Kurasa

Jumamosi, 21 Juni 2014

ATOKA MKOJO NA MBEGU ZA KIUME SEHEMU YA PAJA

Rombo.Paja la mguu wa kushoto wa Hubert Mkenda (49) mkazi wa Kijiji cha Msaranga, Kata ya Kitale, Rombo mkoani Kilimanjaro, limetoboka na kutengeneza sehemu ambayo inapitisha haja ndogo (mkojo) na mbegu za kiume.
Mkenda ambaye ni baba wa watoto saba amekuwa katika hali ya ugonjwa kwa miaka 11 sasa na jitihada za madaktari wa Hospitali za KCMC Moshi na Huruma iliyopo Rombo mkoani humo, hazijamwezesha kuondokana na maumivu makali ambayo yanatokana na tundu hilo.
Tiba ya mwisho aliyoipata ni pale madaktari wa KCMC walipomwekea mpira kwenye nyonga kwa ajili ya kuwezesha kutoa mkojo, lakini wakati mwingine umekuwa ukitoka kupitia kwenye paja na kumsababishia maumivu makali.
“Ninapata maumivu makali mkojo unapopita kwenye paja na ninapokuwa na hisia za mapenzi, mbegu za kiume hupita kwenye shimo lililotoboka kwenye paja,” anasema Mkenda na kuongeza:
“Ni vigumu kueleza maumivu tabu na shida zinazoniandama, maisha yangu yamebadilika ni kama Mungu amechoka kusikia kilio changu lakini bado naamini ananipenda,” ni maneno ya uchungu anayoyasema Mkenda huku akionekana kukata tamaa na kuongea:
Anaendelea: “2003 ni mwaka ninaotamani usingekuwepo kabisa duniani kwakuwa ni mwaka uliobadilisha maisha yangu na kunifanya kuwa mteja wakuhudhuria hospitali kila siku bila matumaini”.
Mkenda alipata ajali ya gari 2003 katika msitu wa Rongai na kujeruhiwa vibaya katika maeneo ya haja kubwa na haja ndogo, ajali ambayo imesababisha kulazwa hospitalini kwa miaka 5 mfululizo na kufanyiwa upasuaji kwa nyakati tofauti mara nane.
Ajali ilivyotokea
Mkenda anasema hakumbuki siku, lakini ulikuwa mwezi Julai 2003, alipoondoka nyumbani kwenda Rongai kufanya kibarua cha kuvuna mahindi kwenye shamba la mtu na alipomaliza kuvuna akiwa na wenzake walipakia mahindi kwenye gari na kuanza safari ya kurejea Mashati, Rombo.
Anasema njiani dereva wa lori walimokuwa wamepakia mahindi, alisimama na kupakia magogo ya miti, kisha kuendelea na safari, lakini wakiwa njiani moja ya gogo lililokuwa limetoka nje ya gari liligonga kwenye mti na kumrusha juu.
“Nilirushwa juu na kutoka huko nilianguka chini kwa kishindo na kukalia gogo kisha kurushwa nje ya gari na kuangukia mti, niliumia vibaya sehemu za haja kubwa na ndogo,” anasimulia Mkenda.
Mkenda anasema alikimbizwa katika Kituo cha Afya Tarakea alikopewa huduma ya kwanza, lakini kutokana na kuvuja damu nyingi sehemu ya haja kubwa, walishauri akimbizwe katika Hospitali ya Huruma.
MWANANCHI

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni