Kurasa

Jumapili, 25 Mei 2014

HATIMAE WANAWAKE TASA KUPATA WATOTO

Wengi miongoni mwa wanawake wanapoolewa ndoto yao kubwa huwa ni kupata watoto.
Ndoto hiyo inaposhindwa kutimia kwa njia ya kawaida, basi juhudi zaidi hufanyika .
Mbinu mpya ya kisayansi ambayo imeanza kushika kasi nchini Kenya ni ile ya kutunga mimba kupitia chupa ama'' test tube'' kwa kiingereza.
Lakini Licha ya furaha ambayo huandamana na kuzaliwa kwa watoto , baadhi ya wazazi wanaopata watoto kwa njia hii hudhalilishwa na jamii
Joyce Kamau ni mama mwenye miaka 41 na hakuweza kupata mtoto kwa miaka saba baada ya kuolewa.
‘’Nilipoolewa sikuweza kupata mtoto, nilitembelea madakatari wengi na kutumia pesa nyingi sana.
Tasa kushika mimba kupitia mbinu za sayansi
Baada ya miaka saba, binamu yangu alinieleza kuwa naweza kupata huduma ya IVF hapa Kenya” Joyce anaeleza.
Joyce anasema baadhi ya rafiki zake walimtenga na kukosa kumwalika katika sherehe za siku ya kuzaliwa kwa watoto wao kwa vile walidhani kwamba hatakuwa na nafasi ya kuwaalika pia katika shere za watoto ambao hana.
Joyce aliolewa akiwa na miaka 33.
Anaamini kuwa ni vyema mwanamke kutokimbilia ndoa wakiwa na umri mdogo.
Wanawake wengi wameendelea kupata nafasi za kujiendeleza kimasomo na kikazi, hali hii imechangia kuchelewa kuolewa na pia kupata watoto.
Daktari Shaunak Khandawala ambaye ni mtaalam wa afya ya uzazi na mwenye uzoefu wa miaka 25, anasema mtindo wa maisha ya kisasa husababisha tatizo la wanawake kutoweza kushika mimba.
Tasa kushika mimba kupitia mbinu za sayansi
Hasa anasema utafiti unaonyesha uwezo wa mwanamke kupata mtoto hupungua mwanamke anapozidi kuwa na umri mkubwa
Dakatari Kandawala anaeleza ' sababu nyingine zinazosabisha tatizo la kutopata mimba ni kama vile mifuko ya uzazi kuharibika kwa sababu ya magonjwa mengi, uchafuzi wa mazingira ,hali ya kuwa na fikra nyingi na manii ya wanaume kupungua.'
Shirika la afya duniani linasema mmoja kati ya wanandoa wanne hawawezi kupata mtoto.
Katika mila nyingi mama tasa hukejeliwa. Wengi wao wanahofu ya kutafuta huduma za afya ya uzazi.
Joyce Kamau alikuwa na ujasiri wa kutafuta huduma hizo kwa miaka saba, ilimgharimu zaidi ya dola elfu kumi na mbili.
Joyce kwa sasa ni mja mzito , na anatarajia kuzaa mapacha.
BBC

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni