Kurasa

Jumamosi, 28 Juni 2014

MASKINI:BINTI ABAKWA NA BABA YAKE,APEWA UJAUZITO NA KUAMBUKIZWA UKIMWI

Musoma.“Amini usiamini hizi ni zama za mwisho mwanangu, mimi hili suala bado haliniingii akilini kabisa, kwani nilizoea kusikia kama hadithi kuwa mzazi ana uhusiano wa mapenzi na mwanawe, lakini leo hii yamenikuta ya kunikuta,” haya ni maneno ya Bhoke Mwita (siyo jina halisi), mama mzazi wa binti anayedaiwa kubakwa na baba yake mzazi kwa miaka minne.
Bhoke anasema kibaya zaidi mwanaye amefanyiwa unyama huo na baba yake mzazi, huku akimwachia doa ambalo haliwezi kufutika milele ambao ni ugonjwa wa Ukimwi.
Tukio hilo linamsababisha Wanjara kunyamaza kwanza kabla ya mahojiano, baadaye anadai binti yake kapewa ujauzito na maambukizi ya Ukimwi na baba yake, ingawa alikuwa hajitambua kuwa ni mgonjwa hatua ambayo imemuumiza na kumtia aibu kwenye jamii.
Mkazi huyo wa Mtaa wa Kigera Kibini, Kata ya Kigera, Manispaa ya Musoma mkoani Mara, anasimlia historia ya maisha yake hadi kuzaa mtoto huyo wa mwisho nje ya ndoa baada ya mumewe kufariki, lakini hatima imekuwa kugeuzwa mke mwenza.
Mwita anasita kuendelea na simlizi kabla binti yake aliyefanyiwa unyama na baba yake, hajasimulia masaibu yake: “Matatizo niliyonayo ni mengi, Mungu pekee ndiye anayefahamu, bado naongezewa msalaba mzito kama huu.”
Ghafla anapaza sauti anaita jina la binti yake aliyefanyiwa ukatili, aliyekuwa chumba kingine na kumtaka aeleze yote yaliyomsibu ili ulimwengu utambue.
Simulizi za binti
Anatokea binti mrembo ila sura yake inaonyesha unyonge, mrefu, mwembamba anasalimia kwa sauti ya upole huku akielekea kwenye kiti kuketi, afya yake siyo ya kuridhisha.
Bila kupoteza muda, binti huyo anadai alianza kuishi na baba yake mwaka 2002 akiwa anaingia darasa la tatu, baada ya mama yake kupata kibarua kwenye nyumba ya watawa.
Anasema baba yake alikuwa akiishi na kaka zake wawili wakubwa ambao walikuwa wamemaliza shule na wakati huo walikuwa wakijihusisha na kazi za vibarua.
Anasimulia kuwa alipofika darasa la tano, baba yake alikuwa akimfuata chumbani kabla ya kaka zake hawajarudi nyumbani na kumtaka afanye naye ngono. Binti huyo anasema kwamba wakati huo alikuwa hafahamu chochote kuhusu mapenzi.
“Nilipoona baba ananipiga kila siku, nilikubali, akawa anakuja chumbani kwangu na wakati mwingine ananiita kwake, tukishamaliza ananiambia niende kwangu kulala, hivyo nikaona kama jambo la kawaida,” anasimulia binti huyo.
MWANANCHI

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni