Natal, Brazil. Kocha Stephen Keshi amewapuuza mashabiki wa soka nchini Nigeria baada ya timu yake kucheza moja ya mechi mbaya za Kombe la Dunia nchini Brazil mapema wiki hii.
“Siku zote nimekuwa nikikosolewa. Hata kama nikishinda ama kwenda sare, siku zote imekuwa hivyo. Hatuna uvumilivu nchini kwetu.
“Kila mchezo wanataka kushinda kwa gharama yoyote. Haileti maana yoyote ninapokuwa nikikosolewa,” kocha huyo alisema baada ya mchezo huo ambao Nigeria ililazimishwa suluhu na Iran.
Malalamiko hayo ya Keshi si mapya. Wakati alipotwaa ubingwa wa Mataifa ya Afrika nchini Afrika Kusini, alisema ametokea katika nchi ambayo kila mtu ni kocha.
Pia si hayo tu, alilazimika kujiuzulu katika moja ya mahojiano yake na mwandishi wa kimataifa lakini alikanusha maneno hayo wakati maofisa wa serikali walipombana na kumtaka aendelee kuiongoza miamba hiyo maarufu kama Super Eagle.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni