visit here again on mukebez.blogspot.com


CHANGE YOUR LIFE

CHANGE YOUR LIFE
Go to Amazon .com and get the copy of this book to make your life better.

Alhamisi, 11 Septemba 2014

USIMAMIZI WA MAADILI CBE WAONGEZA UFAULU

Hatua iliyochukuliwa na uongozi wa Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es salaam (CBE) kuendelea kuweka msisitizo katika usimamizi wa maadili kwa wanafunzi imeanza kuzaa matunda kufuatia kuogezeka kwa ufaulu wa masomo kwa wanafunzi wanaosoma chuoni hapo.
Hayo yamebainishwa leo jijini Dar es salaam na mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es salaam (CBE) Prof. Emanuel Mjema wakati akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu maadhimisho yanayoendelea ya chuo hicho kutimiza miaka 50 tangu kuanzishwa kwake Januari, 1965.
Amesema suala la usimamizi wa maadili kwa wanafunzi na jamii nzima inayoingia chuoni hapo limepewa kipaumbele kikubwa na uongozi wake tofauti na miaka iliyopita hali ilinayokifanya chuo hicho kuwa mfano wa kuigwa vyuo pamoja na taasisi nyingine za elimu ya juu hapa nchini.
“Chuo chetu sasa ni mfano wa kuigwa na vyuo vingine hapa nchini kwa sababu tumeweza kusimamia suala la maadili hasa uzingatiaji wa mavazi yenye staha kwa wanafunzi hali iliyoongeza heshima kwa chuo chetu”.
Mbali na suala la usimamizi wa mavazi kwa wanafunzi Prof amesema chuo hicho kimeendelea kuhakikisha ulinzi na usalama kwa wanafunzi na jamii nzima inayoingia na kutoka katika mazingira ya chuo hicho, kuimarisha ukaguzi katika maeneo yote muhimu ya kuingilia wanafunzi na kuwatambua wanafunzi wote kwa kutumia vitambulisho vyao.
Amefafanua kuwa chuo hicho sasa kinafurahia matunda ya mafanikio ya kutimiza miaka 50 tangu kuanzishwa kwake yakiwemo mabadiliko na maboresho makubwa katika sekta ya elimu hasa ongezeko la udahili wa wanafunzi, ongezeko la fani za masomo na kampasi za chuo hicho katika mikoa mingine nchini ikiwemo Dodoma, Mwanza, Mbeya na Zanzibar.
Prof. Mjema amefafanua kuwa chuo cha CBE sasa kinatimiza miaka 50 kikiwa chuo pekee Afrika ya Mashariki na katika nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) kinachotoa wanafunzi wa shahada ya vipimo.
“Chuo hiki pekee ndicho kinachotoa mafunzo kwa ngazi ya shahada ya vipimo, ni chuo kinachotegemewa sana katika ukanda huu wa nchi za Afrika Mashariki na SADC” Amesisitiza.
Ameeleza kuwa tangu kuanzishwa kwake Januari, 1965 na aliyekuwa Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mwalimu Julius Kambarage Nyerere , chuo hicho kimepata mafanikio makubwa kwa kuongeza idadi ya wanafunzi wanaodahiliwa kila mwaka kutoka wanafunzi 25 mwaka 1965 hadi 14,000 mwaka 2014.
Mafanikio mengine ni kuongezeka kwa kozi za masomo na ngazi za mafunzo hadi kufikia shahada, kuongezeka kwa wakufunzi wenye shahada za uzamivu (PhD) chuoni hapo pamoja na chuo kuanzisha ushirikiano wa elimu na vyuo vikuu vingine nje ya nchi kikiwemo Chuo Kikuu cha Eastern Finland katika utoaji wa mafunzo ya shahada za uzamivu kwa kutumia TEKNOHAMA kwa nchi za SADC.
Ameongeza kuwa katika kipindi cha miaka 50 ya chuo hicho idadi ya kampasi imeongezeka kutoka 1 ya jijini Dar es salaam na kufikia 4 katika mikoa ya Mbeya, Mwanza, Dodoma na upande wa Zanzibar huku idadi ya wahitimu wa chuo hicho ikiongezeka kwa kipindi chote ikiwa zaidi ya wanafunzi Laki moja.
Aidha, katika kuhakikisha chuo hicho kinaendelea kuimarisha ubora wa elimu inayotolewa kwa wanafunzi katika maadhimisho hayo,chuo kinaandaa matukio mbalimbali ya ukusanyaji wa fedha kupitia chakula cha hisani, matembezi, midahalo ya wasomi na mikutano wanafunzi wahitimu wa chuo hicho Zanzibar, Dodoma, Mwanza, Mbeya na Dar es salaam kwa ajili ya ujenzi wa maabara, vyumba vya mihadhara ya wanafunzi na madarasa.
Pia chuo hicho kinaandaa mafunzo ya ujasiriamali yatakayotolewa kwa jamii ikiwa ni sehemu ya kurudisha huduma kwa jamii kwa kuwajengea uwezo wajasiriamali, na kuwajengea uelewa wanafunzi ili waweze kuwa na uchaguzi sahihi wa hatima yao ya baadaye pindi wanapohitimu mafunzo.

Jumatano, 10 Septemba 2014

KATIBA MPYA MWISHO!!

Dodoma.Makubaliano baina ya Rais Jakaya Kikwete na viongozi wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD), kutaka Bunge Maalumu lifikie ukomo Oktoba 4, mwaka huu yamezua sintofahamu mjinihapa huku uamuzi huo ukionekana kuwachanganya viongozi wa Bunge hilo.
Kutwa nzima ya jana, viongozi wa Bunge Maalumu walishinda kwenye vikao vya mashauriano huku wabunge wa CCM wakitarajiwa kukutana jana usiku kwenye makao makuu ya chama hicho kupewa taarifa rasmi za uamuzi huo.
Katika makubaliano baina ya TCD na Rais Kikwete, imeamuliwa kuwa uamuzi wa Rais kupitia Tangazo la Serikali (GN) 254 la kuongeza siku 60 hadi Oktoba 4 uheshimiwe na baada ya tarehe hiyo Bunge liahirishwe.
Uamuzi huo ni kinyume cha azimio la Bunge Maalumu la Agosti 5, 2014 ambalo lilirekebisha Kanuni ya 14 (4) na kuifuta Jumamosi katika siku zilizotajwa kuwa za kazi, pia sikukuu na siku za Jumapili.
Mwenyekiti wa Bunge, Samuel Sitta alikaririwa akiwaambia wajumbe wa Bunge hilo kwamba Rais alikuwa ameridhia kwamba siku 60 alizotoa hazingejumuisha Jumamosi, Jumapili na siku za sikukuu.
Ni kwa msingi huo, Bunge hilo likapanga kwamba lingeendelea na shughuli zake hadi Oktoba 31, wakati Mwenyekiti wa Bunge atakapokabidhi Katiba inayopendekezwa kwa Rais Kikwete.
Hata hivyo, makubaliano yaliyofikiwa baina ya viongozi wa TCD na Rais yanaonekana kuvuruga kabisa ratiba ya Bunge hilo ambalo jana na juzi, Kamati ya Uongozi ilikutana mara kadhaa kuona jinsi ya kunusuru mchakato huo.
Ingawa haikufahamika mara moja kama vikao hivyo vya kamati ya uongozi inayoongozwa na Sitta mwenyewe vinajadili nini, lakini taarifa zimedai huenda kukawa na mabadiliko makubwa ya ratiba.
Habari nyingine zinadai kwamba mabadiliko hayo huenda yakapunguza muda wa baadhi ya shughuli za kazi za Bunge hilo ili liweze kukamilisha kazi yake ikiwamo wajumbe kupiga kura ya uamuzi.
Katika kikao cha jana asubuhi, kamati hiyo ilishindwa kurekebisha ratiba yake ili iendane na siku zilizosalia, hivyo kuahirishwa kwa kuwapa kazi wataalamu wake kuleta mapendekezo ambayo yangejadiliwa jana mchana.
Katibu wa Bunge Maalumu, Yahya Khamis Hamad alithibitisha jana kwamba ratiba ya Bunge imebadilika kutokana na hoja nyingi kukubalika ndani ya kamati.
“Kamati ya uongozi itakutana baadaye (jana) kuangalia vipengele ambavyo hawakukubaliana kwenye kamati ndivyo wavipangie muda na ratiba itajulikana baada ya kikao hicho,” alisema Hamad.
Hofu ya akidi
Hata hivyo, habari zaidi zinadai kwamba uongozi wa Bunge Maalumu ulichanganywa na kuwapo kwa hoja za baadhi ya wajumbe wake kutaka kwenda Makka kwa ajili ya kushiriki Ibada ya Hijja, hali inayotishia akidi kwa ajili ya kuendesha vikao.
Kanuni za Bunge Maalumu zinataka kuwapo kwa nusu ya wajumbe kutoka pande zote za Muungano wakati wa kuendesha vikao vyake na theluthi mbili ya wajumbe hao kila upande wakati wa kufanya uamuzi au kupiga kura.
“Tumetoka kwenye kikao mchana huu na pengine tutaitana tena maana hatujafikia mwafaka, kuna mambo mengi yamejitokeza lakini kubwa ni hili la wenzetu ambao wanataka kwenda Hijja, kuondoka kwao kunaweza kuathiri akidi kwa kiasi kikubwa,” kilisema chanzo chetu kutoka ndani ya kamati hiyo.
Kutokana na matakwa hayo, hivi sasa Ofisi ya Katibu wa Bunge inafanya tathmini ili kufahamu idadi ya wajumbe ambao watakwenda Hijja Septemba 22, mwaka huu, ambao wengi wanatoka Zanzibar.
Hamad alikiri kwamba kuna mambo mengi ambayo ofisi yake inayafanyia kazi na kwamba hilo la Hijja ni mojawapo… “Kwa sasa siko katika nafasi ya kuzungumza kwa kirefu, kikao cha Kamati ya Uongozi kimeisha na bado kuna kazi nyingi za kuona jinsi tunavyoendelea.”
Tayari Bunge hilo limetikiswa na kutokuwapo kwa wajumbe waliosusia vikao tangu Aprili 16, mwaka huu ambao ni wajumbe wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) ambao unaundwa na vyama vya CUF, Chadema na NCCR Mageuzi na baadhi kutoka Kundi la 201.

Jumapili, 7 Septemba 2014

KIGWANGALLA ATANGAZA NIA YA KUGOMBEA URAIS

September 7 2014 Dr. Hamisi ambae ni mbunge wa Nzega kwa ruhusa ya CCM alikutana na Waandishi Dar es salaam akiwa ameongozana na mke wake pamoja na watoto wao na kisha kuweka wazi kwamba yuko tayari kugombea kiti cha Urais kwa tiketi yaCCM 2015.
Yafuatayo ndio ameyasema:
1.‘Leo nitasema neno zito kidogo, litabadilisha sura ya historia yangu milele… kinachotokea hapa kina maana kubwa sana kwa watu wenye historia inayofanana na mimi, wale ambao wameyajua maisha ya shida na kukosa uhakika toka wakiwa tumboni mwa wazazi kutokana na hali za uchumi wa familia zao’
2.
‘Nimeyajua maisha ya mtu mnyonge na masikini kwa kuyaishi na sio kwa kusoma ama kusikia, ninajua mtu akiongelea njaa anamaanisha nini’
3.’Watanzania wanataka kupata huduma bora za afya, elimu, maji, miundombinu…… ukienda kwa Wafanyabiashara wakubwa pale Pugu viwandani ama kwa Matabibu wenzangu hospitali ya taifa Muhimbili au kwa Wafanyabiashara pale sokoni Kariakoo wote watakwambia hawapendi kuona kodi zao zikitafunwa na wachache wasio waadilifu’
HK 16
4.’Watu hawatarajii serikali itabeba mizigo yao yote lakini wanaamini kabisa kwamba tukibadili vipaumbele vyetu, tukibadili namna tunavyoendesha serikali na uchumi wetu, tunaweza kwa kiasi kikubwa kubadili mwelekeo mzima wa maisha ya baadae na kuiondoa Tanzania miongoni mwa nchi masikini kabisa duniani’
1.‘Na mimi kama Watanzania wenzangu wengi nina imani kubwa kabisa kwamba tunaweza kubadili mustakabali wa taifa letu, kufungua milango ya maisha bora zaidi kwa Watanzania, tutatoa fursa sawa kwa kila Mtanzania kuishi kwa matumaini kwamba atabadili maisha yake wakati wowote ule kuanzia leo, tutaweza kuamsha ari ya kila Mtanzania kuongeza bidii kwenye kazi’
‘Ninaamini kabisa kutokea ndani ya mifupa yangu kuwa tukifanya uchaguzi sahihi wa vipaumbele vyetu, tukibadili namna tunavyoendesha uchumi wetu na serikali yetu……. haya ninayoyasema sio ndoto za mchana’
h13Baada ya kuyazungumza yake ya moyoni baadhi ya Waandishi walipata nafasi ya kumuuliza maswali ambapo hili lilikua mojawapo >>> ‘Umetangaza nia kwamba unagombea Urais lakini sijasikia unapitia chama gani au utasimama binafsi?……… na kama ni chama, mpaka sasa hakuna chama chochote ambacho kimefungua milango kwa Wanachama wake kutangaza nia, kwa kufanya hivyo huwezi kuona unakiuka taratibu za chama?
JIBU:‘Nitapitia chama cha mapinduzi, sijawahi kuwa Mwanachama wa chama chochote kile cha siasa zaidi ya CCM na sijawa na fikra za kubadili chama, natangaza nia ya kugombea Urais kupitia chama changu cha CCM, hii ya kwamba sasa hivi ni mapema mno kutangaza nia kwa sababu vyama havijafungua milango ya watu kutangaza nia, sio kweli…. watu wameweka nia za kuutaka Urais toka mwaka 1995 lakini pia kuweka nia sio kufanya kampeni, kinachokatazwa ni kuanza kufanya kampeni kabla ya muda wa kampeni kutangazwa’ –Dr. Hamisi Kigwangalla
‘Nimeamua kuweka wazi nia yangu, sitaki ule unafiki wa kujificha chini ya kivuli cha Ooooh!!….. nimeshauriwa, nimeombwa, nasubiri kuota, mimi ni mkweli na nimetia nia ya dhati kwamba nataka Urais’ –Dr. Kigwangalla
h15‘Vipaumbele vyangu kama napata fursa ya kuwa Rais ni kuboresha huduma za jamii kama maji, afya, elimu… kipaumbele cha pili ni kujenga na kuimarisha miundombinu kama barabara, ndege, reli na bandari…….. kipaumbele cha tatu ni utawala bora, nchi haiwezi kuongozwa bila kuwa na utawala wa sheria yani kila mtu apate haki yake bila kudhulumiwa ‘ –Dr. Kigwangalla

OKWI HURU KUITUMIKIA SIMBA

BREAKING NEWZZZZZZ: MKATABA WA YANGA, OKWI HAUPO NA SASA YUPO HURU KUCHEZEA TIMU YOYOTE AITAKAYO
Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imekutana leo (Septemba 7 mwaka huu) na kupitia masuala mbalimbali ikiwemo mgogoro wa kimkataba kati ya klabu ya Yanga na mchezaji Emmanuel Okwi (pichani kushoto akipokea jezi baada ya kusajiliwa na Simba).
Mkataba huo ulipitiwa na Kamati ikiwemo kumsikiliza mchezaji mwenyewe pamoja na upande wa Yanga, na kuridhika kuwa mkataba kati ya pande hizo umevunjika.Ukiwa ni mkataba wa pande mbili, Yanga ilikiuka kipengele namba 8 kuhusu malipo ya ada ya usajili.
Yanga ikiwa mwajiri, haikutekeleza kipengele hicho cha kimkataba hadi kufikia Juni 27 mwaka huu ilipoandika barua TFF kuomba mkataba huo uvunjwe. Kwa maana hiyo Okwi ni mchezaji huru, hivyo yuko huru kujiunga na timu yoyote.
Mkataba ni uhusiano kati ya mwajiri (Yanga) na mwajiriwa (Okwi), ambapo Kamati imebaini kuwa uhusiano huo haupo, hivyo hakuna mazingira ya pande hizo mbili kuendelea kufanya kazi pamoja.
Pamoja na Yanga kuwasilisha pingamizi la kuwepo mmoja wa wajumbe katika kikao kwa sababu za kimaslahi (conflict of interests), walifahamishwa kuwa kilichopo mbele ya kamati ni mgogoro wa kimkataba kati ya Yanga na Okwi, na si usajili.
Pia lilijitokeza suala la Okwi kutakiwa na klabu ya Wadi Degla ya Misri. Kamati imeiagiza Sekretarieti ya TFF kulifanyia uchunguzi suala hilo na kulitolea taarifa katika kikao kijacho.
Hata hivyo mjumbe huyo hakushiriki katika kuchangia hoja na kutoa maamuzi. Uamuzi wa kamati ulifanyika baada ya majadiliano, hivyo hakukuwa na suala la kupiga kura.
Kuhusu pingamizi la Coastal Union kwa Abdi Banda, Kamati imebaini kuwa klabu hiyo imevunja mkataba kati ya pande hizo mbili kwa kushindwa kumlipa mchezaji huyo mshahara wa miezi mitatu mfululizo kama takwa la mkataba.
Klabu ya Coastal Union iliwakilishwa na mmoja wa viongozi wake, wakati Banda aliwakilishwa na mwanasheria wake.
Vilevile Kamati imekubaliana na pingamizi la Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Morogoro (MRFA) kuhusu wachezaji waliofanyiwa uhamisho kutoka katika mkoa wake bila kulipiwa ada za usajili, hivyo klabu husika zinatakiwa kulipa ada hizo.
Pia Kamati imeagiza klabu zote zilizosajili wachezaji bila kuwafanyia uhamisho, kulipa ada za uhamisho kwa pande husika kabla ya kuanza ligi, vinginevyo leseni zao zitazuiwa hadi watakapolipa.
Mashauri mengine ya pingamizi yatasikilizwa baadaye kwa vile klabu husika hazikupata fursa ya kufika mbele ya kamati.Kamati inasisitiza kwa wanachama wa TFF kuheshimu mikataba.
BONIFACE WAMBURA
KAIMU KATIBU MKUU
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA VYUO VYA UALIMU 2014

MAJINA YA WALIOCHAGULIWA VYUO VYA UALIMU 2014/2015
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
WAOMBAJI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA UALIMU NGAZI YA STASHAHADA YA JUU (MIAKA 3) MWAKA WA MASOMO 2014/2015
MAELEKEZO:
Waombaji waliochaguliwa kujiunga na Mafunzo ya Ualimu mwaka wa
masomo 2014/2015 wanatakiwa kuripoti katika Vyuo walivyopangiwa
tarehe 06/10/2014. Fomu za maelekezo (Joining Instructions) zitatolewa
na chuo husika na zitatumwa kwa waliochaguliwa tu. Waliochaguliwa
wanatakiwa kufika vyuoni wakiwa na mahitaji yaliyoainishwa kwenye fomu
ya kujiunga na Chuo. Aidha, fomu hizi zinapatikana pia kwenye Tovuti ya Wizara: www.moe.go.tz; NACTE: www.nacte.go.tz; na TAMISEMI:
www.pmoralg.go.tzMuhimu:
1. Waombaji waliochaguliwa ni wale wenye ufaulu wa Daraja la I hadi III
2. Waliochaguliwa wanatakiwa kuwasilisha Vyeti halisi vya Baraza la Mitihani
la Tanzania Kidato cha NNE na SITA (CSEE na ACSEE) na vyeti vya kuhitimu
Elimu ya Sekondari na Mafunzo ya Ualimu.
3. Ada ya mafunzo Stashahada ya Juu ni 600,000/= kwa mwaka (Muhula wa
kwanza 300,000/= na muhula wa pili 300,000/=)
4. Wanafunzi watakaosajiliwa Chuoni ni wale waliopo kwenye orodha hii tu na
SIYO vinginevyo, waweza pata orodha hyo kwa kufungua kiunganishi kimoja
wapo hapo chini au kwa kutembelea mfumo wenye majina - bonyeza hapa

Jumatano, 3 Septemba 2014

HATIMA YA BUNGE LA KATIBA MIKONONI MWA RAIS

Dodoma. Hatima ya Bunge Maalumu la Katiba imebaki mikononi mwa Rais Jakaya Kikwete, ambalo limemwandikia barua kiongozi huyo wa nchi kutaka ufafanuzi wa kisheria kuhusu tarehe ya mwisho ya kumaliza vikao vyake.
Hiyo ni kutokana na muda uliopangwa kwenye ratiba ya bunge hilo kuzua utata wa kisheria na kuwapo uwezekano wa mwingiliano na Bunge la Jamhuri ya Muungano na Baraza la Wawakilishi (BLW), Zanzibar.
Ratiba ya Bunge Maalumu la Katiba inaonyesha kuwa limepanga kuhitimisha vikao vyake mwishoni mwa Oktoba, tofauti na tarehe iliyotolewa na Rais Jakaya Kikwete Julai 28, mwaka huu ambayo ilitangazwa katika Gazeti la Serikali (GN) namba 254 la Agosti Mosi.
Tangazo la Rais linaonyesha kuwa awamu ya pili ya Bunge Maalumu ingeanza Agosti 5, 2014 na kumalizika Oktoba 4, lakini ratiba ya Bunge hilo inaonyesha kuwa litamalizika Oktoba 31, siku ambayo mwenyekiti wa Bunge hilo atakabidhi kwa Rais Katiba inayopendekezwa.
Hata hivyo, uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa hadi sasa Serikali bado haijatoa tangazo (GN) lingine kuongeza muda hadi mwishoni mwa Oktoba kama alivyosema Mwenyekiti wa Bunge Maalumu, Samuel Sitta wakati akitoa ufafanuzi wa siku 60 zilizotengwa kwa ajili ya Bunge hilo, Agosti 5 mwaka huu.
Sitta alisema kwa kadiri ya tafsiri, siku za kazi ni Jumatatu hadi Ijumaa ambazo wajumbe wanapaswa kufanya kazi na kwamba Jumamosi na Jumapili siyo sehemu ya siku 60 zilizoongezwa na Rais.
Hata hivyo, Katibu wa Bunge Maalumu, Yahya Khamis Hamad alisema hadi sasa hawajapata maelekezo ya ziada kutoka serikalini ambako waliandika barua ya kuomba ufafanuzi wa kisheria kuhusu suala hilo.
“Tulimwandikia barua, Katibu Mkuu Kiongozi (Ombeni Sefue) kuomba ufafanuzi wa siku hizo kama ambavyo sisi tungependa iwe, lakini hadi sasa bado hatujajibiwa lakini bado siku zipo nadhani tutajibiwa tu wakati mwafaka,” alisema Hamad ambaye pia ni Katibu wa Baraza la Wawakilishi.
Sefue alikiri ofisi yake kupokea barua kutoka Bunge Maalumu ikiomba ufafanuzi ambao ungeliwezesha kuongeza siku kwa lengo la kukamilisha kazi ya kujadili na kuandika Katiba inayopendekezwa na kwamba maombi yao bado yanafanyiwa kazi.
“Bado tuna muda wa kutosha tu, ni kweli tulishayapokea maombi ya Bunge Maalumu kuhusu suala hilo na Mheshimiwa Rais akikamilisha kazi yake watajulishwa tu,”alisema Sefue.
Utata wa kisheria
Licha ya ahadi iliyotolewa na Sitta ni dhahiri kwamba suala hilo lina utata wa kisheria kutokana na kauli iliyowahi kutolewa na Mwanasheria wa Serikali (AG), Jaji Frederick Werema wakati akitoa ufafanuzi wa maana ya siku 70 ambazo Bunge lilikaa mara ya kwanza.
1 | 2 | 3

Jumanne, 2 Septemba 2014

SHUKRANI KWA NDUGU, JAMAA, MARAFIKI NA TAASISI

Siku ya jumatano usiku ilikuwa ni siku ambayo niliuona kabisa mwisho wa mimi kuendelea kufurahia uumbaju wa Mungu katika dunia hii hasa pale nilipokuwa na saini kwaajili ya kufanyiwa upasuaji lakini kwa kwa nguvu zake ameniponya.NAMSHUKURU SANA MWENYEZI MUNGU KWA UPONYAJI WAKE HUU MKUU.

Katika mchakato huo Mwenyezi aliwatumia watu mbalimbali ambao sina budi kuwashukuru hapa kwasababu najua Mungu alikuwa na makusudio yake kuwatumia wao badala ya wengine: