visit here again on mukebez.blogspot.com


CHANGE YOUR LIFE

CHANGE YOUR LIFE
Go to Amazon .com and get the copy of this book to make your life better.

Ijumaa, 18 Aprili 2014

KUMBE BILA WAJUMBE WALIOTOKA HAKUNA KATIBA

Dodoma.Hatua ya baadhi ya wajumbe wa Bunge la Katiba kususia vikao vya Bunge hilo imezua hofu kwamba inaweza kukwamisha mchakato wa kupatikana kwa Katiba mpya hasa katika kufanya uamuzi wa kupitisha ibara za Katiba hiyo.
Wajumbe ambao ni wanachama wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), juzi walitoka nje na kususia vikao vya Bunge hilo kwa madai kwamba hawaridhishwi jinsi mambo yanavyokwenda.
Kanuni za uendeshaji wa Bunge hilo za 2014, zinasema ili ibara au Rasimu ya Katiba iweze kupitishwa itahitaji kuungwa mkono na theluthi mbili ya wajumbe kwa pande zote za Muungano.
Kanuni ya 37 (1), inasomeka: “… ili ibara au rasimu iweze kupitishwa, itahitaji kuungwa mkono na wingi wa theluthi mbili ya wajumbe kutoka Tanzania Bara na theluthi mbili kutoka Zanzibar.”
Taarifa zisizo rasmi zinasema awali ili kuwezesha kupatikana kwa theluthi mbili kutoka upande wa Zanzibar, CCM kilikuwa kinakihitaji kupata kura 16 ikilinganishwa na idadi ya wajumbe wanaokiunga mkono.
Kwa maana hiyo kuondoka kwa wanachama wa Ukawa kunamaanisha kwamba Bunge Maalumu haliwezi kupata akidi inayotakiwa wakati wa kufanya uamuzi wa kupitisha ibara kwa mujibu wa kanuni hizo.
Mwenyekiti mwenza wa Ukawa, Profesa Ibrahim Lipumba alisema jana kuwa hawatarejea katika Bunge hilo hadi kutakapokuwa na maridhiano ambayo kwa upande wao ni kuzingatiwa kwa rasimu iliyotokana na Tume ya Mabadiliko ya Katiba, iliyoongozwa na Jaji Joseph Warioba. Katibu wa Bunge Maalumu, Yahya Khamis Hamad alisema hivi sasa si vyema kutabiri kama wajumbe wa Ukawa watarejea bungeni au la.
“Mimi na wewe hatuwezi kutabiri, maana hawa ni viongozi wa kisiasa, wanaweza kuondoka leo, lakini kesho wakawa na mazungumzo na wenzao halafu wakarejea bungeni na shughuli zikaendelea,” alisema Hamad na kuongeza:
“Ni kweli kwamba kutokuwapo kwao kunaweza kuwa na athari katika kufanya uamuzi, lakini pia hatuwezi kusema ni athari zipi kwa sasa kwa sababu hakuna suala ambalo linapaswa kufanyiwa uamuzi kwa sasa.”
Hamad alisema kama alivyosema Mwenyekiti wa Bunge Maalumu, Samuel Sitta ipo fursa za kufanya mazungumzo na kwamba anaamini ikitumika vizuri, Bunge litaweza kuendelea na kufikia mwisho mwema.
“Kwa hiyo mimi nasema sisi tusubiri, maana hadi sasa hatujapata kufahamu kama kuondoka kwao watarejea baada ya Pasaka, Jumanne ijayo au ndiyo wameondoka moja kwa moja au ni vipi, ndiyo maana nasema ni vigumu kudhania kitakachotokea,” alisema Hamad ambaye pia ni Katibu wa Baraza la Wawakilishi.
Wasusia Kamati ya Uongozi

Alhamisi, 17 Aprili 2014

KIKWETE AWASHAMBULIA WANAOWATUKANA WAASISI.

Dar es Salaam.Rais Jakaya Kikwete amesema ni utovu wa nidhamu na ukosefu wa adabu unaoonyeshwa na baadhi ya Watanzania kuwatukana, kuwadhihaki na kuwakejeli waanzilishi wa Taifa la Tanzania, Mwalimu Julius Nyerere na Sheikh Abeid Amani Karume.
Rais Kikwete alitoa kauli hiyo juzi alipokuwa kwenye mahojiano maalumu na wahariri wa baadhi ya vyombo vya habari (wa Mwananchi hawakuwapo) ya kuadhimisha miaka 50 ya Muungano.
Kauli hiyo ilikuwa ni jibu la moja ya maswali alilokuwa ameulizwa na wahariri hao kuhusu matusi, kejeli na dhihaka ambazo zimekuwa zinaonyeshwa na wajumbe wachache wa Bunge Maalumu la Katiba juu ya waasisi hao wa Tanzania na wabunifu wakuu wa Muungano wa Tanzania.
“Ni kukosa adabu na ni utovu mkubwa wa nidhamu kwa Mtanzania yeyote kuwatukana, kuwadhihaki au kuwakejeli waasisi wa Taifa letu. Hawa ni watu ambao waliifanyia nchi yetu mambo makubwa,” alisema Rais Kikwete na kuongeza:
“Mzee Karume yule aliongoza Mapinduzi yaliyoondoa dhuluma na uonevu pale Visiwani. Waafrika walio wengi walikuwa wanaonewa sana pale Tanzania Visiwani, pengine watu wamesahau, lakini hata pale walipokuwa wanashinda uchaguzi, bado walikuwa hawapewi nafasi ya kuongoza maisha yao wenyewe.”
Rais alisisitiza kuwa ni ukosefu wa adabu kwa yeyote kumshutumu mtu aliyejitolea kiasi hicho ili kubadilisha mfumo dhalimu na kujenga maisha na mazingira ya maisha bora kwa wengi.
“Mzee Nyerere yule ametuachia Taifa moja, lililoungana, lenye umoja, lenye amani na mshikamano. Misingi ambayo aliijenga yeye ndiyo imeendelea kuongoza Taifa letu kwa miaka yote hii,” alisema.
Wakati huo huo, Rais Kikwete alipokea rasmi tuzo ya Kiongozi Bora wa Maendeleo Afrika –kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe aliyeipokea kwa niaba yake huko Marekani, Aprili 9, mwaka huu.
Rais Kikwete alisema amepokea tuzo hiyo na amewazawadia Watanzania wote, kwa sababu wao ndiyo waliochangia maendeleo yaliyomwezesha kupata heshima hiyo.
“Napokea Tuzo hii kwa niaba ya Watanzania wote. Aidha, naitoa kwa Watanzania kwa sababu, hata kama nimekuwa kiongozi, ukweli ni kwamba mafanikio na maendeleo yote yaliyopatikana hadi kutunukiwa tuzo hii, yanatokana na juhudi zetu sote'Alisema Kikwete.

WAKATI MAAFA YANAPOGEUKA NEEMA KWA WENGINE.

Dar es Salaam. Wakati maelfu ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam wakilia na kumboleza kutokana na mvua zilizonyesha kwa siku tatu mfululizo, kwa wengine hali hiyo ilikuwa neema.
Hivi sasa, wakati wenzao wakitathmini hasara na kumalizia misiba kwa walioondokewa na ndugu au jamaa, wao wanahesabu faida na pengine kuombea hali kama hiyo irejee tena ili waendelee kupata kunufaika.
Siku tatu za mwisho wa wiki iliyopita, Jiji la Dar es Salaam lilikumbwa na taharuki iliyotokana na mafuriko. Hata wale wasioishi mabondeni waliiona adha ya mvua hiyo kutokana na maji kutanda karibu kila kona ya jiji.
Kuvusha watu kwenye maji
Hili halikuepukika katika siku hizo za mvua mfululizo kwani kuna baadhi ya maeneo ambayo hakukuwa na usafiri mwingine unaoweza kukuvusha zaidi ya watu hawa.
Kubebwa buku (yaani Sh1,000), kushikwa mkono jero (yaani Sh500). Kauli hiyo ilikuwa ikirudiwa mara kadhaa na vijana waliokuwapo katika eneo la Mto Yombo, karibu na Shule ya Msingi Kilakala Temeke, Dar es Salaam.
“Kuvusha gari tunachaji Sh500, watu wanachajiwa kwa bei tofauti. Ukibebwa unalipa Sh1,000 lakini ukiongozwa kwa kushikwa mkono ni Sh500,” anasema mmoja wa vijana hao aliyejitambulisha kwa jina la Mohamed Pandu. Akizungumzia kuhusu tija ya biashara hiyo, Pandu anasema kuwa ni ya muda mfupi lakini ina faida kwa kuwa hauhitaji kuwa na mtaji wa pesa ama vifaa.
Waendesha bodaboda, bajaji
Kutokana na kuharibika kwa miuondombinu na maji kujaa kwenye barabara uliosababishwa na mvua hizo, usafiri wa daladala uliozoeleka kwa wengi ulikuwa mgumu sana na badala yake pikipiki za abiria, maarufu kama bodaboda, na za matairi matatu (bajaji) zikachukua nafasi.
Kwa kawaida nauli ya bodaboda kutoka Kituo Kikuu cha Mabasi Ubungo mpaka Temeke ni Sh 8,000 au Sh10,000, lakini kwa siku hizo tatu nauli ilipanda hadi kufikia Sh30,000.
Mmoja wa waendesha bodaboda wa Tabata Relini, Hussein Ramadhani alisema kuanzia Ijumaa mvua zilipoanza kunyesha pato lake la siku liliongezeka mara mbili.
Dereva huyo aliongeza kuwa mvua hizo zimekuwa baraka kwake na kama zingeendelea kunyesha, angeneemeka maradufu.
HABARI KWA HISANI YA GAAZETI LALEO LA MWANANCHI.

MPANGO MPYA WA BARABARA DAR!

MABADILIKO YA UELEKEO WA BARABARA KATIKATI YA JIJI LA DAR ES SALAAM KUANZIA SIKU YA TAREHE 28/04/2014. TRAFFIC CIRCULATION AT CBD
Key: 1. RANGI YA NJANO - Njia ya Uelekeo Mmoja {One Way}.
2. RANGI YA BLUE MPAUKO - Njia ya Mielekeo Miwili {Two Way}
3. RANGI YA KIJANI - Mitaa ya Kutembea kwa Miguu Magari marufuku {Walking Streets}
4. RANGI NYEKUNDU - Barabara za kupita Daladala
5. RANGI YA BLUU ILIYOIVA - Barabara za DART
6. DUARA ZA NJANO - Mzunguuko {Roundabout}
7. MSALABA WA KIJANI - Makutano yenye Taa za kuongozea Magari {Singnalized Intersection}
[image]
1. Kipande cha Mtaa wa Samora kuanzia Mnara wa Askari (Askari Monument) hadi Clock Tower Magari kutakuwa na mabadiliko ambayo magari yatakuwa yanaelekea Clock Tower badala ya Askari Monument.
2. Barabara ya Sokoine kuanzia Station hadi Makutano ya Mtaa wa Maktaba Posta Ya Zamani Magari yatakuwa yanaelekea Uelekeo mmoja wa Station Posta ya Zamani tofauti na ilivyo sasa Posta ya Zamani kwenda Station.
3. Barabara ya Kivukoni Kuanzia Posta ya Zamani hadi Ferry itakuwa barabara ya mielekeo miwili (Two Ways).
4. Barabara ya Samora kuanzia Mnara wa Askari hadi Ocean Road Hospitali itakuwa ni barabara ya mielekeo miwili.
5. Daladala Zote zitakazotokea barabara za Makataba zitakunja kulia pembeni ya Jengo la NBC na hadi Makutano ya Mkwepu na kukunja kushito kuingia Sokoine pale Posta ya Zamani na baadaye kukunja kushoto kuingia Makataba na kurudi Posta Mpya .
Kwa Maelezo zaidi Wasiliana na Ofisi za DART
UBUNGO PLAZA GHOROFA YA KWANZA.
AU.
OFISI YA MHANDISI WA MANISPAA YA ILALA
MABALA NA SHOPRITE SUPEEMARKET JIRANK NA KAMATA
Mtaarifu mwingine juu ya mabadiliko haya kuondoa usumbufu ifikapo siku ya Jumatatu 28/04/2014. PASAKA NJEMA
javascript:

Picha ya leo.rais kikwete akiwa na watoto kwenye pantoni

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgOlV5e4E7tJxtufBlkKGQnCgzBbbGAlaZFfc4q4rFl9nDOMoGgN6T4YOgE7PHrcKhiMt8CTQo4ml87W6NJJPd6DRIHFc98Q_wf1W3PRJuZVHzqNtSjwuAAhT6banX8LzABVMpznbD7_hfj/s1600/f1.jpg

CHAMA CHA WAFANYAKAZI CHAANZA KUITIBUA SERIKALI.

SHIRIKISHO la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), limebaini kuwa wafanyakazi wengi nchini bado wanakabiliwa na maisha magumu kutokana na malipo duni ya ujira.
Pia limesema kutozingatiwa kwa sheria za kazi, uchumi usio imara, kukosekana kwa utashi wa kisiasa na vikao vya majadiliano visivyo na tija ndiko kunachangia uchumi wa wananchi kudidimia.
Katibu Mkuu wa TUCTA, Nicholas Mgaya, alibainisha hayo jijini Dar es Salaam jana baada ya kufanyika kwa kikao cha 15 cha Baraza Kuu la shirikisho hilo.
Alisema baraza hilo limebaini kima cha chini cha mshahara kwa sekta zote mbili – za umma na binafsi – bado hakijafikia hata sh 315,000 kima ambacho kimekuwa kikidaiwa kwa takribani miaka tisa iliyopita.
“Kima cha chini cha serikali hivi sasa ni sh 240,000 sawa na sh 8,000 kwa siku, waajiri walio wengi katika sekta binafsi wanalipa kati ya sh 100,000 hadi sh 150,000 kwa mwezi ambayo ni sawa na sh 3,500 na sh 5,000 kwa siku,” alieleza Mgaya.
Alisema Baraza Kuu limebaini ulipaji wa mishahara duni hautokani na kutokuwa na uwezo wa kulipa, bali ni mtindo uliozoeleka wa kutoheshimu nguvu kazi, na kwamba wanaamini nguvu kazi si mojawapo ya vipaumbele vya taifa kwa imani kuwa inapatikana kirahisi na kwa bei rahisi.
“Baraza Kuu pia lilijadili suala la kodi, kwamba licha ya kuwa na malalamiko ya muda mrefu, wafanyakazi wameendelea kubebeshwa mzigo mkubwa wa kodi ya mapato.
“Shirikisho limekuwa likidai kwa muda mrefu kodi ya mapato kwa wafanyakazi iwe chini ya asilimia 10, na kwamba wigo wa walipaji wa kodi hiyo upanuliwe, lakini badala ya serikali kulitazama jambo hili kwa umakini na kitaalamu, imekuwa ama ikiongeza kima cha mshahara kinachoelezwa kwamba hakitozwi kodi au kupunguza asilimia moja,” alieleza Mgaya.
Pia alisema Baraza Kuu lilizungumzia pensheni ambapo limebaini maboresho ya hifadhi ya jamii yaliyokuwa yakisimamiwa na Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), bado hayajasaidia kutatua kero ya muda mrefu ya malipo duni ya pensheni.
Katika hatua nyingine, Mgaya amekiita kikundi cha watu watano kinachompinga kuwa ni cha chuki binafsi za kiungozi, kwa kuwa walishindwa katika uchaguzi wa nafasi aliyonayo.
Alisema kikundi hicho cha watu watano ambao walizungumza na vyombo vya habari wakidai kuwa hawamtaki kwa kuwa ana umri mkubwa, matumizi mabaya ya fedha, kutosimamia vizuri kitega uchumi, kinafanya hivyo kutokana na sababu binafsi za kushindwa katika nafasi hiyo ya ukatibu mkuu.