Kurasa

Jumanne, 8 Machi 2016

UJASIRIAMALI; AINA ZA BIASHARA#TYPE OF BUSINESS#

Karibu tena mpenzi msomaji wetu katika mfululizo wa makala zetu za ujasiriamali.Makala hizi ni muendelezo wa kile kilichoandikwa kwenye kitabu kinachoitwa MIMI NI TAJIRI kinachouzwa mtandaoni kwa shilingi 2500 tu.Kama unahitaji kitabu hiki chenye ushauri wa kibiashara,jinsi ya kutengeneza bidhaa mbalimbali ikiwemo sabuni na shampoo,Mahali yalipo maduka ya malighafi za kutengenezea bidhaa hizo pamoja na bei za malighafi husika, wasiliana nasi kupitia namba yetu 0654627227 au tuandikie kwenye mdeonidas@gmail.com. Leo katika makala hii tutaangalia aina za biashara na jinsi inavyoweza kukusaidia kupata wazo la biashara. Wakati mjasiriamali anafikiria kuhusu wazo la biashara,ni lazima afikirie kuhusu aina mbili za biashara ambazo kupitia hizo mawazo mbalimbali ya kibiashara huweza kupatikana.Aina hizo ni kama ifuatavyo;



HUDUMA.
Hizi ni biashara ambazo hufanyika kulingana na ujuzi wa mtu au mfanyabiashara.Mala nyingi biashara hizi hutegemea mtaji wa kuanzisha tu lakini baada ya hapo hazihitaji kufangasha bidhaa mpya au kufungasha.Pia biashara hizi za huduma huhitaji mitaji kidogo ukilinganisha na aina nyingine ya biashara.Mfano wa biashara ya huduma ni pamoja na hizi zifuatazo;
Huduma za fedha za mitandaoni,
Salon(za kike na za kiume)
Huduma za fedha za mtandaoni(mpesa,togo pesa,airtel money nk)
Mashine za kusaga na kukoboa
Huduma za usafiri(daladala,taxi na bodaboda)
Music au kuimba na kuigiza
Utaalamu kama uanasheria,uandishi,mafundi ujenzi nk.
Kutoa huduma za kilimo kama kulima mashamba ya watu kwa trekta nk.
Kutoa huduma za hospital au zahanati
Kutoa huduma za kielimu kama kufundisha nk.
Hizi ni baadhii au ni mifano michache tu ya biashara za huduma lakini zipo nyingi sana.

2.BIASHARA ZA BIDHAA;
Hizi ni biashara zinazohusiana na kuuza na kununua bidhaa kwa kutegemea faida.Mala nyingi biashara hizi zinahitaji mtaji mkubwa na umakini wa hali ya juu..Ni rahisi sana kwa biashara hizi kuanguka kama mfanyabiashara huasika hatafuata misngi ya biashara.Pamoja na hayo hizi ni biashara ambazo zinaweza kumfanya mtu au kikundi kutajirika sana kama kanuni zitafuatwa.Mfano wa biashara hizo ni kama ifuatavyo;

Biashara za nguo,
Biashara za vyakula
Vifaa vya ujenzi
Biashara ya vifaa vya kielimu
Biashara za vinywaji hususani sehemu zenye joto sana nk.

Bidhaa katika biashara hizi huweza kupatikana kwa mfanyabiashara husika kununua viwandani bidhaa na kuziuza au anaweza kununua kwenye maduka ya jumla na kuziuza lejaleja kwa faida.Pia mfanyabiashara anaweza kutengeneza bidhaa zake mwenyewe katika viwanda vidogo vidogo au vikubwa na na kuziuza

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni