Watu wengi wamekuwa na imani kuwa ili uwe tajiri ni lazima uwe umezaliwa na hulka ya utajiri au umezaliwa kwenye ukoo wa kitajiri.Wengine huenda zaidi kwa kuamini kuwa mtu asiesoma huishia kuganga njaa tu na sio kutajirika.Lakini unapaswa kujiuliza maswali haya; Je! umewahi kusikia mtoto mdogo aliezaliwa akiwa na nguo achilia mbali utajiri?Je! matajiri wote unaowafahamu akiwemo tajiri namba moja Duniani wamezaliwa koo za kkitajiri au wao ndio wamefanya koo zao kuwa za kitajiri?,Lakini pia unapaswa kujiuliza je!matajiri wote unaowafahamu walipata utajiri wakati wakiwa na degree? Ni kitu gani cha ziada ambacho tajiri unaemfahamu alikuwa nacho wakati hajapata utajiri ambacho wewe huna?
Ukifanikiwa kuyajibu maswali yote hayo utagundua kuwa wewe ni tajiri ambae bado ulikuwa hujatambua thamani yako.Mstari mmoja kwenye maandiko unasema
watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa.Kwa bahati mbaya watu wamekuwa wakipotosha mstari huu kwa kuamini kuwa mstari huo unaongelea maarifa ya darasani tu.Maarifa ya Darasani ni sehemu ndogo sana ya maarifa yanayokusudiwa.Binadamu na viumbe wengine tumekuwa tukiishi kwenye mazingira toauti na kujifunza kulingana na mazingira na maisha tunayoishi.Kwa bahati mbaya au nzuri ni kuwa tunapokuwa mazingira mapya tumekuwa tukijifunza na kushabihiana na mazingira tunayoyakuta.
Nimesema kwa bahati mbaya kwasababu ikitokea ukawepo kwenye mazingira ya watu ambao ni maskini na wamekata tamaa ya kuwa matajiri na wewe unaweza kukata tamaa na kuwa maskini maisha yote.
Lakini pia nimesema bahati nzuri kwasababu kama kwenye maisha yako wakati wote unapenda kukaa na watu waliofanikiwa au wenye mawazo ya mafanikio unaweza kujifunza na kufanikiwa kama utakuwa tayari kujifunza.
Ndugu msomaji kwa leo tunaweka kituo tukutane tena wakati mwingine kwa muendelezo wa mada hizi ambazo zinakupatnua zaidi kimawazo.Mada hizi na nyingine zikiwemo utengenezaji wa bidhaa mbalimbali za viwandani zinapatikana kwenye kitabu chetu kinacoitwa mimi ni tajiri ambacho kinauzwa 2500/= tu. Asanteni.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni