Kurasa

Jumapili, 6 Machi 2016

UJASIRIAMALI

Karibu mpenzi msomaji katika mfululizo wa mada zetu za ujasiriamali ambazo zinapatikana katika kitabu maalum cha ujasiriamali kinachoitwa MIMI NI TAJIRI kinachouzwa kwa shilingi 2500 tu.Kama unahitaji kitabu hicho chenye pia maelekezo ya jinsi ya kutengeneza bidhaa mbalimbali na jinsi utakavyopata malighafi wasiliana nasi kwa kutumia namba zetu na utakipata mala moja.

Leo katika muendelezo wa mada zetu tutaangalia mambo yanayoweza kumkwamisha mjasiriamali.



Woga na kutokujiamini; Ujasiri ni kutu muhimu sana katika biashara.Mtaalamu mmoja aliwahi kusema kuwa jasiri ni mtu anaethubutu kufanya kitu ambacho amekuwa akikihofia wakati woga ni hali ya kushindwa kuthubutu kufanya kile unachokihofia katika maisha.Mtaalamu huyo alisema kuwa kutokuwa na hofu kabisa katika maisha ni sawa na upumbavu.Maana yake ni kuwa kila binadamu ana hofu lakini tofauti inaonekana jinsi ambavyo tunazishinda hofu hizo.Kama mfanyabiashara unapaswa kuishinda hofu kwakuwa mala nyingi hofu hutokea kwa jambo ambalo kama utalifanya lunaweza kukuletea manufaa makubwa sana katika maisha.

Kukata tamaa; Woga na kutokujiamini vinaweza kumfanya mtu kukata tamaa.Muandishi wa kitabu hiki huamini kuwa mala zote kukata tamaa huja mwisho na mwisho wa binadamu ni k8ifo(Always giving up is the end and the end is death).Hii maana yake ni kuwa binadamu hupaswi kukata tamaa kabla hujafa.Kumbuka mahitaji ya binadamu hayakati tamaa na yapo kila siku.Mjasiriamali yoyote anaekata tamaa mapema hana sifa ya ujasiriamali na anaweza kuuona mwisho wa biashara yake mapema zaidi ya alivyotarajia.

Matumizi mabaya ya pesa; Mtu yoyote ambae hana nidhamu ya pesa anaingia kwenye kundi la watu waliokosa sifa muhimu za mjasiriamali na mafanikio ya kibiashara kwake huwa ni magumu sana.Mjasiriamali mzuri ni yule ambae matumizi ya pesa kwaajili ya mahitaji yake yanatokana na faida na sio mtaji wala akiba.Pia kama kipato chako kwa siku ni 10000 halafu unatumia 15000 huwezi kufika mbali.

Kutokuweka kumbukumbu; Wataalamu wanasema mali bila daftari huisha bila habari.Hii ni kweli kabisa.Mfanyabiashara anaefanya biashara bila nyaraka za kumbukumbu hujikuta anafilisika bila kujijua.Kumbukumbu huweza kumfanya mtu abadilishe mwenendo wa biashara kama itakuwa inakwenda ndivyo sivyo.

Kutokuwa na vyanzo mbadala; Hii ni changamoto kubwa sana hasa kwa biashara inayochipukia.Biashara inapokuwa ndio tegemeo kubwa kwa mahitaji ya mjasiriamali,wakati mwingine inakuwa ngumu sana kuendelea na huweza kufa kabisa kama tahadhari isipochukuliwa.Ni kawaida sana kwa biashara kupanda na kushuka na hapo ndipo vyanzo mbadala vya pesa vinapohitajika.Vyanzo mbadala huweza kuisaidia biashara kwa kuongeza mtaji au kuisaidia matumizi.

KUMBUKA: Haya ni baadhi tu ya mambo yanayoweza kuikwamisha biashara yako,matatizo mengine mengi hutokea wakati unaendelea na biashara hivyo jiandae.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni