Kurasa

Jumatatu, 30 Juni 2014

JINSI YA KUTENGENEZA SABUNI YA KUNAWIA MIKONO

Moja kati ya mahitaji makubwa ya watu ikiwemo wafanyabiashara za mama lishe,mabucha na nyingine,ni sabuni ya kunawia.Kutokana na mahitaji makubwa waliyonayo watu na kukosekana kwa bidhaa hiyo wahitaji hujikuta wakitumia sabuni ambazo hazikutengenezwa kwa kazi hiyo kama sabuni za unga,shampoo na sabuni za vipande ambazo huwasababishia madhara bila kujijua.
Leo katika somo letu tutajifunza jinsi ya kutengeneza sabuni za kunawia mikono.fuatana nami mwanza mpaka mwisho.

AJALI YAUA TENA NA KUJERUHI


Mtu mmoja amefariki na wengine wawili kujeruhiwa katika ajali mbaya iliyihusisha muendendesha toroli na basi la abirilia huko sengerema,mkoani mwanza.
Tukio hilo lilitokea jana majira ya saa tisa arasili ambapo basi la abiria mali ya kampuni ya Rushanga lenye namba za usajili T312 lililokuwa na abiria likielekea mkoa wa mwanza kutokea Geita kupitia kivuko cha Kamanga lilimgonga muendesha toroli lililokuwa limebeba miti na kusababisha kupasuka kichwa na kupoteza maisha hapo hapo.
Mwili wa marehemu umepelekwa katika hospitali ya wilaya ya sengerema kwa uchunguzi zaidi wakati majeruhi wakipelekwa hospitalini hapo kwaajili ya matibabu.Laiti kama marehemu angevaa kofia ngumu asingekutwa na umauti huo.Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi amin.

Jumamosi, 28 Juni 2014

NI BRAZIL NA COLUMBIA ROBO FAINAL

Nyota wa Colombia James Rodriguez
Nyota wa Colombia na Monaco James Rodriguez alidhibitisha udedea wake katika kombe la dunia alipofunga mabao mawili na kuisaidia Colombia kuwa timu ya pili kufuzu kwa nane bora .
Rodriguez mwenye umri wa miaka 22 alikuwa nyota katika safu ya ushambulizi ya Colombia ilipokuwa ikichuana dhidi ya Uruguay bila mshambulizi wake mwenye utata Luiz Suarez.
Bila shaka mshambulizi huyo sasa atakumbukwa katika mizani sawa na Neymar wa Brazil na Lionel Messi wa Argetina nyota wa Brazil2014 watakapokuwa wakitajwa haswa kutokana na miondoko yake hapo jana katika uwanja wa Rio.Wengi wanaashiria kukosekana na Suarez kuwa kisababu cha kikosi cha Oscar Tabarez kushindwa kusonga mbele katika kipute hicho kinachoendelea huko Brazil.
Mchezaji huyo wa Monaco alitangaza kuwepo kwake uwanjani kwa mkwaju wa dakika ya 28 ya kipindi cha kwanza uliomwacha kipa ya Uruguay Fernando Muslera ameduwaa huku maelfu wa mashabiki wa Colombia wakishangilia kwa nusia tikiti ya Robo fainali ya kombe la dunia .
Nyota wa Colombia James Rodriguez anatarajiwa kuibabashia Brazil
Rodriguez hakuachia hapo, aliendelea kuwa mwiba katika safu ya ulinzi ya Vijana wa Oscar tabarez na juhudi zake zikazaa matunda kunako dakika ya 58 Mshambulizi huyo alipofuma bao la pili na ushindi na kuahakiki nafasi hiyo ya nane bora kwa Colombia.
Kufuatia matookeo hayo sasa Colombia watachuana na wenyeji Brazil katika mechi inayotazamiwa na wengi kuwa ngumu ya kuwania nafasi ya nusu fainali.
Mechi hiyo itachezwa siku yaijumaa katika uwanja wa Fortaleza .
Uruguay ilikosa keke zake za kawaida katika mechi hii ilikuwa bayana kuwa japo Suarez hakuwepo uwanjani mashabiki wake walimsifia na kubeba mabango y kumuunga mkono mshambulizi huyo wa Liverpool ya Uingereza .
Washambulizi wake Maximiliano Pereira na Edinson Cavani fndio waliomjaribu kipa wa Colombia David Ospina.
BBC

MIAKA 1OO TANGU MSABABISHI WA VITA YA DUNIA ALIPOUAWA HUKO SARAJEVO

Shughuli zinafanywa leo kukumbuka tukio la karne kamili iliyopita mjini Sarajevo, ambapo mrithi wa mfalme wa mamlaka ya Austria-Hungary aliuliwa na mzalendo wa Serbia na kuwa chanzo cha kuzuka Vita vya Kwanza vya Dunia.
Vilembwe vya prince huyo, Franz Ferdinand, watahudhuria gwaride litalofanywa katika kasri yao karibu na Vienna, Austria.
Princess Anita Hohenberg, kilembwe cha Franz Ferdinand, aliiambia BBC kwamba Franz Ferdinand daima hakupenda vita:
"Baba wa babu yangu angeshtushwa, angeshtuka kabisa, kwa sababu akijua upungufu wa jeshi lake, kwa sababu alikuwa mkuu wa jeshi.
Vita hivo vilikuwa vibaya, vibaya sana."
Austria sasa haina mfalme.

HOSPILI ZA MATIBABU YA UZAZI ZAPUNGUKIWA MBEGU ZA KIUME

Shahawa
Uingereza inakabiliwa na upungufu wa Mbegu za kiume hali ambayo huenda ikalazimu kiliniki za matibabu ya uzazi nchini humo kuchukua mbegu duni.
Onyo hili limetolewa na shirika la kijamii la matibabu ya uzazi nchini humo BFS.
Inadaiwa kuwa baadhi ya kliniki hizo hutegemea shahawa kutoka nchi za kigeni kutokana na mahitaji yake nchini humo.
Lakini mwenyekiti wa shirika hilo Daktari Allan Pacey amesema kuwa ana wasiwasi kwamba baadhi ya vituo hivyo vya matibabu sasa vinatumia kila njia ili kupata wafadhili wa mbegu hizo.
Amesema kuwa wanawake watakabiliwa na mbinu zitakazogharimu kiasi kikubwa cha fedha iwapo mbegu duni zitatumiwa.
Inadaiwa kuwa upungufu huo unasababishwa na kuondelewa kwa sheria kwamba majina ya wanaotoa mbegu hizo sasa ni sharti yajulikane ikilinganishwa hapo awali ambapo watu wengi walipendelea kuficha majina yao.
Mahitaji ya wafadhili wa shahawa yanazidi kushuka kwa kuwa maendeleo ya matibabu ya uzazi yanawafanya wanaume wengi kutafuta watoto wao wenyewe.
Hatahivyo uhaba wa wafadhili wa mbegu za kiume bado upo.
Takwimu kutoka mamlaka ya kudhibti uzazi wa binaadamu zinaonyesha kuwa moja kati ya mbegu nne za kiume zimetoka katika mataifa ya kigeni.
Takwimu hizo zilikuwa moja katika kila mbegu kumi mnamo mwaka 2005.
BBC

MAAJABU:ALAZWA HOSPITALI KWA LAZIMA BAADA YA KUSEMA HAMUAMINI MUNGU

Mwanamume mmoja katika jimbo la Kano, nchini Nigeria, amepelekwa katika kituo cha matibabu ya kiakili baada ya kusema kuwa hamwamini Mungu.
Taarifa hii ni kwa mujibu wa shirika moja lisilo la kiserikali nchini nIGERIA.
Mubarak Bala alizuiliwa kinyume na matakwa yake hospitalini baada ya familia yake kumpeleka huko kwa matibabu.
Duru katika hospitali hiyo zimesema kuwa mwanamume huyo mwenye umri wa miaka 29 alitibiwa kwa matatizo ya kiakili na kwamba hataendelea kuzuilikwa kwa muda mrefu.
Jimbo la Kano lina idadi kubwa ya waumini wa kiisilamu, na limekuwa chini ya sheria za kiisilamu tangu mwaka 2000.
Kano ni jimbo lenye kufuata sheria za kiisilamu
Shirika hilo la kimataifa limesema kuwa wakati ambapo Bala aliwaambia jamaa wake kuwa hamuamini Mungu, familia yake uilimpekeka kwa daktari kuuliza ikiwa akili yake iko timamu.
Licha ya kufahamishwa kuwa mwanamume huyo hana tatizo lolote la kiakili, familia ya Bala ilitafuta ushauri wa daktari mwingine aliyewafahamisha kuwa hatua yake ya kumkana Mungu, inatokana na matatizo ya kiakili.
Bwana Bala, ambaye ni mwanafunzi wa chuo kikuu, alilazimishwa kupata ushauri wa daktari wa kiakili , ingawa alitumia simu kuwasiliana na wanaharakati wa haki za kibinadamu.
Hospitali ambako alikuwa ana pokea matibabu ilisema katika taarifa yake kuwa Bwana Bala hana tatizo lolote la kiakili na kuwa yuko sawa.
Alilazwa hospitalini kwa sababu alihitaji kuchunguwa na daktari, ilisema taarifa ya hospitali hiyo.
BBC

MASKINI:BINTI ABAKWA NA BABA YAKE,APEWA UJAUZITO NA KUAMBUKIZWA UKIMWI

Musoma.“Amini usiamini hizi ni zama za mwisho mwanangu, mimi hili suala bado haliniingii akilini kabisa, kwani nilizoea kusikia kama hadithi kuwa mzazi ana uhusiano wa mapenzi na mwanawe, lakini leo hii yamenikuta ya kunikuta,” haya ni maneno ya Bhoke Mwita (siyo jina halisi), mama mzazi wa binti anayedaiwa kubakwa na baba yake mzazi kwa miaka minne.
Bhoke anasema kibaya zaidi mwanaye amefanyiwa unyama huo na baba yake mzazi, huku akimwachia doa ambalo haliwezi kufutika milele ambao ni ugonjwa wa Ukimwi.
Tukio hilo linamsababisha Wanjara kunyamaza kwanza kabla ya mahojiano, baadaye anadai binti yake kapewa ujauzito na maambukizi ya Ukimwi na baba yake, ingawa alikuwa hajitambua kuwa ni mgonjwa hatua ambayo imemuumiza na kumtia aibu kwenye jamii.
Mkazi huyo wa Mtaa wa Kigera Kibini, Kata ya Kigera, Manispaa ya Musoma mkoani Mara, anasimlia historia ya maisha yake hadi kuzaa mtoto huyo wa mwisho nje ya ndoa baada ya mumewe kufariki, lakini hatima imekuwa kugeuzwa mke mwenza.
Mwita anasita kuendelea na simlizi kabla binti yake aliyefanyiwa unyama na baba yake, hajasimulia masaibu yake: “Matatizo niliyonayo ni mengi, Mungu pekee ndiye anayefahamu, bado naongezewa msalaba mzito kama huu.”
Ghafla anapaza sauti anaita jina la binti yake aliyefanyiwa ukatili, aliyekuwa chumba kingine na kumtaka aeleze yote yaliyomsibu ili ulimwengu utambue.
Simulizi za binti
Anatokea binti mrembo ila sura yake inaonyesha unyonge, mrefu, mwembamba anasalimia kwa sauti ya upole huku akielekea kwenye kiti kuketi, afya yake siyo ya kuridhisha.
Bila kupoteza muda, binti huyo anadai alianza kuishi na baba yake mwaka 2002 akiwa anaingia darasa la tatu, baada ya mama yake kupata kibarua kwenye nyumba ya watawa.
Anasema baba yake alikuwa akiishi na kaka zake wawili wakubwa ambao walikuwa wamemaliza shule na wakati huo walikuwa wakijihusisha na kazi za vibarua.
Anasimulia kuwa alipofika darasa la tano, baba yake alikuwa akimfuata chumbani kabla ya kaka zake hawajarudi nyumbani na kumtaka afanye naye ngono. Binti huyo anasema kwamba wakati huo alikuwa hafahamu chochote kuhusu mapenzi.
“Nilipoona baba ananipiga kila siku, nilikubali, akawa anakuja chumbani kwangu na wakati mwingine ananiita kwake, tukishamaliza ananiambia niende kwangu kulala, hivyo nikaona kama jambo la kawaida,” anasimulia binti huyo.
MWANANCHI

Ijumaa, 27 Juni 2014

JINSI YA KUTENGENEZA SABUNI YA KUFULIA YA MAJIVU

Hii ni moja kati ya sbuni ambazo ainatumika sana hususani Afrika kutokana na jinsi ambavyo ni rahisi kupatikana.
Malighafi zake ni majivu ya kuni, mafuta ya nazi au ya mawese au ya nyonyo,Glyceline,chumvi kwaajili ya kuleta uzito pamoja na magadi soda.

JINSI YA KUTENGENEZA;

HEBU ANGALIA UNIAMBIE UNAWEZA KUAMINI JAMAA HAWA SIO MAPACHA?

Tumekuwa tukisikia misemo mala nyingi watu wakisema binadamu tumeumbwa wawiliwawili sasa picha hizi zinakuthibitishia kuwa kweli binadamu tuko wawiliwawili.Tafadhalia usisite kutuandikia maoni yako hapo chini unachofikilia.

PSQUARE WAFANYA SHOOTING YA WIMBO MPYA WALIOIMBA NA TI

Kwa taarifa kutoka kwenye chanzo kilicho karibu kabisa na kundi la psquare,wawili hao wamefanya ushirikiano mwingine katika wimbo wao mpya ambao sasa wana ufanyia shooting wakiwa na msanii na rapa mkubwa kabisa nchini marekani TI.Jina la wimbo huo halijapatikana mapema kwa kuwa wawi
li hao bado hawajaamua kuwashirikisha waandishi wa habari.

PICHA MBALIMBALI ZA JAYZ NA BEYONCE KATIKA TOUR YAO YA SASA

Katika hali ya kushangaza mashabiki walionekana kuwa na furaha sana hasa baada ya kuoneshwa video ya Jayz na mkewe Beyonce wakifunga ndoa ya siri huko Miami Marekani.Wanandoa hao waliimba nyimbo zaidi ya arobaini na mbili tarehe 25 june 2014 na hizi ni baadhi ya nyimbo hizo;
Here’s a rundown of songs performed by the couple yesterday.

03 Bonnie & Clyde
Crazy In Love
N*ggas In Paris
Tom Ford
Run The World (Girls)
***Flawless
Yonce
Jigga
Dirt Off Ya Shoulders
Big Pimpin
Naughty Girl
Ring The Alarm
On To The Next One
Clique / Diva
Baby Boy
Haunted
No Church In The Wild
Drunk In Love
Public Service Announcement
Why Don’t You Love Me?
Holy Grail
Fuckwithmeyouknowigotit
Beach Is Better
Partition
99 Problems
If I Were A Boy
I Just Wanna Love You
Single Ladies
Hard Knock Life
Pretty Hurts
Part II (On The Run)
Forever Young
Halo
Lift Off (Outro

DAKTARI WA PISTORIUS APATA MSHTUKO


Daktari wa akili anayetathmini hali ya mwanariadha Oscar Pistorius katika kesi ya mauaji ya mpenziwe Reeva Steenkamp amepatwa na mshtuko wa moyo.

Hatahivyo swala hilo halitarajiwi kucheleweshwa kusikizwa kwa kesi hiyo ambayo itaendelea siku ya jumatatu,upande wa mashtaka umesema.

Bwana Pistorius anatarajiwa kukamilisha siku thelathini za utathmini wa akili yake.

Jaji katika kesi hiyo aliagiza kufanywa kwa ukaguzi huo baada ya shahidi mmoja wa Pistorius kusema kuwa mshtakiwa huyo alikuwa anakabiliwa na ugonjwa wa wasiwasi.

Mwanariadha huyo amekana kumuua mpenziwe kimakusudi na anasema kuwa alimpiga risasi kwa bahati mbaya kupitia mlango wa choo siku ya Valentine mwaka uliopita alipodhani kwamba mwanamke huyo wa miaka 29 alikuwa ni jambazi

Alhamisi, 26 Juni 2014

ROAD TO SUCCESS IS NOT EASY

There is a curve called failure, a loop called confusion, speed bumps called friends, caution lights called family, and you will have flats called jobs.
But, if you have a spare called determination, an engine called perseverance, insurance called faith, and a driver called God, you will make it to a place called success!

SERIKALI YAPIGA MARUFUKU TABIA YA ASKALI KUJIFICHA POLINI

Serikali imepiga marufuku tabia ya askari Polisi wa Kikosi cha Usalama Barabarani, kuvizia magari katika barabara kuu wakiwa na kifaa cha kupima mwendo kasi wa magari.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Peraira Silima, alisema tabia hiyo ya trafiki ni kinyume cha sheria na zinaweza kusababisha ajali.
Hata hivyo, Silima aliwataka madereva kutii Sheria za Barabarani ikiwemo kupunguza mwendokasi na kufafanua kuwa, wakati mwingine askari hutafuta kivuli na hatua hiyo isichukuliwe kuwa wanavizia magari.
Katika swali lake, Ngoye alitaka Serikali ieleze ni hatua gani zimekuwa zikichukuliwa kuhakikisha madereva wanafuata sheria zilizowekwa kama inavyofanyika katika nchi nyingine.
Ngoye pia alitaka Serikali ieleze kwa nini madereva wameendelea kutumia magogo, mawe na majani yenye miba barabarani kuashiria kuwa kuna gari limeharibika, na wakiondoka wanayaacha na wengine wameendelea kuendesha magari huku wakisikiliza simu.
Naye Mbunge wa Musoma Mjini, Vincent Nyerere (Chadema), alihoji kama ni sahihi kwa trafiki kuvizia magari na kifaa cha kupima mwendo kasi.
Akifafanua majibu ya maswali hayo, Silima alisema trafiki kujificha na chombo hicho na kujitokeza kusimamisha gari ni kinyume cha sheria kwa kuwa tabia hiyo inaweza kusababisha ajali.
Kuhusu matumizi ya magogo, majani na mawe, alisema ni kinyume na Sheria na kutaka madereva watumie alama za pembe tatu ambazo ni nzito na kuachana na alama hizo ambazo ni nyepesi ambazo hupeperushwa na upepo.
Silima pia alionya kuwa Serikali iko mbioni kuanza kuwanyang’anya leseni za udereva madereva wote ambao watathibitika kukithiri kwa makosa ya usalama barabarani, na kuzuiwa kabisa kufanya kazi hiyo.
Hatua hiyo itaanza kuchukuliwa mara baada ya kukamilika na kuanza kwa Mfumo mpya wa Nukta, ambao utaweka kumbukumbu za makosa ya madereva ambayo itatumika kuwachukulia hatua hiyo.

KAFULILA NA WELEMA WAKATAA KUPATANISHWA

Tafrani iliyojitokeza bungeni juzi kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali Frederick Werema kumuita Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila(NCCR Mageuzi) tumbili, naye kumjibu kwa kumuita mwizi imeingia katika hatua nyingine ambapo wawili hao wamekataa kusuluhishwa.
Jana asubuhi baada ya Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai, kuahirisha shughuli za Bunge, Mwenyekiti wa Bunge, Mbunge wa Ilala, Mussa Azzan 'Zungu', aliwakuta Werema na Kafulila wakiendeleza mzozo nje ya ukumbi wa Bunge.
Kutokana na hali hiyo, Zungu alijitolea kuwapatanisha huku akijaribu kukaa katikati awashikishe mikono ili yaishe, lakini hakufanikiwa.
Wakati Zungu akifanya jitihada hizo, Werema alilalamika.“Mimi nina watoto na wajukuu unanitukana…kwani ninyi hamkusikia akinitukana?”Alihoji huku baadhi ya waandishi wakishuhudia.
Wakati Werema akilalamika kutukanwa huku Zungu akiwa katikati yao, Kafulila naye alilalamika:“Wewe uliniita mimi mnyama (Tumbili) kumbuka vizuri.”
Werema akijibu malalamiko ya Kafulila, alisema yeye hakuwa na nia ya kumtukana bali alikuwa akielezea msemo wa Wanyankole kuwa tumbili hawezi kuamua kesi ya msituni na kukataa kushikana mkono na Kafulila akisisitiza aombe radhi.
Kutokana na hali hiyo, Kafulila aliondoka kutoka nje ya uzio wa ukumbi wa Bunge bila kuomba radhi huku akimnyooshea kidole Werema, ambaye naye aliingia katika ofisi za Bunge huku akilalamika kutukanwa na Kafulila.
Juzi kabla ya kutoa kauli hiyo, Werema alikuwa akitoa ufafanuzi wa muongozo ulioombwa na Kafulila kuhusu fedha zilizokuwa katika akaunti ya Escrow iliyokuwa Benki Kuu (BoT), ambazo zimelipwa kampuni ya PAP, inayomiliki mitambo ya Kampuni ya Independent Power limited(IPTL).
Werema alisema fedha hizo si za Serikali kama inavyodaiwa na Kafulila kwa kuwa fedha za Serikali hazikai katika akaunti hiyo.
Aliendelea kufafanua kuwa taarifa zinazotolewa zinapotosha umma kuwa serikali imetoa fedha kuilipa IPTL, wakati ukweli ni kuwa fedha hizo ziliwekwa katika akaunti hiyo kutokana na misuguano baina ya wanahisa wawili waliokuwa wamiliki wa IPTL.
Werema alibainisha kuwa mmoja wa wanahisa hao, alikuwa akitaka IPTL ifilisiwe huku mwingine akipinga juu ya jambo hilo mpaka walipouza hisa zao na kumaliza mgogoro huo, ambapo Mahakama iliruhusu mali za kampuni hizo zipewe kwa mwanahisa mpya, PAP.
Werema alisema kuna watu walileta bungeni vipeperushi wakidai ni ushahidi kuhusu utoaji wa fedha hizo za akaunti ya Escrow na kuhusisha na rushwa.
"Kafulila ni miongoni mwa wanaoeneza taarifa potofu…, kama ni tuhuma au kuna rushwa itakuja kujulikana, tusubiri uchunguzi wa vyombo husika,”alisema.
Wakati akizungumza, Werema alitumia mfano wa kabila la Wanyankole, aliosema kuwa wana usemi unaosema kwamba tumbili hawezi kuamua kesi ya msituni.
Kabla ya kufafanua maana ya msemo huo, Kafulila bila kuwasha kipaza sauti alikuwa akipiga kelele kumuita Werema kuwa ni mtuhumiwa hivyo atangaze maslahi yake.
“Naomba nisikilize hata kama ni mtuhumiwa nina fursa ya kusikilizwa …nisikilize wewetumbili,”alijikuta akisema Werema.
Baada ya kusema hivyo, Kafulila hakukubali na yeye bila kuwasha kipaza sauti alisema:“wewe (Werema) ni mwizi tu.”
Kutokana na hali hiyo, Mwenyekiti wa Bunge, Zungu alimuomba Jaji Werema kukaa chini ili atoe ufafanuzi, huku Mbunge wa Ubungo, John Mnyika (Chadema) na Kafulila wakitaka kuzungumza.
Zungu alisema kwa kuwa Bunge lilishaamua kuwa suala hilo lipelekwe Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru) na kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), ni vyema kama Kafulila ana ushahidi wowote, apeleke huko.
Baada ya kutoa muongozo huo, ambao ulisitisha malumbano, Mwenyekiti Zungu alisitisha shughuli za Bunge mpaka jioni na kuondoka huku akisindikizwa na makatibu wa Bunge na wapambe kama kawaida.
Hatua ya Mwenyekiti wa Bunge kuondoka katika ukumbi baada ya kusitisha shughuli za Bunge, ilimpa fursa Jaji Werema kuweka sawa makabrasha yake na kutoka katika kiti chake, ambapo alionekana kama vile anakwenda kumkabili Kafulila.
Wakati hilo likitokea, Mbunge wa Maswa Mashariki, Sylvester Kasulumbai (Chadema), alihama katika kiti chake na kukimbilia alipokuwa amekaa Kafulila.
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, baadhi ya mawaziri walimzunguka Jaji Werema kabla hajamfikia Kafulila na Kasulumbai.
Mawaziri hao ni pamoja na Waziri wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Mahusiano na Uratibu, Stephen Wassira, Waziri wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, Waziri wa Sheria na Katiba, Dk Asha-Rose Migiro, Naibu Waziri wa Afrika Mashariki, Dk Abdullah Juma Saadalla na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, George Simbachawene.
Nje ya Bunge, Kafulila na Mnyika waliitisha mkutano na waandishi wa habari, ambapo walidai kuwa na ushahidi wa kutuhumu baadhi ya mawaziri kusema uongo bungeni kuhusu fedha hizo za Escrow.

MAREKANI YAPANGA KUWASAIDIA WAASI

Rais wa Marekani, Barrack Obama ameliomba Bunge la Congress kiasi cha dola milioni mia tano kwa ajili ya kugharamia mafunzo na kuwapatia silaha Waasi wa Syria.
Bado haijajuliakana ni aina gani ya msaada wa kijeshi ambao Marekani itautoa japo kulikuwa na maombi ya waasi hao wa Syria kuhusu kupewa makombora ya kubeba ya kutungulia ndege ambayo yalitupiliwa mbali kwa kuhofia silaha hizo zisiwaendee wanamgambo wa makundi ya kigaidi.
Ikiwa Bunge hilo litaridhia Ombi la Rais Obama,hii itakuwa mara ya kwanza kwa Jeshi la Marekani kujihusisha moja kwa moja kwenye mgogoro wa Syria, mashirika ya kiintelijensia ya Marekani tayari yanawasaidia waasi nchini Syria.
Waasi wa Syria wanapambana na wanajeshi wa serikali na wanamgambo wa ISIS, ambalo ni kundi la waislamu ambao pia wameteka mpaka ndani ya nchi ya Iraq.

ADHABU YA SUAREZ



Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Uruguay Luis Suarez amefungiwa mechi tisa na shirikisho la kandanda duniani Fifa baada ya kupatikana na hatia ya kumng'ta mlinzi wa timu ya Italia Giorgio Chiellini kwenye mechi yao ya kombe la dunia nchni Brazil.

Suarez pia amefungiwa kutojihusisha na shughuli yoyote ya kandanda kwa miezi minne na kutozwa faini ya dola elfu mia moja.

Taarifa zinazohusianaMichezoKutokana na adhabu hiyo Suarez sasa hatashiriki tena kwenye mechi zilizosalia za kombe la dunia.

Kutokana na adhabu hiyo iliyochukuliwa na kamati ya nidhamu ya Fifa Suarez sasa hatashiriki kwenye mechi ya raundi ya pili kati ya Uruguay na Columbia Juni tarehe 28.

Adhabu hiyo pia inamaanisha Suarez hatashiriki kwenye mechi za Uruguay zijazo za kombe la dunia endapo timu itazidi kusonga mbele na zile zijazo za kufuzu kwa mashindano ya kombe la dunia.

Kamati hiyo ya nidhamu ya Fifa imesema Suarez hatakiwi kuingia kwenye uwanja wowote Uruguay inapocheza wakati wa adhabu hiyo ya kutocheza mechi tisa za kimataifa.

Mwenyekiti wa kamati ya nidhamu ya Fifa Claudio Sulser amesema:"Hatuwezi kuruhusu tabia duni kama hii uwanjani hasa wakati wa kombe la dunia kwani mamillioni ya mashabiki kote duniani wanafuatilia mashindano haya. Kamati ya Fifa imetilia maanani kila kitu kwenye kitendo hicho kabla ya uamuzi huo.Tayari tumemjulisha mchezaji huyo na shirikisho la kandanda la Uruguay.''

Mashabiki wengi duniani wamemshutumu vikali Suarez kwa kumng'ata mchezaji huyo wa Italia kwani hii ni mara ya tatu anapatikana na hatia hiyo.

Lakini mashabiki, waandishi wa habari wa Uruguay na shirikisho la kandanda nchini humo wamemtetea mchezaji wao,wakisema hizo ni njama za kumuangamiza Suarez ambaye huichezea Liverpool ya England

KENYATA AONGOZA KUTUMIA TWITTER


Rais Kenyatta amempiku Paul Kagame wa Rwanda kwa idadi ya wafuasi kwenye Twitter

Rais wa Kenya uhuru Kenyatta ndiye Rais anayejishughulisha zaidi kwenye mtandao wa Twitter barani Afrika.

Kenyatta amempiku Rais wa Rwanda Paul Kagame na mwenzake wa Afrika Kusini Jacob Zuma.

Taarifa zinazohus
ianaKenya, AfrikaKenyatta ambaye amekuwa mamlakani tu kwa mwaka mmoja, amejipatia wafuasi 456,209, yuko mbele ya mwenzake wa Rwanda Paul Kagame mwenye wafuasi 408,353 ambaye amekuwa mamlakani tangu mwaka 2000, miaka sita kabla hata ya Twitter kuanzishwa.

Rais wa Afrika Kusini anayesifika kwa kashfa mbali mbali, Jacob Zuma ana wafuasi 325,896 akishikilia nafasi ya tatu.

Hata hivyo swali ni je maerais hawa hutumia vipi Twitter? Je wao huwa na mazungumzo ya moja kwa moja na wafuasi wao?

Waziri mkuu wa Uganda, Amama Mbabazi '@AmamaMbabazi,' ndiye kiongozi mwenye kuwasiliana zaidi na wafuasi wake duniani kwenye Twitter huku akiwajibu maswali yao kwake.


408,353, idadi ya wafuasi wa Rais Kagame kwenye Twitter

Asilimia tisini na tano ya mawasiliano yake kwenye Twitter ni '@replies,' ishara ya kuwajibu wafuasi wake. Utafiti huu ni kwa mujibu wa utafiti wa kimataifa kuhusu viongozi wanavyojishughulisha na Twitter, wenye mada, Twiplomacy.

Waziri mkuu mpya wa India, Narendra Modi ana wafuasi milioni 4,967,847 , na anaelekea kushinda Ikulu ya white House ambayo ina wafuasi milioni 4,976,734 katika nafasi ya tano.

Zaidi ya asilimia 83 ya mataifa yote duniani yana uwakilishi katika Twitter, na asilimia 68 ya viongozi wana akaunti za twitter kwa mujibu wa utafiti wa shirika la Burson-Marsteller, nchini Marekani.

Viongozi wanaofuatwa sana kwenye Tiwtter ni pamoja na Barack Obama (@BarackObama) akiwa na wafuasi milioni 43, Papa Francis (@Pontifex) ana wafuasi milioni 14 akifuatiwa na Rais wa Indonesia Susilo Bambang Yudhoyono (@SBYudhoyono) akiwa na wafuasi milioni tano.


Jacob Zuma kama rais anashikilia nafasi ya tatu kwa idadi kubwa ya wafuasi wa Twitter Afrika

Rais Barack Obama alikuwa kiongozi wa kwanza kuanzisha akaunti ya Twitter mwaka 2007.

Kati ya serikali 643 zenye akaunti za Twitter ambazo zilitathminiwa katika nchi 161, ni mataifa 32 pekee hasa yaliyo Afrika na Asia ya Pacific ambayo hayana shughuli nyingi kwenye Twitter.

Utafiti huo pia ulifichua kuwa mawaziri wa mataifa ya kigeni hutumia sana Twitter kutafuta ushirikiano wa kidiplomasia

Jumatano, 25 Juni 2014

MWANASHERIA MKUU AMUITA MBUNGE TUMBILI,NGUMI ZATAKA KULIKA BUNGENI

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema, ameteleza ulimi tena na mara hii amejikuta akimuita Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila (NCCR-Mageuzi) tumbili.
Kabla ya kutoa kauli hiyo, Werema alikuwa akitoa ufafanuzi wa mwongozo ulioombwa na Kafulila, kuhusu fedha zilizokuwa katika akaunti ya Escrow iliyokuwa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), ambazo zimelipwa kwa kampuni ya PAP, inayomiliki mitambo ya kampuni ya umeme ya Independent Power Tanzania Limited(IPTL).
Werema alisema fedha hizo si za Serikali, kama inavyodaiwa na Kafulila, kwa kuwa fedha za Serikali, hazikai katika akaunti hiyo.
Alifafanua kuwa taarifa zinazotolewa, zinapotosha umma kuwa serikali imetoa fedha kuilipa IPTL, wakati ukweli ni kuwa fedha hizo ziliwekwa katika akaunti hiyo, kutokana na misuguano baina ya wanahisa wawili, waliokuwa wamiliki wa IPTL.
Werema alibainisha kuwa mmoja wa wanahisa hao, alikuwa akitaka IPTL ifilisiwe, huku mwingine akipinga jambo hilo mpaka walipouza hisa zao na kumaliza mgogoro huo, ambapo Mahakama iliruhusu mali za kampuni hizo, apewe mwanahisa mpya, PAP.
Werema alisema kuna watu walileta bungeni vipeperushi, wakidai ni ushahidi kuhusu utoaji wa fedha hizo za akaunti ya Escrow na kuhusisha na rushwa.
"Kafulila ni miongoni mwa wanaoeneza taarifa potofu…kama ni tuhuma au kuna rushwa, itakuja kujulikana, tusubiri uchunguzi wa vyombo husika,”alisema.
Wakati akizungumza, Werema alitumia mfano wa kabila la Wanyankole, aliosema kuwa wana usemi unaosema kwamba 'Tumbili hawezi kuamua kesi ya msituni'.
Kabla ya kufafanua maana ya msemo huo, Kafulila bila kuwasha kipaza sauti, alikuwa akipiga kelele kumuita Werema kuwa ni mtuhumiwa, hivyo atangaze maslahi yake.
“Naomba nisikilize, hata kama ni mtuhumiwa, nina fursa ya kusikilizwa …nisikilize wewetumbili,”alijikuta akisema Werema.
Baada ya kusema hivyo, Kafulila hakukubali ;na yeye bila kuwasha kipaza sauti, alisema:“Wewe (Werema) ni mwizi tu.”
Kutokana na hali hiyo, Mwenyekiti wa Bunge, Mussa Azan 'Zungu' alimuomba Jaji Werema, kukaa chini ili atoe ufafanuzi, huku Mbunge wa Ubungo, John Mnyika (Chadema) na Kafulila wakitaka kuzungumza.
Zungu alisema kwa kuwa Bunge, lilishaamua kuwa suala hilo, lipelekwe Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru) na kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), ni vyema kama Kafulila ana ushahidi wowote, apeleke huko.
Baada ya kutoa mwongozo huo, ambao ulisitisha malumbano, Mwenyekiti Zungu alisitisha shughuli za Bunge mpaka jioni na kuondoka, huku akisindikizwa na makatibu wa Bunge na wapambe kama kawaida.
Hatua ya Mwenyekiti wa Bunge kuondoka katika ukumbi, baada ya kusitisha shughuli za Bunge, ilimpa fursa Jaji Werema kuweka sawa makabrasha yake na kutoka katika kiti chake, ambapo alionekana kama vile anakwenda kumkabili Kafulila.
Wakati hilo likitokea, Mbunge wa Maswa Mashariki, Sylvester
Kasulumbayi (Chadema), alihama katika kiti chake na kukimbilia alipokuwa amekaa Kafulila.
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, baadhi ya mawaziri walimzunguka Jaji Werema, kabla hajamfikia Kafulila na Kasulumbayi.
Mawaziri hao ni Waziri wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Mahusiano na Uratibu, Stephen Wassira, Waziri wa Sheria na Katiba, Dk Asha Rose Migiro na Naibu Waziri wa Afrika Mashariki, Dk Abdullah Juma Abdullah Saadalla.
Nje ya Bunge, Kafulila na Mnyika waliitisha mkutano na waandishi wa habari, ambapo walidai kuwa na ushahidi wa kutuhumu baadhi ya mawaziri, kusema uongo bungeni kuhusu fedha hizo za Escrow.

MTOTO ACHANWA MAKALIO KWA VIBOKO

Bukoba.Matukio ya ukatili yameendelea kuibuka nchini baada ya kugundulika kwa mtoto mwenye umri wa miaka sita katika Kijiji cha Bwizanduru Kata ya Maruku Wilaya ya Bukoba Vijijini akiwa amefungiwa ndani kwa miezi saba huku makalio yake yakiwa yamechanika kutokana na adhabu ya viboko.
Mtoto huyo aitwaye Erick Emmanuel anatembea kwa shida huku akiwa na makovu mengi mwilini na sehemu ya makalio yake kuharibika vibaya. Amekuwa akipewa adhabu hiyo na baba yake mzazi.
Kwa mujibu wa majirani wa mtoto huyo ambaye anaishi na mama yake wa kambo aitwaye Fidea Emmanuel, anayedaiwa kumtesa mtoto huyo ni baba yake mzazi aliyejulikana kwa jina la Emmanuel Justinian.
Chanzo cha mateso hayo inadaiwa kuwa mtoto huyo hujisaidia ndani na hivyo baba yake mzazi kuamua kumfungia kwa kipindi chote cha miezi saba bila kutoka nje huku kila siku mtoto huyo akipata adhabu kali ya viboko.
Mama wa kambo wa mtoto huyo Fidea Emmanuel aliiambia Mwananchi kuwa mume wake alikuwa akimpa adhabu mtoto huyo mara kwa mara hasa alipojisaidia au kukojoa ndani kwa kutumia fimbo ya mti wa m’buni.
Hata hivyo mama huyo wa kambo na Erick alisema kutokana na hali mbaya ya mtoto huyo iliyotokana na adhabu ya viboko,amekuwa akimtibu kwa kutumia dawa za mitishamba bila ya kufanyiwa vipimo au kupelekwa hospitalini.
Pia, mtoto huyo anaonekana kuwa na michirizi mikubwa katika sehemu ya kifua na tumbo pamoja na makovu makubwa mwilini mwake, alama ambazo zinahusishwa na viboko alivyokuwa akicharazwa na baba yake mzazi.
Naye, Mwenyekiti wa Kitongoji cha Maiga Audax Bayon, alisema kuwa ilikuwa ni vigumu kumuona mtoto huyo kwa kuwa kila aliyemuulizia aliambiwa yuko ndani akijifunza kusoma na watoto wengine jambo ambalo halikuwa kweli.
Mama mzazi wa mtoto huyo Aneth Brand ambaye anaishi Kijiji cha Bugabo wilayani humo alisema miezi saba iliyopita alimpeleka mtoto huyo kwa baba yake na kudai hakuwa na matatizo makubwa yanayomkabili mtoto wake, lakini sasa ana matatizo ikiwamo upungufu wa damu.
Akizungumzia tukio hilo Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Bwizanduru, Edward Mwemezi alisema pamoja na mtoto huyo kufanyiwa ukatili mkubwa kwa muda mrefu alisema familia ilijitahidi kuficha taarifa hizo hata kwa majirani.
Alisema baada ya kuendelea kuenea kwa uvumi wa kuwepo kwa mtoto aliyefungiwa kwa muda mrefu na kupewa mateso katika familia hiyo waliamua kufuatilia na tayari mtuhumiwa amewekwa chini ya ulinzi kwa ajili ya hatua zaidi za kisheria.

SUAREZ KESI YA KUN'GATA TENA

Suarez amesema kuna baadhi ya mambo ambayo hutokea uwanjani na hayapaswi kuzua kashfa
Shirikisho la soka duniani limeanzisha uchunguzi dhidi ya mchezaji wa Uruguay Luis Suarez, baada ya kuonekana akimng’ata mchezaji wa Italia, Giorgio Chiellini wakati wa mechi yao ya kombe la dunia.
Suarez ambaye pia huchezea Liverpool katika ligi ya Uingereza pamoja na shirikisho la soka la Uruguay wana hadi leo kujibu FIFA.
Suarez, aligongana na Chiellini wakati wa mechi yao Jumanne usiku katika awamu ya mtimuano, ambapo Uruguay ilishinda bao moja bila dhidi ya Italia.
Suarez alisema kuwa wawili hao waligongana kwa bahati mbaya
Refari wa mechi hiyo hakuchukua hatua yoyote dhidi ya Suarez.
Ikiwa atapatikana na hatia, Suarez huenda akazuiwa kucheza mechi 24 au kwa miaka miwili.
Suarez mwenyewe tayari amejitetea katika vyombo vya habari nchini Uruguay
"Kuna mambo ambayo hutokea uwanjani,’’ alisema Suarez. “Tuligongana , yeye aligonga kwa bega lake katika sehemu ya mdomo.’’
Chiellini alishusha jezi lake kuonyesha sehemu aliyong’atwa katika bega lake.
"Kuna mambo fulani ambayo hutokea uwanjani na sidhani ni vyema kuanza kuzua kashfa kutokana na mambo kama hayo. Yanapaswa tu kuishia uwanjani,’’ alinukuliwa akisema Suarez.
Chiellini, mwenye umri wa miaka 29, alisema angependa kuona ikiwa FIFA wana ujasiri wa kutumia ushahidi wa video kumuadhibu Suarez, kwa sababu refari aliona lakini hakuchukua hatua.
Tukio hilo lilifanyika kuelekea mwishoni mwa mechi , muda ,mfupi kabla ya Uruguay kuingiza bao la ushindi kwenye mechi hiyo dhidi ya Italia.

BIBI AUAWA KWA KUKATWA SHOKA

Bibi mmoja Mkazi wa mtaa wa Nyahanga, wilayani Kahama Mkoani Shinyanga, Rebeka Sengasenga (82), ameuawa kwa kukatwa na Shoka kichwani kwa kile kinachohisiwa kuwa ni imani za Kishirikina.
Kwa mujibu wa majirani, tukio hilo limetokea jana asubuhi katika Mtaa wa Nyahanga, wilayani humo, ambapo Marehemu Rebeka alienda nyumbani kwa mtoto wake Bundala Sengasenga alikokuwa ameitwa na mke wa Bundala kusaidia kuanika Dengu.
Imeelezwa kuwa Merehemu Rebeka ambaye alikuwa akiishi kwa mwanae mkubwa Stanley Sengasenga katika mtaa huo alifika kwa Bundala baada ya kuitwa na Magreth Richard ambaye ni mke wa Bundala kwa ajili ya shughuli hiyo.
Katika maelezo yake Magreth amesema Mama mkwe wake Marehemu Rebeka alifikia sebuleni, na kwamba wakati yeye yuko nje, alimwona mtu ambaye hakuweza kumfahamu akitoka sebuleni hapo na kukimbia ndipo alipoangalia na kumkuta Rebeka ameuawa.
Taarifa za awali zimedai, kabla ya tukio hilo Magreth ambaye kwa sasa anashikiliwa na jeshi la polisi mjini Kahama kwa mahojiano alienda nyumba ya jirani kuazima Shoka, ambalo baadaye limekutwa kwenye shimo la maji taka nyumbani hapo.
Anayeshikiliwa akilia kwa uchungu ni Magreth anayehisiwa kuhusika na tukio hilo.
Shoka hilo limepatikana baada ya mbinu za kiupelelezi za Jeshi la Polisi kuagiza gari la maji taka kuyavuta maji hayo baada ya majirani kudai hawajaona mtu aliyekimbia na shoka muda huo katika mwelekeo ambao Magreth ameelekeza.
Jeshi la Polisi wilaya ya Kahama limethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba Mwili wa Marehemu umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya Wilaya ya Kahama, huku upelelezi ukiendelea.

Jumanne, 24 Juni 2014

TATIZO LA AJIRA NCHINI MTAJI KWA WANASIASA

SERIKALI imetoa ufafanuzi kuhusu tatizo la ajira nchini, huku wanasiasa waliozungumzia tatizo hilo kuwa ni bomu, wakitakiwa kutoa ushauri wa namna ya kulitegua au kupunguza athari zake kama likilipuka.
Mbali na ushauri huo, Serikali pia imewataka wanasiasa wanaotumia tatizo hilo kisiasa, kuonesha mfano wa kusaidia vijana katika majimbo yao kwanza, badala ya kusubiri siku wakipewa nchi.
Mawaziri wanne walitumia muda wao jana kujibu hoja hiyo, ambayo ni hoja lulu kisiasa, kutokana na hali halisi kuwa sehemu kubwa ya Watanzania ni vijana, hivyo inatazamwa na wanasiasa wengi kuwa ndio watakuwa sehemu kubwa ya wapiga kura.
Kutokana na umuhimu wa ajira katika siasa za leo, Naibu Spika, Job Ndugai hivi karibuni alisema Mtanzania mwenye nia ya kugombea urais mwaka 2015, ili aeleweke kwa wananchi, ni lazima aeleze mikakati ya kuwasaidia vijana kupata ajira.
“Ajira ni tatizo kubwa na lazima lishughulikiwe. Kuna vijana hawaendi shule, lazima watazamwe. Kuna wanaomaliza darasa la saba, kidato cha nne, cha sita na vyuo vikuu.
"Nazungumza kutoka moyoni kabisa. Hizi ni dakika za mwisho za Serikali ya Awamu ya Nne, wale wanaojipanga kwa Awamu ya Tano kama hawataongelea ajira, basi waandike wameumia,”alisema Ndugai.
Alianza Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudentia Kabaka, ambaye alikiri kuwa ajira ni tatizo, lakini akafafanua kuwa si la Tanzania tu, bali pia ni tatizo la kimataifa.
Alisema katika utafiti uliofanyika mwaka 2012, ilionekana ajira ya muda mrefu, inayompa mwajiriwa hifadhi kuwa imeongezeka kwa asilimia 13.5. Ongezeko hilo limetolewa katika sekta ya umma, ambayo imetoa asilimia 35.8 ya ajira huku sekta binafsi ikitoa asilimia 64.2 ya ajira.
Kutokana na mchango mkubwa wa sekta binafsi katika ajira, Kabaka alisema Serikali imekuwa ikiweka mazingira rafiki kwa wawekezaji, ikiwemo ujenzi wa barabara, kuboresha upatikanaji wa nishati ya umeme na mawasiliano.
Alisema wakati wanasiasa wanasema Tanzania kuna tatizo kubwa la ajira, ambalo kitakwimu ni asilimia 11.7, nchini Afrika Kusini ni asilimia 24.9.
“Sasa kabla ya kusema ukipewa nchi utatoa ajira, tuoneshe kwanza katika jimbo lako. Umefanyaje kuongeza ajira katika sekta isiyo rasmi…msidanganye wananchi na kuwachonganisha na Serikali,”alisema.
Kuhusu fursa ya kufanya mafunzo kwa vitendo, Serikali imezungumza na Chama cha Waajiri (ATE) ili watoe fursa hizo kwa wanafunzi wanaotoka katika vyuo mbalimbali.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Asiye na Wizara Maalumu, Profesa Mark Mwandosya, aliamua kuonesha mfano kwa kuanza kutoa ushauri.
Alitoa hatua kumi, alizotaka waajiriwa watarajiwa walio katika soko ambao hawajapata ajira na walio vyuoni na wanaojiandaa kujiunga na vyuo mbalimbali, ili wapate ajira.
Kwanza aliwataka wanafunzi wanaojiunga na vyuo, kama wanataka kuajiriwa, wachukue fani za sayansi, teknolojia na uhandisi.
Pili, aliwataka wanaosomea uhandisi na sayansi, wachanganye fani hiyo na fani ya usimamizi wa biashara.
Tatu, aliwataka wanaochukua fani za sanaa, pia kuchukua fani za usimamizi, kwa maana ya Shahada ya Uzamili ya Usimamizi (MBA).
Profesa Mwandosya pia aliwataka waajiriwa watarajiwa, wasidharau lugha za Kiswahili na Kiingereza ;na wazizungumze kwa ufasaha, lakini akawataka pia kuchukua lugha moja katika ya Kifaransa, Kihispania, Kireno na Kichina.
Hatua nyingine waliyoshauriwa kuchukua ni kutoogopa kushindana katika soka la nje, ikiwemo soko la Afrika Mashariki, Afrika na sehemu nyingine duniani. Kwa mujibu wa Profesa Mwandosya, katika soko hilo la ajira kuna Wakenya, Warwanda na Waganda.
Aliwataka wanafunzi vyuoni kuanza kujijengea kichwani dhana ya kujiajiri, kwa kuwa ni jambo zuri ili wasingoje kupata ajira za Serikali.
Wasomi hao pia walitakiwa waache kuchagua kazi wala ngazi ya kuanzia kazi, kwa kuwa hata aliyesomea uhandisi akianzia kazi ya fundi mchundo, atapanda haraka. Pia, aliwataka wajiamini, wawe wabunifu na kujiunga katika vikundi ili wawezeshwe.
HABARI LEO

BRAZIL NA MEXICO ZATINGA HATUA YA MTOANO




Recife, Brazil. Mabao matatu ya Rafael Márquez, Guardado na Chicharito yametosha kuivusha Mexico katika hatua ya mtoano ya Kombe la Dunia baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-1, wakati Brazil ikikaa kileleni kwa ushindi wa 4-1 dhidi ya Cameroon.

Wawakilishi hao wa Afrika walishatoka baada ya michezo miwili, na walikuwa wakikamilisha ratiba huku Brazil wakitaka nafasi ya kukaa kileleni kwa pointi saba.

Croatia, ambao nao walikuwa na nafasi ya kufuzu kama wangeibuka na ushindi walishindwa kuzuia mabao hayo mawili ya kipindi cha pili na kujitoa wenyewe mashindanoni.

Wenyeji, ambao mabao yao yalifungwa na Neymar (mawili), Fred na Fernandinho, wanaongoza katika Kundi A, ambapo wamefuzu sambamba na Mexico katika hatua ya mtoano ya timu 16.

Kwa matokeo hayo, Brazil sasa itakutana na Chile katika hatua ya mtoano, wakati Mexico ikikutana na Uholanzi katika hatua hiyo.

Wawakilishi wa Afrika, Ivory Coast leo wanashuka dimbani kwa lengo moja tu la kusaka ushindi dhidi ya Ugiriki ili wakijihakikishia nafasi ya kucheza hatua ya 16 ya Kombe la Dunia 2014.

Miamba hiyo ya Afrika imekusanya pointi tatu katika mechi mbili za kundi lake, baada ya kuifunga Japan katika mchezo wa kwanza kabla ta kufungwa na Colombia.

Matokeo ya sare leo yatawatosha kuwavusha, endapo Japan watashindwa kuifunga Colombia katika mchezo wao wa mwisho.

Ugiriki na Ivory Cost zimeshindwa kufuzu kwa hatua ya mtoano katika fainali mbili za dunia zilizopita.

Wakati huohuo; Steven Gerrard atakuwa katika benchi wakati England itakapocheza mechi yake ya mwisho ya Kombe la Dunia dhidi ya Costa Rica - na kutoa nafasi kwa Frank Lampard kuchukua unahodha wa timu hiyo.

Gerrard anatakiwa kuanza kufikiria kuhusu hatma yake baada ya England kutolewa kwenye hatua ya makundi.

Lampard ametangaza kuondoka Chelsea na kiungo huyo mwenye miaka 36, hategemei kuendelea kuichezea England baada ya mechi ya leo.

Jumapili, 22 Juni 2014

OROGI,MKENYA ALIEFUNGA BAO PEKEE LA UBELGIJI DHIDI YA URUSI

Mshambuliaji wa Lille ya Ufaransa , Mkenya Divorc Origi ambaye ni raiya ya Ubelgiji aliyeifungia Ubeljiji bao la pekee na la ushindi dhidi ya Urusi katika mechi yao ya pili ya kundi H amesema kuwa anajivunia kuwa mkenya licha ya kuwa anaiwakilisha Ubeljiji.
Bao hilo la dakika za mejeruhi za mechi hiyo ndiyo iliyoiwezesha Ubeljiji kufuzu kwa mkondo wa pili wa timu kumi na sita bora.
Origi ambaye aliingia kama mchezaji wa akiba baada ya kuondoka kwa Romelu Lukaku alifuma bao hilo la kipekee kunako dakika ya 88 ya kipindi cha pili ya mechi hiyo alipopokea pasi nzuri kutoka kwa Eden Hazard .
Origi Ni bao la kujivunia kwa kenya familia yangu na Ubeljiji
Origi, mwanawe Mike Okoth, mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Kenya, Harambee Stars atakua mchezaji wa kwanza wa Afrika Mashariki kuiwakilisha Ubeljiji, na yuko pamoja na wachezaji nyota kama vile Vincent Kompany wa Manchester City na Eden Hazard wa Chelsea.
Akizungumza na BBC Origi anasema:''aliamua kuichezea Ubeljiji baada ya kutilia maanani mambo mengi kama vile usimamizi mzuri wa kandanda nchini humo, mizizi yake ya kandanda iliyoko huko, marafiki, ushauri wa babake pamoja na Ubelgiji kufuzu kwa kombe la dunia kwani haijulikani ni mwaka upi Kenya itafuzu kwa kombe la dunia.
Origi aliiambia BBC kuwa anafurahia mizizi yake na kuwa anajivunia bao hilo na familia yake iliyokuwa uwanjani kumshabikia .
Origi alisema kuwa hii ilikuwa ni tukuio spesheli kwake kwa Kenya na Ubeljiji.
BBC

URENO HOI KWA MAREKANI,GHANA BADO NAFASI IPO

Bao la kusawazisha la Silvestre Varela
Ureno ambayo ilikuwa imepata pigo kubwa iliposhiindwa katika mechi yake ya ufunguzi na Ujerumani na ilikuja katika mechi hii ikitafuta ushindi wa aina yeyote ilikuepuka fedheha ya kufungashwa virago katika hatua ya makundi katika kombe la dunia linaloendelea huko Brazil.
Kwa upande wao Marekani, ilikuwa inafahamu fika kuwa matokeo baina ya 2-2 naina ya Black Stars ya Ghana na vinara wa kundi G Ujerumani ilikuwa na hatari ya kuinyima fursa ya kushiriki mkondo wa pili wa kombe la dunia kwa hivyo ilikuwa inatafuta ushindi ambao ingeipa tiketi ya moja kwa moja katika hatua ijayo.
Lakini kipenga cha kuanza kwa mechi hii kilpopulizwa, Nani ndiye aliyeiweka Ureno mbele baada ya dakika 5 ya mechi hiyo.
Ureno imejipata taabani baada ya kutoka sare ya 2 -2 na Marekani
Kuanzia hapo nipe nikupe baina ya mahasimu hao wa jadi ikaendelea hadi dakika ya 64 Germaine Jones alipofaidi safu tepetevu ya ulinzi na kuisawazishia Marekani.
Vijana wa Jurgen Klinsmann ndiyo walionekana na tamaa zaidi ya kushiriki mkondo wa pili wa kombe la dunia walipofaidi kona iliyotokana na makosa ya Ricardo Costa
na wakaitumia vyema.
Marekani ilifufua matumaini ya kusonga mbele Clint Dempsey alipovurumisha mkwaju ndani ya neti na kuiweka timu yake mbele , hata hivyo Christiano Ronaldo alimwandalia pasi nzuri na akaisawazishia Ureno katika muda wa ziada wa mechi hiyo.
Ureno imejipata taabani baada ya kutoka sare ya 2 -2 na Marekani
Mwisho wa kuishia Ureno ilijizolea alama yake ya kwanza katika kipute hicho huko Brazil lakini wanahitaji kuilaza Ghana na kuomba kuwa Marekani wakunguwae dhidi ya ujerumani iliwao wafuzu kusonga mbele.
Marekani inahitaji ushindi mkubwa dhidi ya Ujerumani ambayo itakuwa ikitafuta sare ya aina yeyote ilikusonga mbele.
Ghana kwa upande wao sasa wanahitaji kuichapa Ureno na kuomba kuwa Ujerumani nayo itaitandika Marekani iliwafuzu kwa mkondo ujao.
Kufikia sasa ujerumai inaongoza kundi hili ikiwa na jumla ya ponti 4 sawa na Marekani.Ghana ni ya 3 na alama 1 sawa na Ureno .
BBC

Jumamosi, 21 Juni 2014

AMUUA BABA MWENYE NYUMBA KWA KUMDAI KODI

The murder case of a Colorado socialite whose body was found stashed in her resort-home’s closet in February has come to an abrupt halt after a surprise plea deal Friday.
William (Trey) Styler III, 66, who had been renting out Nancy Pfister’s Buttermilk Ski Area home with his wife, pleaded guilty to killing the prominent Aspen native with a hammer, The Aspen Times reported.
The former Denver anesthesiologist’s shocking plea-deal admission before a judge followed the release of his wife, Nancy Styler, and came the same day as the release of Pfister’s friend and personal assistant, Kathy Carpenter.
Both women, who had been charged with first-degree murder in Pfister’s gruesome death, had their charges dismissed.
William Styler instead admitted to having acted alone when he bashed the 57-year-old in the head while she slept on the night of Feb. 24, according to Assistant District Attorney Scott Turner.His victim, whose parents co-founded the Buttermilk ski area, had only recently returned from vacationing in Australia and days before vented frustration on Facebook that her renters’ weren’t paying rent.Defense attorneys argued that claim.
Pfister’s friend and personal assistant Kathy Carpenter, 56, pictured, was also released with first-degree murder charges dismissed against her.
Styler and his wife were collared days later at the Aspenalt Lodge in Basalt on March 3.
Carpenter, who was the one to find Pfister’s body and call 911, was arrested on March 14. Carpenter’s attorney, Greg Greer, said her arrest was based on a word investigators believed they heard her use when she made that call.
While declaring her as innocent all along, they voiced upset at the 56-year-old having been held in jail for 96 days without bail.
Former Denver anesthesiologist William (Trey) Styler III, 66, pleaded guilty to second-degree murder in the death of Aspen native Nancy Pfister in February.
“She’s unemployed. She’s homeless now because she called 911,” Greer vented, according to ABC News.
With his plea deal, William Styler was sentenced Friday to 20 years in a Department of Corrections prison with medical facilities.
Nancy Pfister, 57, was found dead inside her Colorado home just days after returning from a vacation in Australia. Pfister was a prominent local resident whose parents co-founded the Buttermilk ski area.
District Attorney Sherry Caloia suggested the sentence is most likely the equivalency of life for the 66-year-old due to rising health concerns that have since confined him to a wheelchair.
he 66-year-old, seen in court on Friday, was sentenced to 20 years in prison. District Attorney Sherry Caloia estimated that it will likely be a life sentence for him due to his dwindling health.
The victim’s family, who asked the judge for the maximum sentence of 32 years for second-degree murder, called his sentence an injustice.
“It upsets me. There are such things as an eye for an eye,” said Pfister’s daughter, Juliana Pfister, according to the trent

AKAMATWA NA POLISI AKIUZA MTOTO

The Lagos Police command has arrested a middle aged woman for selling a two months old baby for N30,000.
According to Vanguard, the suspect identified as Mrs Victor was arrested following a tip-off at her residence in Sabo Ilaje in Ojo, Lagos.
The suspect is currently detained at State Criminal Investigation Department where a complaint was laid that she was engaged in child trafficking.
She had confessed to the act but refused to name the buyer insisting the person is not well known to her.
A police source says investigation is ongoing to unravel the syndicate.
The trent

MUANDISHI WA HABARI AUAWA

Mwandishi wa habari auwawa Mogadishu
21 Juni, 2014 - Saa 16:55 GMT
Mwandishi wa habari kijana wa Somalia ameuwawa kwenye mripuko wa bomu lilotegwa chini ya gari lake mjini Mogadishu.
Yusuf Keynan alikufa wakati bomu hilo liliporipuka alipotia moto gari, akitaka kuelekea kazini.
Mwandishi wa BBC mjini Mogadishu anasema Yusuf Keynan (aliyefanya kazi katika redio Mustaqbal), alikuwa mwandishi wa habari kijana aliyekuwa akipendwa na hodari katika kazi yake.
Huyo ni mwandishi wa habari wa kwanza kuuwawa nchini Somalia mwaka huu, baada ya waandishi habari kadha kuuwawa kwa mfululizo katika miaka miwili iliyopita.
Shirika la Kuwalinda Waandishi wa Habari linasema kuwa Somalia ni moja kati ya nchi hatari kabisa kwa waandishi.
Hakuna aliyedai kuhusika na mauaji ya kijana huyo.
BBC

AJARI MBAYA MAKONGO DAR ES SALAAM

Kwa mujibu wa Radio One Breaking News, Watu sita wamefariki papo hapo na wengine 12 kujeruhiwa kufuatia ajali mbaya iliyohusisha magari manne iliyotokea eneo la Makongo karibu na hospitali ya Lugalo Dar es salaam.
Baadhi ya mashahuda wa ajali hii wamesema kuwa imesababishwa na uzembe uliofanywa na dereva wa daladala iliyokuwa ikitoka Tegeta kwa kupita upande usio wake.

ATOKA MKOJO NA MBEGU ZA KIUME SEHEMU YA PAJA

Rombo.Paja la mguu wa kushoto wa Hubert Mkenda (49) mkazi wa Kijiji cha Msaranga, Kata ya Kitale, Rombo mkoani Kilimanjaro, limetoboka na kutengeneza sehemu ambayo inapitisha haja ndogo (mkojo) na mbegu za kiume.
Mkenda ambaye ni baba wa watoto saba amekuwa katika hali ya ugonjwa kwa miaka 11 sasa na jitihada za madaktari wa Hospitali za KCMC Moshi na Huruma iliyopo Rombo mkoani humo, hazijamwezesha kuondokana na maumivu makali ambayo yanatokana na tundu hilo.
Tiba ya mwisho aliyoipata ni pale madaktari wa KCMC walipomwekea mpira kwenye nyonga kwa ajili ya kuwezesha kutoa mkojo, lakini wakati mwingine umekuwa ukitoka kupitia kwenye paja na kumsababishia maumivu makali.
“Ninapata maumivu makali mkojo unapopita kwenye paja na ninapokuwa na hisia za mapenzi, mbegu za kiume hupita kwenye shimo lililotoboka kwenye paja,” anasema Mkenda na kuongeza:
“Ni vigumu kueleza maumivu tabu na shida zinazoniandama, maisha yangu yamebadilika ni kama Mungu amechoka kusikia kilio changu lakini bado naamini ananipenda,” ni maneno ya uchungu anayoyasema Mkenda huku akionekana kukata tamaa na kuongea:
Anaendelea: “2003 ni mwaka ninaotamani usingekuwepo kabisa duniani kwakuwa ni mwaka uliobadilisha maisha yangu na kunifanya kuwa mteja wakuhudhuria hospitali kila siku bila matumaini”.
Mkenda alipata ajali ya gari 2003 katika msitu wa Rongai na kujeruhiwa vibaya katika maeneo ya haja kubwa na haja ndogo, ajali ambayo imesababisha kulazwa hospitalini kwa miaka 5 mfululizo na kufanyiwa upasuaji kwa nyakati tofauti mara nane.
Ajali ilivyotokea
Mkenda anasema hakumbuki siku, lakini ulikuwa mwezi Julai 2003, alipoondoka nyumbani kwenda Rongai kufanya kibarua cha kuvuna mahindi kwenye shamba la mtu na alipomaliza kuvuna akiwa na wenzake walipakia mahindi kwenye gari na kuanza safari ya kurejea Mashati, Rombo.
Anasema njiani dereva wa lori walimokuwa wamepakia mahindi, alisimama na kupakia magogo ya miti, kisha kuendelea na safari, lakini wakiwa njiani moja ya gogo lililokuwa limetoka nje ya gari liligonga kwenye mti na kumrusha juu.
“Nilirushwa juu na kutoka huko nilianguka chini kwa kishindo na kukalia gogo kisha kurushwa nje ya gari na kuangukia mti, niliumia vibaya sehemu za haja kubwa na ndogo,” anasimulia Mkenda.
Mkenda anasema alikimbizwa katika Kituo cha Afya Tarakea alikopewa huduma ya kwanza, lakini kutokana na kuvuja damu nyingi sehemu ya haja kubwa, walishauri akimbizwe katika Hospitali ya Huruma.
MWANANCHI

GWAJIMA VS MBASHA INAENDELEA..

Wakati mume wa mwimba Injili Bongo, Flora Mbasha, Emmanuel Mbasha akiachiwa huru kwa dhamana kufuatia kesi ya kudaiwa kumbaka shemejiye, Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima la jijini Dar es Salaam, Josephat Gwajima ameibuka na kunena mazito kuhusiana na sakata hilo.
Mbasha aliachiwa kwa dhamana juzi akitokea Gereza la Keko, Dar baada ya kupandishwa kizimbani kwa mara ya kwanza katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala, Juni 17, mwaka huu na kusomewa mashitaka mawili ya ubakaji ambayo hata hivyo, aliyakana.
ILIVYOKUWA KORTINI
Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Ilala, mheshimiwa Wilbeforce Luago siku hiyo ya Juni 17, alitoa hoja kwamba upande wa jamhuri hauna pingamizi hivyo dhamana ipo wazi.
Alisema mshitakiwa alitakiwa kuwa na wadhamini wawili, mfanyakazi wa serikali na wa kutoka katika taasisi inayotambulika sanjari na shilingi milioni 5 kila mmoja. Mshitakiwa alishindwa kutimiza masharti hayo siku hiyo hadi hadi juzi alipotimiza, akaachiwa.
Mwendesha mashitaka wa mahakama hiyo ambaye ni wakili wa serikali, Nassoro Katuga bila kuchelewa aliitaja kesi hiyo yenye namba CC/186/2004 ambapo rafiki wa Mbasha aliyejitambulisha kwa jina la George Mushi na baba wa mtuhumiwa aitwaye Mwahimu Juma ndiyo waliofanikisha dhamana hiyo. Kesi yake itatajwa tena Julai 17, 2014.
GWAJIMA SASA
Akizungumza na mwanahabari wetu juzi wakati Mbasha akiwa nje kwa dhamana, Mchungaji Gwajima alieleza namna ambavyo sakata hilo limeitikisa Injili nchini Tanzania kutokana na kuibuka kwa madai mengi likiwemo suala la Flora kusemekana amehamia nyumbani kwake kitu ambacho alikipinga.
Gwajima alisema anasikitika sana kuona ndoa ya Flora na Emmanuel Mbasha inatikisika akizingatia Flora ni muumini wake hivyo moja kwa moja ugomvi wao unaonekana kutia dosari mwenendo mzima wa uinjilishaji katika jamii.
“Naumizwa sana na sakata hili lakini hivi karibuni niliamua kuwaita ndugu wa pande zote mbili (Flora na Mbasha) nikazungumza nao kwa kirefu na tukamaliza tofauti zote lakini tatizo likabaki lile la kisheria zaidi (mashitaka ya ubakaji kwa Emmanuel),”alisema Gwajima ambaye makao makuu ya kanisa lake yapo Kawe jijini Dar.
AANDAA TAMKO ZITO
Mchungaji Gwajima alisema kutokana na sakata hilo kugusa Injili, ameandaa tamko zito ambalo atalitoa rasmi atakaporudi safari yake ambayo hakueleza anakokwenda.
“Hatuwezi kukaa kimya juu ya hili, nasafiri lakini nikirudi tu nitatoa tamko rasmi kwa kuwaalika waandishi wa habari,”alisema.
IBADANI JUMAPILI
Katika hatua nyingine, ndani ya ibada ya kanisa hilo iliyofanyika Jumapili iliyopita, Mchungaji Gwajima alitumia dakika kama 15 katika mahubiri yake kutupa kile kilichodaiwa kuwa ni jiwe gizani ambapo wengi waliamini ni kuhusiana na sakata hilo.
“Mimi siyo kama wale, sijibu hoja kama zile, mfano ukiwa unaoga halafu chizi akachukua nguo zako na ukamkimbiza nani ataonekana chizi? Tatizo la Watanzania ni kuwa wakisikia kitu kipya kinaanza kwao badala ya kukithamini wanakididimiza ili kisiendelee, lakini mimi siyo kama wao,”alisema.
Aliongeza:“Mimi kila mwaka naenda Japan na ninawa-lecture Wajapani ambao pia huja hapa kanisani zaidi ya 40 kila mwaka na mwaka huu watakuja Septemba, lakini Watanzania hawashtuki na kuja kujifunza juu ya ufufuo wa wafu wengi wao wanakalia kuandika stori kwenye magazeti lakini mimi siyo kama wale.”
AMEFUNGUKIA SAKATA LA MBASHA?
Ingawa Mchungaji Gwajima hakueleza moja kwa moja kuhusu tukio la Mbasha lakini maneno hayo yalitafsiriwa kwamba ni ya kujibu hoja zinazomhusisha yeye na tukio hilo.
Anaendelea:”Mimi nimehubiri nchi zaidi ya 53 duniani na nyingi za Ulaya na Marekani halafu mtu amekaa Magomeni miaka yote anatengeneza stori ya gazeti, unatarajia niijibu, mimi siyo kama wale nimetumwa na nina kazi natakiwa kuifanya duniani na siwezi kufa mpaka niimalize.”
“Inawezekana mlishawaangamiza wengi kabla ya mimi, kwa kuwatungia stori hizo za uongo lakini mimi siyo kama wale na mwezi huu wa nane ninaendelea na mkutano Iringa, waache waandike lakini mimi ni chombo kingine na siyo kama wale.”
DONGO GIZANI?
Baadhi ya waumini waliokuwa katika ibada hiyo, walibaki njia panda na katika giza nene ingawa wengi waliamini alitupa vijembe katika sakata la Mbasha haswa alipokuwa akisema, ‘mimi siyo kama wale’.

Ijumaa, 20 Juni 2014

APEWA MWANAMKE KAMA ZAWADI

Uchunguzi umeanzishwa nchini Afrika Kusini kuhusu madai kuwa mkuu wa shirika la habari la SABC alikabidhiwa msichana mwenye umri wa miaka 23 kama zawadi.
Tume inayohusika na maswala ya usawa wa kijinsia, imesema kuwa imepokea malalamiko kwamba viongozi wa kitamaduni walimkabidhi Mkuu shirika la habari la serikali SABC, Hlaudi Motsoeneng mke kama zawadi.
Viongozi hao walikuwa sehemu ya kikundi cha wazee wa kitamaduni waliokuwa wanataka vipindi zaidi vya lugha yao kupeperushwa kwenye televisheni hiyo.
Serikali imesema kuwa tabia hiyo ni ya kuchukiza sana na kwamba inajuta jambo kama hilo lilitokea.
'Wazazi walikubali'
Tukio hilo linasemekana kutokea wakati wa ziara ya hivi karibuni ya Hlaudi Motsoeneng katika mkoa wa Limpopo Kaskazini mwa nchi hiyo ambako yeye na maafisa wengine wakuu walikutana na wazee hao.
Taarifa ya serikali ilisema, ''Tabia ya kutumia wanawake kama zawadi na kufafanishwa na mifugo wanaotolewa kama zawadi wakati msichana anapooleka ni utamaduni usio kubalika na ni kinyume na haki za binadamu na pia ni kama matusi kwa demokrasia na uhuru wa watu. ''
Takriban wasichana 10 waliorodheshwa mbele ya maafisa hao huku wakitakiwa kuchagua.
'Alichagua aliyempendeza'
Serikali ya Afrika Kusini imesema jambo hilo limehujumu utamaduni
Bwana Hlaudi Motsoeneng alichagua mwanamke mmoja ambaye alimfurahisha.
"wasichana wote waliambatana na wazazi wao. Wazazi walifahamu kilichokuwa kinaendelea na inaarifiwa kuwa wote walikubali.
Kwa mujibu wa jarida Sowetan, bwana Motsoeneng alichagua msichana aliyekuwa na umri wa miaka 23 ambaye pia ni mwanafunzi.
Alipigwa picha akiwa kifua uchi akisimama kando yake.
Pia inaarifiwa alikabidhiwa Ng'ombe na Ndama.
Wizara ya maswala ya wanawake nchini humo, ilisema tabia hiyo ni hujuma kwa utamaduni
"tabia ya kutumia wanawake kama zawadi ungedhani ni n'gombe, bila shaka ni hujuma kwa utamaduni, '' ilisema taarifa ya wizara hiyo.
Msemaji wa kituo cha SABC, Kaizer Kganyago, aliambia BBC kuwa hajapokea habari yoyote kuhusu uchunguzi unaofanywa na tume hiyo na kwamba ikiwa ina swali lolote kuhusiana na tukio hilo, inapaswa kuhoji viongozi hao wa kitamaduni.
Lakini msemaji wa tume hiyo, Javu Baloy naye aliambia BBC kuwa ujumbe tayari umewasilishwa kwa wote waliohusika na mapendekezo ya dhabu yatatolewa mwezi ujao.
BBC

JAMAA AFUMWA AKIFANYA NGONO NA MKE WA RAFIKI MPANGAJI MWENZAKE

Mume aliyejulikana kwa jina moja la Ngosha, mkazi wa Mabibo jijini Dar, amemfumania rafiki yake aitwaye Jazira akiwa chumbani na mkewe Jack wakiivunja amri ya sita ya Mwenyezi Mungu.
Tukio hilo lilitokea Jumanne iliyopita saa 12 alfajiri ambapo ilidaiwa kuwa Jack alikuwa chumbani na mwanaume huyo ambaye ni mpangaji, wenzake wakipeana maraha.
Imedaiwa kuwa, wawili hao walikuwa wakimtegea Ngosha akitoka kwenda katika shughuli zake, Jazira alikuwa akizama katika chumba cha rafiki yake na kufanya mchezo wa kikubwa.
Wapangaji wenziye na Jack wamedai kuwa, mke huyo wa mtu ambaye ana miezi miwili tangu aolewe kutoka mkoani Tabora, amekuwa kero katika nyumba hiyo kwani amekuwa akipiga kelele za kimahaba nyakati za asubuhi ambapo watu wengi wanakuwa wakielekea kazini.
“Hata sisi wanawake tunaoishi nyumba hiyo tuna waume zetu tunawalilia lakini kinachotusikitisha mwenzetu anamlilia Jazira badala ya mumewe ambaye anakuwa amekwenda kazini,”alisema mmoja wa wapangaji wa nyumba hiyo.
Imeelezwa kuwa, siku hiyo mlinzi wa msikiti alikwenda kumwamsha Ngosha kwenda kusogeza gari lake ili watu wapite na alipofika katika chumba chake, alikuta mlango wa sebuleni ukiwa wazi lakini hakukuwa na mtu, ila chumbani kwake kulisikika redio ikizungumza kwa sauti kubwa.
Jirani mmoja aliyedai kuchoshwa na tabia hiyo, alimshauri mlinzi huyo kwenda kusikiliza kwenye dirisha la chumba hicho na waliposikia sauti za kimahaba wakakubaliana wamtonye mjumbe wa Serikali ya Mtaa wa Kanuni, Mabibo aliyetajwa kwa jina la Asha ambaye alifika na kusikia ‘mchezo’ ukiendelea chumbani.
Wakati huohuo, Ngosha akapigiwa simu kuja kushuhudia mchezo huo mchafu wa mkewe alioufanyia ndani ya chumba chake.
Mashuhuda wa tukio hilo walisema, alipofika Ngosha nyumbani na kutonywa kilichotokea alipandwa na hasira na kuangusha varangati kwa rafiki yake lakini baadaye akatulizwa, akamtaka Jazira amlipe shilingi milioni 1.2 ili amuachie mke moja kwa moja.
Jazira alisema hakuwa na kiasi hicho isipokuwa anaweza kulipa shilingi laki mbili tu, jambo lililomfanya Ngosha kuomba msaada wa askari mgambo na kumpeleka mgoni wake Kituo cha Polisi cha Urafiki kwa ajili ya hatua zaidi za kisheria.

VITAMBULISHO VYA MPIGA KURA KUTOLEWA UPYA

VITAMBULISHO vya kupiga kura nchini, vitatolewa upya kwa wananchi wote, ikiwa ni sehemu ya mchakato wa kuboresha daftari la kudumu la wapigakura. Mchakato huo wa kutoa vitambulisho upya, utakaotekelezwa Septemba mwaka huu, utagharimu Sh bilioni 293 .
Tofauti na vitambulisho vya awali vya karatasi vilivyotolewa kwa mara ya kwanza mwaka 2004, vipya vitakuwa vya plastiki. Vimebadilishwa kutokana na matumizi ya teknolojia mpya katika uandikishaji.
Teknolojia itakayotumika ni ya Biometric Voter Registration (BVR), ambayo inachukua au kupima taarifa za mtu za kibaiolojia au tabia ya mwanadamu na kuzihifadhi katika Kanzidata (database) kwa ajili ya utambuzi.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji mstaafu Damian Lubuva, alisema hayo jana wakati akifungua mkutano kati ya tume na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari, kuhusu uboreshwaji wa daftari la wapiga kura.
Alisema katika uboreshaji huo, wapigakura wa zamani, kwa maana waliokuwa kwenye daftari la sasa, watatakiwa kwenda katika vituo vya kujiandikisha kuchukuliwa taarifa zao hasa alama za vidole, picha na saini zao katika mfumo mpya wa BVR na hatimaye kupewa vitambulisho vipya.
Alisema vitambulisho hivyo vipya, vitatolewa papo hapo uandikishaji ukikamilika na vitakuwa vya plastiki ngumu na namba ya mpigakura itakayoonekana kwenye kitambulisho hicho, itakuwa ni ya kudumu na pekee kwa mpiga kura husika.
“Vitambulisho hivi vitatumika kupiga kura katika uchaguzi mkuu ujao pamoja na kura ya maoni ya Katiba mpya na kuhitimisha matumizi ya vitambulisho vya wapiga kura vya awali,” alisema Lubuva.
Akiwasilisha mada katika mkutano huo kuhusu maandalizi hayo kwa kutumia mfumo wa BVR, Mkurugenzi wa Uchaguzi, Julius Malaba alisema wapigakura watakaokuwa na kadi za zamani, watatakiwa kwenda na kadi hizo katika kituo cha kujiandikisha kurahisisha kuhamisha taarifa zao za awali katika mfumo mpya.
“Hata hivyo, kupotea ama kuharibika kwa kadi ya awali, hakumzuii mpiga kura kwenda kituoni kujiandikisha na kupewa kadi mpya,” alisema.
Wenye umri miaka 17 Alisema kundi lingine litakalohusika katika uboreshwaji huo ni watu ambao ifikapo siku ya uchaguzi mkuu mwakani, watakuwa wametimiza umri wa miaka 18.
Pia, wale ambao hawakuwahi kujiandikisha katika madaftari yaliyopita kwa sababu mbalimbali, watahusika katika uboreshaji wa daftari.
Alisema baada ya kukamilika kwa uboreshwaji huo, daftari la awali litawekwa wazi katika maeneo husika na tarehe za ukaguzi, zitatangazwa ili kila aliyejiandikisha kwenda kukagua na kuona kama taarifa zake, zimeandikwa na kuchukuliwa kwa usahihi.
“Kipindi hicho pia kinatoa nafasi kwa wapigakura waliojiandikisha katika kata kuweka pingamizi kwa wale watakaoonekana wameandikishwa katika daftari lakini hawana sifa kama wasiokuwa raia au wasiotimiza umri unaotakiwa kisheria,” alisema.
Alisema matumizi ya mfumo wa BVR, yataweza kutoa majibu kwenye changamoto zilizojitokeza katika mifumo mingine iliyotangulia na kuwezesha kuondoa wapigakura, waliojiandikisha zaidi ya mara moja, kutambua wapigakura siku ya uchaguzi na kuhamisha wapigakura waliohama.
BVR ni uandikishaji tu Hata hivyo, Lubuva alisema mfumo huo wa BVR utatumika kwa ajili ya kuandikisha wapigakura pekee na si kwa ajili ya kupiga kura kielektroniki au vinginevyo.
Alisema matumizi ya mfumo huo, yametokana na changamoto zilizojitokeza katika matumizi ya Optical Mark Recognition (OMR) na kufanya daftari la kudumu la wapigakura kuwa na kasoro na kusababisha wadau wa uchaguzi kuhoji uhalali wake.
Akijibu maswali ya waandishi wa habari, Lubuva alisema vifaa kwa ajili ya kazi hiyo vimekwishaagizwa. Tume itavipokea Agosti mwaka huu ili kuanza uboreshaji huo huku vifaa vichache kwa ajili ya mafunzo kwa watendaji vitapokewa mwezi Julai na kuanza mfunzo hayo.
Uandikisha kwenye vitongoji Alisema kwa sasa uandikishaji utafanyika katika ngazi ya vitongoji, vijiji na mitaa, tofauti na awali ambapo vilikuwa katika ngazi ya mtaa. Sasa vituo vya kujiandikishia, vimeongezeka kutoka 24,919 hadi 40,015 ili kuwa karibu na wananchi na kuongeza mwamko wa kujiandikisha na kupiga kura. Mchakato wa uandikishaji ukianza, huduma zitakuwepo kwa siku 14 kituoni.
Maandalizi Alisema maandalizi ya awali yamekamilika, kinachofuata ni mafunzo na kuanza uboreshwaji wa daftari utakaogharimu Sh bilioni 293 wanazopata kutoka serikalini na tayari sehemu ya fedha, wameshapokea na kutumika kukagua vituo .
Naibu Katibu wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura na Tehama, Dk Sist Cariah, akizungumzia suala la vitambulisho vya taifa na hivi vya wapigakura, alisema vitambulisho hivyo ni tofauti kwani wao wanatoa kwa ajili ya kukamilika kwa muda maalumu lakini vile vya taifa ni endelevu.
Alisema kwa sasa, vitambulisho vya taifa hawajakamilisha kutoa hata Dar es Salaam pekee hivyo ni vigumu kutumika kwa uchaguzi ujao na kura ya maoni kwa Katiba mpya lakini wakikamilisha vitambulisho vya taifa , vitatumika katika uchaguzi.
Alisema katika mfumo huo mpya, watawasiliana na Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) kuweza kuwaondoa wote waliofariki kwa kutumia takwimu za hospitalini na vyeti vya vifo vitakavyotolewa.

Alhamisi, 19 Juni 2014

FACEBOOK WAOMBA RADHI KWA HITILAFU ZA LEO ASUBUHI

fb
Wamiliki wa mtandao wa kijamii wa Facebook ambao una watumiaji wengi zaidi duniani wamelazimika kutoa maelezo juu ya kuondoka hewani kwa mtandao huo kwa muda wa dakika 30 dunia nzima.
fb2
Msemaji wa Facebook amenukuliwa akisema kuwa “Mapema leo asubuhi tulipata tatizo kubwa la watu kushindwa kuingia na kuandika chochote au kupost picha katika mtandao wetu kwa muda wa dakika 30″
Anaendelea kwa kusema kuwa wametatua tatizo hilo haraka na kufanikiwa kurejesha mtandao huo hewani kwa asilimia 100 ambapo pia ameomba radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza.
fb3
Wakati mtandao huo ukiwa chini na watu kushindwa kupost wengi walihamishia hasira zao kwa kuandika kupitia Twitter.
Asilimia 78 ya watu wanaotumia mtandao wa Facebook dunia nzima walishindwa kabisa kutumia mtandao huo kwa dakika 30 wakati asilimia 21 ya watu waliweza kuingia.

WABUNGE WA KAMATI YA BAJETI INAYOONGOZWA NA CHENGE WANALIPWA MILION 15{15000000/- KWA MWEZI

Dodoma.Mbunge wa Muhambwe (NCCR –Mageuzi), Felix Mkosamali amesema Kamati ya Bajeti ya Bunge haina kazi ya kufanya badala yake imegeuka pango la ufisadi na kupendekeza ifutwe mara moja kwa kuwa inawachanganya wabunge huku ikitafuna fedha za walipa kodi bila huruma.
Mkosamali alitoa tuhuma hizo juzi alipokuwa akichangia hotuba ya Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2014/15. Alisema kila inapokutana, wajumbe wake wanalipwa posho ya Sh500,000 kiwango ambacho ni kikubwa zaidi ukilinganisha na wanacholipwa wajumbe wa kamati nyingine za Bunge.
Kamati hiyo inaongozwa na Mbunge wa Bariadi Magharibi (CCM), Andrew Chenge ambayo pia Mbunge wa kuteuliwa, James Mbatia ambaye ni Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi na Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani (Wizara ya Fedha), ni mjumbe wake.
Wakati Mkosamali akitoa tuhuma hizo na kulitaka Bunge lifanye tathimini kama bado kuna haja ya kuwa na kamati hiyo, aliwatupia lawama wajumbe wake kwamba wanatengeneza mtandao wa rushwa kutoka kwa mashirika ambayo yanadaiwa kodi.
“Hakuna jipya katika kamati hiyo, sisi tumekaa humu ndani wao wako nje, wakija wanaanza kutuvuruga na hapa ninapozungumza wao wamejifungia huko na Tanapa eti wamewaita wajadiliane nao kuhusu ulipaji wa kodi, ni usanii mtupu kwani wanajadili nini wakati wameshawasilisha bajeti yao,” alisema.
Aliituhumu Serikali na wabunge wa CCM kuwa ni chanzo cha kuwafanya Watanzania waendelee kuishi katika umaskini uliotopea na kumpiga kijembe Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisema amekuwa mtu wa kutoa kauli ambazo mwishowe anashindwa kuzisimamia.
“Mfano Waziri Mkuu alitoa kauli hapa kuwa atapunguza ununuzi wa magari ya VX, hakuna kilichofanyika na hakuna kitakachofanyika imebaki kuwatuliza watu, kwa nini isiletwe sheria hapa?” alihoji.
Alisema kauli ya kupunguza matumizi ya Serikali haijafanikiwa kwani imesababisha watu kubuni mbinu mbadala na hivyo kuendelea kutafuna fedha za umma bila ya huruma huku viongozi wengi wakitawaliwa na ubabaishaji.
Alitolea mfano wa sheria za Ghana kuhusu masuala ya ukopaji kwamba Katiba ya nchi hiyo inatoa nafasi kwa Bunge kujadili mkopo unaokopwa na namna utakavyotumika wakati Tanzania wanakaa watu wawili na kufanya uamuzi.
Alipoulizwa kuhusu madai hayo Mjumbe wa Kamati ya Bajeti, Joseph Selasini alisema anayepaswa kulitolea majibu suala hilo ni Katibu wa Bunge au Mkosamali mwenyewe kutoa ushahidi.
Hata hivyo, Mkurugenzi wa Shughuli za Bunge, John Joel alipoulizwa alisema anayepaswa kulizungumzia ni Mkosamali mwenyewe ambaye naye alipoulizwa jana alisema maelezo yake yalikuwa sahihi kwa kuwa anavyo vielelezo vyote.

HEMEDI PHD KUMUOA MENEJA WAKE

Muigizaji na muimbaji mwenye mikogo inayozidi bilioni za Dr Dre, Hemedy PHD amesema baada ya ‘kuchafua sana’ sasa ameamua kutulia na msichana mmoja ambaye anatarajia kufunga naye ndoa mwezi November mwaka huu.
“Nimeshachafua sana, yaani more than sana,”alikiri Hemedy kupitia XXL ya Clouds FM.“Ikafika hatua mpaka nikaona kwamba hii lazima iishe yaani kwasababu umri unaenda mama yangu anategemea vingi kutoka kwangu[...] kwahiyo mwisho wa siku nikapata msichana ambaye nikaona she is the right person for me, anaendana na mimi anakubaliana na ninachokifanya”.
Hemedy amesema licha ya kuwa hakuwa amejiandaa kwa ndoa hivi karibuni lakini ameitaja sababu ya kuamua kufunga ndoa mwezi November.
“kitu ambacho alichokuwa anataka zaidi ni mtoto na kama ilivyo kikawaida mtoto hawezi kuzaliwa nje ya ndoa, kwahiyo I was like boo siko tayari mimi ni star lazima nifanye kitu kikubwa kwenye yangu harusi yangu akasema as long as dini inaruhusu tufunge ndoa ya kihalali ambayo kidini haina gharama, so hiyo ndoa inakaribia kufungwa halafu tutapanga kuja kuparty, kwahiyo Novemba Inshallah nitakuwa mume wa mtu”.
Huyu ndiye mke mtarajiwa wa Hemedy aitwaye Muna aka Momo
Hemedy amemtambulisha rasmi mpenzi wake huyo kwa jina la Muna au Momo ambaye anadai amekuwa nae katika uhusiano nae nyuma ya pazia kwa mwaka mmoja na nusu na miezi 9 toka amtambulishe.
Ameongeza kuwa mke wake mtarajiwa ndiye meneja wake kikazi na…,
“Kitu kingine ambacho watu walikuwa hawakifahamu mke wangu mtarajiwa ndio meneja wangu right now ndio anammanage Hemedy from bed to stage”.
Hemedy ameongeza kuwa kwa sasa anapenda afahamike kama Hemedy aka Pappi na sio PHD sababu maana halisi ya PHD inafanana na tabia aliyokuwa nayo ya ‘kuchafua’ ambayo ameamua kuipa mgongo.
“The name PHD kidogo inaelekea ukingoni kwasababu maana halisi ya PHD ni jina flani ambalo kiukweli haliko…kuanzia sasa ningependa kutambulika kama Pappi”.Alisema Pappi.

KOCHA WA NIGERIA ATETEA MCHEZO MBAYA WA TIMU YAKE

Natal, Brazil. Kocha Stephen Keshi amewapuuza mashabiki wa soka nchini Nigeria baada ya timu yake kucheza moja ya mechi mbaya za Kombe la Dunia nchini Brazil mapema wiki hii.
“Siku zote nimekuwa nikikosolewa. Hata kama nikishinda ama kwenda sare, siku zote imekuwa hivyo. Hatuna uvumilivu nchini kwetu.
“Kila mchezo wanataka kushinda kwa gharama yoyote. Haileti maana yoyote ninapokuwa nikikosolewa,” kocha huyo alisema baada ya mchezo huo ambao Nigeria ililazimishwa suluhu na Iran.
Malalamiko hayo ya Keshi si mapya. Wakati alipotwaa ubingwa wa Mataifa ya Afrika nchini Afrika Kusini, alisema ametokea katika nchi ambayo kila mtu ni kocha.
Pia si hayo tu, alilazimika kujiuzulu katika moja ya mahojiano yake na mwandishi wa kimataifa lakini alikanusha maneno hayo wakati maofisa wa serikali walipombana na kumtaka aendelee kuiongoza miamba hiyo maarufu kama Super Eagle.

Jumatano, 18 Juni 2014

BAADA YA USAILI WA WATU ZAIDI YA 10000 HAWA NDIO WALIOFUZU

MAJINA YA WALIOITWA KWENYE USAILI WA PILI IDARA YA UHAMIAJI
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
Wasailiwa 1,281 kati ya 6,115 waliofanya usaili wa kwanza tarehe 13 Juni, 2014 jijini Dar es Salam kuomba nafasi ya Mkaguzi Msaidizi wa Uhamiaji (Assistant Inspector of Immigration) wanatarajiwa kuingia duru ya pili na ya mwisho ya usaili huo baada ya kufanikiwa kufaulu usaili wa kwanza.
Usaili huu ambao utafanyika kwa awamu utaanza tarehe 23 Juni hadi 03 Julai, 2014 na utafanyikia katika Bwalo la Maafisa Magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam kuanzia saa 1.30 asubuhi.
Tofauti na usaili wa kwanza ambao ulikuwa wakuandika na ulihusisha maswali ya hesabu na ufahamu wa jumla, usaili wa awamu ya pili utakuwa wa maswali ya ana kwa ana ambao utahusisha kupima uwezo wa msailiwa kujieleza na kufafanua mambo.
Kuchaguliwa kwa wasailiwa hawa kulifanyika baada ya kusahihisha majibu yao na majina kuingizwa katika mfumo wa kimtandao ambao ulisaidia kuchagua wasailiwa waliopata alama hamsini na kuendelea.
Majina ya wasailiwa hawa yanapatikana katika Tovuti ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, www.moha.go.tzna ya Idara ya Uhamiaji, www.uhamiaji.go.tzna watatakiwa kuja na vyeti vyao halisi vya kuzaliwa, vya shule na picha mbili za pasipoti.
BOFYA LINK HIYO HAPO CHINI KUSOMA MAJINA YA WALIOITWA KWENYE USAILI
http://www.moha.go.tz/ phocadownload/Kuitwa%20Kwenye % 20Usaili_Uhamiaji.pdf
http://www.moha.go.tz/ phocadownload/Kuitwa%20Kwenye % 20Usaili_Uhamiaji.pdf
Awali, kiasi cha wasailiwa 10,801 waliitwa kwa ajili ya usaili wa kwanza
baada ya kupokea maombi yao, lakini waliohudhuria ni 6,115 na kati yao ndio walipatikana 1,281 ambao watasailiwa ili kupata watakaojaza nafasi sabini (70) za Mkaguzi Msaidizi wa Uhamiaji katika Idara ya Uhamiaji.
SgnIsaac J. Nantanga
0754 484286
MSEMAJI,
WIZARA YA MAMBO YANDANI YA NCHI
Thursday, June