visit here again on mukebez.blogspot.com


CHANGE YOUR LIFE

CHANGE YOUR LIFE
Go to Amazon .com and get the copy of this book to make your life better.

Alhamisi, 28 Aprili 2016

TAZAMA JINSI MTOTO HUYU ALIVYOSHAMBULIWA NA MBWA.


PICHA;MTOTO AKIWA AMEJERUHIWA VIBAYA.

Katika hali ya kushangaza mbwa amemshambulia na kumuumiza mtoto mdogo aliekuwa anatembea na baba yake huko Liverpool.Baada ya tukio hilo gari la kubebea wagonjwa liliitwa mala moja ili kumpeleka mtoto huyo hospital.

MAMBO YA KUZINGATIA WAKATI UNABUNI JINA LA BIASHARA YAKO.

business: Portrait thinking handsome man looking up with idea light bulb above head isolated on gray wall background
PICHA;FIKIRIA KWA MAKINI KUHUSU JINA LA BIASHARA YAKO.

Wafanyabiashara wamekuwa wakichukulia jina la biashara kama kitu cha kawaida na sio moja kati ya vipaumbele katika mambo yao muhimu ya kuzingatia wakati wa kuanzisha biashara.Kufanya hivyo ni makosa kimsingi kwa sababu huweza kuleta madhara makubwa katika biashara yako hususani wateja wako wanapokutana na wateja wapya wanaohitaji kuijua biashara yako.

Jumanne, 26 Aprili 2016

NINA UHAKIKA MENGI KATI YA MAMBO HAYA HUYAFAHAMU.


Black flying fox bat hangs upside down in a tree
PICHA;POPO AKIWA JUU YA MTI.
  • Popo ndio mnyama pekee anaeweza kupaa angani.

FAHAMU KUHUSU WAKALA WA MAJENGO

PICHA(realestateslandny.blogspot.com)

Katika maeneo tunayoishi tunapotaka kununua,kuuza au kupangisha nyumba pamoja na viwanja tumezoea kuwatumia watu tunaowaita madalali.Bahati mbaya madalali hawa wanakuwa hawana chochote kinachomtambulisha au kitakachokupa wewe ulinzi endapo mambo yatakwenda vibaya.Utakuta mahali wamekaa vijana wengi tu maarufu kama kijiwe na wameweka kibao kimeandikwa madalali wa viwanja na nyumba wanapatikana hapa.

TAZAMA MSICHANA HUYU WA KAZI ALICHOMUWEKEA BOSI WAKE KWENYE JUICE.

PICHA;DADA WA KAZI AKIWEKA MKOJO KWENYE JUICE YA BOSS WAKE.

Familia moja huko Kuwait ambayo imeamua kuficha utambulisho wake imepost katika mtandao video inayomuonesha dada wa kazi wa familia hiyo akiweka mkojo ulioaminika kuwa ni wa kwake kwenye juice ya bosi wake.

ANGALIA MCHEZAJI HUYU WA REICISTER CITY ALIVYONUSURIKA KUFA


PICHA;MHUDUMU AKIMSAIDIA DEMARAY GRAY.

Mchezaji Demaray Gray wa timu ya Reicister City amenusurika kukatwa vibaya au pengine hata kufa baada ya kukoswakoswa kukatwa vibaya na mapanga ya helcopter wakati akielekea kwenye utoaji wa zawadi za PFA siku ya jumapili.

ONA MCHUNGAJI ALICHOMFANYA HUYU JAMAA KAMA SEHEMU YA MAOMBI.


PICHA;CUTHBERT VICTOR ALIEMWAGIWA MAJI KAMA SEHEMU YA MAOMBI.

Jumatatu, 25 Aprili 2016

TAZAMA KILICHOTOKEA KWA MSANII HUYU WA NIGERIA (PICHA)


PICHA;ALIEKUWA MR NIGERIA NA MUIGIZAJI EMMANUEL IKUBESE.

Picha hizi huwezi kuamini kwamba ni behind the scene ya cinema inayochezwa na msanii Emmanuel Ikubese na zimetengenezwa na special effect.Tazama picha zaidi hapa.

HIKI NDICHO KINACHOSABABISHA UPUNGUFU WA AJIRA TANZANIA.

PICHA;WANAFUNZI CHUO KIKUU MUHIMBILI WAKIANDAMANA.

Katika miaka ya hivi karibuni Tanzania imekumbwa na tatizo kubwa la uhaba wa ajira.Wasomi wamekuwa wengi sana ukiringanisha na ajira zilizopo nchini kitu ambacho kinafanya wasomi wetu kufanya kazi ambazo hazifanani na elimu wanayopata pamoja na kulipwa mishahara duni ambayo haiwezi kumpa mtu motisha wa kufanya kazi kwa juhudi na maarifa.

TAZAMA JINSI MAJAMBAZI HAWA WALIVYOCHOMWA MOTO. (ONYO;PICHA HIZI SI ZA KAWAIDA)


PICHA;MOJA KATI YA WEZI AKIWA AMEUNGUA VIBAYA.

Katika hali ya kusikitisha na muendelezo wa raia kuchukua sheria mkononi,wawili kati ya majambazi saba waliokamatwa na wananchi walipigwa vibaya na hatimae kuchomwa moto huko Nigeria.

TAZAMA SAMAKI ALIEVULIWA NA HUYU JAMAA.(PICHA)

PICHA; SAMAKI AINA YA OAR ALIEVULIWA HUKO TAIWAN.

Mvuvi mmoja huko Taiwani alifanikiwa kumvua samaki mkubwa aina ya OAR aliekuwa na urefu wa mita tano.Kwa mujibu wa wataalamu,samaki huyo alievuliwa alikuwa ni mtoto kwasababu aina hiyo ya samaki huwa wanakuwa wakubwa kufikia kiwango cha urefu wa mita 1000 na ni mala chache sana kufanikiwa kuwavua samaki hao kwasababu wanakaa kwenye kina kirefu sana cha bahari.

Jumapili, 24 Aprili 2016

AMUUA MKEWE BAADA YA KUGOMA KUMZALIA WATOTO.


PICHA;MAREHEMU HELEN PRECIOUS.

Polisi katika jimbo la Nassarawa nchini Nigeria wamemkamata jamaa mmoja aliefahamika kwa jina la Okala Joseph kwa kumuua kwa kumpiga risasi mke wake Helen Precious kutokana na kuwa na ugomvi wa muda mrefu juu ya mpango wa uzazi katika familia hiyo.

UMESHAIONA VIDEO MPYA YA LADY JAYDEE #NDINDINDI# BONYEZA HAPA KU PLAY#



#MUKEBEZI TV# LADY JAYDEE NDINDINDI OFFICIAL MUSIC VIDEO.
Kama unataka kutazama video zaidi unaweza kutazama upande wa kulia wa blog hii,Bonyeza #MUKEBEZI TV# kutazama zaidi.

Kama unamaoni zaidi kuhusu Video hii na ungependa mhusika ajue unachofikiria andika maoni yako hapa chini na yatamfikia mhusika.

HILI NI MOJA KATI YA MAMBO MABAYA WANAYOFANYA MASTAA#ONE OF BAD HABIT OF FAMOUS PEOPLE#

PICHA;MTOTO WA 50 CENT AKILIA BAADA YA KUKUTANA NA BABA YAKE KWA MALA YA KWANZA.

Mastaa wengi hususani vijana wamekuwa na tabia nyingi ambazo zimekuwa hazikubaliki katika jamii.Lakini wanapoulizwa wamekuwa wakijitetea kuwa wanaishi maisha ya kistaa.

UBONGO WA MWANAMIELEKA HUYU KUTOLEWA KWA WANASAYANSI# THE BRAIN OF THIS WRESTLER TO BE DONATED FOR SCIENCE RESEARCH#


PICHA;CHYNA, MWANAMIELEKA WA ZAMANI WA WWE.

Ubongo wa manamieleka wa zamani wa WWE mwanadada CHYNA aliekutwa akiwa amefariki dunia katika apartment yake siku ya jumatano utatolewa kwa ajili ya uchunguzi wa kisayansi.

HIKI KINATHIBITISHA ALIE BORA KATI YA MFANYA KAZI NA MFANYA BIASHARA.

PICHA;BUSINESS MAN

Umewahi kujiuliza swali hili kwamba

 ni nani alie bora na anae enjoy maisha zaidi kati ya mfanya kazi na mfanyabiashara?

Katika jamii zetu tumekuwa tukihimizwa toka tuko wadogo kusoma kwa bidii ili siku moja tuje kuwa na moja kati ya proffessional kama Udactari,Uhandisi,Ualimu (kama alivyo muandishi wa mada hii),Urubani,Uanasheria,Uandishi wa habari(kama alivyo muandishi wa mada hii) na fani nyingine nyingi.Tumekuwa tukiaminishwa hivyo na sisi tukiwaaminisha watoto wetu kwamba unapokuwa na moja kati ya fani hizo basi una uhakika wa kuwa na maisha bora.

BIASHARA INAHITAJI UMAKINI,TAZAMA KICHWA HIKI KILIVYOHARIBU BIASHARA(PICHA)


PICHA;KICHWA CHA KUKU KILICHOKUTWA KWENYE CHAKULA.

Jumamosi, 23 Aprili 2016

MOTISHA NA FAIDA ZAKE #MOTIVATION AND ITS ADVANTAGES#

PICHA (Getty Images);WEWE NA WAFANYAKAZI WAKO MNAHITAJI MOTISHA.


Katika kila tunachokifanya binadamu

motisha ni kitu ambacho kinahitajika sana.Motisha ni msukumo au shinikizo unalolipata kufanya jambo fulani kwa mategemeo fulani.Motisha zinaweza kuwa hasi au chanya.

Mwili wa binadamu umeumbwa katika mfumo wa kutamani na kukinai mambo.Unaweza kutamani sana kufanya jambo fulani lakini baada ya kulifanya kwa muda fulani ukakinai na kutaka kufanya jambo lingine kutokana na sababu mbalimbali.

Kuna mbinu mbalimbali unazoweza kuzitumia kujipa motisha wewe na wafanyakazi wako ili kuendelea kufanya kazi kwa ari ileile;

>>LIKIZO<<
Mwili wa binadamu pia huchoka na inafikia kipindi unahitaji kupumzika.Wafanyabiashara wamekuwa na tabia ya kufanya kazi siku zote 365 za mwaka bila kupumzika kitu ambacho kinaweza kupunguza morali ya kufanya kazi.

Unapaswa kuwa na utaratibu maalum ambao utakufanya wewe na wafanyakazi wako kuwa na mapumziko walau mala moja kwa mwaka kwenda kutembelea ndugu na marafiki.

Kumbuka swala la likizo halijalishi unafanya biashara ndogo kiasi gani,unahitaji mapumziko!!.

>>MAFUNZO<<
Unapaswa pia wewe kama mfanyabiashara kujipa motisha kwa kuhudhuria mafunzo mbalimbali yanayotolewa kwaajili ya biashara.Mafunzo haya yatainua tena ari ambayo itakuwa inaonekana kupotea kwani watoa mafunzo wengi huwa na tabia ya kuhamasisha.Lakini pia kama kuna mambo mapya utayapata katika mafunzo hayo utakuwa na ari ya kutaka kuyaongeza katika biashara yako na hivyo kuifanya biashara yako kuwa bora zaidi.

>>KUFANYA TOUR<<
Ni vizuri sana wewe kama kiongozi kupanga safari za kutembelea maeneo mbalimbali ya kihistoria na mbuga za wanyama kama sehemu ya motisha.
Pamoja na kuwapa ari wafanyakazi wako,pia hii husaidia kubadili mazingira waliyozoea na hatimae kupata changamoto mpya ambazo huweza kuwasaidia katika utendaji wao.

Asante sana mpendwa msomaji kwa leo na tukutane tena wakati mwingine kuendelea na mada zetu hizi za biashara na maendeleo.

Ijumaa, 22 Aprili 2016

UONGOZI KATIKA BIASHARA #BUSINESS MANAGEMENT#


PICHA(Bing.com);Uongozi sio ukali
.
Hujambo mpenzi msomaji mtu wangu wa kazi na karibu tena katika mfululizo wa mada zetu hizi ambazo kwa kipengele hiki tunamalizia kabla ya kuanza kukuletea upande wa pili ambapo tutakuwa tunaangalia biashara mbalimbali na fulsa nchini Tanzania. Tutaangalia mitaji yake ya kuanzia,faida zake,changamoto zake na hasara zake.Cha msingi ni wewe kuwa msomaji namba moja wa chombo hiki cha habari na kuendelea kufuatilia kila siku bila kukosa. Ni wakati mwingine tena ambapo Tunamshukuru mwenyezi MUNGU kwa kuendelea kutupatia pumzi yake.

Leo katika mada hii tutaangalia uongozi katika Biashara yako na unapaswa kunifuatilia kuanzia mwanzo mpaka mwisho.Kama utakuwa na swali au maoni tafadhali andika hapo chini baada ya kusoma mada hii nami nitakujibu wakati huohuo.Tutahakikisha kila comment inayoandikwa hapa inajibiwa ipasavyo.TUENDELEE..

Alhamisi, 21 Aprili 2016

TAZAMA KITUKO HIKI KILICHOFANYWA NA NDEGE HAWA MBUGANI SERENGETI,TANZANIA(PICHA)




Picha hizi zinazoonesha ndege hawa wakipigania chakula zilizopigwa kwenye mbuga ya SELENGETI na mpigapicha maarufu Roie Galitz zimewashangaza wengi na zimekuwa gumzo kubwa sana mtandaoni kwa sasa.
Jambo la kushangaza ni kuwa mnyama waliokuwa wanampigania ndege huyo carcass alikuwa ni mkubwa kiasi kwamba wangeweza kula wote na kushiba.

Jambo lingine la kuchekesha ni kuwa wakati baadhi ya ndege wakipigana wengine waliitumia nafasi hiyo kula chakula na kushiba kabla na wao hawajatimuliwa.Unaweza kuzicheki picha hizi hapa na kufurahia kituko hichi kinachowakilisha vituko vingi vya wanyama katika mbuga zetu hususani za Tanzania.

Jumatano, 20 Aprili 2016

AFYA,JINSI YA KUILINDA NA UMUHIMU WAKE KATIKA BIASHARA #HEALTH,HOW TO PROTECT IT AND ITS IMPORTANCE IN BUSINESS#


PICHA(Bing.com); AFYA DHAIFU INAWEZA KUATHIRI KAZI ZAKO.

Uhali gani mpenzi msomaji na mpenda maendeleo ambae umekuwa ukijipa muda kidogo kupitia mitandao inayokuelimisha kama huu badala ya kupoteza muda tu kwenye mitandao ya kijamii.Karibu sana kwenye mfululizo wa mada zetu hizi na nina imani kubwa sana kuwa baada ya kusoma mada hii utakuwa umeongeza kitu katika benki yako ya mambo ambayo tayari umeshapitia kwenye mtandao huu na kuelimika.Kwa wale wageni hapa kumbuka kusoma mada nyingine zilizopita za kibiashara ambazo zitakupa mfululizo mzuri na hatimae unapojifunza jinsi ya kutengeneza bidhaa mbalimbali utakuwa na ujuzi mkubwa wa kufanya biashara na Mungu atakubariki

Jumanne, 19 Aprili 2016

VAN DIESEL AONESHA PICHA ZA KUSHOOT MOVIE MPYA INAYOKARIBIA KUJA YA FAST & FURIOUS 8.


PICHA;FAST & FURIOUS COMING SOON


Staa wa movie series the FAST & FURIOUS VAN DIESEL ameshare kwenye mtandao wake wa twitter picha mbalimbali zikionesha ujio wa Movie mpya ya FAST & FURIOUS 8 zikionesha maeneo mbalimbali ambapo movie hiyo inaandaliwa pamoja na kumtambulisha muigizaji mpya anaechukua nafasi ya marehemu paul walker. FANYA KUZIANGALIA HAPA BAADHI YA PICHA HIZO.


KUTOKA INSTA

HIVI NDIVYO LINAVYOONEKANA DARAJA LA KIGAMBONI

MISINGI YA MAFANIKIO. #THE FOUNDATION TO SUCCESS#

3d white business person in a job interview with the curriculum vitae and social networks profile  3d image  Isolated white background   Stock Photo - 16723453
PICHA(www.123rf.co);INTERVIEW KIKIWA NI KIPIMO KIMOJAWAPO CHA KUMPA MTU KAZI.

Hujambo mpendwa msomaji na karibu tena katika mfululizo wa mada zetu ambazo kwa wewe unaetembelea mtandao kwa lengo la kuongeza kitu katika maisha yako iwe maarifa au mafanikio utakuwa unafaidika sana na mada hizi ukilinganisha na walio wengi ambao huingia mtandaoni na kutazama mambo ambayo hayana msaada katika maisha yao kimwili,kiakili na kiroho.

Kwa wale wanaofuatilia mada hizi zimekuwa zikiletwa mfululizo kuanzia ujasiriamali ninini? mpaka pale ambapo tutaona mwisho wake ni upi.Kumbuka mada hizi zinapatikana katika kitabu kinachoitwa MIMI NI TAJIRI kinachouzwa mtandaoni.Tunakaribisha yoyote ambae atakuwa tayari kukitoa kitabu hiki katika mfumo wa hard copy awasiliane na sisi.

Leo kama kilivyotangulia kichwa cha Habari tutaangalia Misingi au kanuni za mafanikio katika biashara na mambo mengine.

Kanuni za mafanikio yoyote yale ziko katika maeneo matatu KUJIAMINI,JUHUDI NA UWEZO (KKK).CONFIDENCE,COMMITMENT AND COMPETENCE (CCC).Unaweza kuita kwa jina lingine 3K au 3K.

Jumatatu, 18 Aprili 2016

Jumapili, 17 Aprili 2016

JINSI YA KUTENGENEZA BATIKI #HOW TO MAKE BATIK#


PICHA(ubatik.wordpress.com)

Hujambo mpenzi msomaji na karibu sana katika ukurasa huu ambao pamoja na habari tutakuwa tunajifunza mambo mbalimbali ambayo yanaweza kutusaidia kujikwamua na umaskini.Kama mna kumbukumbu nzuri,siku za karibuni nimekuwa nikiwaambia kuwa nitawaletea masomo ya jinsi ya kutengeneza bidhaa mbalimbali za viwandani.Leo katika somo letu tutaanza kujifunza jinsi ya kutengeneza BATIKI na naomba mnifuatilie kuanzia mwanzo mpaka mwisho wa masomo haya na myafanye kwa vitendo na MUNGU atawabariki.

TABIA BINAFSI/HULKA NA ATHARI ZAKE KATIKA BIASHARA. #PERSONALITY AND ITS BUSINESS EFFECTS#

PICHA(Photobucket.com);OPRAH WINFRED.mwanamke aliefanikiwa duniani.

Umewahi kutafakari jinsi unavyojichukulia na jinsi unavyotaka watu au jamii ikuchukulie.Tambua kuwa mala nyingi jamii hupenda kufanya au kukufanyia vile unavyojifanyia mwenyewe.

Ijumaa, 15 Aprili 2016

JINSI YA KUTENGENEZA SABUNI ZA MICHE #HOW TO MAKE BAR SOAP#

MAHITAJI;

(I)CAUSTIC SODA
(II)MAFUTA YA NAZI,MISE,MBOSA AU MAWESE AU YA NYONYO
(III)MAJI
(IV)PAFYUM
(V)HYDROGEN PEROXIDE
(VI)CHUMVI KWAAJILI YA KUIFANYA SABUNI NZITO NA ISIISHE HARAKA

JINSI YA KUTENGENEZA;

Jumanne, 12 Aprili 2016

NENO SMART NA MAANA YAKE KATIKA BIASHARA. #THE WORD SMART AND ITS MEANING IN BUSINESS#



.

Watu wengi tumekuwa tukilitumia neno SMART kuonesha jinsi mtu alivyo msafi na nadhifu.Lakini katika mafanikio wataalamu wanasema katika neno SMART kuna herufi tano(5) ambazo kama mtu atazifuatilia kwa makini atakuwa ni mtu mwenye mafanikio yasiyo kifani.Katika neno hili kuna herufi za kiingereza ambazo kila herufi inawakilisha neno muhimu sna katika maisha.Maneno hayo ni SPECIFIKI AU MSIMAMO,MEASURABLE AU INAYOPIMIKA,ATTAINABLE AU INAYOFIKIKA,REARISTIC AU HALISIA NA TIME BOND AU INAYOENDA NA MUDA.Sasa tuliangalie neno mojamoja;

Jumamosi, 9 Aprili 2016

UTAJIRI #WEALTH#

PICHA;WARREN BUFFETT.MMOJA WA MATAJIRI WAKUBWA DUNIANI.

Karibu sana mpenzi msomaji katika muendelezo wa mada zetu ambazo zinahusu Biashara na ujasiriamali,mada ambazo zinapatikana katika kitabu chetu kinachouzwa kwenye mtandao kinachoitwa MIMI NI TAJIRI.Tunashauri wasomaji wetu kuanza kusoma mwanzo kabisa wa mada hizi ambazo tulianza kwa kuangalia maana ya ujasiriamali,jinsi ya kupata mitaji na makao ya biashara.Pamoja na hayo pia kuna mafunzo ya jinsi ya kutengeneza bidhaa mbalimbali ikiwemo Batiki na Sabuni za aina mbalimbali.

Leo tunaendelea na mada yetu tuliyoianza inayohusu UKWELI KUHUSU UTAJIRI. ambayo tuliishia kwa kuona ni jinsi gani unaweza ku adopt mazingira yakakufanya kuwa Tajiri.

Jumatatu, 4 Aprili 2016

UKWELI KUHUSU UTAJIRI #THE TRUTH ABOUT WEALTH#

PICHA;Matajiri wakubwa Duniani.

Watu wengi wamekuwa na imani kuwa ili uwe tajiri ni lazima uwe umezaliwa na hulka ya utajiri au umezaliwa kwenye ukoo wa kitajiri.Wengine huenda zaidi kwa kuamini kuwa mtu asiesoma huishia kuganga njaa tu na sio kutajirika.Lakini unapaswa kujiuliza maswali haya; Je! umewahi kusikia mtoto mdogo aliezaliwa akiwa na nguo achilia mbali utajiri?Je! matajiri wote unaowafahamu akiwemo tajiri namba moja Duniani wamezaliwa koo za kkitajiri au wao ndio wamefanya koo zao kuwa za kitajiri?,Lakini pia unapaswa kujiuliza je!matajiri wote unaowafahamu walipata utajiri wakati wakiwa na degree? Ni kitu gani cha ziada ambacho tajiri unaemfahamu alikuwa nacho wakati hajapata utajiri ambacho wewe huna?

Ukifanikiwa kuyajibu maswali yote hayo utagundua kuwa wewe ni tajiri ambae bado ulikuwa hujatambua thamani yako.Mstari mmoja kwenye maandiko unasema

Ijumaa, 1 Aprili 2016

PICHA YA SIKU #PHOTO OF THE DAY#;IT WAS AMAIZING

ILIKUWA MIAKA,MIEZI,WIKI NA HATIMAE SIKU IKAFIKA BWANA MUKEBEZI DEONIDAS(BLOGGER) NA BI JOYCE MATHEW WALIPOAMUA KUUACHA UKAPELA NA KUFUNGA PINGU ZA MAISHA.ALILOUNGANISHA MUNGU MWANADAMU ASITENGANISHE.

Ijumaa, 25 Machi 2016

4.MAKAO YA BIASHARA.#BUSINESS CENTER#

Karibu tena mpendwa msomaji,ambae ni mfanyabiashara na wewe ambae unataka kuanza biashara au umeamua tu kujiongezea maarifa kuhusu biashara.Huu ni muendelezo wa mada zetu ambazo zinapatikana katika kitabu chetu kinachitwa MIMI NI TAJIRI kinachouzwa hapa kwa bei ya 2500/= tu.Kitabu hicho kina baadhi ya mambo muhimu ambayo hayachapishwi hapa kama vile jinsi ya kutengeneza bidhaa mbalimbali kama batiki,shampoo na nyingine zaidi ya nane,mahali ambapo unaweza kupata malighafi za kutengeneza bidhaa hizo na bei za malighafi husika.

Leo katika mada yetu tunaangalia makao ya biashara.

Jumamosi, 19 Machi 2016

MITAJI KUTOKA TAASISI ZA FEDHA #CAPITAL FROM FINANCIAL INSTITUTIONS#

Hujambo mpenzi msomaji na  karibu tena katika mada zetu za ujasiriamali ambazo zimekuwa zikiletwa kwako kwa mfululizo maalum.

Leo tunaendelea na mada ambayo tayari tulishaianza ya Mitaji na vyanzovyake ambapo mala ya mwisho tuliishia kutoa mfano wa jamaa ambae alisafiri kutoka mkoani mpaka jijini Dar es salaam akiwa na nauli tu lakini bado alifanikiwa kuwa miongoni mwa watu wenye fedha mjini.

Katika muendelezo leo tutaangalia mitaji kutoka taasisi za fedha.

Alhamisi, 17 Machi 2016

MITAJI KATIKA UJASIRIAMALI

Hujambo mpenzi msomaji na karibu tena katika mfululizo wa mada zetu hizi za Ujasiriamali ambazo zinaletwa kwako na mimi mshauri wako wa mambo ya kibiashara MUKEBEZI DEONIDAS.Mada hizi zimechukuliwa kutoka katika kitabu ambacho kiko sokoni kwa sasa kinachoitwa MIMI NI TAJIRI ambacho huuzwa kwa shilingi elfu mbili na mia tano tu.Hata hivyo tunashukuru kwa muitikio wa watu wengi mnaoendelea kujinunulia kijitabu hiki chenye maarifa ya kutosha ikiwemo jinsi ya kutengeneza bidhaa mbalimbali kama batiki na nyingine nane za aina tofauti,Mahali yanakopatikana maduka ya malighafi pamoja na bei za malighafi hizo.Mada hizi tatu nilizozitaja hazitaweza kuchapishwa hapa na kwa hivyo wale watakaonunua kitabu hiki ndio pekee watakuta mada hizo au watakaonunua mada mojamoja ambazo huuzwa wa shilingi mia tano tu.Tumia mawasiliano yetu kama unataka kujipatia kitabu hiki au mada hizi zilizotajwa hapa.0654627227.

Leo tunakuletea mada inayohusu mtaji katika biashara au ujasiriamali

Ijumaa, 11 Machi 2016

JINSI YA KUTAFUTA MASOKO KATIKA BIASHARA. #HOW TO GET MARKET#

Hujambo mpenzi msomaji, karibu tena katika mfululizo wa mada zetu za ujasiriamali zinazoletwa kwako na mimi muelimishaji wako Mukebezi,Deonidas.Ndugu msomaji huu ni mfululizo wa mada zinazopatikana katika kitabu kinachoitwa MIMI NI TAJIRI ambacho tunakiuza kwa njia ya mtandao kwa shilingi elfu mbili mia tano tu (2500/=). Tunaona muitikio wa kununua vitabu hivi umekuwa ni mkubwa sana kwani watu zaidi ya 40 wameshapata kitabu hiki na ni matumaini yetu kwamba wanayafurahia yaliyomo na kuyafanyia kazi. Pamoja na watu wengi kujitokeza baadhi yenu mmelalamika kuwa hamna email ambazo mngeweza kutumiwa kitabu hiki na mkatoa ombi vitoke katika mfumo wa hard copy yani viprintiwe.Kutokana na hilo tunakaribisha mtu yoyote mwenye mapenzi mema ambae yuko tayari kuprint vitabu hivi,awasiliane nasi kwa kutumia mawasiliano yetu na hatutasita kufanya makubaliano nae.

Pia ndugu msomaji katika kitabu hiki kuna maelekezo ya jinsi ya kutengeneza bidhaa mbalimbali kama sabuni,batiki,tomato nk,ambapo bidhaa nane zimeandikwa kwenye kitabu lakini kutokana na maombi ya baadhi ya watu ambao wameshanunua kitabu hiki,mada hiyo ambayo ilitakiwa ndio iandikwe wiki hii katika kulasa zetu haitawekwa na badala yake tutaendelea na jinsi ya kutafuta masoko ya biashara yako.Ukitaka kujua jinsi ya kutengeneza bidhaa hizo nunua na usome kitabu chetu cha mimi ni tajiri na utakutana na bidhaa nane tofautitofauti.
Mpendwa msomaji soko ndio moyo wa biashara.

Jumanne, 8 Machi 2016

UJASIRIAMALI; AINA ZA BIASHARA#TYPE OF BUSINESS#

Karibu tena mpenzi msomaji wetu katika mfululizo wa makala zetu za ujasiriamali.Makala hizi ni muendelezo wa kile kilichoandikwa kwenye kitabu kinachoitwa MIMI NI TAJIRI kinachouzwa mtandaoni kwa shilingi 2500 tu.Kama unahitaji kitabu hiki chenye ushauri wa kibiashara,jinsi ya kutengeneza bidhaa mbalimbali ikiwemo sabuni na shampoo,Mahali yalipo maduka ya malighafi za kutengenezea bidhaa hizo pamoja na bei za malighafi husika, wasiliana nasi kupitia namba yetu 0654627227 au tuandikie kwenye mdeonidas@gmail.com. Leo katika makala hii tutaangalia aina za biashara na jinsi inavyoweza kukusaidia kupata wazo la biashara. Wakati mjasiriamali anafikiria kuhusu wazo la biashara,ni lazima afikirie kuhusu aina mbili za biashara ambazo kupitia hizo mawazo mbalimbali ya kibiashara huweza kupatikana.Aina hizo ni kama ifuatavyo;

Jumapili, 6 Machi 2016

UJASIRIAMALI

Karibu mpenzi msomaji katika mfululizo wa mada zetu za ujasiriamali ambazo zinapatikana katika kitabu maalum cha ujasiriamali kinachoitwa MIMI NI TAJIRI kinachouzwa kwa shilingi 2500 tu.Kama unahitaji kitabu hicho chenye pia maelekezo ya jinsi ya kutengeneza bidhaa mbalimbali na jinsi utakavyopata malighafi wasiliana nasi kwa kutumia namba zetu na utakipata mala moja.

Leo katika muendelezo wa mada zetu tutaangalia mambo yanayoweza kumkwamisha mjasiriamali.

Ijumaa, 4 Machi 2016

MAANA HALISI YA UJASIRIAMALI

1. MAANA YA UJASIRIAMALI.

Ujasiriamali ni ile hali ya mtu kuona fulsa na kuzifanyia kazi kwa lengo la kujipatia kipato. Kwa mfano mtu anapoishi mazingira ambayo watu wamekosa nishati ya umeme anaweza kutumia kama fulsa kwa kuuza vifaa vya umeme wa jua akajipatia kipato.Mala nyingi mjasiriamali anakuwa na sifa zifuatazo;