Kurasa

Jumanne, 20 Mei 2014

HII YA HUYU JAMAA KUFUNGWA MIAKA 17 BILA KOSA INAONESHA JINSI WANASHERIA WANAVYOKOSEA.

Mwanamume aliyefungwa jela kwa miaka kumi na saba kimakosa ameombwa radhi nchini Uingereza.Mwanamume huyo alihukumiwa jela baada ya mahakama kumpata na hatia ya kosa la kujaribu kumbaka mwanamke ingawa tume ya kuchunguza kesi za watu waliofungwa jela kimakosa imemuomba radhi.
Victor Nealon, 53, alihukumiwa kwa kosa la kumshambulia mwanamke nje ya ukumbi wa densi mwaka 1996.
Aliomba tume ya kuchunguza kesi za wafungwa waliohukumiwa kimakosa kuchunguza kesi yake ingawa alipuuzwa mara mbili.
Hukumu yake ilifutiliwa mbali mwaka jana.
Tume hiyo sasa imesema ilipaswa kuchunguza kesi yake kwa umaakini ingawa hilo halikufanyika.
Mwenyekiti wa tume hiyo Richard Foster amenukuliwa akisema: "ninajuta sana kwa sababu kuna jambo fulani katika kesi hii ambalo hatukulichunguza vyema, tunamuomba radhi mwathiriwa. ''
'kukosa kuchunguza'
Bwana Nealon, ambaye siku zote alikana madai ya njama ya kumbaka mwanamke , alikamatwa baada ya mwanamke kudai kuwa mwanamume huyo alimdhulumu kimapenzi akiwa anarejea nyumbani kutoka klabuni katika mtaa wa Redditch.
Mtuhumiwa alifungwa jela baada ya mahakama kumpata na hatia na kumhukumu maisha jela.
Alisema kuwa alitaka tume hiyo kuchunguza ushahidi wote uliotolewa katika kesi hiyo.
Mawakili wake hata hivyo ndio waliochunguza ushahidi huo na kupata chembechembe za DNA ambazo sio zake bali za mtu asiyejulikana na kukosoa polisi kwa kuficha ushahidi huo.
Hukumu yake hatimaye ilifutiliwa mbali mwaka 2013.
Alisema: 'Ningekuwa nimeondoka jela miaka kumi au kumi na miwili iliyopita lakini kutokana na kosa la tume kukosa kuchunguza kesi yangu, ilinibidi kuhudumia kifungo kwa kosa ambalo sikufanya.''

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni