Kurasa

Jumapili, 24 Aprili 2016

HIKI KINATHIBITISHA ALIE BORA KATI YA MFANYA KAZI NA MFANYA BIASHARA.

PICHA;BUSINESS MAN

Umewahi kujiuliza swali hili kwamba

 ni nani alie bora na anae enjoy maisha zaidi kati ya mfanya kazi na mfanyabiashara?

Katika jamii zetu tumekuwa tukihimizwa toka tuko wadogo kusoma kwa bidii ili siku moja tuje kuwa na moja kati ya proffessional kama Udactari,Uhandisi,Ualimu (kama alivyo muandishi wa mada hii),Urubani,Uanasheria,Uandishi wa habari(kama alivyo muandishi wa mada hii) na fani nyingine nyingi.Tumekuwa tukiaminishwa hivyo na sisi tukiwaaminisha watoto wetu kwamba unapokuwa na moja kati ya fani hizo basi una uhakika wa kuwa na maisha bora.


Kutokana na imani hiyo mkazo mkubwa umekuwa kumaliza shule ukiwa umefaulu vizuri na kuomba kazi uliyosomea ili uanze kupata mafanikio uliyoyaota toka utotoni.Sasa tatizo linakuja unapochagua kuacha shule na kuanza kufanya biashara,au ujaribu kuwashawishi wazazi wako na jamii kwamba unataka kuwa mfanyabiashara,hakuna atakae kuelewa.

Tuangalie kwa jicho la tatu kwa mifano halisi;

Ukitafakari kwa kina utagundua kuwa kuchagua kufanya kazi ni kuchagua kuwa mtumwa hususani kama huna malengo ya muda mrefu na muda mfupi kwenye kazi unayofanya.Kumbuka unapomaliza shule unakwenda kuomba kazi kwenye kampuni au shirika fulani.Kampuni hiyo unayoomba kazi inamilikiwa na mtu au watu na bahati nzuri au mbaya ni kuwa wengine umawapita elimu kwa mbali sana.Kwa mfano mmiliki wa magazeti pendwa Tanzania Erick Shigongo amekuwa akiongea kwenye makongamano mbalimbali kuwa pamoja na kwamba hana elimu kubwa ya kutisha anachokifanya kinawazidi kwa mbali sana wenye madegree.Kitu ambacho ni kweli.
PICHA; SHIGONGO NA WAANDISHI WA HABARI.

Maeneo tunayofanya kazi ni biashara za watu na walianza kidogo mpaka kufika hapo walipo. Fuatilia historia za kina bill gate,Said Salim Bakhresa na wengine wengi utagundua kuwa sio shule iliyowafikisha hapo bali ni uthubutu na ubunifu ukijumlisha na kujiamini na kuushinda woga yani ujasiri.

Kutokana na hilo ni dhahiri kuwa biashara ni bora kuliko kazi kwasababu mfanyabiashara yuko huru na anafanya kitu ambacho ni chake so anakifanya kwa upendo na umakini wa hali ya juu.

Mfanyakazi makini ni yule anaefanya kazi huku akiwekeza kidogokidogo mpaka anapokuwa tayari kumiliki Biashara yake zake na kuzisimamia.Mfanyakazi mtumwa ni yule anaefanya kazi akiwa na mawazo kuwa siku moja atakuja kustaafu na kupata pensheni itakayomuwezesha kujenga nyumba nzuri.

Mfanyakazi mzuri ni yule anaehakikisha kuwa kila kitu anachonunua kutokana na mshahara wake kinazalisha zaidi fedha.Mfanyakazi mtumwa ni yule ambae anaona ufahali kununua vitu ambavyo vinazidi kumuongezea matumizi kama magari makubwa na kwenda kustarehe sehemu za ghalama kubwa na baada ya hapo anasubiri mwisho wa mwezi mwingine.

Tunapaswa kuwaheshimu watu wanaoanza biashara bila kujari wana mtaji mdogo kiasi gani kwasababu kuna watu wengi sana hata hapo mtaani kwako unapoishi ambao wametajirika kutokana na biashara zao ndogo huku wakiwaacha mbali watu ambao waliendelea na shule zamani wakati wao wakiishia darasa la saba na kufanya biashara.

ASANTE SANA NA TUKUTANE WAKATI MWINGINE.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni