Kwa wanawake wanaoolewa na wapenzi ambao ni chaguo lao wenyewe, ni kitendo kisichokubalika kitamaduni katika baadhi ya maeneo ya Pakistan.
Mamia ya wasichana huuawa kwa kisingizio cha kuolewa na watu wasiokubalika na familia zao kila mwaka
Wanaharakati wa kutetea haki za binadamu, wanaamini kuwa kwa kuwa mauaji hayo hufanywa na familia zenyewe, huwa ni vigumu kufikisha kesi hizo kortini.
BBC

APELEKWA MAHAKAMANI KWA KUMNYIMA UNYUMBA MMEWE

Kuna kituko kimetokea nchini Uingereza ambapo mwanamume mmoja kwa jina David Mason, mwenye umri wa miaka 30, alimshitaki mkewe Brenda kwa kumnyima haki yake ya "UNYUMBA" au kukataa kushiriki tendo la ndoa.Mwanamke huyo alimfanyia mgao wa wiki moja kila mwezi wa kitendo cha ndoa mumewe kwa hofu ya kushika mimba kwa mara ya tatu.
Kwa mujibu wa jarida la mtandao la Mirror, la Uingereza, Bwana Mason, ambaye kazi yake ni fundi mitambo alishinda kesi hiyo mwaka 1980.
Lakini mkewe alikataa rufaa ambapo Mason alipoteza kesi hiyo baada ya majaji kusema kuwa mahakamaisingeweza kuamua kuwa mkewe Mason alimkosea.

Jumanne, 27 Mei 2014

GOOGLE KUTENGENEZA GARI ZA KUJIENDESHA ZENYEWE

Kampuni ya Teknologia ya Google imesema itaanza kutengeneza magari yasiyohitaji madereva .
Kampuni hiyo ambayo imejijengea sifa kwa njia ya kipekee ya utendakazi wake katika sekta ya kiteknolojia imekuwa ikikarabati magari ya kawaida.
Gari hilo la kiteknolojia halitakuwa na usukani.
Magari bila Usukani
Litakuwa linaendeshwa kwa kubofya tu.
Google imesambaza picha ya gari hilo ambalo inasema ni la kutumiwa mijini na linapaswa kuwa chambo kwa wale ambao bado hawana imani na teknolojia hii ya hali ya juu.
Gari linalojiendesha
Muasisi wa kampuni hiyo Sergey Brin alizindua gari hilo la kipekee katika mkutano na wanahabari huko California.
Brin alisema kuwa teknolojia hiyo inauwezo mkubwa wa kuimarisha maisha ya watu .
Watafiti wa magari yanayojiendesha yenyewe bado wanajadili iwapo kuwepo kwa magari hayo mabarabarani yatakuwa na upungufu wowote ikiwemo dhana kuwa itachangia ongezeko la msongamano wa magari .
BBC

YAMETIMIA YA MCHUNGAJI:BONGO MUVIE PIGO JINGINE

IKIWA zimepita siku chache tangu msiba wa mwigizaji na muongozaji filamu za Kibongo, Adam Kuambiana, mwigizaji mwingine, Rachel Haule ‘Recho’, amefariki dunia jana asubuhi.
Inaelezwa kifo cha Recho kimesababishwa na uzazi, ambapo alijifungua kwa upasuaji na mtoto kufariki. Kutokana na hali hiyo, alilazwa chumba maalumu cha uangalizi ‘ICU’ na baadaye kufariki dunia.
Mwenyekiti wa Bongo Movie, Steve Mengele ‘Steve Nyerere’, alisema msiba upo Sinza kwa Remmy jijini Dar es Salaam kwa mjomba wa marehemu.
Hata hivyo, Steve alisema wapo katika mchakato wa kuiomba familia kumzikia hapa jijini Dar es Salaam, ili wadau mbalimbali wa filamu waweze kushiriki mazishi yake, badala ya kwenda Songea kama wanavyotaka.
Recho alianza rasmi kuingia katika sanaa ya maigizo mwaka 2009, katika kikundi cha Mburahati, kabla hajajiingiza rasmi kwenye uigizaji wa filamu.
Moja ya sifa zilizomfanya kujulikana, ni tabia ya kupendelea kuvaa nguo fupi, jambo ambalo alipohojiwa, alisema zinamfanya ajisikie huru na amani pindi anapofanya shughuli zake.

TAIFA STARS YASHINDA KIDUCHU TENA

TIMU ya soka ya Tanzania, Taifa Stars, jana ilivuna ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Malawi katika mechi ya kirafiki ya kimataifa iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
Ushindi huo ni ishara njema kwa Stars inayosaka makali ya kuwanyoa Zimbabwe na kuwatupa nje ya kampeni ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa Afrika mwakani nchini Morocco.
Stars inakabiliwa na mechi hiyo ya marudiano hatua ya kwanza ya kampeni za kwenda Morocco dhidi ya Zimbabwe itakayochezwa Juni Mosi, mjini Harare kuwania tiketi ya kutinga hatua ya pili.
Kama Stars itafanikiwa kuing’oa Zimbabwe, itakutana na mshindi wa jumla kati ya Msumbiji na Sudan Kusini, na ikivuka hapo itaungana na timu za Zambia, Cape Verde na Niger katika kundi F.
Mechi ya jana ilianza kwa kasi ndogo, huku kila timu ikijitahidi kumsoma mwenzie ili kuepuka sare ya bila kufungana kama ilivyokuwa mechi ya kwanza ya kirafiki baina ya nchi hizo iliyochezwa Uwanja wa Sokoine, jijini Mbeya mapema mwezi huu.
Dakika ya 17, Stars nusura ijipatie bao, lakini shuti la umbali wa mita 20 la Kelvin Friday lilipaa sentimita chache juu ya lango la Malawi.
Dakika ya 37, mshambuliaji Amri Kiemba aliipatia Stars bao pekee kwa shuti dogo, akimalizia pasi ya kiungo-mkabaji Shomari Kapombe aliyepanda kusaidia mashambulizi.
Kipa wa Stars, Deogratius Munishi ‘Dida’ alifanya kazi ya ziada na kukataa katakata nyavu zake zisitikiswe, baada ya kupangua shuti maridadi la Chimango Kaira, aliyefumua mkwaju huo kutokea upande wa kushoto kwenda lango la Kaskazini.
Hadi filimbi ya mwamuzi Israel Nkongo kuashiria mapumziko, Stars ilikuwa mbele kwa bao 1-0.
Kipindi cha pili, kilianza kwa Malawi kushambulia wakisaka bao la kusawazisha na wakakosa mabao matatu dakika za 47, 61 na 85 kwa mtokea benchi Rodrick Gonani kukosa baada ya kipa wa Stars, Dida kupangua na kuwa kona tasa.
Gonani alikosa bao jingine kwa staili hiyo akiunga pasi ya Bashiri Maunde katika lango tupu, Dida akiwa amepotea.
Stars inasafiri kwenda Zimbabwe kusaka sare, huku wenyeji wakitakiwa kushinda zaidi ya mabao 2-0 ili kusonga mbele.
Mara ya kwanza na mwisho kwa Stars kucheza fainali za Afrika ni mwaka 1980, hivyo mkakati wa timu hiyo ni kucheza fainali hizo kwa mara ya pili hapo mwakani.
Stars: Deogratius Munishi ‘Dida,’ Himid Mao/Haruna Chanongo, Edward Charles, Said Moradi, Joram Mgezeke, Shomari Kapombe, Simon Msuva/Ramadhani Singano, Erasto Nyoni, Kelvin Friday/Amri Kiemba/Mwinyi Kazimoto na Khamisi Mcha.
Malawi: Richard Chipuwa, Moses Chabvula, Limbikani Mzava/Christopher Banda, John Lanjesi, Foster Namwera, Phillipe Masiye Young Chimodzi/Bashiri Maunde, Gabadinho Mhango/Rodrick Gonani, Chimango Kaira, Joseph Kamwendo na Atusaghe Nyondo/Robin Ngalande.

BERNAD MEMBE ASISITIZA KUWA M23 NI RAIA WA RWANDA

Tanzania kwa mara ya Kwanza imesema inayo uhakika kuwa waasi wa M23 walioondolewa nchini Jamuhuri ya Kongo ni ni raia Rwanda.Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo Benard Membe ameliambia Bunge la Tanzania kuwa anao uhakika kuwa waasi M23 walitokea nchini Rwanda.
Hii ni Mara kwanza kwa Tanzania kukiri hadharani kuwa inao uhakika kuwa waasi hao ni raia wa Rwanda.
Tanzania ni miongoni mwa nchi ambazo zimepeleka majeshi Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambayo kwa kushirikiana na yale ya umoja wa Mataifa yaliwaondoa waasi hao DRC
Benard Membe Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania
Matamshi hayo ya Waziri huyo aliyatoa wakati alipokuwa akiwasilisha hotuba ya Bajeti ya Wizara yake ambapo pia alikiri kuwa bado uhusiano wa Tanzania na Rwanda sio mzuri.
Hata hivyo upande wa Upinzani mlishambulia Waziri huyo wa Mambo ya nje Benard Membe wakidai kwamba Waziri huyo anachochea kuvurugika kwa uhusiano wa Watanzania na Rwanda kwa kuhisi kuwa M23 ni Wanyarwanda nahata kutaka achukuliwe adhabu kali.
Mbali na tuhuma hizo Waziri Membe alizidi kusisitiza kuwa waasi wa M23 ni raia wa Rwanda akisema hiyo ni ripoti ya Umoja wa Mataifa.
Mbali na waziri baadhi ya wabunge wanamuunga mkono waziri Membe kuwa waasi wa M23 ni raia wa Rwanda wao.
Matamshi haya Waziri wa Tanzania kuhusu M23 bado haijulikana ni kwa namna gani utaathiri uhusiano wa Tanzania na Rwanda kama utakuwepo huenda ukajulikana hapo baadae.

MPYA:BOKO HARAMU WAUA TENA WATU 24 WAKIWEMO WANAJESHI 11

Wasichana wanaozuiliwa na Boko Haram
Taarifa kutoka mjini Buni Yadi katika jimbo la Yobe Kaskazini mwa Nigeria, zinasema kuwa watu 24 wakiwemo wanajeshi 11 wameuawa katika shambulizi dhidi ya kambi za wanajeshi.
Inaarifiwa kuwa kundi la Boko Haram ndilo linashukiwa kufanya mashambulizi hayo.
Wakaazi wanasema washambuliaji waliwasili katika eneo hilo kwa magari kumi ya kawaida na gari moja la kijeshi.
Waliwaambia wanakijiji kutokuwa na hofu kwani nia yao haikuwa kuwadhuru raia bali maafisa wa usalama.
Wanajeshi 11, polisi 13 akiwemo mwanamke mmoja waliuawa.
Pia waliteketeza majengo na magari ikiwemo makazi ya kiongozi mmoja wa kijadi na kituo kimoja cha polisi.
Taarifa zaidi bado zinajitokeza pole pole hasa kwa kuwa mawasiliano yamekuwa magumu kutokana na miundo mbinu mibovu.
Jimbo la Yobe ni moja ya majimbo matatu ambayo serikali imeweka sheria ya kutotoka nje usiku. Licha ya sheria hiyo mashambulizi ya mara kwa mara yamekuwa yakishuhudiwa mengi yakifanywa na Boko Haram.
BBC

MKURUGENZI WA TANESCO NA MKEWE WAFIKISHWA KIZIMBANI KWA WIZI WA MILION 31

ni
ALIYEKUWA Mkurugenzi wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), William Mhando, mke wake Eva Mhando, na wenzao watatu, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, wakikabiliwa na mashitaka sita ikiwemo matumizi mabaya ya madaraka, kughushi na kujipatia Sh. Milioni 31.7 kwa njia ya udanganyifu.
Kadhalika, Mhando anakabiliwa na matumizi mabaya ya madaraka kwa kuipa zabuni Kampuni ya Santa Clara Supplies Ltd, huku akijua ana maslahi nayo na kwamba anaimiliki yeye, mke na watoto wake.
Washtakiwa hao walisomewa mashitaka yake mbele ya Hakimu Mkazi Frank Moshi.Mbali na Mhando na Eva, washtakiwa wengine ni, France Mchalange, Sophia Misidai na Naftali Kisinga.
Mwendesha Mashitaka wa Taasisi wa Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Leonard Swai alidai kuwa kati ya Aprili Mosi na Desemba 31, mwaka 2011 katika ofisi za Makao Makuu ya Tanesco jijini Dar es Salaam, Mhando akiwa mwajiriwa kama Mkurugenzi wa shirika hilo, alitumia vibaya mdaraka yake.
Alidai kuwa, Mhando alitumia vibaya madaraka yake kwa kuamgalia maslahi yake binafsi baada ya kuipa zabuni ya kusambaza vifaa vya ofisi kampuni hiyo inayongozwa na mke wake, Eva na watoto wake, vyenye thamani ya Sh. Milioni 884.5 na kuisababishia kampuni hiyo kupata faida ya Sh. 31,747,000 kinyume cha sheria .
Katika shitaka la pili, ilidaiwa kuwa kati ya Januari 6 na Julai 30, mwaka 2011, mahali pasipofahamika, jijini Dar es Salaam, Eva alighushi taarifa ya ukaguzi wa fedha ya Kampuni ya Santa Clara Ltd, akionyesha kwamba imekaguliwa na Finx Capital House Desemba mwaka 2010.
Swai alidai katika shitaka la tatu, Agosti 9, mwaka 2011 jijini Dar es Salaam, mshtakiwa Eva alighushi nyaraka za umiliki wa hisa kutoka Santa Clara Supplies Ltd kwenda Eveta John Shing’oma huku akijua siyo kweli.
Upande huo wa Jamhuri ulidai katika shitaka la nne, Agosti 5, mwaka 2011 katika ofisi za Makao Makuu ya Tanesco, jijini, mshtakiwa Eva aliwasilisha nyaraka za manunuzi za kughushi akionyesha kwamba taarifa hiyo imeandaliwa na Finx Capital House huku akijua siyo kweli.
Katika shitaka la tano, ilidaiwa kuwa kati ya Aprili Mosi na Oktoba 31, mwaka 2011 jijini Dar es Salaam, Eva akiwa kama Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Santa Clara Limited kwa nia ovu, alijipatia faida ya Sh. Milioni 31.7 kutoka Tanesco baada ya kuwasilisha nyaraka za ukaguzi za kughushi.
Ilidaiwa katika shitaka la sita, Oktoba 17, mwaka 2011 katika ofisi za Tanesco, mshtakiwa wa tatu hadi wa tano, Mchalange, Misidai na Kisinga wakiwa watumishi wa shirika hilo, walipokea nyaraka za kughushi na kusababisha Kampuni ya Santa Clara Supplies Limited kupewa mkataba wa kusambaza vifaa vya ofisini.
Ilidaiwa kuwa mkataba huo ulisababisha kampuni hiyo kupata mkataba wa zabuni ya kusambaza vifaa vya Sh. Milioni 884.5 na kupata faida ya Sh. Milioni 31.5.
Washtakiwa walikana mashitaka hayo na mahakama iliwataka washtakiwa kuwa nawadhamini wawili watakaosaini hati ya dhamana ya Sh. Milioni 8, kuwasilisha hati za kusafiria mahakamani na wasitoke nje ya Mkoa wa Dar es Salaam, bila kibali cha mahakama.
Washtakiwa walitimiza masharti hayo na wako kwa dhamana hadi Juni 13, mwaka huu kesi hiyo itakapotajwa.

ASALITI NA KUVUNJA NDOA SIKU 13 BAADA YA KUFUNGWA

Inaweza kuingia kwenye headline kama tukizihusisha ndoa zilizodumu kwa muda mfupi tena zikifungwa kwa baraka zote kuanzia kwa wazazi hadi kwa Mungu kulingana na sehemu ilikofungwa ndoa hii ambapo ilikua kanisani.
Bonface Oduor ambaye ndiye bwana harusi amesema >>‘Alini saliti baada ya siku 13 ya harusi yetu ilofanyika wikendi ya pasaka’.
Wasiwasi na Uwoga mkubwa wa Bonface Oduor ilitimia hivi maajuzi tu baada ya kumfumania mkewe akishiriki tendo la ndoa na mwanaume mwingine ikiwa ni siku 13 tu baada ya harusi yao.
Jamaa ambaye alimfumania mkewe aitwae Sarah Kayuga kwenye hotel moja ya hotel za Nairobi akiwa na jamaa mwingine.
Harusi
wawili hao walikua wakirejea nyumbani baada ya honeymoon ya siku tano pamoja katika jiji la kifahari la Malindi pwani ya Kenya.
Harusi yao ya kufana ilifungwa kwenye kanisa la Pentecostal Assemblies of God Diani Mombasa Aprili 13 ambapo Oduor amedai ilikua ni ya kupoteza muda na pesa na kaapa kutoishi tena na mwanamke huyo na kujihusisha na mahusinaoya kimapenzi tena kwani hana imani tena na wanawake.
Hata hivyo Wawili hao waliamua kuachana baada ya oduor kugundua kua sarah alikua ametupa picha zake kwenye mtandao wa wozzup akiwa uchi.

ASKARI LAKI MOJA NA NUSU KUSIMAMIA KOMBE LA DUNIA BRAZIL

Mawaziri wa ulinzi nchini Brazil wameweka wazi kuwa zaidi ya vikosi vya kijeshi laki moja na nusu (150,000) vitasambazwa nchini humo kuhakikisha kunakuwa na usalama wa kutosha wakati mashindano ya mwaka huu ya kombe la dunia.
Kwa mara ya kwanza mpira unarejea katika ardhi yake ya nyumbani kwa zaidi ya miaka 60 wakati Brazil ikiwa katika maandalizi ya mwisho ya kuwa mwenyeji wa michuano hiyo mikubwa zaidi duniani ambapo kwa kiasi fulani hali ya usalama imeonekana kuwa si nzuri kufuatia maandamano ya hapa na pale.
Kumekuwa na maandamano ya wananchi wenye hasira wasiotaka mashindano hayo yafanyike, wengi wamekuwa na hasira juu ya kiasi cha pesa kilichotumika kwa ajili ya maandalizi yake zaidi katika kipindi ambacho nchi inakabiliwa na mtikisiko wa kiuchumi.
Tza.

MAAFISA WA UMOJA WA MATAIFA NAO WAKIONA CHA MTEMAKUNI SYRIA

Wapiganaji wa kiisilamu nchini Syria
Maafisa sita wa kikosi cha Umoja wa Mataifa waliokuwa wanachunguza madai ya kutumiwa kwa gesi ya Chlorine nchini Syria pamoja na madereva watano wameshambuliwa.
Taarifa kutoka wizara ya mambo ya nje ilisema maafisa hao walishambuliwa walipokuwa wanajaribu kufika kijiji cha Kafr Zaita katika mkoa wa Hama.
Punde tu baada ya kutoka katika gari lao kwenda kuanza kazi, papohapo mlipuko wa bomu ukatokea.
Hata hivyo duru zinasema kuwa maafisa hao wote wako salama.
Serikali ya Syria hapo awali ilisema kuwa maafisa hao walikuwa wametekwa nyara na magaidi walipokuwa wanasafiri kupitia mkoa wa Hama.
Mkurugenzi wa shirika la kudhibiti silaha za kemikali, Ahmet Uzumcu, alielezea wasiwasi kuhusu usalama wa maafisa hao.
"Wachunguzi wetu walikuwa nchini Syria kuchunguza madai ya matumizi ya gesi ya Chlorine kushambulia watu,'' alisema afisa huyo.
Wachunguzi hao walikuwa wanajaribu kufika kijiji cha Kafr Zaita kilicho chini ya udhibiti wa waasi, ambako inadaiwa mashambulizi sita ya kutumia gesi ya Chlorine yamefanyika katika miezi miwili.
Wiki jana wanaharakati, walitoa kanda inayodaiwa kuonyesha wanaume na watoto wakitibiwa katika hospitali moja baada ya bomu lililokuwa na Chlorine kurushwa na ndege ya jeshi na kumuua msichana mmoja.
Chlorine ni kemikali ya viwandani ambayo imepigwa marufuku ya shirika la kudbibiti zana za kemikali.
Credit:BBC.

Jumatatu, 26 Mei 2014

SHABIKI AWASHAMBULIA WANAMUZIKI KWA MSUMENO

Wanamuziki wawili wa bendi ya wanamuziki nchini Japan AKB48 wamejeruhiwa vibaya baada ya kushambuliwa na shabiki wao mmoja kwa kutumia msumeno.
Rina Kawaei mwenye umri wa miaka 19, na mwenzake Anna Iriyama 18, walikuwa wanakutana na mashabiki wao mjini Takizawa Jumapili wakati mwanamume mmoja alipowashambuliwa kwa msumeno.
Walipata majereha mikononi mwao na kwenye vichwa vyao. Mfanyakazi wao mmoja pia alijeruhiwa katika shambulizi hilo.
Kundi hilo linashikilia rekodi ya dunia kwa kuwa bendi kubwa zaidi ya wanamuziki duniani.
Polisi wamemkamata kijana mwenye umri wa miaka 24 kama mshukiwa wa shambulizi hilo.
Wasichana hao wawili walifanyiwa upasuaji na huenda wakaondoka hospitalini baadeye leo.
Rina Kawaei, alipata majeraha katika kidole chake
Tamasha walilokuwa wameandaa kufanyika Jumatatu , limefutilia mbali.
Bendi hiyo ni maarufu sana nchini Japan na katika mataifa mengine ya Asia.
Kadhalika kundi hilo lilianza kwa kuwa na wasanii 48 ingawa idadi hiyo imeongezeka hadi 140.
Kila mwaka mtu mmoja huteuliwa kujiunga na kundi hilo na pia wanachama hawaruhusiwi kuwa na ushirikiano wa kimapenzi.
Bendi hiyo iligonga vichwa vya habari mwaka jana wakati mmoja wa wasanii wake aliponyoa nywele zake zote kichwani na baadaye kuwoamba radhi mashabiki katika kanda ya video aliyoiweka kwenye mitandao ya kijamii.
Alikamatwa na wenzake akiwa na mpenzi wake.
CREDIT:BBC

WAJIUA BAADA YA KUPOTEZA MATUMAINI YA REAL MADRID KUCHUKUA KOMBE(KILLING THEMSELVES AFTER LOOSING HOPE OF MADRID WINNING CHAMPIONS TITLE

Two football fans – 39-year-old Mr. Olusoga Ogunbanjo and 42-year-old Mr. Bambo Sholeye – on Saturday slumped and died in Lagos Island, during the UEFA Champions League final between Atletico Madrid and Real Madrid. Both were said to be supporters of Real Madrid.
Although their team (Real Madrid) later won the championship in extra time with three more goals after their equaliser in the dying minutes of regulation time, the duo were said to have slumped and died following the inability of Real Madrid to equalise after rival Atletico Madrid had taken the lead by an early goal in the first half of the match. Sholeye, a member of staff of the Lagos State Waste Management Authority (LAWMA) of No 49/51 Apatira Street, off Olushi Street, Lagos Island, who had watched the match at a nearby shop, was said to have left the place in frustration after regulation time.
Deeply upset by the failure of Real Madrid to equalise the one goal scored by Atletico Madrid in the first half of the match, Sholeye was said to have brought out a chair in front of his house to relax when he suddenly slumped.
Although he was rushed to the general hospital by family members and neighbours, he was declared dead on arrival. The other football fan who was to meet his untimely death was Ogunbanjo, a refrigerator technician who resided at No 23A, Smith Street, off Evan Street, Lagos Island.
He was also a diehard supporter of Real Madrid. Popularly know as Soga by his friends, Ogunbanjo, who was said to have gone for a shave at a salon and met other football enthusiasts there, decided to watch the match with them.
When the tension became unbearable among fans who had lost hope of Real Madrid winning the champions league cup, another fan was said to have noticed how Soga was slumped on his seat and quickly raised the alarm.
He was also rushed to the emergency section of the Lagos General Hospital where he was confirmed dead by medical doctors on duty. The duo were buried yesterday morning at a public burial ground at Lagos Island by their relations in accordance with Islamic rites.
Credit:TRENT

Jumapili, 25 Mei 2014

HATIMAE WANAWAKE TASA KUPATA WATOTO

Wengi miongoni mwa wanawake wanapoolewa ndoto yao kubwa huwa ni kupata watoto.
Ndoto hiyo inaposhindwa kutimia kwa njia ya kawaida, basi juhudi zaidi hufanyika .
Mbinu mpya ya kisayansi ambayo imeanza kushika kasi nchini Kenya ni ile ya kutunga mimba kupitia chupa ama'' test tube'' kwa kiingereza.
Lakini Licha ya furaha ambayo huandamana na kuzaliwa kwa watoto , baadhi ya wazazi wanaopata watoto kwa njia hii hudhalilishwa na jamii
Joyce Kamau ni mama mwenye miaka 41 na hakuweza kupata mtoto kwa miaka saba baada ya kuolewa.
‘’Nilipoolewa sikuweza kupata mtoto, nilitembelea madakatari wengi na kutumia pesa nyingi sana.
Tasa kushika mimba kupitia mbinu za sayansi
Baada ya miaka saba, binamu yangu alinieleza kuwa naweza kupata huduma ya IVF hapa Kenya” Joyce anaeleza.
Joyce anasema baadhi ya rafiki zake walimtenga na kukosa kumwalika katika sherehe za siku ya kuzaliwa kwa watoto wao kwa vile walidhani kwamba hatakuwa na nafasi ya kuwaalika pia katika shere za watoto ambao hana.
Joyce aliolewa akiwa na miaka 33.
Anaamini kuwa ni vyema mwanamke kutokimbilia ndoa wakiwa na umri mdogo.
Wanawake wengi wameendelea kupata nafasi za kujiendeleza kimasomo na kikazi, hali hii imechangia kuchelewa kuolewa na pia kupata watoto.
Daktari Shaunak Khandawala ambaye ni mtaalam wa afya ya uzazi na mwenye uzoefu wa miaka 25, anasema mtindo wa maisha ya kisasa husababisha tatizo la wanawake kutoweza kushika mimba.
Tasa kushika mimba kupitia mbinu za sayansi
Hasa anasema utafiti unaonyesha uwezo wa mwanamke kupata mtoto hupungua mwanamke anapozidi kuwa na umri mkubwa
Dakatari Kandawala anaeleza ' sababu nyingine zinazosabisha tatizo la kutopata mimba ni kama vile mifuko ya uzazi kuharibika kwa sababu ya magonjwa mengi, uchafuzi wa mazingira ,hali ya kuwa na fikra nyingi na manii ya wanaume kupungua.'
Shirika la afya duniani linasema mmoja kati ya wanandoa wanne hawawezi kupata mtoto.
Katika mila nyingi mama tasa hukejeliwa. Wengi wao wanahofu ya kutafuta huduma za afya ya uzazi.
Joyce Kamau alikuwa na ujasiri wa kutafuta huduma hizo kwa miaka saba, ilimgharimu zaidi ya dola elfu kumi na mbili.
Joyce kwa sasa ni mja mzito , na anatarajia kuzaa mapacha.
BBC

WAMISRI WAANZA KUPIGA KURA KUMCHAGUA RAIS WAO

Raia wa Misri watapiga kura kwa muda wa siku mbili kumchagua rais mpya chini ya ulinzi mkali kuhakikisha mchakato wa upigaji kura unafanyika kwa usalama. Karibu maafisa wa usalama laki mbili wameshika doria kote nchini Misri serikali ikionya dhidi ya hatari za usalama zinazoweza kusababishwa na itikadi kali za kiislam .
Adbel Fatah al-Sisi Kiongozi wa kijeshi wa zamani aliyeongoza mapinduzi ya kijeshi dhidi ya rais wa awali Mohammed Morsi anatarajiwa kupata ushindi kwa u rahisi.
Oparesheni kubwa ya usalama inayoendelea nchini Misri ni ushahidi kamili kuwa utawala wa sasa unaoungwa mkono na jeshi unatambua kuwa ugaidi unaoungwa mkono na Waislamu wenye itikadi kali upo na unaweza kuteguliwa wakati wo wote.
Mbinu ya kukabiliana na ugaidi huo ya Abdel Fatah al-Sisi haijabadilika ila tu ni magwanda yake ya kijeshi ya field Mashel yaliyojaa medali yaliyobadilishwa na nguo za kiraia.
Ametangaza katika kampeni yake kuwa anaunga mkono kuangamizwa kabisa kwa kundi la Muslim Brotherhood ambalo limeshuhudia maelfu ya wanachama wake wakizuiliwa na mamia wakihukumiwa vifo.
Bwana Sisi ametoa wito kwa watu wanaotakia Misri amani na utangamano baada ya miaka kadhaa ya mapinduzi na ghasia na ameheshimiwa kiwango cha kusujudiwa na wengine hivi kwamba unaweza kununua peremende au chokoleti dukani iliyopachikwa picha yake.
Mpinzani wake mwenye mrengo wa kushoto, Hamdeen Sabbahi, anatajwa katika vyombo vya habari ambavyo vinaoenekana kuamua tayari kuwa yeye atashindwa katika Uchaguzi unaoanza leo.
Ingawa wapiga kura wana mazoea ya kubadilika dakika za mwisho kabla ya uchaguzi lakini wengi nchini Misri watashangaa iwapo Bwana Sisi hashindi uchaguzi huu, na tena kwa urahisi.
BBC

MATOKEO YA UCHAGUZI YANAONESHA KUWA BILIONEA PETRO PEROSHENKO ANAONGOZA NA ATAKUWA NDIE RAIS MPYA UKRAIN

Matokeo yanayotokana na maoni ya wapigaji kura yanaonesha kuwa biliyoneya anayetengeneza chakileti, Petro Poroshenko, ameshinda katika duru ya kwanza ya uchaguzi wa rais wa Ukraine.
Inakisiwa amepata asili-mia 56 ya kura.
Matokeo rasmi hayatotangazwa hadi Jumatatu.
Bwana Poroshenko alisema azma yake ni "kumaliza vita na kuleta amani", na alisema Ukraine daima haitokubali Urusi "kulikalia" jimbo la Crimea.
Waziri Mkuu wa Urusi, Dmitri Medvedev, alizuru Crimea wakati upigaji kura unaendelea, hatua ambayo serikali ya Kiev imesema ni uchokozi wa kusudi.
Upigaji kura ulisonga mbele ingawa vituo vya kupigia kura havikufunguliwa katika miji ya Mashariki ya Donetsk na Luhansk.
Bbc

MZINDAKAYA AGOMA KUMSAMEHE ADUI YAKE KANISANI


Mbunge wa zamani wa jimbo la Kwela, Mzee Chrisant Mzindakaya amekataa kumsamehe hadharani Mbunge wa sasa wa Sumbawanga Mjini, Bw. Aeshi Hilali baada ya kupewa fursa ya kushikana mikono jukwaani na kusameheana.
Haya yametokealeo mchana (Jumapili, Mei 25, 2014) kwenye ibada ya kumuweka wakfu Askofu Mteule Conrad Nguvumali wa Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Rukwa iliyofanyika kwenye Uwanja wa Nelson Mandela, mjini Sumbawanga.
Mzee Mzindakaya alikataa kufanya hivyo akisema yeye ni mkristu lakini hakuwa ameandaliwa kiroho kwa ajili ya tukio hilo. “Hapa ni shughuli ya kanisa na si mkutano wa Chama. Lazima niwe mkweli leo sijajiandaa kwa jambo hili… Mimi ni mtu mzima, nafsi ya msamaha inahitaji maandalizi, nahitaji maandalizi ya kiroho,” alisema.
Hata hivyo, alikiri kwamba amekubali msamaha alioombwa na Bw. Aeshi lakini hawezi kuutoa katika shughuli ya Kanisa. “Nilishamwambia Mwenyekiti wa CCM mkoa aitishe mkutano, wazee wa chama wawepo na sisi wawili tuwepo kwa sababu nimetukanwa sana kama vile sijaifanyia jambo lolote nchi hii,” alisisitiza.
“Niliwaeleza pia waandae mikutano ya nje kule kwa wanachama ambako nilichafuliwa sana. Nikisema nimemsamehe hapa nitakuwa mnafiki,” aliongeza.
Kwa upande wake, Bw. Aeshi ambaye alipewa nafasi ya kwanza kuomba msamaha, alisema anatambua kwamba bega haliwezi kukizidi kichwa na yeye kama mtoto anamuomba msamaha Mzee Mzindakaya kwa yaliyopita ili waweze kufanya kazi pamoja na kuleta maendeleo kwa wakazi wa jimbola Sumbawanga Mjini.
“Natambua kuwa mimi ni mtoto na siku zote mdogo atabaki kuwa mdogo lakini naomba busara zake ili tushirikiane kuleta maendeleo ya mkoa wetu… yaliyopita si ndwele tugange yajayo. Nimetamka maneno haya mbele ya viongozi wa dini na mbele ya Mungu kwa kuwa najua yuko hapa,” alisema.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Mhandisi Stella Manyanya ndiye aliwaomba Mzee Mzindakaya na Bw. Aeshi wapande jukwaani na kupeana mikono na kisha akawapa kila mtu fursa ya kutoa neno.
Mhandisi Manyanya alisema siku ya leo ni ya kipekee na akaona asipoteze fursa hiyo bali aitumie kuwaomba viongozi hao ambao wamekuwa na uhasama wa muda mrefu wayamalize kwa kupeana mikono hadharani.

CHAMPIONS LEAGUE YASABABISHA MAUAJI NIGERIA

Gari lilolukuwa na mlipuaji wa kujitolea muhanga mjini Jos.
Maafisa wa polisi nchini Nigeria wanasema kuwa watu watatu wameuawa baada ya mtu wa kujitolea muhanga kujilipua katika mji ulio katikati ya Nigeria Jos.
Mlipuko huo ulitokea karibu na eneo ambalo mashabiki wa soka walikuwa wakiangalia kinyanganyiro cha fainali za kombe la kilabu bingwa barani ulaya.
Ripoti zinasema kuwa mlipuaji huyo alikuwa amelilenga eneo hilo,lakini gari lake likalipuka kabla ya kufika.
Shambulizi hilo linajiri siku kadhaa tu baada ya takriban watu 118 kupoteza maisha yao katika milipuko miwili ya mabomu yaliotegwa ndani ya gari katika mji huo.

RAIS KIKWETE ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA KIFO CHA MPIGA PICHA WA MLIMANI TELEVISION MAXIMILIAN

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia salamu za rambirambi Waziri wa Habari Mheshimiwa Dkt.Fenella Mukangara kufuatia kifo cha Mpiga picha wa kituo cha television cha Mlimani, Ndugu Maximilian John kilichotokea alfajiri ya kuamkia tarehe 24 Mei,2014.
“Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Bwana Maximilian kilichotokana na maradhi ya Moyo, Sukari na Shinikizo la damu. Kifo hicho ni pigo na pengo kubwa kwa tasnia ya habari hapa nchini,”Amesema Rais Kikwete katika salamu hizo.
“Bw. Maximilian atakumbukwa kwa uchapakazi wake na uhodori katika kazi zake siku zote. Kifo ni maandiko ya Mwenyezi Mungu hivyo hatuna budi kumshukuru kwa yote.
“Nakutumia salamu zangu za dhati kuomboleza msiba huu. Aidha, kupitia kwako, naitumia familia ya Ndugu Maximilian, pole za dhati ya moyo wangu kwa kuondokewa na mzazi na mhimili wa familia. Aidha, salamu hizi ziwafikie pia wanahabari wote, wafanyakazi wenzake, ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu. Nakuomba uwajulishe kuwa naelewa machungu yao katika kipindi hiki na nawaombea subira na uvumilivu.
Ninaungana nao kumwomba Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, aiweke peponi roho ya marehemu. Amen,” amesema Rais katika salamu hizo.
Ndugu Maximilian John ameacha mke na watoto wanne.
Imetolewa na;
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
Ikulu – Dar es Salaam. 24 Mei,2014

HATIMAE JAYZEE AGOMA KUHUDHULIA HARUSI YA KANYE WEST ILIYOFANYIKA JANA

Hatimaye Rapa maarufu wa muziki wa nchini Marekani Kanye West na mwanadada anayemake headlines kila kukicha Kim Kardashian wamefunga pingu za maisha na kuwa mume na mke huko Florence nchini Italia. Wapenzi hao walisafiri kwa nyakati tofauti kutoka jijini Paris nchini Ufaransa ambako waliungana na familia zao katika ile Pre Wedding Party.
Taarifa zinadai kuwa wanandoa hao wapya walipanga kufunga ndoa hiyo huko Chateau de Versailles lakini sheria za Ufaransa hazikuwaruhusu kufanya hivyo kutokana na hata mmoja wao kutokuwa na uraia wa nchi hiyo.
Cha kushangaza ni kwamba si Jay Z wala Mke wake Beyonce aliyehudhuria katika harusi hiyo na kuishia kutuma salamu za pongezi licha ya kuwepo kwa uvumi kuwa Jay Z atakuwa msimamizi wake kutokana na ukaribu na urafiki mkubwa waliokuwa nao.
Tza

HATIMAE JAYDEE AWA MSANII TANZANIA WA KWANZA KUFIKISHA LIKES 300000 FACEBOOK NA HIKI NDIO ALICHOSEMA

Lady Jaydee
Yoooooh!! Mmmefika laki tatu 300,000 na kuzidi, nawashukuru sana. Fanyeni kubarikiwa leo, kesho, kesho kutwa na milele amina. Mapenzi tele toka kwa JayDee

Jumamosi, 24 Mei 2014

WATOTO WAGOMBEA URITHI KABLA YA MAZISHI YA BABA YAO

SINA hakika kama watu wote duniani wana kawaida ya kurithi mali za wazazi wao pindi wanapofariki, lakini nina uhakika utamaduni huu upo kwa sehemu kubwa sana katika jamii zetu sisi Waafrika na hususan Watanzania, ingawa kuna tofauti kadha wa kadha za jinsi ya kugawa au kugawana.
Pamoja na kutambua kuwa utamaduni huu upo miongoni mwetu, lakini pia sina hakika kama kweli Watanzania wote tunafahamu vema sheria zinazotuongoza katika migawanyo ya mali pale inapotokea mzazi amefariki na wanafamilia wakaamua kugawana bila ya kuzingatia wosia wa marehemu.
Katika hali ya kawaida ya maisha yetu sisi wanadamu, ni dhahiri kitaaluma watu wote haiwezekani tukawa wanasheria, lakini kwa uwepo wa hao wanataaluma ya sheria, na sisi wengine pale linapotokea jambo fulani linalohitaji utatuzi wa kisheria basi ni vema kuwatafuta ili watupe miongozo ya jinsi ya kutatua mambo yetu.
Tusipowatafuta watu wenye taaluma hiyo tunaweza kujikuta tunaingia kwenye matatizo makubwa zaidi ya hayo tuliyokuwa tunakusudia kuyatatua.
Nasema hivi kutokana na wanafamilia fulani jijini Dar es Salaam ambao mbali ya kuwa na watu kadhaa waliobahatika kwenda shule vizuri, cha ajabu mara baada ya baba yao kufariki watoto wote wa marehemu pamoja na baadhi ya ndugu zao wengine wakajikuta wanaingia katika mzozo mkubwa uliosababisha hadi kutishiana maisha, kisa? Jinsi ya kugawana mali alizoziacha baba yao.
Mzee huyo ambaye katika maisha yake alioa mara tatu ambapo aliwataliki wake wawili (wa kwanza na wa pili) kabla ya mauti kumkuta, lakini alitambua kuwa wanawake alioishinao pamoja na watoto wao wote wana haki ya mgawo wa mali zake.
Kwa busara zake aliamua kuandika kabisa mgawanyo kamili wa mali zake ili kuepusha shari ambayo alitegemea ingeweza kutokea kama asingeandika urithi na kuukabidhi kwa mwanasheria.
Baada ya mauti kumfika mzee huyo, mmoja wa wana ndugu aliwasomea wosia aliouacha juu ya mgawanyo wa mali zake, ambao ulifanana kidogo na ule wa Mzee Madiba kwa kuwapa wanafamilia wote pamoja na baadhi ya ndugu zake wa karibu, lakini akamtema kabisa katika orodha ya mgawo huo mmoja wa wake zake kama alivyofanyiwa Winnie Mandela!
Katika hali ya kushangaza tofauti na matarajio ya wengi kuwa mara baada ya wosia wa marehemu kusomwa, tena ukiwa umetoka kwa mwanasheria ungerahisisha zoezi zima la mgawanyo wa mali za marehemu, lakini kwa wanafamilia hiyo hali ikawa kinyume kabisa!
Hakuna aliyetaka kukubaliana na wosia huo na kudai kuwa umechakachuliwa na wala hawatambui cha mwanasheria wala huyo ndugu yao – mzee aliyekabidhiwa wosia huo na mwanasheria ili ausome kwa wanafamilia pamoja na watu wote waliokuwepo hapo msibani!
Moja ya kitu ambacho marehemu alisisitiza sana kwa familia yake kupitia wosia huo, ni kuwataka wasithubutu kuiuza nyumba yake bali wanaweza kuipangisha ili pesa za kodi ziwasaidie wadogo zao wadogo ambao bado wapo shuleni.
Kutokana na dalili za wanafamilia hao kuonyesha kutotaka kutambua kuwa kuna mambo ya kuzingatiwa kisheria katika mgawanyo wa urithi tangu pale walipokataa kuukubali wosia wa marehemu baada ya kusomwa, kabla hata mzee wao hajamaliza wiki moja kaburini tangu azikwe, tayari walikwishapata mteja wa kumuuzia nyumba waliyosisitizwa wasiiuze!
Hatimaye wakafanikiwa kumpata mnunuzi na wakaiuza nyumba hiyo kwa milioni kadhaa za nguvu huku nafsi zao zikiwa zimejaa furaha kubwa sana.
Kwa ulimbukeni wao walidhani hizo sh milioni 200 walizofanikiwa kuzipata kwa kuiuza hiyo nyumba wangekaa nazo katika kipindi cha maisha yao yote, wakagawana kwa mbwembe nyingi na kuanza kufanya mambo kibao kwa pupa ikiwa ni pamoja na matanuzi ya jeuri ya pesa.
Sasa pesa imekatika, nyumba ya baba yao haipo tena, wadogo zao shule ni mgogoro mtupu, na wao wenyewe wanaugulia majeraha ya kufulia bila sabuni! Je, leo hii watakuwa wageni wa nani?
Hayo siyo mambo hata kidogo, kwanini mkatae wosia wa baba yenu aliyewaandikia kabla hajafa? Sasa baba hayupo tena duniani, nyumba nayo mmeinywa na nyinyi wenyewe kila siku ni mifarakano.
Msije mkasingizia mmerogwa, hapo hakuna cha mchawi wala mlozi, bali hizo ni dalili za mwanzo wa laana ya kwenda kinyume na matakwa ya marehemu baba yenu.

SHERIA NI MSUMENO,HAKIMU NAE AFIKISHWA MAHAKAMANI.

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) wilayani Bunda, Mara imemfikisha mahakamani Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Kibara A, Witness Lameck (38) kwa tuhuma ya kuomba na kupokea rushwa kutoka kwa wavuvi.
Ofisa mtendaji huyo ameunganishwa kwenye kesi hiyo inayomkabili pia Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Kewnkombyo, Emmanuel Mng’wale (37), aliyefikishwa mahakamani hapo Mei 19 mwaka huu, kwa tuhuma hiyo.
Akiwasomea mashitaka yao mbele ya Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Bunda, Hamad Kasonso, Mwanasheria wa Takukuru, Eric Kiwia alisema washitakiwa wote walitenda kosa hilo kati ya Aprili 22 na 23 mwaka huu.
Kiwia alidai hakimu huyo aliandika hati bandia na kugonga mhuri wa mahakama na sahihi yake na kisha kumpatia ofisa mtendaji huyo, ili azipeleke kwa wavuvi kwamba wanashitakiwa kwa makosa ya uvuvi haramu.
Alidai kuwa hati hizo zililenga kuwabambikizia kesi wavuvi hao na kuwatisha ili watoe rushwa kati ya sh 60,000 hadi 150,000.
Ilidaiwa mahakamani hapo na wakili huyo kwamba ofisa mtendaji huyo alizisambaza hati hizo kwa wavuvi hao huku akiwaomba watoe kiasi hicho cha fedha, ili kesi zao zifutwe, vinginevyo wangehukumiwa kifungo ch miezi sita jela.
Kwa mujibu wa wakili huyo, baadhi ya wavuvi walitoa kiasi hicho cha fedha huku wengine wakitoa taarifa Takukuru, ambako uchunguzi ulibaini kuwa hati hizo ni bandia kwa vile watuhumiwa hawakuwa na kesi zinazowahusu.
Washitakiwa wote walikana mashitaka yao na kupewa dhamana hadi Juni 16 mwaka huu kesi hiyo itakapotajwa tena mahakamani hapo.
Kwa mujibu wa Takukuru wilayani hapa, wavuvi waliotoa rushwa hiyo inasadikika ni wengi na kuongeza kuwa taasisi hiyo imeamua kushirikisha wavuvi watano kwa ajili ya ushahidi katika kesi hiyo.

WATANZANIA WATAKIWA KULA PANYA

MUKEBEZI BLOG/(DOUBLE LL KIDS): Dar es Salaam. Watanzania wameshauriwa kufuga na k...: Dar es Salaam. Watanzania wameshauriwa kufuga na kula panya aina ya ndezi wakieleza kuwa nyama hiyo haina mafuta mengi, ikiwa pia na virutub...
Dar es Salaam. Watanzania wameshauriwa kufuga na kula panya aina ya ndezi wakieleza kuwa nyama hiyo haina mafuta mengi, ikiwa pia na virutubisho muhimu na vilivyo adimu.
Rai hiyo imetolewa na wataalamu kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) katika Maonyesho ya Vyuo Vikuu nchini yaliyofanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Wataalamu hao walisema kuwa ili kukabiliana na uharibifu wa kuchoma moto misitu kwa ajili ya kuwatafuta wanyama hao, ni vyema wananchi wakaanza kuwafuga kwa kuwa nyama yao ina ladha nzuri na ni laini.
Mhadhiri Mwandamizi wa SUA, Idara ya Uzalishaji, Mirende Matiko alisema kuwa ingawa wanyama hao wanafugwa kwa wingi katika nchi za Afrika Magharibi, hapa nchini ufugaji wake unakabiliwa na changamoto nyingi.
“Wakulima wetu hapa tunawapa wafuge, siku chache baadaye ukienda utaambiwa walikufa, lakini ukiwauliza majirani wanakuwambia ‘jamaa aliwachinja’, ni sawa na kumpa mkulima mbegu halafu anakula,” alisema Matiko.
Akizungumzia namna nyama hiyo inavyoliwa, Matiko alisema: “ Nyama yake ina viinilishe vingi, yanatupwa manyoya na miguu yake tu, vitu vingine vyote vinaliwa. Tena utumbo ndiyo mtamu sana, si unajua wanakula nyasi tu.”
Alisema wanyama hao wana faida nyingi kiuchumi ikiwamo kuongeza pato la kaya, kuchangia uwindaji endelevu, kutunza bioanuwai pia nyama yao ni gharama nafuu, ikilinganishwa na nyingine.
“Mtu akitaka kufuga wanyama hao anatakiwa kuwa na banda madhubuti lenye ubora, chakula na maji safi yawepo bandani muda wote na upandishaji ufanyike katika muda mwafaka,” alisema.
Mhadhiri huyo alitoa hadhari kwa wafugaji akiwataka kuwakamata wanyama hao kwa umakini kutumia chandarua, kuepuka kusababisha majeraha.
Ndezi ni jamii ya nungunungu na pimbi, wakiwa wa aina mbili, ambapo wadogo huwa na uzito wa kati ya kilo nne hadi sita na wakubwa hufikia hadi kilo tisa. Wanyama hao hupendelea kuishi kwenye maeneo yanayolimwa mashamba ya miwa, ulezi na mpunga.
Hata hivyo, Dk Loth Mulungu alisema kuwa wawindaji wa ndezi porini husababisha madhara makubwa ikiwamo uchomaji wa misitu, uharibifu wa bioanuwai, kukanyaga mazao mashambani na upotevu wa muda.
Mmoja wa watazamaji waliotembelea Banda la SUA, Elizabeth Maro alisema kuwa ingawa kwa muda mrefu amesikia watu wakila mnyama huyo. Binafsi hawezi kula nyama yake kwa kuwa anaamini hana tofauti na panya wengine.
“Siwezi kumla kwa namna yoyote, huyu ni panya tu ndiyo maana hata jina lake kwa Kiingereza anaitwa ‘canerat’, maana yake panya mla miwa,” alisema.

BAADA YA KUTOKURIDHISHWA NA UCHAGUZI RAIS BANDA WA MALAWI AUFUTA NA KUTAKA URUDIWE NDANI YA SIKU 90

Rais Joyce Banda wa Malawi ameamuru kusitishwa mara moja kwa shughuli ya kuhesabu kura na kutangaza matokeo ya uchaguzi mkuu wa nchi hiyo ulifanyika jumanne iliyopita.Akizungumza Ikulu mjini Lilongwe muda mfupi uliopita ameiamuru Tume ya uchanguzi MEC kusitisha shughuli hiyo na kutangaza kuwa uchaguzi urudiwe ndani ya siku 90 kutoka leo na kwamba yeye hatogombea tena urais wa nchi hiyo.
Mwandishi wa BBC Baruan Muhuza amearifu kutoka mjini Lilongwe kuwa Dr Banda amesema amelazimika kuchukua hatua hiyo kutokana na kile alichokiita kuvurugwa kwa mtiririko mzima wa shughuli za upigaji kura,kuhesabu na hata namna ya kusimamia utoaji wa matokeo yake.
Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi ya Malawi Jaji Mackson Mbendera amesema kuwa anawasiliana na mwanasheria mkuu wa serikali ili kuangalia uwezekano wa amri hiyo ya Rais kutekelezwa na kama haijavunja sheria ya nchi.

MASKINI:MAITI YA AMINA NGARUMA YAZIKWA LEO JIJINI DAR ES SALAAM

Leo yalikua ni Mazishi ya aliyekua muimbaji wa African Revolution na baadae Double M Sound Amina ngaluma ambaye alifariki mchana wa Mei 15 akiwa Thailand ambako ndiko alikohamishia makazi yake kikazi ambapo alikua akifanya kazi na band ya Jambo Survivors.
Kifo cha Amina Ngaluma ‘Japanese’ kilitokea baada ya kuumwa kwa siku nne ambapo mume wake alipozungumza amesema kiongozi wa band yao huko Thailand alimwambia Amina alilazwa hospitali kutokana na maumivu makali ya kichwa,mwili wa Amina Ngaluma ulipokelewa jana Mei 23 na saa 6 kasoro za usiku taratibu za kuutoa mwili huo nje zilikamilika.
Amina ngaluma amezikwa mchana wa leo kwenye makaburiya Machimbo Mnarani Dar es salaam.mahali ambako inaishi familia yake.

WATU MAARUFU KULIKO WOTE KATIKA TWITTER 2014 KWA MUJIBU WA FORBES

Twitter’s 10 most popularaccounts - Katy Perry(over 50 million followers), Justin Bieber, Barack Obama, Lady Gaga, YouTube, Taylor Swift, Britney Spears, Rihanna, Instagram, Justin Timberlake. Not exactly sure what I was expecting here… guess I was hoping for more scientists or novelists or philosophers or business executives or something like that. Maybe it’s just another sign, as that great old Sports Illustrated section is titled, “that the Apocalypse is upon us.” (Personally, I was rather disturbed that no Kardashians made this list.)

BABA LA MIAKA 59 LAMBAKA MTOTO WA MIAKA 12 NA KUMUHONGA 200/-

Morogoro. Jeshi la Polisi mkoani Morogoro linamshikilia Mohamed Mgende (59) mlinzi na mkazi wa Msamvu Ndege Wengi kwa tuhuma za kumbaka binti wa miaka 12, mwanafunzi wa darasa la tano Shule ya Msingi Msamvu B.
Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi mkoani Morogoro, Leonard Paulo alisema kuwa tukio hilo lilitokea Mei 21, mwaka huu saa 11 jioni, Manispaa ya Morogoro.
Kamanda Paulo alisema kuwa, mtuhumiwa alikutwa chumbani akiwa na binti huyo na inaaminika alikuwa akijiandaa kumbaka kwa vile alishavua nguo na kujifunga taulo.
Akielezea namna taarifa hizo zilivyowafikia, Paulo alisema binti huyo alimweleza mwalimu wake (jina linahifadhiwa) kuhusu namna anavyofanyiwa vitendo vya ubakaji na mtuhumiwa huyo na ndipo mwalimu huyo alipotoa taarifa polisi.
Alisema mwanafunzi huyo alimweleza mwalimu wake kuwa, alianza kubakwa na mtuhumiwa huyo tangu akiwa darasa la nne na kwamba alishindwa kuwaeleza wazazi wake kwa sababu mtuhumiwa alimtishia kumuua kama angesema.
“Taarifa za awali zinaonyesha kuwa mtuhumiwa alikuwa akiishi jirani na familia anayotoka binti huyo na kila alipombaka alimnunulia chips na kumpa Sh200 au 500,” alisema Kamanda Paul.
Pia mtuhumiwa huyo alikuwa akimdanganya binti huyo kuwa anamiliki ghorofa jambo ambalo siyo kweli kwani ghorofa alilomwonyesha alikuwa akifanya kazi kama mlinzi.
“Kuna taarifa zaidi kuwa alikuwa akiwabaka mabinti wengine, hatuwezi kuthibitisha kwa sasa ila tunaendelea na uchunguzi,” alisema.
Aliwataka wananchi kushirikiana na polisi ili kubaini kama alishawahi kuwafanyia vitendo hivyo watoto wengine.
Mama mzazi wa binti huyo (jina limehifadhiwa) alipata mshtuko na kupoteza fahamu.
VIA:MWANANCHI

Ijumaa, 23 Mei 2014

MGANGA AMNYONGA NA KUMKATA SEHEMU ZA SIRI MTOTO WA MIAKA NANE.

MTOTO Fausta Geofrey (8), mkazi wa wilayani Muleba, ameuawa kikatili kwa imani za kishirikina na mganga wa kienyeji kwa kunyongwa na kisha kukatwakatwa mapanga na kuondolewa baadhi ya viungo vyake, zikiwemo sehemu za siri.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, George Mayunga, alisema jana kuwa tukio hilo lilitokea Mei 21 mwaka huu, saa 1:30 asubuhi katika Kijiji Cha Bisole, Kata ya Muhutwe, Wilaya ya Muleba.
Alisema mtoto huyo ambaye alikuwa mwanafunzi wa Shule ya Msingi Kitunga, akiwa na wenzake wakielekea shuleni, walipofika eneo la mganga huyo wa kienyeji, Mujingwa John (20 alimkamata na kumpeleka ndani kwake kisha kumnyonga hadi kufa.
Kamanda Mayunga alisema mganga huyo baada ya kumkaba shingo mtoto huyo, alimkata mkono wa kushoto, masikio, sehemu za siri na sehemu nyingine za mwili.
Alisema viungo hivyo alivibanika ili vikauke na baadae atengeneze dawa kwa matumizi mengine.
Kamanda Mayunga alisema baada ya kutoa viungo hivyo, sehemu ya mwili iliyobaki alichimba kaburi chini ya kitanda chake na kuvizika kisha kuweka nyasi juu yake.
Alisema siku ya tukio wazazi wa mtoto huyo walipatwa na wasiwasi baada ya mtoto wao kutorudi nyumbani, hivyo walitoa taarifa kituo cha polisi Muleba.
Kamanda Mayunga alisema baada ya taarifa kufika kituo cha polisi walishirikiana na wazazi kumtafuta wakapata habari za mtoto huyo kuchukuliwa na mganga huyo na alipokwenda kuhojiwa alikana, lakini alipobanwa alikiri na kuwaeleza anaye lakini ameshakufa.
Alisema alifanya hivyo kwa sababu ya kukosa fedha za kujikimu kimaisha.
“Nilikuwa nataka kuwa tajiri ndiyo maana nilijiingiza kwenye uganga,” alisema mtuhumiwa huyo ambaye bado anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa uchunguzi zaidi.
TANZANIA DAIMA

WATAALAMU WAINGILIA DHAHABU YA WANANCHI LOLIONDO KWA BABU.

MKUU wa Wilaya ya Ngorongoro, Elias Wawa Lali, amesema kuwa wataalamu wa madini wanaendelea na utafiti kubaini endapo madini yanayoendelea kuchimbwa na wananchi kwenye maeneo ya milima na Mtoni kwenye Kijiji cha Samunge ni dhahabu kweli.
Aidha amekanusha taarifa zilizozagaa kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kuwa kuna ongezeko kubwa la watu kwenye kijiji hicho toka maeneo mbalimbali ya nchi tokea kubainika kuwepo kwa dhahabu hiyo katikati ya Machi mwaka huu, akisema kuwa wageni hawazidi asilimia 5.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa jana, alisema kuwa wataalamu hao kutoka ofisi ya madini Kanda ya Kaskazini wanatazamiwa kumpatia matokeo ya utafiti huo wakati wowote.
Wawa Lali alisema kuwa hakuna madini yanayookotwa juu ardhi bali yanachimbwa, huku akionya kuwa huenda upotoshaji huo unafanywa ili kunufaisha baadhi ya watu ikiwemo kijiji hicho ambacho hutoza sh 10,000 kwa kila mtu anayeingia.
Hata hivyo, alisema kuwa baada ya matokeo ya wataalamu wa madini kutolewa na ikibainika ni madini ya aina gani yanayopatikana Samunge, serikali itatoa muongozo juu ya namna ya kuyachimba ili kuepuka maafa yanayoweza kujitokeza endapo watu wataachwa kuchimba holela kama ilivyo sasa.
Alifafanua kuwa hakuna watu 4,000 kwenye Kijiji cha Samunge kama inavyoelezwa, kwani kwa mujibu wa tathmini iliyofanyika kijijini hapo, watu wanaochimba madini hayo ni kati ya 500 hadi 600 na kati yao wenyeji wa kijiji hicho ni asilimia 80.
Alisema kuwa wengine asilimia 10 wanatoka ndani ya Kata ya Samunge na tano wanatoka wilayani Ngorongoro, huku asilimia tano tu ndio wanaotoka nje ya Kata ya Samunge.

UTEUZI WA NAFASI ZA UONGOZI UDSM

UDSM Alumni
APPOINTMENT OF
PRINCIPALS, DEANS AND DIRECTOR
This is to inform the University of Dar es Salaam community and the general public that the Acting Chancellor, Ambassador Nicholas A. Kuhanga, in exercise of the powers vested upon him under section 55 of the Universities Act No. 7 of 2005, has made the following appointments for the remainder of the 2012/2013-2014/2015 triennium.

MPIGA PICHA WA MLIMANI TELEVISION AFARIKI DUNIA

R.I.P MAXMILLIAN NGUBE, SHUJAA WA KAMERA MLIMANI TV, UTAKUMBUKWA DAIMA
10:06 AM No comments
Wingu zito latanda baada ya tasnia ya habari kupokea kwa uchungu na masikitiko makubwa, kifo cha mzee wetu Max aliyejulikana zaidi kama papaa Max.
Alikuwa ni mfanyakazi hodari kutoka Mlimani TV, hakika wanamlimani na wapenzi wa tasnia ya habari kwa ujumla wamemkosha shujaa, kipenzi cha wengi na msema kweli,
Alikuwa ni mpiga picha hodari wa Mlimani TV kwa muda mrefu sana, Tutakukumbuka daima.
Alipenda kujulikana kama papaa Max na msiba utakuwa nyumbani kwa marehemu maeneo ya tegeta, mtandao huu utaendelea kukujuza juu ya mengi kuhusiana na mpiga picha huyu maarufu.
endelea kuwa nasi…!
Mungu ailaze Roho ya marehemu Maximillian Ngube mahara pema peponi.Amina

MASHABIKI WA URUGUAY WATISHIA KUMUUA ALIEMUUMIZA SUAREZ

Suarez;Wauruguay wamtishia Dummett
Jeraha la Suarez sasa mashabiki wa Uruguay wamlaumu mlinzi wa Newcastle Paul Dummett.
Mlinzi wa Newcastle Paul Dummett ametishiwa maisha yake na mashabiki wa Uruguay wanaomlaumu kwa kusababisha jeraha lililomlazimu Luis Suarez kufanyiwa upasuaji ambao sasa wanahofu huenda ikaathiri uwezo wake katika kombe la dunia .
Suarez; Wauruguay wamtishia Dummett
Mashabiki hao walimtumia Dummett, 22 jumbe kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter wakimkaripia kwa kumchezea Suarez visivyo alipoonyeshwa kadi nyekundu liverpool ilipoilaza Newcastle 2-1 uwanjani Anfield.
Suarez;Wauruguay wamtishia Dummett
Uruguay imeratibiwa kufungua kampeini yao kombe la dunia katika kundi D dhidi ya Costa Rica mnano Juni 14 na kisha kuchuana dhidi ya Uingereza siku tano baadaye.
Dummett ametajwa katika kikosi cha Wales kinachopangiwa kuchuana na Uholanzi katika mechi ya kujipima nguvu juma lijalo.

FACEBOOK YAMUOKOA MKWEZI WA MILIMA NA KIFO

John All aliyeokolewa na facebook
Mkwezi wa milima mirefu ameokolewa kutoka futi 80 bondeni alipoandika ''Nahitaji msaada'' katika mtandao wa Facebook
Profesa huyo wa jiografia aliwaambia marafiki zake wa Facebook kuwa alikuwa ameanguka ndani ya bonde la Himalaya umbali wa futi 19,600 kwenda chini.
Profesa John All aliandika taarifa hii kwenye ukurasa wa facebook wa ‘'American Climber Science Program’' baada ya kuanguka kwendye bonde hilo. All mwenye umri wa miaka 44 aliteguka bega, kuvunja mbavu tano, goti, na kiwiko.
All aliandika, ‘’ tafadhali muwafahamishe waokoaji wa Global, John amevunjika mkono, mbavu na huenda anavuja damu ndani ya mwili. Tafadhali harakisheni’’
Marafiki wake wa Facebook waliona video ya All akiwa na majeraha na kuwajulisha waokoaji kilichokuwa kikitendeka na kisha kuwasisliana na All na kumwambia kuwa atapata msaada.
Baada ya saa kadhaa, All aliandika kwenye ukurasa huo wa Facebook kuwa waokoaji hawangeweza kumpata kwa kutumia helikopta kwa hivyo angejitahidi ingawa kulikuweko na baridi na alikuwa na maumivu mengi.
Baada ya saa 19, profesa All aliokolewa na kupelekwa hospitalini mjini Kathmandu ambako anapata matibabu.
BBC

MOURINHO AKEBEHI UBINGWA WA ARSENAL

Miezi kadhaa iliyopita kocha wa Chelsea Jose Mourinho alimpa jina la “Special in Failure” mpinzani wake Arsene Wenger ambaye ni kocha wa klabu ya Arsenal.
Moja ya sababu kuu ya Mourinho kumpa jina hilo Wenger ni kutokana na kushindwa kwake kuiongoza Arsenal kushinda ubingwa kwa kipindi cha takribani miaka 9.
Lakini mapema wiki iliyopita, Wenger aliiongoza Arsenal kushinda ubingwa wa FA Cup, na wakati huo Mourinho alikuwa akijiandaa na safari ya kwenda barani Africa kwa ajili ya kufanya kazi za ubalozi wake wa shirika la chakula duniani WFP.
Mourinho alialikwa na kituo cha Channel 4 kwa ajili ya Interview kuzungumzia mambo mambo mbalimbali juu ya safari yake ya Africa, lakini pia mambo yanayohusiana na soka, na moja kati ya swali aliloulizwa lilikuwa juu ya kufikiria kubadilisha mtazamo wake juu ya Wenger kuhusu kuwa bingwa wa kufeli: Mourinho alijibu – “Katika miaka 9 iliyopita Arsenal wameshinda kombe moja tu la FA Cup……….mmmmh huu utakuwa muda mzuri kwao.”

MASKINI:MAMA AJIFUNGUA MTOTO WA AJABU ASIE NA KIUNO WALA MIKONO HANDENI

Tangu mwaka 2012 zaidi ya watoto 154 wamezaliwa na wanawake walio juu ya umri wa miaka 50. Miongoni mwao, wamo waliotokana na teknolojia ya upandikizaji.
Pamoja na madaktari kuonya kuwa kuzaa katika umri mkubwa kunahatarisha maisha ya mama na mtoto, wanawake hasa matajiri wamekuwa wakizaa katika umri mkubwa. Wilayani Handeni Mkoa wa Tanga, Mwajuma Seif (50) aliweka rekodi ya kujifungua watoto mapacha katika umri huo.
Lakini Mwajuma ana kingine cha ziada tofauti na wanawake wengi wanaozaa katika umri huo; alizaa kwa njia ya kawaida na si kwa teknolojia ya upandikizaji.
Tofauti nyingine ya mwanamke huyo si kwamba alizaa katika umri huo kwa kuwa hakuwa na mtoto; ujauzito huo ulikuwa ni wa 13.
Daktari anayemwangalia Mwajuma, Elinisa Mushi anasimulia mkasa wa mwanamke huyo akisema pamoja na umri, kingine kilichomshangaza ni mtoto wa ajabu aliyemzaa .
Anaeleza kuwa walimpokea Mwajuma, ambaye ni mkazi wa Kata ya Sindeni zaidi ya mwezi mmoja uliopita akiwa na ujauzito, lakini walishangazwa na tumbo la mama huyo kwani lilikuwa kubwa sana kiasi cha kuhisi kulikuwa na tatizo fulani. Ndipo walipoamua kuanza kumfanyia uchunguzi.
Baada ya kupima ujauzito huo kwa kutumia mashine yaultra sound(kamera ya mionzi), waliona ni kweli tumboni kuna watoto wenye maumbo yasiyoeleweka hivyo walitaka kumsafirisha kumpeleka Hospitali ya Mkoa wa Tanga, Bombo lakini walishindwa kutokana na hali yake.
Anasema baada ya kugundua kuwa hawataweza kumsafirisha kutokana na hali yake, ilibidi wamuweke katika ulisimamizi maalumu hadi siku ya kujifungua. Alijifungua kwa njia ya upasuaji.
Katika upasuaji, madaktari walimtoa mtoto wa kwanza mwenye umbo la ajabu akiwa na kilo sita na wa pili akiwa na kilo 1.5.
Anafafanua kuwa mtoto alipotolewa tumboni ingawa hakuwa wa kawaida, alikuwa anapumua. Baada ya muda alianza kutoka maji na saa moja baadaye alifariki dunia. Mtoto mwingine aliishi kwa siku moja na akafariki.
“Alikuwa na kilo sita pia alikuwa amevimba sana. Huu ni uzito mkubwa sana kwa mtoto. Baada ya muda mfupi alianza kutoka maji hadi mwili ukapungua kiasi na baadaye alifariki. Mwenzie aliendelea kuishi kwa saa 24,” anasema Dk Mushi.
Mtoto huyo alizaliwa akiwa na miguu yote miwili, lakini iliyoungana na kichwa chenye mdomo na masikio yanayoonekana kwa mbali. Hana kiuno wala mikono.
MWANANCHI

Alhamisi, 22 Mei 2014

AWARUSHIA MABOMU POLISI WASIKAMATE MHALIFU.

Watu wawili wamejeruhiwa katika mlipuko uliotokea mjini Mombasa pwani ya Kenya.
Miongoni mwa wawili hao ni afisa wa polisi aliyekimbizwa katika hospitali ya mkoa kupokea matibabu.
Shambulio hilo lilitokea wakati maafisa wa polisi walimkamata mshukiwa wa ugaidi, na hapo pakatokea mtu wa pili aliyewarushia guruneti katika jitihada ya kumuokoa mshukiwa aliyekamatwa.
Mbunge wa Mvita kutoka eneo hilo, Abdulswamad Sharrif ambaye ni miongoni mwa viongozi waliofika katika eneo hilo punde baada ya mlipuko huo, amelaumu udhaifu katika idara ya ujasusi Kenya kwa kutoweza kutambua mipango ya mashambulio kama hayo kabla ya yafanyike, ili kuweza kuyatibua.
Akizungumza na BBC Abdulswamad amesema, 'Ni lazima tuweze kukubali kasoro iko wapi, ili tuweze kujua suluhisho litakuja vipi'.
Shabulio hilo limetokea wakati usalama umeimarishwa nchini Kenya kutokana na tisho la kutokea shambulio la kigaidi dhidi ya maeneo ya umma.
Katika siku za hivi karibuni Kenya imekuwa ikikabiliwa na mashambulio kadhaa katika maeneo mbali mbali nchini ukiwemo mji huo wa Mombasa na Nairobi, yaliosababisha vifo vya watu kadhaa na wengine wengi kujeruhiwa.
Ni hivi juzi tu watu 10 waliuawa huku zaidi ya hamsini walijeruhiwa katika milipuko miwili iliotokea katika Soko kubwa la nguo la Gikomba katika mji mkuu Nairobi.

HONGERA BWANA GABRIEL NDERUMAKI KWA KUTEULIWA KUWA MHARIRI MTENDAJI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bwana Gabriel Lyimo Nderumaki kuwa Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali, Tanzania Standard NewsPapers (TSN).
Kulingana na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue, Uteuzi huu umeanza tarehe 19 Mei, 2014.
Kabla ya uteuzi huo Bwana Nderumaki alikuwa Kaimu Mhariri Mtendaji wa Kampuni hiyo.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
22 Mei, 2014

JESHI LAPINDUA SERIKALI THAILAND

Mkuu wa majeshi nchini Thailand ametangaza mapinduzi , akisema jeshi sasa linachukua udhibiti wa serikali.
Katika taarifa iliyotolewa kupitia kwa televisheni, mkuu huyo wa majeshi alisema jeshi litarejesha utawala wa kisheria na kufanya mageuzi ya kisiasa.
Majeshi yalizingira eneo la tukio mjini Bangkok ambapo makundi ya kisiasa yamekuwa yakifanya mazungumzo kwa siku ya pili na kuwachukua viongozi wao.
Mapinduzi haya yanakuja baada ya miezi kadhaa ya ghasia za kisiasa na kuwekwa kwa sheria ya kijeshi.
Jeshi litatuma vikosi na magari kuwasindikiza waandamanaji kutoka maeneo ya maandamano , afisa wa kijeshi alilieleza shirika la habari la Reuters.
Ghasia za hivi karibuni zialianza katika mji mkuu wa Thailand mwishoni mwa mwaka jana, wakati waziri mkuu Yingluck Shinawatra alipovunja bunge la nchi hiyo .
Waandamanaji waliweka vizuizi kwenye maeneo ya mji wa Bangkok katika kipindi cha mwezi mmoja.
Mapema mwezi huu , mahakama ilimuamuru kuondolewa madarakani kwa Bi Yingluck kwa madai ya kutumia vibaya mamlaka.
Thailand imekabiliwa na mzozo wa kupigania mamlaka tangu kaka yake Bi Yingluck , Thaksin Shinawatra, kung'olewa mamlakani na jeshi kama waziri mkuu mnamo mwaka 2006.

MGOMBEA UWAZIRI MALAWI AJINYONGA BAADA YA MATOKEO.

Naibu waziri wa serikali za mitaa wa Malawi amejipiga risasi na kujiua nyumbani kwake mjini Lilongwe.
Godfrey Kamanya alikuwa anayegombea kutetea kiti chake cha ubunge katika jimbo la Nzonzi Kusini amejiua alfajiri ya leo katika mojawapo ya vyumba vya nyumba yake iliyopo Area Ten mjini Lilongwe.
Mwili wa marehemu umehifadhiwa kwenye hospitali kuu ya Kamuzu mjini humo, na jeshi la polisi litatoa taarifa rasmi ya kifo hicho baada kukamilisha uchunguzi.
Haijajulikana sababu za Kamanya kujiua japokuwa ameacha barua ya maelezo ambayo polisi wataitoa baadae.
Matokeo ya kura bado hayajatangazwa rasmi katika kile kinachosemekana kuwa uchaguzi wenye ushindani mkali sana.
Afisa mkuu wa uchaguzi, amesema kuwa mfumo wa elektroniki umeharibika na maafisa wanatumia matokeo kwa njia ya barua pepe.

BILIONEA ANAEMILIKI UTAJILI WA $8.8 BILION AAMLIWA KUTOA TALAKA YA $4.5 BILION KWA MKEWE.

Mahakama nchini Uswisi imeamuru Dmitry Rybolovlev, mmiliki wa klabu maarufu ya Ufaransa, AS Monaco kumlipa zaidi ya dola za kimarekani 4.5 bilioni mke wake wa zamani Elena Rybolovleva katika kile kinasemwa kwamba ni moja ya talaka au usuluhishi wa ndoa ghali wa kihistoria duniani.
Mwenendo wa kesi hiyo ya ndoa ilianza mapena mwaka 2008 wakati mke wake huyo wa zamani alidai kiasi cha dola za kimarekani 5.77 bilioni kutoka mwa tajiri huyo wa kirusi. Wote wa umri wa miaka 47 na walikaa kwenye ndoa miaka 24.
Katika hukumu hiyo ya mahakama mke huyo wa zamani wa bilionea wa kirusi alipewa vitu vyenye thamani paundi 146 milioni katika eneo la Gstaad. Mwanamama huyo alipewa pia majumba mawili katika jiji la Colony, sehemu ambayo wanandoa hao wa zamani walikuwa wakiishi na binti zao wawili na kuhakikishia kupewa ulinzi wa binti zao Anna mwenye umri wa miaka 13 na Ekaterina mwenye miaka 14 ambaye ni binti maarufu kwenye jamii.
Wanandoa hao walikutana kama wanafunzi katika chuo kikuu cha Perm nchini Urusi, na wakafunga ndoa mwaka 1987. Walikuwa mahakama kwa muda wa miaka sita katika vita kali vya kimahakama ambapo bilionea Rybolovlev aliweka upinzani mkali kuhusu mali zake ghali mno katika majiji ya Marekani na mali ya thamani paundi 100 milioni katika kisiwa cha Skorpios nchini Ugiriki.
Rybolovlev pia anamiliki nyumba Hawaii ambayo alinunua kutoka kwa muigizaji Will Smith, na ghorofa lenye urefu wa mita 6,744 katika jiji la Manhattan. Mwaka 2008, pia alinunua ghorofa kutoka kwa Donald Trump yenye urefu wa mita 33,000 kwenda juu la sq ft Maison L’ Amitie kwa dola za kimarekani 95 milioni.
Katika jarida la Forbes orodha ya mwaka 2014, Dmitry Rybolovlev alikuwa nafasi ya 147 kati ya mabilionea duniani na thamani halisi ya utajiri wake ni dola bilioni 8.8.

WATOTO WA MASKINI KUSOMA BURE

SERIKALI kupitia halmashauri zote nchini ina mpango wa kuwasaidia na kuwalipia ada na michango mingine wanafunzi ambao wazazi wao hawana uwezo.
Kauli hiyoilitolewa bungeni jana na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa, alipokuwa akijibu swali la nyongeza la mbunge wa Viti Maalum, Kulthum Mchuhuli(CUF), aliyetaka kujua makakati wa serikali kuhusiana na wanafunzi ambao hawajapata matokeo yao kwa sababu ya kutolipa ada za mitihani.
“Siwezi sema wale wote asilimia saba ambao hawajalipa na kushindwa kupata matokeo yao kwamba ni masikini, lakini wanafunzi ambao hawalipiwi na halmashauri sisi wote na wahisani tunawajibu wa kuwasaidia ili waweze kupata matokeo yao,”alisema Waziri Kawambwa.
Katika swali la msingi, Mchuchuli alitaka kujua ni wanafunzi wangapi wa kidato cha nne ambao hawajapata matokeo yao kwa sababu ya kutolipa ada za mitihani.
Akiendelea kujibu swali hilo, Waziri Kawambwa alisema serikali itajitahidi kwa kila namna, ili wanafunzi hao wapate matokeo yao.
Alisema katika matokeo ya mtihani wa kidato cha nne mwaka jana, watahiniwa 31,518 kati ya watahiniwa 404,083 waliofanya mtihani huo matokeo yao yalizuiwa kwa sababu ya kutolipa ada.
Alieleza idadi hiyo ni sawa na asilimia 7.79 ya watahiniwa waliofanya mtihani huo.
Hata hivyo, alisema matokeo yaliyozuiwa hufunguliwa mara moja baada ya mtahiniwa husika kulipa ada yake.
“Hadi Mei 8 mwaka huu, jumla ya watahiniwa 7,1314 wameshawasilisha ada zao na kufunguliwa matokeo yao na hivyo idadi ya watahiniwa ambao bado hawajawasilisha malipo yao ya ada ni 24,204,”alisema Dk. Kawambwa.
Aliwasihi wazazi na walezi wa watahiniwa ambao matokeo yao yamezuiliwa, kulipa ada hizo mapema, ili matokeo hayo yaweze kufunguliwa na kutoa fursa kwa wanafunzi hao kuendelea na kozi mbalimbali.
TANZANIA DAIMA

Jumatano, 21 Mei 2014

MAMAAKE ZITO ALAZWA CHUMBA CHA WAGONJWA MAHUTUTI

Dar es Salaam.Mwenyekiti wa Chama cha Walemavu Tanzania, (Chawata), Shida Salum, yuko katika chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu (ICU) katika Hospitali ya Ami, Masaki, Dar es Salaam akisumbuliwa na maradhi ya saratani.
Shida ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema na mama mzazi wa Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe amelazwa tangu juzi. Alianza kusumbuliwa na maradhi hayo mapema Agosti mwaka jana lakini hali yake ilibadilika mapema mwaka huu akiwa mjini Dodoma akisubiri kuapishwa pamoja na wajumbe wengine wa Bunge Maalumu la Katiba.
Akizungumza hospitalini hapo jana, Zitto alisema baada ya hali ya mama yake kuwa mbaya alishindwa kuendelea kukaa Dodoma kusubiri kuapishwa na alipelekwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), ambako aligundulika kuwa na saratani ya shingo ya kizazi na kupatiwa tiba kwa mwezi mmoja kabla ya kupelekwa India kwa matibabu zaidi.
Alisema kabla ya kupelekwa hospitalini hapo, alikuwa akiendelea kupata matibabu akiwa nyumbani, lakini hali yake ilibadilika juzi.
Zitto alisema hali ya mama yake haijatengemaa tangu aanze kusumbuliwa na maradhi hayo. Alisema kutokana na maradhi hayo ya mama yake, ameshindwa kuhudhuria Bunge la Bajeti linaloendelea mjini Dodoma.
“Hali ya mama kwa kweli siyo nzuri, lakini nina imani itakuwa nzuri na kuendelea na shughuli za ujenzi wa taifa kama zamani,” alisema Kabwe.
Tangu kuanza kwa Bunge la Bajeti, Zitto alionekana Dodoma mara moja tu, siku ilipowasilishwa Ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).
MWANANCHI

ATEKWA NA KUISHI NA MTEKAJI KINDOA KWA MIAKA 10

Mwanamke mmoja, wa miaka 25, aliyepotea miaka 10 iliyopita, amewaambia polisi kuwa alilazimika kuolewa na aliyemteka nyara na kisha kupata mtoto naye.
Mwanamke huyo, kutoka Santa Ana, ambaye jina lake halikutajwa, aliwasiliana na polisi baada ya kumpata dadake katika mtandao wa Facebook.
Isidro Garcia, mwenye umri wa miaka 41, alikamatwa Jumanne kwa tuhuma za kuteka nyara, kubaka na kumdhulumu mwanamke huyo.
Katika taarifa yao, polisi walisema kuwa Garcia alikua anaishi na familia ya mwanamke huyo wakati ambapo alitoweka.
Unyanyasaji wa miaka kumi
Taarifa hiyo ilisema kuwa unyanyasaji huo ulianza mwaka wa 2004, wakati ambapo Garcia na mamake muathiriwa walikua wachumba.
Garcia aliishi pamoja na mamake muathiriwa na wanawe wa kike huko Santa Ana, ambao ni mji katika kaunti ya Orange.
Garcia alimteka mwanamke huyo akiwa na umri wa miaka 15
Madai ya polisi ni kuwa Garcia alianza kumnyanyasa kijinsia mwathiriwa katika mwezi wa Juni, mwaka huo.
Miezi miwili baadaye, alimshambulia mamake muathiriwa, kisha akamleweshaa msichana huyo, na kumpeleka maili 26 kaskazini, hadi Compton, alikomfungia na kumzuia.
Garcia alimtisha msichana huyo dhidi ya kurudi kwa familia yake.
Wawili hao waliikwepa polisi kwa muda
Mara nyingi, Garcia alimdhulumu msichana huyo kimwili na kwa njia ya ngono.
Maisha ya kifungo
Walifanya kazi pamoja katika huduma moja ya usafi, usiku. Muathiriwa alishindwa kabisa kujinusuru na aliendelea kuishi na Garcia akidhulumiwa.
Mwaka wa 2007, Garcia alimlazimisha mwanamke huyo waoane na mwaka wa 2012, wawili hao wakapata mwana.
Ni juzi tu, ambapo muathiriwa huyo aliwasiliana na dadake kupitia mtandao wa Facebook na hatimaye alipata ujasiri wa kuwasiliana na polisi.
Vyombo vya habari viliripoti kuwa polisi waliitwa katika nyumba hiyo siku ya Jumatatu jioni ili kuhudumia tukio la kinyumbani na ndipo muathiriwa huyo akawaambia alikua ametekwa kwa muda wa miaka 10.
Garcia aliyekamatwa Jumanne, bado hajasomewa mashtaka yake kamili.

ANGALIA MAMBO 5 YANAYOFANYA WACHINA KUFANIKIWA KIBIASHARA.

Secrets Of Success: 5 Lessons From Chinese Entrepreneurs


There’s a reason why people of Chinese origin make up nearly a quarter of the world’s billionaires.
According to the Hurun Rich List, people of Chinese origin account for 24% of the world’s billionaires.
Sure, China has the world’s second largest economy and its citizens constitute a fifth of the planet’s population.
But it is still ranked a lowly 121 on Index Mundi’s list of nations based on GDP (PPP) per capita. Indeed, it is sandwiched between Ecuador and the Caribbean territory of Montserrat, neither of which is an economic superpower.
So if China punches above its weight when it comes to producing entrepreneurs, what can it teach the rest of us about business?
1. Don’t rush decisions
In the West, we make decisions in a hurry. Being ‘busy’ is a badge of honor, and we expect everything to be done yesterday. In China, entrepreneurs take their time over the things that matter. They take time to make decisions and they take time to trust people. They get criticized for dragging their feet, but they get their priorities straight.
2.Do seize opportunities
Wonder why the Chinese already have a powerful presence in resource-rich Africa? They know a good opportunity when they see one, and they’re not afraid to seize it. Once they’ve set their mind to something, Chinese entrepreneurs are very good at doing. Hence they transform their businesses quickly. So what if your company produces electro-components today? It can still generate electricity tomorrow.
3. Know how to adapt
Change does not scare Chinese entrepreneurs. They are continually learning and adapting their business models to fit different circumstances. Those who say the Chinese can’t innovate or only produce low-quality goods do so at their peril. They are becoming more innovative and producing better-quality goods all the time.
4. Look on the bright side
Most of us sound off about government policies that we dislike. But Chinese entrepreneurs don’t waste their energy whining about things they can’t change. They just get on with it. Billionaires in the making are natural optimists; they don’t let politicians spoil their day.
5. Be a decent person
Chinese entrepreneurs care about reputation and integrity. They believe that losing face is shameful so they have a strong sense of honor. Equally, they expect others to deliver on their promises. And they value their communities and their families greatly. They know that building a successful business is a team effort.
China is one of the world’s most exciting economies, and its business leaders continue to amaze and inspire other entrepreneurs around the world. That’s why EY is bringing the Strategic Growth Forum to Shanghai this week from 22-23 May 2014. We want to learn how China punches above its weight – and we know you do, too.
FORBES

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI AUNGA MKONO UASI LIBYA.

Wizara ya maswala ya ndani ya Libya imetoa taarifa ikisema kuwa inaunga mkono kampeini dhidi ya serikali inayoongozwa na jenerali wa zamani wa jeshi la taifaaliyeasi serikali tawala .
Hata hivyo waziri husika Salih al-Mazig baadaye alikanusha kumuunga mkono jenerali muasi Khalifa Haftar, aliyeanzisha operesheni ijumaa iliyopita.
Jenerali Haftar amezindua kampeini ya kivita inayolenga kuingoa mamlakani utawala uliomrithi aliyekuwa kiongozi wa taifa hilo Maummar Gaddafi kuanzia kwa bunge lililoshambuliwa siku ya jumapili.
Jenerali huyo aliongoza wapiganaji wake kuvamia mji wa Benghazi katika kampeini anayoiita "Libya's Dignity".
Jenerali huyo anailaumu serikali kwa kuwatepetevu dhidi ya wapiganaji waasi.
Wizara ya maswala ya ndani tayari imemuunga mkono katika mtandao wake wa kijamii wa Facebook.
Wizara zaasi serikali Libya
Jumatatu hii kiongozi wa jeshi la wanahewa la Libya Jenerali Guma al-Abany, alitoa ujumbe wa kumuunga mkono Jenerali huyo aliyestaafu akisema hatua yake ni jambo la kupigiwa mfano kwa walibya wazalendo.
Kiongozi wa jeshi la wanamaji Brigadia jenerali Hassan Abu-Shannaq,alinusurika jaribio la mauaji muda mchache tu baada ya kutangaza kumuunga mkono jenerali huyo aliyezindua vita dhidi ya wapiganaji wakiislamu ambao wanalumiwa kwa utovu wa usalama nchini Libya.
Serikali imempuzilia mbali jenerali Khalifa Haftar na ikasema kuwa haitajiuzulu .
Takriban watu 100 wameripotiwa kuuawa tangu mapigano hayo kuzuka ijumaa iliyopita na kuilazimisha serikali kuitisha uchaguzi wa haraka tarehe 25 mwezi juni .
Iwapo uchaguzi huu utaendelea mbele basi utakuwa ni uchaguzi wa pili tangu aliyekuwa rais Muammar Gaddafi kungolewa madarakani mwaka wa 2011.
Hadi kufikia sasa Libya imekuwa na mawaziri wakuu watatu tangu mwezi Machi mwaka huu.

WAJAWZITO KULA UDONGO HUSABABISHA UPUNGUFU WA AKILI KWA WATOTO

Udongo unaoliwa na wanawake katika baadhi ya nchi Afrika
Wanawake wanaokula udongo wakiwa wajiwazito wamo katika hatari ya kuwafanya watoto watakowajifungua kutofanya vizuri shuleni.
Utafiti uliofanywa na shirika la African Council for Gifted and Talented unaonyesha kuwa watoto ambao kina mama wao walikuwa wakitumia udongo hawamakiniki darasani.
Mkuu wa shirika hilo Profesa Humprey Obora amewaambia wanahabari jijini Nairobi kuwa utafiti huo umefanywa kwa watoto wanaopelekwa katika taasisi hiyo ambayo hujihusisha kutambua na kukuza vipawa vya watoto wakiwa bado wachanga.
Kwa kawaida wanawake wengi hutumia udongo huo baadhi wakidai kuwa wana upungufu wa madini ila wengi wao huzidisha matumizi yake.
Mtoto akiwa kwenye tumbo la mamake
Zaidi ya wazazi 4000 walihusishwa katika utafiti huo lakini ni 1000 tu ambao maoni yao yalitumika kuandaa ripoti ya utafiti huo.
Taasisi hiyo ilikuwa ikifuatilia matokeo ya watoto hao wakiwa shuleni kwa muda wa miaka minne na wakatambua kuwa wale ambao hawakuwa imara darasani mama zao walikuwa na historia ya kutumia udongo wakiwa wamebeba mimba zao.
Watafiti hao wanasema kuwa kutokana na hayo ubongo wa watoto waliozaliwa huchelewa kushika mambo.
Wasimamizi wa mradi huo waliwahusisha wazazi kutoka katika sehemu mbalimbali nchini Kenya ambako kuna vituo vya shirika la African Council for Gifted and Talented.
Kadhalika utafiti huo unaonyesha kuwa wanawake katika miaka ya ishirini huwa na hamu kubwa kutumia udongo.
BBC

ANGALIA FID Q ALIVYOMUONYA DYNA KUACHA KUTUMIA MIKOROGO KATIKA MISTARI YAKE

Fid Q na Dayna na Fid Q ameingia hasa utata wa kwenye line zake kadhaa kwenye wimbo wa Sina Muda wa Jcb ambazo zimeonekana kumhusu moja kwa moja Dayna.
Fid Q ameonekana kama anamfokea Dayna kwa kutumia mkorogo unao badilisha ngozi yake na kuonekana mweupu kitu ambacho Fid Q amedai kuwa Dayna anaukimbia uafrika,Mistari ya Verse hiyo iko hivi.
“Hi Dayna, sikufichi ulikua unahusika/
au mtoto wa uswazi ‘ akijichubua ‘ haimaanishi anaukimbia uafrika?/
nisikize Dayna..please.. najua uko busy kiaina na hizi ni aina tu za uchizi au kama vipi bye DAYNA/
HUUH.. now back to you fools/
Soudy brown kamtafuta Fid Q ambapo alipoulizwa kuhusu hili majibu yake alidai kuwa katika ngoma hiyo hamzungumzii Dayna Msanii bali anamzungumzia Dayna msichana anayeishi nae kitaani maeneo ya Mikocheni kwa Nyerere.
Dayna huyo wa kiafrika alikua mweusi sasa hivi amejichubua ngozi yake na kuwa mweupe ambapo baadae Fid Q aliuchambua kiutaalam mstari huo na kusema kuwa wadada wanaofanya hivyo wanaua melanie.
Ambacho ni kitu muhimu sana kwenye ngozi na hupatikana zaidi kwenye ngozi nyeusi ya kiafrika chembechembe ambazo huilinda ngozi isiunguzwe na jua.
Majibu ya Dayna baada ya kupigiwa simu na Soudy Brown kutaka kujua kama ameshaisikia hiyo line ya Fid Q alichokijibu ni ameisikia na anamuheshimu Fid Q kwa wazo lake ila kwa wakati huu amepunguza kidogo kutumia mikorogo.

KUTANA NA KIJANA MWENYE UKIMWI ANAEWAELIMISHA VIJANA WENZAKE JUU YA UGONJWA HUO KWA MITANDAO

Kijana mwenye umri mdogo amekuwa akifanya kampeni kwenye mtandao ili mafunzo bora zaidi yatolewe katika shule kuhusu maradhi ya HIV nchini Uingereza.
Luke Alexander aliye na umri wa miaka kumi na tisa anasema kuwa vijana wengi wenye umri mdogo hawapati mafunzo mwafaka yanayoweza kuwasaidia kuuepuka ugonjwa huo.
Shirika la kujitolea linalohusiana na maswala ya UKIMWI Terrence Higgins Trust, linasema kuwa swala hilo hugusiwa tu wakati wa somo la Sayansi, hivyo basi wanafunzi wengi hukosa kupata elimu muhimu kuhusu maradhi ya ukimwi.
Serikali iliambia idhaa ya BBC Newsbeat mjini London kwamba ni lazima wanafunzi wajifunze kuhusu magonjwa yanayoambukizwa kwa ngono kama vile UKIMWI, kama sehemu ya masomo ya jinsia na uhusiano.
'Kisa cha Luka'
''Nimeishi na ugonjwa wa UKIMWI kwa mwaka mmoja sasa, na inashangaza jinsi maisha yangu yalivyobadilika.
''Unaposikia habari zinazosambaratisha ndoto zako namna hii, kwa kweli unapata mtazamo mpya wa mambo, na wakati mwingine, maisha yanakosa manufaa.
''Nilikuwa na umri wa miaka 19 nilipopimwa na kupatikana na ugonjwa huu.
''Sikujua mengi kuhusu UKIMWI, na kwa hivyo nikadhani ugonjwa huo hauwezi kuepukika, na kwamba maisha yangu yangekumbwa na upweke na machungu, kabla ya kuugua na kuaga dunia ningali kijana mdogo.
''Labda hayo yangekuwa kweli miaka ya themanini, lakini sasa ni mwaka wa 2013, na baada ya uoga wangu wa kwanza, nilifurahi kugundua kwamba maisha yangu hayatakuwa kama kifungo cha maisha, bali kama msururu mrefu wa maisha.
''Nilipata ufahamu na uelewa kuhusu UKIMWI kwa filamu nilizotazama kama vile Philadelphia na Transpotting.
''Lakini kwa kweli, nilijifunza chochote kuhusiana na UKIMWI shuleni? Hapana.
''Ninapotafakari kuhusiana na masomo yangu ya shule ya upili, ni jambo la kuvunja moyo kugundua kwamba sikujifunza chochote kuhusiana na ugonjwa huu.
''Kumbukumbu zangu kuhusu somo la jinsia na uhusiano shuleni, ni kumsikiliza tu mwalimu mwenye aibu akizungumzia mimba, kuavya mimba na maradhi ya Chlamydia kwa kugusia tu.
'Ukosefu wa elimu'
''Niliponyanyua mkono na kuuliza kuhusu ngono nilitarajia jibu lenye utaalamu na lenye kuhusisha, lakini nilitazamwa kama mtu mwenye kinyaa na kujibiwa kuwa hilo halipendekezwi.
''Mimi sasa ni mwanaharakati wa kuhamasisha kuhusu UKIMWI, anayefanya uandishi ili kujaribu kuwaelimisha watu kuhusiana na maswala ya virusi hivyo, na kujaribu kuondoa unyanyapaa unaohusiana na swala hili.
Wakfu wa Luke mjini London
''Mimi hupata angaa jumbe 10 wa kuuliza maswali kutoka kwa vijana wadogo walioambukizwa ugonjwa huu kila siku.
''Mbali na mashauri waliopewa walipopimwa, wao huwa na hakika kuwa wanakwenda kuaga dunia.
''Wengi wao husema kwamba hawajawahi kufunzwa chochote kuhusiana na ugonjwa wenyewe wakiwa shuleni au nyumbani, na wengine huamini kuwa ni kama kifungo cha maisha.
'Maisha ya kaiwada'
''Ni sawa sawa kabisa na ninapowaambia rafiki zangu kuhusu hali yangu. Wawili wao, Charlotte Young na Charlotte Morris( walioonyeshwa kwenye picha), wote walihofia kwa ningekufa, walipogundua kuwa nina ugonjwa wa UKIMWI.
''Wote walioshuhudia matangazo ya kuogofya kwenye runinga na usambazaji wa vijikaratasi vya afya miaka ya themanini walijua misimamo yao, lakini wakasahau vizazi vipya.
''Wengi wana hisia kwamba magonjwa ya zinaa yanaweza kutibiwa kwa tembe zinazopatikana katika maduka ya kawaida ya dawa.
Marafiki wa Luca
''Wakati nikikiri kwamba sikujua kuhusu ugonjwa wa UKIMWI, na kwamba niliambukizwa kutokana na upuuzi wangu wa kufanya mapenzi bila kinga, ni aibu kubwa kwamba sijui zaidi.
''Mwaka jana kampuni la Ofsleg lilidai kwamba zaidi ya thuluthi moja ya shule nchini Uingereza hazikutoa mafunzo mazuri kwa wanafunzi kuhusiana na somo la jinsia na uhusiano.
''Kwa mtazamo wangu, shida hii inaendelea huku masomo ya ngono yakiwazuia vijana kujifunza chochote kuhusu kujikinga kimapenzi na kuiachia nambari yenye bahati mbaya kuchukuliwa na ugonjwa usio tiba, na ambao hawajawahi kusikia kuuhusu.”
BBC

WEZI WA WIMBO WA PHARRELL WILLIAMS WAKAMATWA IRAN

Kanda hiyo inaonyesha watu wakicheza katika barabara za mjini Tehran
Kikundi cha mashabiki wa muziki nchini Iran walioiga wimbo maarufu wa mwanamuziki maarufu wa Marekani Pharrell Williams, 'Happy' wamejipata matatni baada ya kukamatwa na polisi.
Kanda ya video waliyoirekodi wakiiga wimbo huo, inaonyesha vijana watatu na wanawake kadhaa ambao hawakuwa wamejitanda mitandoa, wakicheza densi kwenye barabara za nchi hiyo na kwenye paa za nyumba mjini Tehran.
Mkuu wa Polisi, Hossein Sajedinia, alisema kuwa kanda ya video inayoonyesha vijana hao wakicheza, imekiuka maadili ya jamii.
Kituo cha televisheni ya serikali kilionyesha vijana hao wakikiri makosa siku ya Jumanne.
Inaarifiwa maelfu ya wananchi wa Iran wamekamatwa katika miaka 35 iliyopita wakisherehekea na kujiburudisha kwa mambo ambayo serikali inaona kama ya kukiuka maadili.
Hata hivyo vijana hao wanaosema ni waigizaji wanadai kuwa walihadaiwa kushiriki katika kanda hiyo na watu waliokuwa wanatafuta waigizaji wakisema ulikuwa kama mtuhani kwao.
"waliniambia kuwa wanatengeza filamu na kuwa walikuwa na kibali na ndio maana nikakubali kushiriki,'' alisema mmoja wa vijana waliokamatwa.
Mtuhumiwa mwingine alisema walionasa kanda hiyo waliwaahidi kwamba hawataisambaza.
Kanda hiyo imetazamwa na watu 40,000
'Wamekiuka maadili'
Kulingana na taarifa ambazo bado hazijathibitishwa, watu 13 walikamatwa kuhusiana na kanda hiyo, ingawa idadi kamili ya waliokamatwa haijatangazwa rasmi.
Pharrel aliyeteuliwa kwa tuzo la Oscar kwa wimbo wake huo mwaka huu ambao umekuwa maaruufu sana duniani, alielezea kukasirishwa na hatua ya vijana hao kukamatwa.
"yani siamini kama watoto hawa walikamatwa kwa kujaribu kueneza furaha,'' alisema Pharrell katika ukurasa wake wa Facebook.
Pharrell aliteuliwa kwa tuzo la Oscar mwaka huu
Chini ya sheria za kiisilamu, sharti mwanamke ajitande kutoka kichwani hadi katika viganja vya mguu.
Polisi ambao jukumu lao ni kuhakikisha kuwa sheria ya mavazi inafuatwa, hushika doria mara kwa mara katika barabara za mji mkuu Tehran.
Kanda hiyo ya "Happy we are from Tehran" ilionekana kwenye mtandao wa Youtube tarehe 19 Mei na kufikia sasa imetazamwa mara 40,000.
Baadhi wametuma ujumbe wa kukejeli serikali ya Iran wakisema kuwa Iran ni nchi ambako ni hatia kwa mtu kuwa na furaha.
Wimbo halisi wa Pharrell 'Happy' umepelekea maelfu ya watu kote duniani kuiga video ya wimbo huo na kutengeza video zao wenyewe. Kutoka Kenya, Marekani , Uingereza yaani nchi nyingi duniani tu, watu wameiga video hiyo kwa kutengeza yao wenyewe.

HOSEN MUBARAK JELA MIAKA MITATU

Rais aliyeondolewa madarakani nchini Misri, Hosni Mubarak amehukumiwa jela miaka mitatu.Wanawe wawili Alaa na Gamal wamepata kifungo cha miaka minne kila mmoja.
Wendesha mashitaka walisema kuwa wanawe Mubarak waliponda mamilioni ya dola pesa za umma zilizotengewa kukarabati ikulu ya Rais na badala yake wakafanyia ukarabati nyumba zao za kifahari.
Wametakiwa kulipa pesa hizo za serikali na kutozwa faini ya dola milioni tatu.

WENGINE 17 WAUAWA BORNO NIGERIA

Watu 17 wameuawa katika shambulizi lililofanywa dhidi ya kijiji kimoja Kaskazini Mashariki mwa Nigeria.
Mji wa Alagarno ambao uko katika jimbo la Borno, uko karibu na mji wa Chibok ambako wasichana zaidi ya miambili walitekwa nyara na kundi la wapiganaji wa kiisilamu la Boko Haram wiki tano zilizopita.
Hili ni shambulizi la hivi karibuni kufanywa nchini Nigeria wakati nchi hiyo ikikumbwa na kitendawili cha kuwatafuta zaidi ya wasichana miambili waliotekwa nyara na Boko Haram.
Juhudi hizo zinawashikirisha wataalamu wa ujasusi wa kimataifa kutoka Israel, Marekani na Uingereza.
Pia limetokea siku moja tu baada ya milipuko miwili kutokea mjini Jos katika jimbo la Plateau ambapo takriban watu 118 waliuawa Jumanne usiku.
Juhudi za kuwatafuta maiti bado zinaendelea.
Mwandishi wa BBC nchini Nigeria anasema kuwa shambulizi lililofanyika mjini Jos, lilisababishwa na Boko Haram na kwamba huenda ni ujumbe kwa serikali kuwa wapiganaji hao wanaweza kushambulia wakati wowote wanapotaka.
BBC

MAAJABU MENGINE:MAELFU YA WANANCHI WAELEKEA LOLIONDO KWA BABU KUFUATA DHAHABU

Arusha.Maelfu ya watu wamemiminika tena katika eneo la Samunge, Wilaya ya Ngorongoro Mkoa wa Arusha, safari hii siyo kunywa Kikombe cha Babu Mchungaji Ambilikile Mwasapile, bali kupata dhahabu inayodaiwa kugundulika katika eneo hilo.
Habari kutoka katika eneo hilo zinasema kuwa watu wanazidi kumiminika katika kujipatia madini hayo yaliyobainika katika mashamba ya watu na maeneo ya kingo za Mto katika Kijiji cha Mgongo kilichopo jirani na Kwa Babu.
Diwani wa Samunge, Jackson Sandea alisema maelfu ya watu kutoka maeneo mbalimbali nchini wamefurika katika kijiji ambacho kuna mto na madini ya dhahabu yanapatikana hapo.
“Hadi sasa kuna watu zaidi ya 4,000 na bado wanaongezeka, hii inaweza kuwa ni zaidi ya kipindi kile cha Babu wa Kikombe. Dhahabu hii inapatikana mtoni tu, watu wanakusanya michanga na kupata dhahabu, hakuna mtu ambaye anachimba,” alisema Sandea.
Alisema tofauti na maeneo mengine, dhahabu ya Samunge inaonekana ni ya Watanzania wote kwani ipo eneo la mto ambao unamilikiwa na Serikali na ndiyo sababu watu wanaingia kwa wingi.
“Kuna wengine wanapata hata mashambani lakini mtoni ndipo inapatikana kwa wingi zaidi,” alisema.
Ulinzi waimarishwa
Diwani huyo alisema ulinzi umeanza kuimarishwa katika eneo hilo akisema hali ikiachwa kama ilivyo, kunaweza kutokea vurugu kubwa na hata mauaji.
“Sisi kama viongozi, tumeweka utaratibu mzuri wa kuchimba madini kiusalama na hata wale ambao wameanza kuuza mashamba yao, tunawawekea utaratibu mzuri,” alisema.
Maofisa madini kutua Samunge
Kamishna wa Madini Kanda ya Kaskazini, Alex Magayane alisema jana kwamba baada ya kupokea taarifa za kugundulika kwa dhahabu katika eneo la Samunge, maofisa wake wanajiandaa kwenda kijijini hapo.
Alisema taarifa za kitaalamu kuhusu akiba ya madini hayo iliyopo Samunge itatolewa baada ya maofisa hao kufika katika eneo hilo na kufanya utafiti.

KUMBUKUMBU:LEO TUNAKUMBUKA KUZAMA KWA MV BUKOBA,TUNAJIFUNZA NINI KWA TUKIO HILO.

Ilikuwa tarehe 21 mwezi wa 5 mwaka 1996, wakati ambapo nchi nzima ya Tanzania ilizizima kwa SIMANZI na MAJONZI. Wakati Rais Benjamin Mkapa alipotangaza na kuthibitisha ajali ya Meli ya Mv Bukoba, ambayo alipoteza maisha ya wa Tanzania wenzetu zaidi ya mia nne 400.. Leo ni miaka 18, toka kutokea kwa tukio hilo, ambalo limeacha kumbukumbu mbaya kwetu kama Taifa. Tuzidi kuwaombea wenzetu, lakini pia tutafakari kila mmoja wetu kwa nafasi yake, JE USAFIRI WA MAJINI TANZANIA NI SALAMA..!!??

Jumanne, 20 Mei 2014

BAADA YA KUJUA KUWA MENEJA EWURA ALIJINYONGA POLISI SASA KUCHUNGUZA SABABU

Dar es Salaam.Aliyekuwa Meneja wa Biashara ya Petroli wa Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura), Julius Gashaza alijinyonga kwa tai. Taarifa iliyotolewa jana Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Temeke, Engelbert Kiondo imesema.
Baada ya taarifa hiyo, Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam imeunda jopo kuchunguza sababu za kifo hicho.
Meneja huyo alikutwa amekufa katika Gesti ya Mwanga Lodge iliyopo Yombo na kifo chake kinaelezwa kutokea katika mazingira ya kutatanisha. Alijinyonga muda mfupi baada ya kuwasili Dar es Salaam akitokea Dodoma ambako alihudhuria mkutano kwenye Kamati ya Bunge ya Bajeti.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alisema jana kuwa jopo hilo litaongozwa na Mkuu wa Upelelezi kanda hiyo, Jaffary Mohamed atakayeshirikiana na wataalamu wa Maabara Kuu ya Polisi, daktari bingwa wa Polisi na serikalini.
Kova alisema jeshi hilo linafanya uchunguzi ili kuondoa utata ulioanza kujitokeza kuhusiana na kifo chake baada ya taarifa kuzagaa kwamba kilitokana na kutoelewana na viongozi wenzake katika masuala ya kikazi.
Alisema uchunguzi huo ukikamilika, jalada litapelekwa kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ili hatua za kisheria zichukuliwe.
“Kinachofanyika ni kupata maelezo ya kina kuhusu mwenendo wa shughuli za marehemu na hali iliyomsibu kabla ya kifo chake kwani hakuacha ujumbe wowote wa maandishi au wa mdomo,” alisema Kova.
Alisema maelezo mbalimbali ya mashahidi yanaendelea kuchukuliwa ili kufahamu kama kuna kosa la kijinai, kiutawala au yote.
Kamanda wa Mkoa wa Temeke
Kamanda Kiondo alisema: “Uchunguzi ninaoufahamu hadi sasa ni kuwa Gashaza alijinyonga kwa kutumia tai yake, akiwa bafuni katika hoteli ya Mwanga. Alitumia stuli kupanda juu, stuli ilianguka na tai ilikatika ndipo mauti yakamfika,” alisema.
Alisema mwili wake ulionekana kuvimba kutokana na kujinyonga na inaonekana mshipa wa hewa ulizibwa na kusababisha kifo chake.
Kamanda Kiondo alisema kutokana na kuthibitika kuwa Gashaza amejinyonga, uchunguzi utakaofanyika ni kujua chanzo cha kujinyonga.
VIA:MWANANCHI.

GHASIA ZAKWAMISHA TENA UCHAGUZI NCHINI MALAWI.

Jeshi lilitumwa kudhibiti ghasia zilizozuka wakati wa uchaguzi mkuu nchini Malawi unaoonekana kama mtihani wa kweli kwa utawala wa rais Joyce Banda unaogubikwa kwa kashfa ya rushwa.
Kufikia kumalizika kwa uchaguzi huo jana, baadhi ya vituo vya kupiga kura tayari vilikuwa vimeanza kuwasilisha matokeo. Hasira na ghasia zilisababisha kutofanyika uchaguzi katika baadhi ya vituo nchini humo. Inaarifiwa kwamba raia waliokosa kupiga kura watapata fursa leo ya kuwachagua viongozi wawatakao.

MASKINI:MWILI WA MAREHEMU AMINA NGARUMA KUWASILI IJUMAA NA KUZIKWA JUMAMOSI.

Mwili wa Ngaluma kuletwa Dar Ijumaa
MWILI wa mwimbaji mahiri nchini aliyefariki dunia wiki iliyopita nchini Thailand, Amina Ngaluma ‘Japanese’ unatarajiwa kuwasili Dar es Salaam Ijumaa wiki hii.
Kwa mujibu wa mume wa marehemu, Rashid Sumuni tayari taratibu muhimu kuhusiana na kuuleta mwili huo nyumbani zimefanyika na wana amini mambo yataenda kama wanavyotarajia.
“Naomba niwajulishe kuwa mwili wa mke wangu utaondoka Thailand Alhamisi wiki hii kwa ndege ya KLM na utawasili Dar es Salaam siku inayofuata saa tatu usiku.
“Tunaamini kama mambo yataenda kama tulivyopanga baada ya mwili kuwasili basi Jumamosi tutamhifadhi mwenzetu. Msiba upo kwa wazazi wa marehemu Kitunda, Machimbo, Dar es Salaam ambako ndiko maziko yatafanyika.
“Kimsingi imekuwa ngumu kusema tutazika lini, kwa sababu bado mwili haujaletwa, lakini tayari familia kwa kushirikiana na sehemu alikokuwa anafanya kazi na Watanzania wengine waishio kule tumeshamaliza taratibu zote zilizokuwa zikihitajika ili kuuleta mwili nchini,” alisema Sumuni kwa masikitiko.
Pia alivishukuru vyombo vya habari kwa kuwa karibu na familia yao wakati wa kipindi hiki kigumu, lakini akiomba wanapotaka kutoa habari kuhusiana na msiba huo wawasiliane na wahusika wa familia ili kupata taarifa sahihi zaidi.
Ngaluma aliyepata kung’ara na bendi mbalimbali nchini, alifariki dunia Alhamisi iliyopita kwa shinikizo la damu akiwa Thailand alikokuwa akifanya shughuli za muziki katika bendi ya Jambo Survivor.
Wakati wa uhai wake alitamba na bendi mbalimbali zikiwemo African Revolution ‘Tamtam’, Double M Sound ‘Mshikemshike’ na TOT Plus zote za Dar es Salaam.
Pia alipigia makundi ya Arusha Sangoma, Sayari Band na Less Mwenge yote ya Arusha na Mangelepa na Sky Sound za Kenya. Pia amepata kufanya shughuli za muziki kwa miezi sita nchini Uganda.
Baadhi ya nyimbo alizotunga wakati wa uhai wake ni Manyanyaso Kazini na Mapendo alizotunga akiwa Tamtam, wakati Double M Sound alitunga nyimbo za Wajane na Ukewenza.
Pia alitoa albamu yake binafsi iitwayo Jitulize yenye nyimbo kama Vidonge, Pete ya Uchumba, Good Night, Uombalo Hutopata, Jitulize na Mzigo wa Moto.
Baadhi ya nyimbo alizopata kuimba na kumpatia umaarufu mkubwa ni Mgumba, Maisha Kitendawili, Ndugu Lawama, Zawadi ya Watanzania, Ugumu wa Maisha na Call Box zote zikitungwa na Muumin Mwinjuma ‘Kocha wa Dunia’. Mungu amuweke mahali pema peponi. Amin.

WALEMAVU WAFUNGA BARABARA YA KARUME

Walemavu wameandamana na kufunga barabara maeneo ya Karume kwa kukaa katikati ya barabara, jijini Dar es salaam wakidai serikali iwarudishie maeneo yao ya zamani waliokuwa wakifanyia biashara.
Walemavu hao wamedai kuwa kuwa serikali iliwadanganya kuwa waondoke katika maeneo ya awali na wangepewa maeneo mengine pale Karume lakini hadi leo hawajapewa maeneo hayo na wao wanazidi kuteseka.

HII YA HUYU JAMAA KUFUNGWA MIAKA 17 BILA KOSA INAONESHA JINSI WANASHERIA WANAVYOKOSEA.

Mwanamume aliyefungwa jela kwa miaka kumi na saba kimakosa ameombwa radhi nchini Uingereza.Mwanamume huyo alihukumiwa jela baada ya mahakama kumpata na hatia ya kosa la kujaribu kumbaka mwanamke ingawa tume ya kuchunguza kesi za watu waliofungwa jela kimakosa imemuomba radhi.
Victor Nealon, 53, alihukumiwa kwa kosa la kumshambulia mwanamke nje ya ukumbi wa densi mwaka 1996.
Aliomba tume ya kuchunguza kesi za wafungwa waliohukumiwa kimakosa kuchunguza kesi yake ingawa alipuuzwa mara mbili.
Hukumu yake ilifutiliwa mbali mwaka jana.
Tume hiyo sasa imesema ilipaswa kuchunguza kesi yake kwa umaakini ingawa hilo halikufanyika.
Mwenyekiti wa tume hiyo Richard Foster amenukuliwa akisema: "ninajuta sana kwa sababu kuna jambo fulani katika kesi hii ambalo hatukulichunguza vyema, tunamuomba radhi mwathiriwa. ''
'kukosa kuchunguza'
Bwana Nealon, ambaye siku zote alikana madai ya njama ya kumbaka mwanamke , alikamatwa baada ya mwanamke kudai kuwa mwanamume huyo alimdhulumu kimapenzi akiwa anarejea nyumbani kutoka klabuni katika mtaa wa Redditch.
Mtuhumiwa alifungwa jela baada ya mahakama kumpata na hatia na kumhukumu maisha jela.
Alisema kuwa alitaka tume hiyo kuchunguza ushahidi wote uliotolewa katika kesi hiyo.
Mawakili wake hata hivyo ndio waliochunguza ushahidi huo na kupata chembechembe za DNA ambazo sio zake bali za mtu asiyejulikana na kukosoa polisi kwa kuficha ushahidi huo.
Hukumu yake hatimaye ilifutiliwa mbali mwaka 2013.
Alisema: 'Ningekuwa nimeondoka jela miaka kumi au kumi na miwili iliyopita lakini kutokana na kosa la tume kukosa kuchunguza kesi yangu, ilinibidi kuhudumia kifungo kwa kosa ambalo sikufanya.''