Kurasa

Jumatano, 21 Mei 2014

KUTANA NA KIJANA MWENYE UKIMWI ANAEWAELIMISHA VIJANA WENZAKE JUU YA UGONJWA HUO KWA MITANDAO

Kijana mwenye umri mdogo amekuwa akifanya kampeni kwenye mtandao ili mafunzo bora zaidi yatolewe katika shule kuhusu maradhi ya HIV nchini Uingereza.
Luke Alexander aliye na umri wa miaka kumi na tisa anasema kuwa vijana wengi wenye umri mdogo hawapati mafunzo mwafaka yanayoweza kuwasaidia kuuepuka ugonjwa huo.
Shirika la kujitolea linalohusiana na maswala ya UKIMWI Terrence Higgins Trust, linasema kuwa swala hilo hugusiwa tu wakati wa somo la Sayansi, hivyo basi wanafunzi wengi hukosa kupata elimu muhimu kuhusu maradhi ya ukimwi.
Serikali iliambia idhaa ya BBC Newsbeat mjini London kwamba ni lazima wanafunzi wajifunze kuhusu magonjwa yanayoambukizwa kwa ngono kama vile UKIMWI, kama sehemu ya masomo ya jinsia na uhusiano.
'Kisa cha Luka'
''Nimeishi na ugonjwa wa UKIMWI kwa mwaka mmoja sasa, na inashangaza jinsi maisha yangu yalivyobadilika.
''Unaposikia habari zinazosambaratisha ndoto zako namna hii, kwa kweli unapata mtazamo mpya wa mambo, na wakati mwingine, maisha yanakosa manufaa.
''Nilikuwa na umri wa miaka 19 nilipopimwa na kupatikana na ugonjwa huu.
''Sikujua mengi kuhusu UKIMWI, na kwa hivyo nikadhani ugonjwa huo hauwezi kuepukika, na kwamba maisha yangu yangekumbwa na upweke na machungu, kabla ya kuugua na kuaga dunia ningali kijana mdogo.
''Labda hayo yangekuwa kweli miaka ya themanini, lakini sasa ni mwaka wa 2013, na baada ya uoga wangu wa kwanza, nilifurahi kugundua kwamba maisha yangu hayatakuwa kama kifungo cha maisha, bali kama msururu mrefu wa maisha.
''Nilipata ufahamu na uelewa kuhusu UKIMWI kwa filamu nilizotazama kama vile Philadelphia na Transpotting.
''Lakini kwa kweli, nilijifunza chochote kuhusiana na UKIMWI shuleni? Hapana.
''Ninapotafakari kuhusiana na masomo yangu ya shule ya upili, ni jambo la kuvunja moyo kugundua kwamba sikujifunza chochote kuhusiana na ugonjwa huu.
''Kumbukumbu zangu kuhusu somo la jinsia na uhusiano shuleni, ni kumsikiliza tu mwalimu mwenye aibu akizungumzia mimba, kuavya mimba na maradhi ya Chlamydia kwa kugusia tu.
'Ukosefu wa elimu'
''Niliponyanyua mkono na kuuliza kuhusu ngono nilitarajia jibu lenye utaalamu na lenye kuhusisha, lakini nilitazamwa kama mtu mwenye kinyaa na kujibiwa kuwa hilo halipendekezwi.
''Mimi sasa ni mwanaharakati wa kuhamasisha kuhusu UKIMWI, anayefanya uandishi ili kujaribu kuwaelimisha watu kuhusiana na maswala ya virusi hivyo, na kujaribu kuondoa unyanyapaa unaohusiana na swala hili.
Wakfu wa Luke mjini London
''Mimi hupata angaa jumbe 10 wa kuuliza maswali kutoka kwa vijana wadogo walioambukizwa ugonjwa huu kila siku.
''Mbali na mashauri waliopewa walipopimwa, wao huwa na hakika kuwa wanakwenda kuaga dunia.
''Wengi wao husema kwamba hawajawahi kufunzwa chochote kuhusiana na ugonjwa wenyewe wakiwa shuleni au nyumbani, na wengine huamini kuwa ni kama kifungo cha maisha.
'Maisha ya kaiwada'
''Ni sawa sawa kabisa na ninapowaambia rafiki zangu kuhusu hali yangu. Wawili wao, Charlotte Young na Charlotte Morris( walioonyeshwa kwenye picha), wote walihofia kwa ningekufa, walipogundua kuwa nina ugonjwa wa UKIMWI.
''Wote walioshuhudia matangazo ya kuogofya kwenye runinga na usambazaji wa vijikaratasi vya afya miaka ya themanini walijua misimamo yao, lakini wakasahau vizazi vipya.
''Wengi wana hisia kwamba magonjwa ya zinaa yanaweza kutibiwa kwa tembe zinazopatikana katika maduka ya kawaida ya dawa.
Marafiki wa Luca
''Wakati nikikiri kwamba sikujua kuhusu ugonjwa wa UKIMWI, na kwamba niliambukizwa kutokana na upuuzi wangu wa kufanya mapenzi bila kinga, ni aibu kubwa kwamba sijui zaidi.
''Mwaka jana kampuni la Ofsleg lilidai kwamba zaidi ya thuluthi moja ya shule nchini Uingereza hazikutoa mafunzo mazuri kwa wanafunzi kuhusiana na somo la jinsia na uhusiano.
''Kwa mtazamo wangu, shida hii inaendelea huku masomo ya ngono yakiwazuia vijana kujifunza chochote kuhusu kujikinga kimapenzi na kuiachia nambari yenye bahati mbaya kuchukuliwa na ugonjwa usio tiba, na ambao hawajawahi kusikia kuuhusu.”
BBC

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni