visit here again on mukebez.blogspot.com


CHANGE YOUR LIFE

CHANGE YOUR LIFE
Go to Amazon .com and get the copy of this book to make your life better.

Jumatano, 27 Aprili 2016

HUU NI MFANO WA JINSI UTAPELI WA VIWANJA UNAVYOFANYIKA WILAYANI BAGAMOYO.


Naitwa JOYCE, 
Mwaka 2014 nilifanikiwa kununua eneo la kiwanja lililokuwa na thamani ya shilingi 1500000/=. Kutokana na mambo kuwa magumu sikufanikiwa kuliendeleza kwa kujenga wakati huo lakini nilikuwa naendelea kuweka akiba ili angalau nijenge katika eneo hilo.


Nikiwa sina hili wala lile siku moja nilipigiwa simu na mtu ambae nilimuweka kufanyia usafi eneo hilo na akaniambia kuwa eneo langu lilikuwa limeshajengwa msingi.Taarifa hiyo ilinishtua sana na ndipo nilipoamua kutembelea eneo hilo kushuhudia kwa macho yangu.

Nilipofika katika eneo lile ni kweli kama taarifa ilivyonifikia,lilikuwa limechimbwa choo pamoja na kujengwa msingi.Kama hiyo haitoshi nilikuta mtu akimwagilia msingi huo tayari kabisa kwaajili ya kuendelea na ujenzi wa nyumba hiyo.

Nilimpigia simu anaemiliki nyumba ile baada ya kuchukua namba kwa mdogo wake na ndipo nilipofahamu jinsi ishu ilivyofanyika;

Dada yule mmiliki wa msingi wa nyumba ile aliuziwa eneo hilo mwezi wa kwanza mwaka 2016 na mtu aliefahamika kwa jina la BULAI.Mtu huyu Bulai katika mkataba wangu wa mauziano alisaini kama Shahidi wa alieniuzia eneo hilo aliefahamika kwa jina la ALLI.Maana yake ni kuwa wakati BULAI akiwa anafahamu dhahiri kwamba eneo hilo lilishakuwa linamilikiwa na mtu mwingine aliamua kuliuza tena kwa tamaa ya pesa.

Wakati BULAI anauza eneo hilo aliekuwa ameniuzia eneo hilo bwana ALLI alikuwa na kesi mahakamani ambayo hata hivyo ilimsababishia kufungwa jela kwa kesi hizohizo za viwanja.Kwa hiyo kinachoonekana hapa ni kuwa BULAI aliamua kuuza mala ya pili viwanja alivyouza na rafiki yake ALLI akijua kuwa ali ana kesi na aingeweza kutoka.

Cha kufurahisha zaidi ni kuwa BULAI  aliuza kiwanja hicho kwa mala ya pili kwa mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Sanzale ambae kwa wakati huo hakuwa yule ambae alitumika katika mauziano ya kiwanja wakati mimi nanunua.Ninachojiuliza hapa ni kwamba hawa wanyeviti wanapoachiana madaraka hawapeani taarifa za kutosha kuepuka migongano.

Tulijaribu kumtafuta BULAI na kumuuliza imekuwaje akauza kwa mala ya pili eneo ambalo lilishauzwa na yeye akiwa shahidi? Alichojibu yeye ni kuwa haitwi Bulai na kitambulisho chake cha uraia hakina jina hilo (Kumbuka vitambulisho hivyo viliandikishwa mwaka 2015) wakati mwenyekiti wa zamani alietumika wakati wa mauziano yetu anamfahamu haswa.

Kwa sasa hakuna kinachoendelea katika kiwanja hicho kwani hata yule aliekuwa anajenga amesitisha ujenzi huo baada ya songombingo hilo.Pia kinachofanya kuwe na kutegeana ni kwasababu taarifa zilizopatikana zaidi ni kuwa wamiliki wa eneo hilo ni wanne na kila mmoja anasisitiza kuwa eneo hilo ni lake.

Tunaziasa mamlaka husika kuwa makini na maswala haya ya migogoro ya ardhi ambayo ukiangalia kwa undani utagundua kuwa kukosekana kwa umakini wa viongozi husika ndio kunakosababisha matatizo yote haya.Hivi vitatizo vidogovidogo ndio vinavyokuwa na hatimae kuleta matatizo makubwa yanayosababisha viongozi husika kuitwa majipu.

Haiwezekani raia mmoja au wawili wajiamini kuuza maeneo mala mbili,tatu au hata mala nne bila woga huku wakiwa hawana kitu kinachowafanya kuwapa kiburi hicho.Ikiwezekana wote wanaohusika na vipele hivi vidogovidogo ni vyema wakachukuliwa hatua ili kuepusha kipele kugeuka kuwa jipu.

Kwa wale ambao wanampango wa kununua maeneo maeneo mbalimbali,tafadhali kuweni makini msije mkajikuta mnanunua maeneo ambayo si ya kwenu na hatimae kuingia hasara isiyokuwa na sababu kama hasara aliyoipata dada aliejenga msingi katika eneo sio lake ya shilingi takribani 4000000/=.
                                                
                                            ASANTENI SANA.
Toa maoni yako hapa chini kuhusiana na taarifa hii.Na pia unaweza ku share habari hii facebook pamoja na Twitter.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni