Kurasa

Jumatano, 28 Mei 2014

FAMILIA YAMUUA NDUGU YAO KWA MAWE KWA KUJICHAGULIA MUME

Mwanamke mmoja nchini Pakistan amepigwa mawe na familia yake wakiwemo babake na ndugu zake wa kiume hadi kufariki. Aliuawa nje ya jengo la mahakama mjini Lahore.
Mwanamke huyo aliuawa kwa kuolewa na mtu ambaye alikuwa chaguo lake mwenyewe.
Farzana Bibi, mwenye umri wa miaka 31, aliolewa na Muhammad Iqbal miezi michache iliyopita bila ya idhini ya familia yake.
Polisi wanasema kuwa mwanamke huyo alishambuliwa na familia yake.
Kaka zake na binamu yake mmoja walimshika alipokuwa akiingia mahakamani na kuanza kumpigwa kwa mawe . Alifariki popo hapo.
Waliomuua walikimbia kabla ya polisi kufika katika eneo hilo.
Babake msichana huyo amekamatwa ingawa washukiwa wengine wangali hawajulikani waliko.
Kwa wanawake wanaoolewa na wapenzi ambao ni chaguo lao wenyewe, ni kitendo kisichokubalika kitamaduni katika baadhi ya maeneo ya Pakistan.
Mamia ya wasichana huuawa kwa kisingizio cha kuolewa na watu wasiokubalika na familia zao kila mwaka
Wanaharakati wa kutetea haki za binadamu, wanaamini kuwa kwa kuwa mauaji hayo hufanywa na familia zenyewe, huwa ni vigumu kufikisha kesi hizo kortini.
BBC

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni