KARIBU SANA MUKEBEZI BLOG #SAUTI YA WATU#. BLOG YA HABARI ZISIZO ZA KAWAIDA NA UJASIRIAMALI INAYOONGOZA TANZANIA.
Kurasa
▼
Jumanne, 24 Juni 2014
BRAZIL NA MEXICO ZATINGA HATUA YA MTOANO
Recife, Brazil. Mabao matatu ya Rafael Márquez, Guardado na Chicharito yametosha kuivusha Mexico katika hatua ya mtoano ya Kombe la Dunia baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-1, wakati Brazil ikikaa kileleni kwa ushindi wa 4-1 dhidi ya Cameroon.
Wawakilishi hao wa Afrika walishatoka baada ya michezo miwili, na walikuwa wakikamilisha ratiba huku Brazil wakitaka nafasi ya kukaa kileleni kwa pointi saba.
Croatia, ambao nao walikuwa na nafasi ya kufuzu kama wangeibuka na ushindi walishindwa kuzuia mabao hayo mawili ya kipindi cha pili na kujitoa wenyewe mashindanoni.
Wenyeji, ambao mabao yao yalifungwa na Neymar (mawili), Fred na Fernandinho, wanaongoza katika Kundi A, ambapo wamefuzu sambamba na Mexico katika hatua ya mtoano ya timu 16.
Kwa matokeo hayo, Brazil sasa itakutana na Chile katika hatua ya mtoano, wakati Mexico ikikutana na Uholanzi katika hatua hiyo.
Wawakilishi wa Afrika, Ivory Coast leo wanashuka dimbani kwa lengo moja tu la kusaka ushindi dhidi ya Ugiriki ili wakijihakikishia nafasi ya kucheza hatua ya 16 ya Kombe la Dunia 2014.
Miamba hiyo ya Afrika imekusanya pointi tatu katika mechi mbili za kundi lake, baada ya kuifunga Japan katika mchezo wa kwanza kabla ta kufungwa na Colombia.
Matokeo ya sare leo yatawatosha kuwavusha, endapo Japan watashindwa kuifunga Colombia katika mchezo wao wa mwisho.
Ugiriki na Ivory Cost zimeshindwa kufuzu kwa hatua ya mtoano katika fainali mbili za dunia zilizopita.
Wakati huohuo; Steven Gerrard atakuwa katika benchi wakati England itakapocheza mechi yake ya mwisho ya Kombe la Dunia dhidi ya Costa Rica - na kutoa nafasi kwa Frank Lampard kuchukua unahodha wa timu hiyo.
Gerrard anatakiwa kuanza kufikiria kuhusu hatma yake baada ya England kutolewa kwenye hatua ya makundi.
Lampard ametangaza kuondoka Chelsea na kiungo huyo mwenye miaka 36, hategemei kuendelea kuichezea England baada ya mechi ya leo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni