Wanaume TMK,Tip Top Connections kupamba mechi ya simba&Yanga
Makundi mawili maarufu ya muziki wa kizazi kipya nchini TMK family na Tip Top Connections wanatarajiwa kupamba mechi za ligi kuu Vodacom ya Simba na Yanga na ile ya Azam FC dhidi ya JKT Ruvu inayochezwa kesho Jumamosi jijini dar es salaam.
Uwepo wa burudani hizo ni sehemu ya mkakati wa mdhamini mkuu wa ligi hiyo kampuni ya huduma za mawasiliano ya simu za mkononi ya Vodacom ya kuhitimisha msimu wa ligi wa 2013/2014 kwa kishindo na burudani ya aina yake.
Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim amesema kundi la Tip Top Connections likinogeshwa na msanii mahiri Ma D litaipamba mechi ya watani wa jadi ya Simba na Yanga kwenye uwanja wa taifa huku TMK wanaume family wakiwasindikiza washabiki wa mabingwa Azam FC kwenye uwanja wa Azam Complex
"Tumeamua kuifunga ligi yetu kwa mtindo wa aina yake kwa kutoa burudani kwa mabingwa wapya Azam FC pamoja na kuipamba mechi ya Yanga ambao walikuwa mabingwa watetezi na washindi wa pili wa msimu huu tunaoumalizia"Alisema Mwalima katika taarifa yake kwa vyombo vya habari
Mwalim amesema mechi zote mbili zinatarajiwa kuvutia hisia za maelfu ya wapenda soka nchini kutokana na kila mechi kuwa na umuhimu wake katika historia na rekodi za soka nchini na hivyo ni wazi maelfu ya washabiki watafurika kwenye uwanja wa Taifa na Azam Complex huku wengine wakifuatilai mechi hizo kupitia matangazo ya moja kwa moja ya redio na Luninga
"Mechi zote mbili ni muhimu sana huku Azam akitaka kuweka rekodi ya kumaliza msimu bila ya kupoteza mchezo huku timu zenye utani wa jadi za Simba na Yanga zikishuka dimbani huku kila mmoja akitaka kulinda heshima mbele ya mwezake"Aliongeza Mwalim.
Mwalim amesema maandalizi yote kwa upande wao wameyakamilisha na kwamba kilichobakia sasa ni kwa washabiki kufika uwanjani ili kuona ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara inavyohitimishwa kwa mbwembwe za aina yake.
Amesema katika mechi hizo, Vodacom itakabidhi kombe kwa mabingwa wapya Azam FC pamoja na medali kwa timu ya Yanga na Mbeya City zinazomaliza nafasi ya pili na ya tatu katika msimamo wa mwisho wa ligi hiyo.
"Wakati wote tunaangalia ni vipi tunaweza kufanya mambo yatakayoinogesha ligi hii kuu ya Vodacom, na hivyo ni imani yetu kwamba makundi haya mawili ya burudani ni sahihi na yanahadhi inyoendana na ligi na michezo husika,"Aliongeza Mwalim
Burudani katika viwanja vyote viwili inatarajiwa kuanza mapema majira ya saa saba ili kutoa nafasi nzuri kwa washabiki kupata burudani yakutosha kabla ya kuanza kwa mechi majira ya saa kumi alasiri
KARIBU SANA MUKEBEZI BLOG #SAUTI YA WATU#. BLOG YA HABARI ZISIZO ZA KAWAIDA NA UJASIRIAMALI INAYOONGOZA TANZANIA.
Ijumaa, 18 Aprili 2014
TAHADHARI YA ELNINO SIKU TATU ZA PASAKA!
LICHA ya mabadiliko yasiyo ya kawaida yaliyojitokeza katika utabiri wa hali ya hewa kuhusu mvua za El Nino hafifu, Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imesema kuna uwezekano wa kuwapo kwa vipindi vifupi vya mvua kubwa.
Mabadililko hayo yanahusu utabiri uliotolewa na TMA kuanzia Oktoba hadi Desemba, mwaka huu kuwa kungekuwa na El Nino hafifu maeneo mengi nchini.
Akizungumza ofisini kwake jana, Mkurugenzi wa Huduma za Utabiri wa TMA, Dk Hamza Kabelwa alisema katika utabiri waliofanya siku mbili zilizopita, umeonyesha uwezekano wa kuwapo kwa vipindi vifupi vya mvua kubwa hivyo wananchi wanatakiwa kuchukua tahadhari.
Mamlaka hiyo tangu Septemba mwaka huu, ilisema joto la Bahari ya Pacific limeongezeka ikiwa ni kiashiria kingine cha mwendelezo wa mvua za El Nino hafifu.
Iliwataka wananchi kuwa makini na mabadiliko hayo ambayo yanaweza kusababisha mafuriko.
“Kuna uwezekano wa mvua kubwa kunyesha kwa kipindi hiki kifupi kama zinavyoendelea, wananchi wanatakiwa kuchukua tahadhari hasa wale wanaoishi mabondeni,” alisema Kabelwa. Kabelwa alisema mabadiliko hayo ya hali ya hewa hayajawahi kutokea katika miaka iliyopita na yamekuwa ni yakushangaza. Alisema kutokana na hali hiyo, taasisi zinazohusika na hali ya hewa Afrika (ICPAC) watakutana.
na Kanda ya Kusini mwa Afrika (SADC-CSC) kwa mara ya kwanza zitakutana kufanya uchambuzi wa mifumo ya hali ya hewa Desemba 5, mwaka huu.
“Novemba 5 hadi 13, mwaka huu mkutano utafanyika nchini Kenya na kumalizikia Zambia, baada ya mikutano ya kikanda kumalizika mamlaka yetu itatoa marejeo ya utabiri wa mvua kwa nchi nzima,” alisema Kabelwa.
Haba

HISTORIA YA BAKHRESA NA MAFANIKIO YAKE.
tunakuletea mjasiliamali mwenye mafanikio afrika ya mashariki ambaye alianza na biashara ya mabaki ya mazao ya baharini, kushona viatu, biashara ya viazi na baadae mgahawa. Leo hii ni milionea anayemiliki rasilimali mbalimbali za viwanda, pamoja na vyombo vya usafiri ndani na nje ya nchi. M jasiliamali huyu si mwingine bali ni Said Salim Awadh Bakhresa
HATUJADIRI RASIMU YA CCM'WASEMA UKAWA.
Dodoma.Bunge Maalumu la Katiba sasa lipo katika hati hati ya kuendelea kutokana na viongozi wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), kutangaza kuwa hawatakuwa tayari kujadili rasimu tofauti na iliyowasilishwa na Jaji Joseph Warioba bungeni.
Wakizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jana katika Ukumbi wa Pius Msekwa bungeni, viongozi wa Ukawa, Profesa Ibrahim Lipumba, James Mbatia, Freeman Mbowe na Tundu Lissu, walisema wataitetea rasimu hiyo, ndani ya Bunge na kwenye Kamati.
“Rais Jakaya Kikwete amekuja bungeni siyo kufungua Bunge la Katiba bali kaja na mapendekezo ya rasimu ya CCM, sisi tutajadili rasimu ya wananchi ya Jaji Joseph Warioba ambayo inazungumzia muundo wa Muungano wa Serikali tatu,” alisema Profesa Lipumba.
Kutokana na msimamo huu wa Ukawa huenda Bunge litakwama kwani kwa mapendekezo ya CCM yenye Muundo wa Muungano wa Serikali mbili ni lazima kuandikwa upya Rasimu ya Katiba au kufanyika mabadiliko makubwa.
Profesa Lipumba alisema katika majadiliano juu ya rasimu, Ukawa watajikita kutumia Rasimu ya Katiba waliyopewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba, ambayo imeeleza mapendekezo kwa nini yamefikiwa katika kila hoja,” alisema.
Hata hivyo, alisema wamesikitishwa sana na Rais Jakaya Kikwete, badala ya kufungua Bunge alijikita katika kuchambua rasimu na kuikosoa tume aliyoiunda mwenyewe.
“Rais Jakaya Kikwete siyo tu amemdhalilisha Jaji Warioba pamoja na wajumbe wa Tume, bali amewadhalilisha wananchi waliotoa maoni kwani hata takwimu alizotoa za kupinga rasimu siyo za kweli,” alisema Profesa Lipumba.
Alisema muundo wa Serikali tatu ndio mawazo ya wananchi ambayo yamekusanywa na watu wenye heshma wakiwapo Jaji Warioba aliyewahi kuwa Waziri Mkuu na Makamu wa Rais na Jaji Augustino Ramadhani ambaye pia amewahi kuwa Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jaji Mkuu wa Zanzibar.
Alisema kauli za Rais badala ya kuimarisha umoja zimewagawa Watanzania kwani ametoa vitisho ambavyo havina sababu hasa kwa Wapemba bila kujua kuna Wanyamwezi wanaoishi Zanzibar.
Mbatia
Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia ambaye pia ni mjumbe wa Bunge hilo, alisema kwa kauli ya juzi ya Rais Kikwete, kutangaza kuwapatia Zanzibar; watu, ardhi, mamlaka kamili na kusimamia uhusiano wa kimataifa ni kuvunja rasmi Muungano,
Mbatia alisema Rais Kikwete pia amewagawa Watanzania katika kauli zake ikiwa ni pamoja na ile ya Wapemba kwa kulima vitunguu katika Jimbo la Kibakwe kana kwamba ni makosa.

IJUMAA KUU ILA DAA......
Juma Khamis (kwa msaada wa maandiko)
Leo ni Siku ya Ijumaa Kuu, ambapo wakristo duniani kote wanaungana wenzao, kukumbuka mateso aliyoyapata Yesu Kristo, wakati aliposulubiwa msalabani huko Jerusalem, yapata miaka 2, 000 iliyopita
Kumbukumbu hii, inaadhimishwa kwa ibada ya Ijumaa Kuu iliyojaa historia ya mateso ya Yesu Kristu.
Tendo la Yesu kufa msalabani linaonesha jinsi Yesu Kristu alivyokubali kubeba makosa ya wakiristu ikiwa ni fidia ya maisha kwa Mungu.
Hata hivyo, kufa msalabani hakuna maana kuwa Yesu alikuwa na dhambi.
Maandiko ya kikiristu (biblia) yanabainisha kuwa Yesu alikubali kuzibeba dhambi za wafuasi wake katika mwili wake juu ya msalaba, ili wapate kufa wakiwa hawana dhambi na kuishi kwa ajili ya uadilifu.
Kwa kadiri ya mafundisho ya Kanisa Katoliki, dhambi ni matendo yoyote ya makusudi ambayo mtu anayotenda kwa kwenda kinyume na mapenzi ya Mungu, yaani kuvunja amri 10 za Mungu.
Ili dhambi iitwe dhambi ni lazima itendwe kwa makusudi, yaani na mtu mwenye akili timamu.
Ijumaa kuu inaadhimishwa wakati dunia leo ikiwa imegubikwa na matendo mengi ya dhambi, huku matendo mazuri ya kumtukuza Mungu yakipungua na matendo mabaya ya kishetani yakitawala nafsi za watu na kusababisha watu waishi katika ulimwengu wa kutupiana mpira.
Serikali kwa upande inalaumu madhehebu ya dini, vivyo hivyo madhehebu ya dini yanailaumu serikali kwamba imekuwa laini mno kuruhusu na kuachia kila kitu, hata yale yanayokiuka maadili ya jamii
Kwa upande mwingine wazazi wanalaumu kuwa watoto wa siku hizi hawana heshima, watoto nao wanalaumu wazazi kuwa wao wamelegea katika suala la malezi, yaani wazazi wamekuwa huria mno katika suala la malezi na hawaishi na kutenda kulingana na umri wao.
Mfano mdogo tu, baba wa miaka 60 leo anafikishwa mahakamani kwa kulawiti mtoto wa miaka 12.
Pia kuna kutupiana mpira kati ya masikini na matajiri, kwamba maskini wanalalamika kuwa matajiri ndio chanzo cha uozo wote katika jamii, watu maarufu kujihusisha dawa ya kulevya na athari zake zinawakumba watoto wa maskini.
Pia mvutano mwingine ni kati ya nchi maskini na tajiri, Afrika inazilaumu nchi za Magharibi kuwa zinaua maadili ya Kiafrika kwa kusambaza utamaduni wake mchafu.
Lakini cha kujiuliza, hakuna sera zinazopaswa kuwekwa na nchi kama hizo kuzuia uingiaji wa tamaduni hizo?.
Kwa mfano, angalia suala la ndoa za mashoga, kuna nchi za Kiafrika zimeruhusu kufungisha ndoa za mashoga.
Ndio tendo la ushoga lilikuwepo lakini halikuwa limewekewa sheria ya kuliruhusu mpaka kwenye nyumba za ibada lifanyiwe ibada na kurasimishwa rasmi kuwa huyu mwanamume ni mke wangu na mimi mwanamume mwenziwe ni mume wake.
Sikuu ya Ijumaa kuu inafuatiwa na Pasaka ambayo historia yake imeanza mbali.
Siku hii ndio aliyofufukua Yesu Kiristu baada ya kusulubiwa msalabani.
Kabla ya kuja kwa dini ya Kikiristu, watu walikuwa na dini mbali mbali lakini baada ya kuanza, watu walianza kupuuza utamaduni wa kuabudu miungu na taratibu za watu wa mataifa mbali mbali, walianza kusherehekea sikukuu ya Pasaka, kama ishara ya kukubali utamaduni mpya.
Utamaduni mpya ulihimiza watu waache kuabudu miungu na kumfuata Yesu Kristo kama mfalme na mwokozi wa watu wote duniani.
Jina la Pasaka limetokana na neno la Kiebrania lenye maana ya pasaka.
Jina hilo lina maana ya kupita juu, kukaa juu au mlinzi kama ilivyoandikwa katika Biblia.
Sherehe za Pasaka ya Kikristo ni chimbuko la sherehe ya Pasaka ya Kiyahudi.
Kwa Kiswahili majina ya sherehe za Kikristo na Kiyahudi, hazitofautiani kwa kuwa tukio la kusulubiwa na kufufuka kwa Yesu Kristo lilitokea wakati wa sikukuu ya Pasaka ya Kiyahudi mwaka wa 30 kabla ya Kristo.
Kwa mujibu wa historia ya dini ya Kikristo, wakristo wa kwanza walikuwa Wayahudi.
Awali Wayahudi hao walikuwa wakisherehekea sikukuu ya Kiyahudi pamoja na kumbukumbu ya kufufuka kwa Yesu Kristo.
Hata hivyo, Wayahudi waliojikita kwenye dini ya Kikristo, waliamua kutenganisha sherehe hizo na kufuata kalenda tofauti, kwa lengo la kuimarisha dini ya Kikristo.
Pasaka ya Kiyahudi ni miongoni mwa sikukuu muhimu na yenye mtazamo wa kipekee kwa Wayahudi, kwani inatumika kukumbuka jinsi Wanaisraeli walivyofanikiwa kuwa huru, baada ya
Pasaka ya Kikristo inashabihiana sana na Pasaka ya Kiyahudi kutokana na historia ya Pasaka hizo mbili.
Kwa mujibu wa maandiko Musa alitumwa na Mungu kuwaondoa Wanaisraeli katika hali ya utumwa katika nchi ya Misri kisha kuwaongoza kwenda nchi ya ahadi.
Hata hivyo, mfalme wa Misri mwenye cheo cha Farao alikaidi amri ya Mungu na kuendelea kuwashikilia Wanaisraeli.
Kama ilivyo kwa Wayahudi, Pasaka ya wakristo inahesabiwa kuwa sikukuu muhimu kabisa katika ukiristo.
Tarehe ya Pasaka inafuata mwandamo wa mwezi, hivyo sikukuu hiyo haina tarehe maalumu katika kalenda ya kawaida.
Lengo la siku hii ni kuhimiza umoja aliokuwa nao Yesu Kristu kwani maandiko yanasema kabla Yesu Kristo hajasulubiwa msalabani alifanya karamu na kula pamoja na wanafunzi wake ili kuhimiza umoja na ushirikiano baina yao.

ZIJUE TABIA ZA MJASILIAMALI WA KWELI.
KANUNI AU TABIA ZA MJASIRIAMALI
TABIA AU SIFAZA UJASIRIAMALI.
Ni tabia gani unahitaji ili upate mafanikio katika biashara au shuguri yoyote unayofanya?
ili ufanikiwe katika shughuri au biashara unayofanya au unayotarajia kufanya ni lazima uwe na mtazamo sahihi na mtazamo chanya. ujasiriamali una kanuni zake amboazo ni muhimu sana ili mtu afikie mafanikio aliyoya panga,kama mtu akishindwa kufuata kanuni hizo basi anakuwa na nafasi ndogo ya kupata mafanikio katika shughuri yake.
KANUNI ZA UJASIRIAMALI
Tabia za ujasiriamali zinaweza kusomwa au kufundishwa na mtu akaelewa na kuzifuata,lakinitabiazinginehazifundishiki hizi ni zile tabia ambazo mtu anazaliwa nazo. Kila binadamu anauwezo tofauti katika kufikili,kufanya maamuzi,kufanya kazi kwa bidii,tofauti hizi ndizo ambazo haziwezi kufundishika. Jambo la kutia moyo ni kwamba tabia ambazo zinafundishika ni muhimu sana kwa mjasiriamali au mtu yeyote anayetaka kufanikiwa katika biashara. Zifuatazo ni tabia za ujasiriamali.
1.kuthubutu
hii ni tabia muhimu sana kwa mjasiriamali,hapa tunazungumzia uwezo na utayali wa kufanya maamuzi ya kuingia katika biashara fulani au mradi fulani huku ukiwa umeondoa nidhamu ya woga. Watu wengi ni waoga wa kuchukua hatua au kuthubutu kuingia katika biashara,mradi n.k,watu wanaogopa hasara,hawajui jinsi ya kuendesha amradi weyewe. Mtu ili aitwe mjasiliamali ni lazima awe na uwezo wa kuhtubutu kufanya jambo, lakini jambo atakalo thubutu kufanya lazima afanye utafiti wa kutosha il baadaye limletee tija. Waswahili mwanasema” UWOGA NI UMASIKUNI”.
2.Nidhamu
Hii pia ni kanuni muhimu sana kwa mjasiriamali,mjasiriamali lazima awena na nidhamu katika biashara yake,awe na nidhamu katika matumiza yake ya pesa na ni lazima awe na nidhamu ya kufanya kakazi kwa bidii.nidhamu ni hanzo ch mafanikiao. Mfano mfanyabiashara wa duka ni lazima uwe na nidhamu kwa wateja wake ili awasimkimbie.
3.Umakini na uelevu
Wale waliofanikiwa sio tu walikuwa tayari kufanya akazi bali waliweka umakini mkubwa katika kazi waliyokuwa wakifanya. Mjasiriamali anatakiwa kuwa makini kwa kila jambo,anatakiwa kujua soko linaendaje na pia ni lazima awe muelevu wa kutambua mabadiriko yanayojitokeza katika soko ,uzalishaji na uendeshaji kwa ujumla.
4.kuwa na uwezo wa kuongoza
mjasiriamalia lazima awe na uwezo wa kuongoza na kutoa maamuzi. Baadhi ya watu wanadai uongozini kalama ombayo mtu anazaliwa nayo au anapewa na Mungu,ni kweli mtu anaweza kuzaliwa na kipaji cha kuongoza,lakini mtu anaweza kujifunza na akawa kiongozi mzuri. Katika ujasiliamali uongozi ni jambo muhimu sana,mjasiliamli lazima aweze kuogoza biashara yake au mradi wake vizuri. Mjasiriamali lazima awe na uwezo wa kusimamia wafanyakazi na kutumia mbinuza uogozi ili apate matunda kwaklile ambacho anafanya.
5.Kupenda kufanya kazi (kufanya kazi kwa bidii na maarifa)
Kitu kikubwahapa ni lazima mjasiriamli awe anaipenda kwa dhati shughuri anayofanya hii itamasahidia kufanya kazi basi kaziyo haitakuwa mgumu bali,bali utakuwa unafanya kitu ambacho kwa ko ni hobi na mwisho wa siku utafanya kazi kwa bidii na amaarifa. Watu waliofanikiwa ni wachapakazi.hivyo ni muhimu kuwa na tabia ya kufanya kazi kwa bidii.
6.Uaminifu na ukweli
Hii nayo ni tabia ambayo mjasiriamali anatakiwa kuwanayo,watja wengi wanapenda mtu mwamifu na mkwali. Kama mjasiriamali ni lazima ufanye kazi yako katika mazingira ya uamifu na ukweli ili upate wateja wengi,lazima uwe mkweli katika beizako. Uongo katika biashara ni sumu ambayo itaua biashara yako.
7.Dhamira
Mtu yeyote naweza kujiita mjasiriamali lakini kiukweli mafanikio yanahitaji uelewa wa kutosha,kufanya kazi kwa didii huku ukiwa umeweka mbele lengo au dhaira. Lengo au dhamila ni motisha tosha itakaoyo kupa msukumo mpaka kufikia mafanikio. Dhamira ya kweli inahijajika kabla hujaingia katika biashara au mradi fulani.
8.Kwenda na wakati
Mjasiriamali lazima aende na wakati iliaweze kutambua mabadiriko mbalimbali yanayo jitokeza katika masoko na uzalishaji wa bidhaa kwa ujumla. Kwenda na wakati hakutampa nafasi mjasiriamaili kuachwa nyuma katika ushindani wa kibiashara katika soko huria,kwenda na wakati pia kunatoa fulsa kwa mjasiriamali kujua njia mpya za uzalishaji. Njia ambazo zinaweza kukusaidia kwenda na wakati ni pamoja na kusoma magazeti,kufanya utafiti,kurambaza katika mitandao mbalimbali.
Tabia ambazao zimeorodheswa hapo juu ni tabia za ujumla ambazo mjasiriamali anatakiwa kuwa nazo,lakini kama huna baadhi ya tabia hizo usifadhaike kwani

JESHI LA KUIUA SIMBA HILI HAPA.
Kikosi cha Young Africans
Young Africans imerejea jana jijini Dar es salaam na kuendelea na maandalizi ya mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu ya Vodacom dhidi ya timu ya Simba SC mchezo utakaopigwa kwenye dimba la Uwanja wa Taifa siku ya jumamosi majira ya saa 10:00 kamili jioni kwa saa za Afrika Mashariki.
Kikosi cha Young Africans kimeweka kambi eneo la Bahari Beach kujiandaa na mchezo huo ambao ni muhimu kwa watoto wa Jangwani kuhakikisha wanafanya vizuri na kupata ushindi mzuri wa kumalizia ligi.
Kocha Mkuu wa Young Africans amesema vijana wake wapo katika hali nzuri kuelekea mchezo wa jumamosi, kwani hakuna majeruhi hata mmoja katika kikosi chake cha wachezaji 20 walioingia kambini kujiandaa na mchezo huo.
Hans amesema Vijana wake wanazidi kuonyesha mabadiliko makubwa kiuchezaji, mafunzo yake wanaonekana kuyaelewa vizuri hivyo kikubwa anaomba waendelee kuwa katika hali nzuri kuelekea mchezo na ana imani kikosi chake kitaibuka na ushindi.
"Nina uzoefu na michezo wa watani wa jadi, huwa inakua migumu kwa kila timu kutokana na kila timu kutaka kuonyesha wapenzi, washabiki na wanachama wake kuwa wako vizuri, Simba ni timu nzuri lakini bado sioni kikwazo cha kutuzuia tusiibuke na ushindi katika mchezo huo" alisema Hans.
Leo jioni kikosi kitafanya mazoezi katika Uwanja wa Bko Beach Veterani ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mchezo huo wa jumamosi ambapo kikosi cha Young Africans mpaka sasa kinashika nafasi ya pili kikiwa na pointi 55 huku kikiwa kimecheza michezo 25, Simba wakiwa nafasi ya nne na pointi 37 huku wakiwa wamecheza michezo 25.
Kikosi cha Young Africans kilichoingia kambini kujiandaa na mchezo huo ni:
Walinda milango:Deogratias Munish "Dida" na Ally Mustafa "Barthez"
Walinzi:Juma Abdul, Mbuyu Twite, Oscar Joshua, Ibrahim Job, Rajab Zahir, Kelvin Yondani na Nadir Haroub "Cannavaro"
Viungo:Frank Domayo, Hassan Dilunga, Salum Telela, Hamis Thabit, na Nizar Khalfani
Washambuliaji: Didier Kavumbagu, Mrisho Ngasa, Jerson Tegete, Hamisi Kizza, Hussein Javu na Saimon Msuva.

Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)