Pia ndugu msomaji katika kitabu hiki kuna maelekezo ya jinsi ya kutengeneza bidhaa mbalimbali kama sabuni,batiki,tomato nk,ambapo bidhaa nane zimeandikwa kwenye kitabu lakini kutokana na maombi ya baadhi ya watu ambao wameshanunua kitabu hiki,mada hiyo ambayo ilitakiwa ndio iandikwe wiki hii katika kulasa zetu haitawekwa na badala yake tutaendelea na jinsi ya kutafuta masoko ya biashara yako.Ukitaka kujua jinsi ya kutengeneza bidhaa hizo nunua na usome kitabu chetu cha mimi ni tajiri na utakutana na bidhaa nane tofautitofauti.
Mpendwa msomaji soko ndio moyo wa biashara.
Soko maana yake ni wateja wa biashara husika.Mjasiriamali bora ni yule ambae ana ujuzi wa kutosha kutafuta masoko au wateja.Katika masoko kuna wateja wa bidhaa na walaji wa bidhaa.Mteja wa bidhaa ni yule anaenunua bidhaa husika bila kujali kama ataitumia au la.Kwa mfano baba anapopita dukani kumnunulia mtoto wake pipi baba anakuwa mteja na mtoto anakuwa ni mlaji wa bidhaa yako. Hawa wote ni muhimu sana katika biashara na mfanyabiashara yoyote lazima afikirie umuhimu wa wote wawili wakati anapotaka kuanzisha au kuendeleza biashara yake.
2.1MBINU ZA KUTAFUTA MASOKO.
Kama nilivyotangulia kusemajasiriamali bora ni yule mwenye mbinu bora za kutafuta masoko kwa sababu bila soko imala hata kama bidhaa ni bora kiasi gani biashara inaweza kuyumba.
Kuna mambo mbalimbali yanayoweza kumsaidia mjasiriamali kupata soko la bidhaa au huduma yake kama ifuatavyo;
Ubora wa bidhaa; kama mjasiriamali atakuwa anatengeneza au kuuza bidhaa au huduma bora na zenye kiwango kuliko washindani wake ni rahisi sana kuwavutia wateja pamoja na walaji.
Mabango na vipeperushi;Njia hii imekuwa ni ya asili kwa wafanyabiashara wengi hususani Afrika mashariki.Pamoja na hayo baadhi ya wafanyabiashara wamekuwa wakiikwepa kutokana na gharama.Pamoja na gharama zake njia hii huwafanya wateja kujua huduma au bidhaa anayouzan na tofauti kati yako na washindani wako.Katika mitaa ambako tumekuwa tukifanya biashara zetu tumekuwa tukishuhudia mala kadhaa wateja wakipita mbele ya biashara zetu na kusoma mabango au vipeperushi tunavyoweka mbele ya biashara zetu.
Mpangilio wa biashara.Hii pia ni nnjia nzuri ssana ya kuwafanya wateja kununua bidhaa aua huduma ya mfanyabiashara.Bidhaa au huduma iliyopangilia vizuri humfanya mteja kuiona na hivyo kuinunua.Bidhaa lazima ipangwe katika hali ya kuonekana na usafi.
Mawasiliano;
Hii ni njia nyingine maarufu sana ya kutafuta soko.Njia hii huumiwa sana na kampuni kubwakubwa lakini pia biashara ndogo.Kwa wale wafanyabiashara ambao hutengeneza bidhaa zao wenyewe huweza kuandika mawasiliano yao ikiwemo email sanduku la posta au namba za simu.Katika zama hizi za sayansi na teknolojia wafanyabiashara pia hutumia website kuwasiliana na wateja na kutangaza bidhaa zao.
Vyombo vya habari;Njia hii pia ni maarufu sana na wafanyabiashara wengi waliofanikiwa huitumia.Mfanyabiashara huweza kutangaza biashara yake kwa kutumia redia,television pamoja na magaazeti.Njia hii pia ni ghali sana lakini huweza kukuletea wateja wengi na faida kubwa kwa muda mfupi.
Bei za bidhaa; Mala nyingi wateja hupenda bidhaa za bei nafuu.Mfanyabiashara bora na mwenye lengo la kupata wateja huangalia bei za bidhaa za washindani,bei alizonunulia bidhaa na faida yake binafsi.Ni rahisi sana kupata wateja wapya kama mfanyabiashara atapunguza kidogo bei za bidhaa zake bila kuathiri faida yake.Wafanyabiashara wengi wamekuwa wakipanga bei kubwa katika bidhaa kiwa malengo ya kujipatia faida kubwa matokeo yake huwakimbiza wateja.
Asante sana wasomaji wetu,na hapa ndio tunafika mwisho wa mada yetu kwa leo.Wakati mwingine tutaangalia ni jinsi gani unaweza kupata mitaji kulingana na biashara unayoitaka,faida na hasara zake.Kwa wale ambao mmekuwa mkihitaji kitabu hiki hususani ili kujua baadhi ya mambo ambayo hayatachapwa hapa kama jinsi ya kutengeneza bidhaa mbalimbali, jinsi ya kupata maighafi za kutengenezea bidhaa na bei za malighafi hizo mnaweza kuwasiliana na sisi kwa nja ya ujumbe mfupi wa maandishi kwenye 0654627227. Tafadhali sana kama unataka kupata huduma tuma ujumbe kwa sababu watu wengi wanapiga na inakuwa ngumu sana kuongea na wote.
-
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni