Kurasa

Jumatatu, 25 Aprili 2016

HIKI NDICHO KINACHOSABABISHA UPUNGUFU WA AJIRA TANZANIA.

PICHA;WANAFUNZI CHUO KIKUU MUHIMBILI WAKIANDAMANA.

Katika miaka ya hivi karibuni Tanzania imekumbwa na tatizo kubwa la uhaba wa ajira.Wasomi wamekuwa wengi sana ukiringanisha na ajira zilizopo nchini kitu ambacho kinafanya wasomi wetu kufanya kazi ambazo hazifanani na elimu wanayopata pamoja na kulipwa mishahara duni ambayo haiwezi kumpa mtu motisha wa kufanya kazi kwa juhudi na maarifa.
Lakini kabla ya kumtafuta mchawi wa tatizo hili tunapaswa kujiuliza maswali haya kwanza;
Je! nini hasa sababu ya tatizo hili la ajira nchini?
Je!Sababu hizo zinaweza kurekebishwa?
Ni kwa mikakati gani tatizo hili litapatiwa ufumbuzi wa kudumu na lisijirudie mala kwa mala kama ilivyo sasa?.

Kama ilivyo kawaida,unapotaka kuzima moto ni lazima uzime chanzo halisi cha moto huo badala ya kuhangaika na ndimi au moshi.Tatizo hili kwa uchunguzi wangu nimegundua limesababishwa na mambo kadhaa kama ifuatavyo;

KUISHI MAZOEA;
Toka zamani jamii zetu hususani za kiTanzania zimejenga imani kwamba maisha mazuri yanakuja kwa mtu kusoma na kupata alama nzuri shuleni na hatimae kuajiriwa mahali fulani.Wakati jamii ikiendeleza mapokeo hayo ambayo yamekuwa yakirithishwa kizazi kimoja baada ya kingine ilisahau kuwa maeneo ambayo vijana wanaomba ajira yanapaswa kuongezwa kama ambavyo vijana wamekuwa wakihitimu vyuo vikuu mwaka hadi mwaka.Lakini pia walisahau kwamba waanzilishi wa maeneo hayo ya kazi ni vijana hao wasomi,Serikali na jamii kwa ujumla.

Matokeo ya kujisahau huko ni kuongezeka kwa vijana wasomi huku wakiwa wameweka imani ya kuajiriwa na kupungua maeneo ya kuajiri vijana hao.HILI NI JIPU AMBALO LINAENDELEA KUIVA TARATIBU.

UBUNIFU MDOGO;
Hiki ni kipengele ambacho kinachoendeleza jipu hilo na kama viongozi wa Serikali hususani katika sekta husika wasipokuwa makini mambo yataendelea kujirudia na hivyo kulifanya tatizo kuendelea kuwa kubwa badala ya kulitatua.Hapa zinahitajika mbinu za kudumu ambazo zitakuwa za kudumu kuepuka tatizo kujirudia.

Kwa mfano kumekuwa na swala la kuwapa mikopo wanafunzi wa elimu ya juu kila mwaka na urejeshwaji wake umekuwa wa kusua sua.Kwa mtazamo wa harakaharaka i lazima urejeshwaji wa mikopo hiyo uwe ni wa kusuasua kwasababu mkopeshaji ambae ni Serikali hana uhakika na chanzo cha mapato cha mkopaji ambacho kingerudisha mkopo huo.

Kumbe hapa tunapata jibu gumu linalotokana na swali rahisi kwamba badala ya Serikali kuwakopesha wanafunzi kupata elimu ilitakiwa pia kuwakopesha wahitimu fedha kwaajili ya kuifanya kazi ya elimu wanayopata na hatimae kurejesha mkopo,kuwa na maendleo binafi na nchi kwa ujumla.

MFANO WA SULUHISHO;
Ni vizuri sasa Serikali ikaanzisha mpango maalum wa wahitimu kuunda vikundi na kusajili kampuni.Baada ya hapo Serikali itenge fedha maalum kwaajili ya kuwakopesha wahitimu hao kuendesha vikundi au kampuni hizo ambazo watazirejesha kidogokidogo kwaajili ya kusaidia vikundi na kampuni nyingine zinazoanzishwa.
Kampuni hizo zinapaswa kuwa na usimamizi maalum kutoka Serikalinin ili kuzifanya ziendeshwe kwa mafanikio na hatimae kuipata tija ya elimu yetu.

KUTOA MIKOPO KWAAJILI YA ELIMU BILA ELIMU HIYO KUZALISHA KINACHOKUSUDIWA PIA NI UFISADI.TUNAPASWA KUUPIGA VITA UFISADI HUO.

Tuandikie maoni hapa kama una maoni yoyote kuhusiana na unachokisoma hapa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni