Kurasa

Jumanne, 26 Aprili 2016

FAHAMU KUHUSU WAKALA WA MAJENGO

PICHA(realestateslandny.blogspot.com)

Katika maeneo tunayoishi tunapotaka kununua,kuuza au kupangisha nyumba pamoja na viwanja tumezoea kuwatumia watu tunaowaita madalali.Bahati mbaya madalali hawa wanakuwa hawana chochote kinachomtambulisha au kitakachokupa wewe ulinzi endapo mambo yatakwenda vibaya.Utakuta mahali wamekaa vijana wengi tu maarufu kama kijiwe na wameweka kibao kimeandikwa madalali wa viwanja na nyumba wanapatikana hapa.


Madalali hawa uchwala wamekuwa na madhara makubwa sana kwa wamiliki na hata wanunuzi wa nyumba pamoja na viwanja kutokana na wengi wao kuwa matapeli na kuuza viwanja au nyumba za watu zaidi ya mala moja.

Leo katika mada yangu nitaelezea kuhusu biashara ya wakala wa majengo ambao kimsingi wanafanya kazi hizi za madalali isipokuwa hawa wanatambulika kisheria na chochote kikitokea wao ndio wanachukua jukumu.

Wakala wa majengo kama alivyo dalali ni mtu anaesaidia watu kuuza au kununua ardhi au nyumba.Kwa kawaida wakala huyo lazima ajue thamani ya mali anayotaka kuinadi pamoja na mapungufu yake kwasababu kimsingi hatakiwi kumdanganya mteja wake.Pia wakala mzuri anatakiwa ajue kuitangaza biashara na pia ajue kufanya makubaliano na mteja.

Kama ishu itakuwa ni kumsaidia muuzaji kuuza mali yake,wakala wa majengo atapaswa kumsaidia muuzaji katika kupanga bei ili ile rahisi kwake anapokuwa anakubaliana na mteja wa mali hiyo.Pia wakala huyo atakuwa na jukumu la kuwapeleka wateja ilipo mali inayouzwa na kuwaonesha mazingira yote ya mali hiyo,kujibu maswali kama mteja ana maswalli na kuwapa taarifa zote muhimu kuhusiana na mali hiyo mpaka pale ambapo mteja atakuwa amevutiwa kununua mali hiyo na hapo ndipo ambapo biashara inafanyika.

Kama ishu itakuwa ni kumsaidia mnunuaji basi wakala atapaswa kumuuliza mteja wake aina ya nyumba au kiwanja anachohitaji na taarifa zote muhimu na kwa kutumia taarifa za majengo au viwanja alizonazo anaweza kumpeleka mteja wake kwenye eneo au nyumba anayotaka na kumkutanisha na mmiliki wa mali hiyo na hatimae biashara kufanyika.

ELIMU YA WAKALA WA MAJENGO.
Kwa kawaida wakala wa majengo anakuwa na elimu kuhusiana na kazi hiyo lakini pia anakuwa na leseni au kibali cha kufanya kazi hiyo.Elimu yake inakuwa ni programu maalum ambazo zinamruhusu kupata leseni na kumpa mamlaka kisheria kuwa wakala.


Mpendwa msomaji tukutane wakati mwingine wakati tutakapokuwa tunaangalia biashara nyingine.
Kwa maoni zaidi unaweza kutuandikia hapo chini kwenye kiboksi chetu cha maoni.Unaweza pia kushare post hizi kwenye icon zinazoonekana hapo chini.Bonyeza icon hapo chini zenye herufi f kushare facebook na t kushare twitter.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni