Geneva, Uswisi.Lionel Messi ni mchezaji mwenye thamani kubwa duniani kutokana na kulipwa karibu mara mbili zaidi ya Cristiano Ronaldo anayemfuatia.
Hiyo ni kwa sababu umri wa Messi ni miaka 26 wakati Ronaldo ana miaka 29.
Pia Raheem Sterling ni mchezaji mdogo (19) na mkubwa ni Andres Iniesta (30) walioingia katika orodha hiyo ya wachezaji 25 wanaolipwa zaidi kwenye fainali za Kombe la Dunia.
Utafiti huo, uliofanywa na Chuo Kikuu cha Uswisi kiitwacho Neuchatel kwa kushirikiana na OptaPro, uliangalia thamani za wachezaji wa ligi tano kubwa za Ulaya kwa kutazama mishahara yao na gharama za uhamisho.
Messi kwa sasa ana thamani ya Pauni 175.6 milioni za Kiingereza akifuatiwa na Cristiano Ronaldo mwenye thamani ya Pauni 92.7 milioni za Kiingereza huku Eden Hazard akishika nafasi ya tatu kwa thamani ya Pauni 66.7 milioni,
Wachezaji 23 kati ya 25 walioshika nafasi za juu kwenye tafiti hiyo ni washambuliaji. Walobaki ni viungo wakabaji ambao ni Sergio Busquets na Paul Pogba.
Katika kundi hilo la wanasoka 25, 11 wanatoka Ligi Kuu ya Uingereza, nane wanacheza Hispania huku Ufaransa, Ujerumani na Italia zikitoa wachezaji wawili kila mmoja.
Katika soko la juu la nyota hao 11, Ronaldo na Gareth Bale (Pauni 51.2m) wamenunuliwa kwa gharama kubwa zaidi kwani Messi hajahama Barcelona toka ajiunge nao.
Kyle Walker na Luke Shaw pia wameingia katika kikosi cha wachezaji 11 wenye thamani zaidi duniani, kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na CIES Football Observatory.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni