visit here again on mukebez.blogspot.com


CHANGE YOUR LIFE

CHANGE YOUR LIFE
Go to Amazon .com and get the copy of this book to make your life better.

Jumatatu, 6 Oktoba 2014

MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA KATIKA BIASHARA

1. Thaminisha bidhaa unazo uza
Iwe biashara ndogo au kubwa bidha unazouza ni muhimu ziwe zenye ubora na muonekano mzuri utakaomvutia mteja.Watu hupenda vitu vizuri, bora na vinavyodumu hivyo ni vema utengeneze bidha zenye ubora na thamani“A good businessman serves quality products to his customers.’’
2. Fanya biashara ya kipekee
Fikiri na kuwa mbunifu katika kubuni na kuibua biashara mpya. Mfano kama mahali unapotaka kufanya biashara kuna M-PESA, AIRTEL MONEY, maduka ya nguo, show room ya vitu vya makazini na majumbani au biashara nyingine maarufu. Ikiwa mahali pa biashara kuna mzunguko wa watu wengi na kuna mazingira ya kupata faida nzuri unaweza kufanya biashara kama wanazofanya wengine lakini bado una kila sababu ya kuongeza biashara nyingine kwa kubuni na kuibua biashara mpya tofauti na za wafanyabiashara wengine. Kufanya hivyo utaweza kuwa mfanyabiashara wa kipekee kwa kuwa na huduma nyingi ambazo watu huhitaji kuhudumiwa. Moja ya siri ya kuongeza wateja katika biashara yako ni kuwa na huduma nyingi anazohitaji mteja. Kuwa mjanja kwa kujua wateja wako wanataka nini ili uweze kuwasogezea huduma karibu.
3. Pata ushauri kwa watu waliofanikiwa kibiashara
Unapokuwa katika wakati mgumu wa kutatua matatizo yako ya kibiashara au unapokuwa na utata katika kufanya maamuzi sahihi ya namna ya kuanza biashara ni vizuri utafute ushauri kutoka kwa watu ambao tayari wamefanikiwa katika biashara kama yako. Pia unaweza kutafuta watu wa kukufundisha jinsi ya kufanya biashara yani“Business Mentors”ambao watakusaidia kupata ujuzi sahihi na kukupatia maarifa kuhusu biashara yako.
4. Uza bidhaa zako kwa bei inayokubalika na wengi
Wateja hupenda kununua vitu kwaBEI POA!hivyo ni muhimu kujua utauza bidha zako kwa bei kiasi gani. Hapa si maanishi uuze bidha kwa bei rahisi bali uzingatie bei ambayo wateja wengi wanaweza kukidhi.
Mfano; Unataka kufanya biashara ya kuuza keki, gharama ulizotumia kutengeneza na kuandaa keki ni shilingi 8,500/= kwa keki moja badala ya kutaka faida kubwa kwa kuuza shilingi 20,000/= unaweza kuuza kwa shilingi 13,500/= ambayo utapata faida ya shilingi 5,000/= mathalan vilevile utapata wateja wengi na kuuza keki nyingi kuliko kuuza kwa bei kubwa ambayo utapata wateja kidogo.
5. Tangaza biashara yako
Biashara ni matangazo hivyo ukitaka biashara yako ikue kwa kupata wateja wengi huna budi kuitangaza ili watu waifahamu. Siku hizi kuna njia nyingi za kutangaza biashara ikiwemo kupitia wavuti (website / blog) , radio, runinga au hata mabango. Kumbuka tumia maneno mazuri ya kuvutia na kushawishi wateja.
6. Jiamini na usikate tamaa katika biashara
Kuna wakati unapoanza biashara mambo huwa mabaya hivyo ni vema ujiamini na utafakari ni wapi umekosea au ni nini cha kufanya ili uboreshe biashara yako. Wakati mwingine unapoanzisha biashara inachukua muda watu kujua unauza nini hivyo swala la muda wa watu kujua biashara yako nalo ni jambo la kuzingatia. Hakuna mafanikio ya haraka hivyo uvumilivu na ukakamavu wako ni muhimu sana katika kukuza biashara yako. Kumbuka usikae na kusubiri sana watu waifahamu biashara yako, weka na zako bidii katika kuongeza na kupanua mtandao wa wateja wako.
7. Fanya biashara uipendayo
Inaaminika kuwa ikiwa mtu atafanya kazi aipendayo basi ataifanya kwa uhodari na utashi wake kuweza kupata mafanikio makubwa, swala hili ni muhimu katika kuamua ni biashara gani unapenda kuifanya. Mfano kama wewe umesomea fani ya uhandisi wa majengo ni vema ukafanya biashara kwa kuanzisha biashara yako ya mambo ya ujenzi. Kama unapenda kupika fungua mgahawa au fanya kazi inayohusiana na fani unayopenda. Maendeleo na mafanikio makubwa ya kazi yeyote ile huletwa kwa kufanya kazi unayoiridhia na kuipenda.
Hayo ni mambo machache na ya kawaida ya kuzingatia katika biashara yako, kuwa na ndoto kubwa ya kufanikiwa kibiashara ni vizuri lakini pia penda kujua mengi kuhusu mahusiano ya biashara yako na wateja wako kwani biashara ni watu hivyo kuwa makini kwa kila hatua unayopiga kibiashara ili kuepuka hasara.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni