Kurasa

Ijumaa, 4 Machi 2016

MAANA HALISI YA UJASIRIAMALI

1. MAANA YA UJASIRIAMALI.

Ujasiriamali ni ile hali ya mtu kuona fulsa na kuzifanyia kazi kwa lengo la kujipatia kipato. Kwa mfano mtu anapoishi mazingira ambayo watu wamekosa nishati ya umeme anaweza kutumia kama fulsa kwa kuuza vifaa vya umeme wa jua akajipatia kipato.Mala nyingi mjasiriamali anakuwa na sifa zifuatazo;



Kujituma,motisha,kutambua fulsa kwa haraka,kuthubutu,kujitegemea,kujenga mahusiano na watu, kuanzisha na kuendesha miradi,kuongoza,kushawishi,kuwa na maleng,kuthubutu pamoja na tahadhari.

Sio lazima kuwa na sifa zote hizi lakini mala nyingi wajasiriamali wanaofanikiwa ni wale wanaoamini kuwa wanaweza.

1.2 Mambo muhimu ukiwa mjasiriamali;
→Kujituma; Mafanikio yoyote katika biashara yanatokana na kujituma,hii ina maana kuwa mjasiriamali anatumia nguvu na muda wake wote kwaajili ya biashara yake.
→Ijue hasara; Siku zote ukiwa mjasiriamali unapaswa kufahamu kuwa biashara yoyote lazima itakuwa nafaida na hasara na kama mjasiriamali uwe tayari kupata hasara kama unavyokuwa tayari kupata faida.Hii itakusaidia sana kisaikolojia kama mambo hayatakwenda sawa.
→Kubadilika; Ukiwa mjasiriamali lazima uwe tayari kubadilika.Hii in maana kuwa kila siku fulsa mpya huweza kutokea katika mazingira yetu na zile za zamani kupata ufumbuzi.Mjasiriamali mzuri ni yule anaeangalia na kuyaona mabadilko yanayotokea katika soko au biashara na huduma anayotoa mjasiriamali

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni