visit here again on mukebez.blogspot.com


CHANGE YOUR LIFE

CHANGE YOUR LIFE
Go to Amazon .com and get the copy of this book to make your life better.

Jumapili, 25 Januari 2026

THE REQUEST FOR SPONSORSHIP

The Catholic Church Choir named MOYO SAFI WA BIKIRA MARIA BAGAMOYO has an honour to kindly ask you who is reading this post now, to support them to get their important requirements which are necessary for their work of spreading the word of God to continue through singing.The following is the list of their current requirements;
1.Keyboard or piano
2.Drums
3.Kayamba
4.whistle 
5.Mike
6.Conducting buttons 
7.Ipads for sight reading
8.Printer
9.Computer
please if you find out that you can buy us one of these requirements, or you have one and you want to donate,you can contact us through the following contacts;

+255 624 376 886 (WhatsApp number)
Email; mdeonidas@gmail.com 

Thank you so much in advance 

Deonidas Mukebezi 
The CHoir General Secretary 

Ijumaa, 23 Machi 2018

MWALIMU KUTEGEMEA VIBOKO NI KUKIRI UDHAIFU.

 

 Walimu pamoja na wazazi Tanzania tumekuwa na utaratibu ambao sasa umegeuka kuwa utamaduni wetu wa kutumia viboka kuwaadabisha watoto wetu. Wakati huohuo sisi watu wazima tulikataa utaratibu huo kwa nguvu kweli wakati wakoloni walipokuwa wanautekeleza kwetu.( hii inachekesha kweli).Mala nyingi nimekuwa nikiwaambia watoto wadogo kuwa sio vizuri kumfanyia binadamu mwenzako kile ambacho usingependa wewe kufanyiwa. Kwanini sisi tunawafanyia watoto wadogo matendo haya!!.

Kila binadamu kulingana na umri alionao ikiwa ni mtoto,kijana au mzee ana mapungufu ambayo binadamu wa umri mwingine hawayapendi.Vijana wanafanya mambo ambayo wazee hawapendi,Wazee hufanya mambo ambayo watoto hawapendi na ndio mana wakati mwingine utamsikia mtoto anauliza swali kama, kwa nini mzee yule anakunywa pombe au anampiga mama yake Bakari kila siku??. Sasa je watoto nao wakiona wazee au vijana wanafanya makosa kwa nini wasiruhusiwe kuwachapa wazee?? au ndio ile sheria ya mwenye nguvu ndio atasurvive.

KWA WALIMU; Hebu jaribu kujipima uwezo wako wa kumsaidia mtoto kuwa na tabia njema bila kumuumiza.Mimi nilikuwa moja kati ya walimu wanao amini sana viboka.Sasa hivi nikimuona mwalimu anamchapa mwanafunzi namuona kama mwalimu aliefell kila kitu na hata hastahiri kumfundisha mwanafunzi jinsi ya kuendesha maisha na kuwa mtu mwenye furaha wakati yeye anashindwa kumfurahisha mwanafunzi huyo. Ukiweza hasa kuzifuata mbinu mbali mbali za kuwasaidia wanafunzi kuwa na tabia njema utajikuta unaipenda kazi yako kiasi kwamba hata ukiwa ni siku ya kufunga shule unjisikia kulia kwasababu wanafunzi unawaona kama familia yako na wanajisikia hivyo hivyo. Hakuna kitu ninachofurahi kila siku asubuhi nikienda kazini kama kuona kundi la wanafunzi wakinishangilia baada ya kuniona mwalimu wao nawasili kazini. TUACHE KUWAFANYA WANAFUNZI MAADUI ZETU KWASABABU HUWEZI KUMFUNDISHA ADUI YAKO AKAKUELEWA. Sitaki kuwaacha walimu hapa bila kuwapa kamfano ka jinsi unavyoweza kusaidia tabia njema kwa wanafunzi; Soma tabia za wanafunzi wako wote na ujue kila mmoja anapenda nini.Mwanafunzi anapokosea jambo mwambie siku hiyo hatafanya kile anachokipenda ikiwa ni kucheza mpira au rede. Huu ni mfano tu wa adhabu ambazo hazimuumizi mwanafunzi mwili wake bali zinampa motisha kufanya vizuri.Zipo nyingi ambazo kama mtu anahitaji msaada anaweza kunitumia ujumbe kwenye 0626641484 tukakubaliana jinsi ya kusaidiana kwa hili. MOJA KATI YA MAMBO NINAYO YAPIGANIA SASA HIVI NI KUPATA MSAADA KUTOKA KWA WADAU WA ELIMU TUWEZE KUWA NA MADARASA AMBAYO YATAKUWA KAMA YA MFANO WA JINSI YA KUWAFUNDISHA WATOTO WAKIWA NA FURAHA,HURU NA KUIJUA THAMNANI YA ELIMU.Kama wewe ni mmoja wapo pia tafadhari usisite hakuna juhudi inayopotea bure.

KWA WAZAZI; Tafadhari sana wazazi msitumie watoto kama sehemu ya kumalizia hasira zenu.Watoto wanarugha mbalimbali ambazo zinaashiria upendo na kila mmoja anarugha yake ambayo ukiigundua ukaifanyia kazi basi mtoto huyo atafanya unachotaka badala ya kumpiga mifimbo kila siku.
Mfano kuna watoto (pamoja na watu wazima) ambao lugha yao ya upendo ni Zawadi.Yani mtoto huyu au mtu huyu ukiwa unampa zawadi basi mwambie chochote atakuwa anakufanyia kwasababu unampa furaha ya maisha yake.LUGHA HIZI ZA UPENDO ZIKO TANO NA KILA BINADAMU ANA LUGHA YAKE. Wazazi pia kama unataka kujua zaidi kuhusu lugha za upenda kwa mwanao na mkeo au mumea na jinsi ya kuzitumia ukapata faraja ya maisha na mtoto akaacha kukusumbua nitumie ujumbe ili tujue tunasaidiana vipi.


Jumatatu, 5 Machi 2018

WE ARE BACK!

Welcom dear readers of this blog. We are now back and we assure you with very important contents which will capture your attention! So please stay tuned!.

Alhamisi, 28 Aprili 2016

MAMBO YA KUZINGATIA WAKATI UNABUNI JINA LA BIASHARA YAKO.

business: Portrait thinking handsome man looking up with idea light bulb above head isolated on gray wall background
PICHA;FIKIRIA KWA MAKINI KUHUSU JINA LA BIASHARA YAKO.

Wafanyabiashara wamekuwa wakichukulia jina la biashara kama kitu cha kawaida na sio moja kati ya vipaumbele katika mambo yao muhimu ya kuzingatia wakati wa kuanzisha biashara.Kufanya hivyo ni makosa kimsingi kwa sababu huweza kuleta madhara makubwa katika biashara yako hususani wateja wako wanapokutana na wateja wapya wanaohitaji kuijua biashara yako.

Jumanne, 26 Aprili 2016

NINA UHAKIKA MENGI KATI YA MAMBO HAYA HUYAFAHAMU.


Black flying fox bat hangs upside down in a tree
PICHA;POPO AKIWA JUU YA MTI.
  • Popo ndio mnyama pekee anaeweza kupaa angani.

FAHAMU KUHUSU WAKALA WA MAJENGO

PICHA(realestateslandny.blogspot.com)

Katika maeneo tunayoishi tunapotaka kununua,kuuza au kupangisha nyumba pamoja na viwanja tumezoea kuwatumia watu tunaowaita madalali.Bahati mbaya madalali hawa wanakuwa hawana chochote kinachomtambulisha au kitakachokupa wewe ulinzi endapo mambo yatakwenda vibaya.Utakuta mahali wamekaa vijana wengi tu maarufu kama kijiwe na wameweka kibao kimeandikwa madalali wa viwanja na nyumba wanapatikana hapa.

Jumatatu, 25 Aprili 2016

HIKI NDICHO KINACHOSABABISHA UPUNGUFU WA AJIRA TANZANIA.

PICHA;WANAFUNZI CHUO KIKUU MUHIMBILI WAKIANDAMANA.

Katika miaka ya hivi karibuni Tanzania imekumbwa na tatizo kubwa la uhaba wa ajira.Wasomi wamekuwa wengi sana ukiringanisha na ajira zilizopo nchini kitu ambacho kinafanya wasomi wetu kufanya kazi ambazo hazifanani na elimu wanayopata pamoja na kulipwa mishahara duni ambayo haiwezi kumpa mtu motisha wa kufanya kazi kwa juhudi na maarifa.

TAZAMA JINSI MAJAMBAZI HAWA WALIVYOCHOMWA MOTO. (ONYO;PICHA HIZI SI ZA KAWAIDA)


PICHA;MOJA KATI YA WEZI AKIWA AMEUNGUA VIBAYA.

Katika hali ya kusikitisha na muendelezo wa raia kuchukua sheria mkononi,wawili kati ya majambazi saba waliokamatwa na wananchi walipigwa vibaya na hatimae kuchomwa moto huko Nigeria.

TAZAMA SAMAKI ALIEVULIWA NA HUYU JAMAA.(PICHA)

PICHA; SAMAKI AINA YA OAR ALIEVULIWA HUKO TAIWAN.

Mvuvi mmoja huko Taiwani alifanikiwa kumvua samaki mkubwa aina ya OAR aliekuwa na urefu wa mita tano.Kwa mujibu wa wataalamu,samaki huyo alievuliwa alikuwa ni mtoto kwasababu aina hiyo ya samaki huwa wanakuwa wakubwa kufikia kiwango cha urefu wa mita 1000 na ni mala chache sana kufanikiwa kuwavua samaki hao kwasababu wanakaa kwenye kina kirefu sana cha bahari.

Jumapili, 24 Aprili 2016

UMESHAIONA VIDEO MPYA YA LADY JAYDEE #NDINDINDI# BONYEZA HAPA KU PLAY#



#MUKEBEZI TV# LADY JAYDEE NDINDINDI OFFICIAL MUSIC VIDEO.
Kama unataka kutazama video zaidi unaweza kutazama upande wa kulia wa blog hii,Bonyeza #MUKEBEZI TV# kutazama zaidi.

Kama unamaoni zaidi kuhusu Video hii na ungependa mhusika ajue unachofikiria andika maoni yako hapa chini na yatamfikia mhusika.

HILI NI MOJA KATI YA MAMBO MABAYA WANAYOFANYA MASTAA#ONE OF BAD HABIT OF FAMOUS PEOPLE#

PICHA;MTOTO WA 50 CENT AKILIA BAADA YA KUKUTANA NA BABA YAKE KWA MALA YA KWANZA.

Mastaa wengi hususani vijana wamekuwa na tabia nyingi ambazo zimekuwa hazikubaliki katika jamii.Lakini wanapoulizwa wamekuwa wakijitetea kuwa wanaishi maisha ya kistaa.

UBONGO WA MWANAMIELEKA HUYU KUTOLEWA KWA WANASAYANSI# THE BRAIN OF THIS WRESTLER TO BE DONATED FOR SCIENCE RESEARCH#


PICHA;CHYNA, MWANAMIELEKA WA ZAMANI WA WWE.

Ubongo wa manamieleka wa zamani wa WWE mwanadada CHYNA aliekutwa akiwa amefariki dunia katika apartment yake siku ya jumatano utatolewa kwa ajili ya uchunguzi wa kisayansi.

HIKI KINATHIBITISHA ALIE BORA KATI YA MFANYA KAZI NA MFANYA BIASHARA.

PICHA;BUSINESS MAN

Umewahi kujiuliza swali hili kwamba

 ni nani alie bora na anae enjoy maisha zaidi kati ya mfanya kazi na mfanyabiashara?

Katika jamii zetu tumekuwa tukihimizwa toka tuko wadogo kusoma kwa bidii ili siku moja tuje kuwa na moja kati ya proffessional kama Udactari,Uhandisi,Ualimu (kama alivyo muandishi wa mada hii),Urubani,Uanasheria,Uandishi wa habari(kama alivyo muandishi wa mada hii) na fani nyingine nyingi.Tumekuwa tukiaminishwa hivyo na sisi tukiwaaminisha watoto wetu kwamba unapokuwa na moja kati ya fani hizo basi una uhakika wa kuwa na maisha bora.

BIASHARA INAHITAJI UMAKINI,TAZAMA KICHWA HIKI KILIVYOHARIBU BIASHARA(PICHA)


PICHA;KICHWA CHA KUKU KILICHOKUTWA KWENYE CHAKULA.

Jumamosi, 23 Aprili 2016

MOTISHA NA FAIDA ZAKE #MOTIVATION AND ITS ADVANTAGES#

PICHA (Getty Images);WEWE NA WAFANYAKAZI WAKO MNAHITAJI MOTISHA.


Katika kila tunachokifanya binadamu

motisha ni kitu ambacho kinahitajika sana.Motisha ni msukumo au shinikizo unalolipata kufanya jambo fulani kwa mategemeo fulani.Motisha zinaweza kuwa hasi au chanya.

Mwili wa binadamu umeumbwa katika mfumo wa kutamani na kukinai mambo.Unaweza kutamani sana kufanya jambo fulani lakini baada ya kulifanya kwa muda fulani ukakinai na kutaka kufanya jambo lingine kutokana na sababu mbalimbali.

Kuna mbinu mbalimbali unazoweza kuzitumia kujipa motisha wewe na wafanyakazi wako ili kuendelea kufanya kazi kwa ari ileile;

>>LIKIZO<<
Mwili wa binadamu pia huchoka na inafikia kipindi unahitaji kupumzika.Wafanyabiashara wamekuwa na tabia ya kufanya kazi siku zote 365 za mwaka bila kupumzika kitu ambacho kinaweza kupunguza morali ya kufanya kazi.

Unapaswa kuwa na utaratibu maalum ambao utakufanya wewe na wafanyakazi wako kuwa na mapumziko walau mala moja kwa mwaka kwenda kutembelea ndugu na marafiki.

Kumbuka swala la likizo halijalishi unafanya biashara ndogo kiasi gani,unahitaji mapumziko!!.

>>MAFUNZO<<
Unapaswa pia wewe kama mfanyabiashara kujipa motisha kwa kuhudhuria mafunzo mbalimbali yanayotolewa kwaajili ya biashara.Mafunzo haya yatainua tena ari ambayo itakuwa inaonekana kupotea kwani watoa mafunzo wengi huwa na tabia ya kuhamasisha.Lakini pia kama kuna mambo mapya utayapata katika mafunzo hayo utakuwa na ari ya kutaka kuyaongeza katika biashara yako na hivyo kuifanya biashara yako kuwa bora zaidi.

>>KUFANYA TOUR<<
Ni vizuri sana wewe kama kiongozi kupanga safari za kutembelea maeneo mbalimbali ya kihistoria na mbuga za wanyama kama sehemu ya motisha.
Pamoja na kuwapa ari wafanyakazi wako,pia hii husaidia kubadili mazingira waliyozoea na hatimae kupata changamoto mpya ambazo huweza kuwasaidia katika utendaji wao.

Asante sana mpendwa msomaji kwa leo na tukutane tena wakati mwingine kuendelea na mada zetu hizi za biashara na maendeleo.

Ijumaa, 22 Aprili 2016

UONGOZI KATIKA BIASHARA #BUSINESS MANAGEMENT#


PICHA(Bing.com);Uongozi sio ukali
.
Hujambo mpenzi msomaji mtu wangu wa kazi na karibu tena katika mfululizo wa mada zetu hizi ambazo kwa kipengele hiki tunamalizia kabla ya kuanza kukuletea upande wa pili ambapo tutakuwa tunaangalia biashara mbalimbali na fulsa nchini Tanzania. Tutaangalia mitaji yake ya kuanzia,faida zake,changamoto zake na hasara zake.Cha msingi ni wewe kuwa msomaji namba moja wa chombo hiki cha habari na kuendelea kufuatilia kila siku bila kukosa. Ni wakati mwingine tena ambapo Tunamshukuru mwenyezi MUNGU kwa kuendelea kutupatia pumzi yake.

Leo katika mada hii tutaangalia uongozi katika Biashara yako na unapaswa kunifuatilia kuanzia mwanzo mpaka mwisho.Kama utakuwa na swali au maoni tafadhali andika hapo chini baada ya kusoma mada hii nami nitakujibu wakati huohuo.Tutahakikisha kila comment inayoandikwa hapa inajibiwa ipasavyo.TUENDELEE..